Thursday, February 21, 2019

Christian Mother of 11 Poisoned to Death in Uganda by Muslim Sister-In-Law Months After She Left Islam



A Christian mother of 11 was poisoned to death last week by her Muslim sister-in-law in an eastern Ugandan village, neighborhood sources told a leading Christian persecution watchdog organization.
Namumbeiza Swabura, a Muslim convert to Christianity, succombed to food poisoning last Wednesday after enduring months of constant threats from local Muslims after she and her husband — a former Islamic school teacher [sheikh] — accepted Jesus Christ as their Lord and Savior in August 2014, sources informed Morning Star News.
Swabura is survived by her husband, Mugoya Muhammad, and her 11 children, the youngest being a 5-month-old infant.
Sources allege that Swabura's sister-in-law, Jafaran Wowa, visited Swabura at her home around 4 p.m. last Wednesday in Kibuku District's village of Nabuli and offered to prepare Swabura a meal known in Uganda as matoke, which consists of cooked plantains.
After preparing the dish, Wowa did not eat any and left quickly after Swabura finished consuming it. When Muhammed arrived back at the house shortly after his sister left, Swabura was complaining about an extreme stomach pain. The report states that Swabura told her husband that the pain started almost immediately after she ate the meal that Wowa cooked for her.
As Swabura's condition worsened, her face grew pale, she began to vomit and her nose began bleeding uncontrollably.
While Muhammad frantically tried to find a rental car in order to drive his wife to the hospital, Swabura died inside the home. Since he was financially unable to pursue legal action for the loss of his wife, Muhammad buried Swabura the very next day.
The source who spoke with Morning Star News said they believe that Wowa was encouraged and possibly paid by other Muslims to carry out the murder of her convert sister-in-law, which she knew would leave 11 children without a mother.
"We suspect that Muhammad's sister, Jafaran Wowa, was given a lot of money to carry out the heinous act," the area source said. "This was a deadly drug, like rat poison or Bromethalin."
Swabura and Muhammad have received numerous death threats since their conversion from Islam to Christianity last November, which is considered by some hardline Muslims to be apostasy and a crime punishable by death.
"We are fearing for our lives as the Muslims are threatening to kill us if we continue in Christianity," Muhammad told Morning Star News in an interview in May.
The couple's pastor, James Kalaja, who pastors the New Hope Church in Nabuli, has also received threats for his leadership role in the church, which has forced him to move his family to another village that he feels is a less dangerous environment for them. Kalaja asserted that Christians are not safe in Nabuli.
"I only go to conduct service," Kalaja told Morning Star News. "Christians are facing threats here and the Muslims would not like to see a church in Nabuli village. It is sad that we have just lost our sister. The Christians are shaken by her death. We have been praying for Muhammad due to several threatening messages that he has been receiving through his phone."

Source: Christian Post 

JE, YUKO WAPI MUNGU BABA KWENYE AGANO LA KALE?

Image may contain: sky, cloud, text and outdoor
Ukweli unaoshangaza ni kwamba watu walioishi ziku za Agano la Kale walikuwa na uelewa mdogo sana juu ya Mungu Baba. Bali yeye alikuwepo na kwa kweli ametajwa mara-kadhaa.
Moja ya sababu zilizomfanya Kristo aje duniani kama mwanadamu ilikuwa ni kumdhihirisha Baba (Yohana 1:18; 5:37; 8:19; 14:7; Luka 10:22). Asingeweza kumdhihirisha iwapo kama Mungu wa Agano la kale ambaye ndiye Waisraeli walimjua, alikuwa ni Baba.
Tena basi kisababisho cha kwanza cha kuwepo kwa Mtu ambaye hatimaye alikuwa ndiye Baba kinapatikana kwenye sura ya kwanza kabisa ya ya Biblia. “Mungu akasema, Na tumfanye [sio mimi] mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;....” (Mwanzo 1:26). Hii haiashirii “uwingi wa mwenyezi” kama wasomi na wanazuoni wengine wanavyofikiri).
Kwenye aya ya 2 tumepewa jina linguine la “Bwana [YHVH] Mungu”” kama mshiriki mlengwa wa matendo na maneno wa hii “sisi.” Kumbe huyu –Wamilele (ambayo naiyo maana ya neno YHVH)—ndye kila mara ndiye anayeshughulika na wanadamu kama ujumbe wa Biblia unavyosema. Kwenye Mwanzo 14:18, tunamkuta Mtu huyu akiwa kama “mfalme wa amani na haki” (Melkizedeki kwenye Waebrania), “mfalme wa Salemu” (amani). Thibitisho? Usemi unaotumika hapa ni wa kumuelezea Melkizedeki huyu “kumeshuhudiwa kuwa anaishi”—kuwa ni wamilele (Waebrania 7:8). Kwa uthibitisho zaidi wa mwonekano huu wa Melkizedeki, msomaji anakaribishwa kuagizia jarida letu linalotolewa bure linaloitwa “Usiri kuhu Melkizedeki Umetatuliwa”.
Jambo la kuliangalia hata hivyo ni kwamba, Melkizedeki, YHVH, ndiye ambaye hatimaye alikuwa ni Yesu Kristo, aliyefanyika kuwa Mungu Mwana, ambaye kwa wakati ule alikuwa ni Kuhani (linganisha na Waebrania 7:1 na aya nyingine zinazofuatia na Waebrania 8:1), wa “Mungu Aliye Juu Sana”.(Mwanzo 14:18-22). Sasa, ni nani huyu basi aliyejulikana kama Mungu Aliye Juu Sana, mtu ambaye alikuwa ni kuhani? Basi Yesu mwenyewe na ajibu: “…Baba ni MKUU kuliko mimi. (Yohana 14:28).
Ni kweli,
Lakini hebu na tupate uhakika. Je, alikuwa ni Yesu Kristo gani mwana wa “na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;” malaika alimwambia Mariamu kabla hata Yesu mimba yake haijatungwa kwamba “kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu … Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu,” (Luka 1:35,32).
Luka 8:28 na Marko 5:7 zinathibitisha kuwa Yesu ni “Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana” na Mwana wa Mungu Aishie Juu Sana”. Baba ametajwa mara mbili zaidi kwa jina hili kwenye Agano Jipya—Matendo 7:48 na 16:17.
Ni nani basi Yesu anayetuambia tumuombe dua zetu? Ni Baba (Mathayo 6:9). Na ni nani ambaye Daudi alikuwa anamuomba? “Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.” (Zaburi 57:2). Na tena “Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu” (Zaburi 7:17).
Ndiyo, inawezekana kuwa kwa hakika Daudi alimjua Yule ambaye hatimaye atakuwa Baba (kumbuka, asingeweza kumuitwa Baba na huku akiwa bado hajawahi kuwa na Mwana. Melkizedeki, YHVH alikuwa hajawa Mwana bado). “Neno la Bwana [YHVH] kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako” Zaburi 110:1; Waebrania 1:13
Daudi aliimba, “Bwana alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake” (IISamweli 22:14).
Je, Musa pia alilijua hilo? “Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu…” Kumbukumbu la Torati 32:8).
Nebukadneza mpagani kwa hakika asingeona ni vigumu kuwaamini washiriki wawili walio mbalimbali lakini pamoja kwenye familia ya Mungu. Wababelonia waliabudu miungu mingi sana ya uwongo. Baada ya Nebukadneza kusababisha watu watatu wafungwe na watupwe kwenye tanuru la moto, hatimaye alichungulia ndani na kuwaona “Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.” (Danieli 3:25-26).
Nabii Danieli aliona kinabii kurudi kwa ufufuo na kupaa mbinguni kwa Kristo na kwenda mbinguni kwa Baba ili akaupokee Ufalme (pia soma Luka 19:11,12,15): “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa” (Danieli 7:13-14). Huyu “Mzee wa Siku” anayetajwa hapa anamaanisha ni Baba ingawaje kwenye aya ya 9 inaonyesha kuwa Mwana anaweza pia kuitwa “Mzee wa Siku” sawa tu na anavyoweza kuitwa Wamilele [YHVH].
Huenda hata manabii wanaweza kuwa na fununu kidogo zinazoonyesha kuwa Mungu alijulikana kama familia: “Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?” (Mithali 30:4).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

JE, YESU NI MUNGU?

Image may contain: cloud, sky, text, nature and outdoor


Na je, Yesu ndiye Yahova Baba wa Milele? Je, kuna Mungu mwingine zaidi ya huyu Mmoja? Tafadhali Nifafanulie.”
Maswali haya ili kuyajibu kwa kina yanahitaji makala iandikwe ukurasa mzima. Na makala kama hiyo itayaonekana ikiendelezwa kwenye nakala zijazo za Kwanini Yesu ni Mungu http://www.maxshimbaministries.com/…/je-bwana-yesu-anapataj… . Jibu litakalotolewa kwenye kipande hiki cha makala litakuwa ni fupi na litakosa maelezo ya kina kufafanua.
Ndiyo, Yesu ni Mungu, vinginevyo asingeweza kuwa Mwokozi wa wanadamu.1). Iwapo kama Yesu angekuwa ni mwanadamu tu basi kifo chake kingekuwa cha kutoa dhabihu ya kulipa deni la adhabu ya kumfanya mwanadamu mmoja aliyeichukua adhabu ya kosa kwa kuvunja au kuiasi Torati ya kiroho ya Mungu. Kwa kuwa ni Mungu Baba ndiye aliyeumba vitu vyote kupitia kwa Yesu Kristo.
(Waefeso 3:9) na kwa kuwa vimhusivyo mwanadamu vilifanywa na Yesu Kristo (Yohana 1:1-5 pamoja na aya ya 14; na aya ya 10; 1Wakorintho 8:6; Wakolosai 1:12-19). Yeye ndiye Muumbaji na kwa hiyo ni Mungu, na maisha yake aliyoyatoa yana thamani kubwa kuliko kiasi chochote cha mlinganisho wa ya wanadamu wote.
(2). Maisha pekeyake yanaweza kuanzisha maisha mengine. Hii ndiyo kanuni ya ki-Biokemia kwa kuwa Uzima wa Milele ni ZAWADI kutoka kwa Mungu, basi ni Mungu tu mwenye kuwa na uweza wa kutokufa ndiye anayeweza kuutoa uzima huu. Na kama Yesu angekuwa ni mwanadamu tu, basi tusingeweza kuupata uzima wa milele kupitia kwake na asingeweza kuwa Mwokozi. Wanadamu hawezi kuwa na uzima wa milele ndani yake mwenyewe, lakini kama Mungu alivyo kuwa “Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake” (Yohana 5:26 na 1Yohana 5:11-12).
Kwa upande mwingine lakini, Yesu ni mwanadamu pia. Kwa kuwa ni mwanadamu ndiye aliyeziasi Sheria za Mungu ambaye yuhai wakati wote ((Yohana 1:1-2) ndipo kwa kweli alifanyika kuwa mwanadamu katika mwili (aya ya 14). Yeye aliyekuwa Mungu hakika akafanyika kuwa mwanadamu mwenye mwili (1Yohana 4:2-3). Alitungwa mimba na kuzaliwa na bikira Mariamu (Mathayo 1:18, 16, 23; na 2:2). Hakufanyika kuwa mwili tu, bali alifanyika pia kuwa mwanadamu kimwili na damu. (Waebrania 2:14).
Yesu aliijiita mara kwa mara kuwa ni Mwana wa ADAMU, na pia Mwana wa MUNGU, (Mathayo 16:13-17). Yuko SAWA na Mungu (Wakolosai 2:6). Aliitwa Mungu (Yuda 1:24-25; Tito 2:10,13). Kwa hiyo yeye ni Mungu. Biblia ina nukuu nyingi kuhusu jambo hili na zilizo hapo juu ni chache tu kati ya nyingine nyingi zinazoshuhudia.
Ndiyo, Yesu ni “Yehova” ingawaje neno hili limetafsiriwa vibaya kwenye Biblia ya Kiingereza ya Reversed Version. Jina asilia la Kiebrania lina consonanti “YHVH”. Lilipoandikwa kwa Kiebrania, vokali ziliachwa na zilisikika kwenye matamshi tu. Kwa hiyo, jina hasa lilikuwa halijulikani. Bali kwa leo inadhaniwa kuwa lilikuwa ni “Yahwe”. Maana yake kwa Kiingereza ni “WAMILELE” au “MWENYE KUISHI MILELE” au “ANAYE KUISHI NA KUDUMU KWA UWEZA WAKE MWENYEWE PASI KUTEGEMEZWA”. Ilistahili kuwa “Yahwe”, au ni kama ilivyozoeleka kuitwa “Yehova”, au ni kama ilivyoandikwa kwenye Biblia ya Authorised Version “BWANA” wa Agano la Kale ni Mungu Baba wa Yesu Kristo. Haya ni makosa makubwa sana! “Yahwe alikuwa ni Mungu wa Israeli. Na ndiye aliyekuwa anajulikana kuwa ni Mungu pekee kwenye ibada za Israeli. Wao hawakumjua Mungu Baba.
Kwenye Mwanzo 1 jina la Kiebrania lililotumika kutafsiri jina “Mungu” ni “Elohim”. Hili ni jina lenye umoja wenye muunganiko na wengi ndani yake kama tunavyotaja “kanisa” au “familia”. Kanisa na familia vinajumuisha watu wengi ndani yake, zaidi ya mmoja, lakini bado linaitwa kanisa au familia moja. Kwa mtazamo wa aina hii jina “Elohima” linaashiria wote wawili, Mungu Baba na Yahwe ambaye ni “Logos” au NENO la Mungu ambaye kwao Roho anatokea, Roho Mtakatifu ambaye ni UZIMA, KITU HALISI na UWEZA wa Mungu.
Yesu analipokuwa akiliombea Kanisa alisema kwamba waumini wake wote wawe “kitu KIMOJA” (Yohana 17:11, 21). Kanisa ni Mwili MMOJA, lakini limeundwa kwa waumini wengi (1Wakorintho 12:12). Na mume na mke ni MWILI MMOJA, lakini wanaonekana kuwa ni watu wawili walio mbalimbali. Kwa hiyo Kristo na Mungu Baba ni Mungu MMOJA, na sio Miungu miwili, na—“ELOHIM” Mmoja. Na ndio maana Elohim alisema “NA tumfanye mtu kwa mfano WETU” (Mwanzo 1:26).
Yahwe alikuwa ndiye “NENO” au msemaji wa ofisi ya Uungu—mshiriki wa pili. Mara tu baada ya Mungu kuanza KUONGEA na wanadamu, ilikuwa ni yuhu “Yahwe” ndiye aliyekuwa akiongea nao (imetafsiriwa “BWANA” kwenye tafsiri ya Authorised na “Yehova” kwenye tafsiri ya Revised Version). Tazama kwenye Mwanzo 2:16, 18, nk, na pia tazama kwenye Kutoka 20:2, nk—kila mara inasema “Yahwe” kwenye tafsiri asilia ya Kiebrania “NENO” aliyefanyika mwili. Ili kuthibitisha hili kunahitaji masomo ya kina na yatakayogharimu kurasa nyingi kwa mamia ili kuthibitisha hili.
Ili kuthibitisha kiufupi, fananisha na Isaya 6:1-3 na 10 na Yohana 12:39-41; Isaya 8:13 na 1Petro 2:7-8; Isaya 40:3 na Mathayo 3:3 na Marko 1:3. Yohana alitengeneza njia kwa ajili ya “Yahwe” (Isaya 40:3) ambaye ndiye Kristo (Marko 1:12-15) kwenye Ufunuo 1:17, 8 na 22:13, Yesu Kristo (pia tazama Ufunuo 22:16 kwa uthibitisho kuwa alikuwa ni Yesu aliyekuwa anasema) alijiita kuwa yeye ni “Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa Kwanza na wa MWisho”. Kwenye aya zilizo kwenye Isaya 44:6 na 48:11-12, (aya za 17-18 zinaonyesha kuwa ni Yahwe aliyekuwa akinena) na Isaya 41:4, YAHWE ni wa Kwanza na wa Mwisho Kwenye 1Wakorintho 10:1-4 “MWAMBA” wa Agano la Kale ulikuwa ni Kristo. Kwenye Kumbukumbu la Torati 32:3-4; IISamweli 22:2-3, 32; na Zaburi 18:1-2; “MWAMBA” huu huu ni Yahwe. Wakati Musa alipokuwa anaongea na YAHWE, na kumuuliza jina lake, (Kutoka 3:4-5, 13), alimjibu kuwa jina lake ni MIMI NIKO (aya ya 6 na 14) na YAHWE (aya ya 15). Pia tazama Kutoka6:2-3. Kwenye Yohana 18:5-8, mara tu baada ya Yesu kujitambulisha kwa makutano walioongozwa na Yuda kuwa yeye ni “MIMI NIKO” (kiponauni cha “yeye” kwenye uandishi mlalo kimeongezwa pasipo uvuvio, na hakikuwepo kwenye nakala asilia za mwanzoni), ndipo walirudi nyuma na kuanguka chini. Tena kwenye Yohana 8:56-58, Yesu aliijiita mwenyewe “MIMI NIKO”. Pia kwenye Ufunuo 1:10 na mahali pengine.
Mtu mwenye Uungu ambaye ndiye MKOMBOZI wetu ni Yesu Kristo (Yohana 4:42, Wagalatia 3:13, Wafilipi 3:20, Tito 2:10-14, Luka 1:58-59, nk, nk. Yesu Yule ndiye YAHWE, tazama kwenye Isaya 49:7; Isya 60:16; ambapo panasema pia kuwa yeye “Mwenyezi wa Yakobo”—(kwa hiyo, kuwa ni WA Yakobo kunamaanisha mwana, au uzao wa Yakobo)—Mwenyeenzi wa wana wa Yakobo. Pia kwenye Isaya 48:17 inasema YAHWE ndiye Mkombozi, na Mtakatifu wa Israeli—Ndiye aliye Mtakatifu wa Israeli! Ni sawa na ilivyoelezewa kwenye Isaya 43:14. Kumbuka pia aya inayofuatia (15), YAHWE ni Mtakatifu wa Israeli, Muumbaji wa Israeli, Mfalme wa Israeli. Sasa tega usikivu wako kwenye Matendo 3:14 ambako ni Kristo waliomkataa Wayahudi alikuwa ni huyuhuyu “MTAKATIFU—YAHWE! Pia tazama Matendo 2:27 na Marko 1:24.
Je, Daudi mchungaji alikiwa ni nani?—Zaburi 23:1, YAHWE. Kwenye Yohana 10:11, Yesu alisema kuwa yeye alikuwa ni mchungaji. Pia Waebrania 13:20, na 1Petro 2:24-25, na 5:2-4. Ni YESU KRISTO anayekuja tena Kimwili na akiwa Mfalme wa Wafalme kutawala, kuja KUYAFANYA MAMBO YOTE UPYA, (Ufunuo 19:13, 15; 17; 14; 1:5; na Matendo 3:20-21). Mchungaji Mkuu anayekuja KUTAWALA akiwa kama MFALME wa Mfalme wote ni YAHWE—Ezekieli 34:11, 30-31; na sasa weka mtazamo wako kwenye Isaya 2:1-4 na Mika 4:1-4— Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana [YAHWE] utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu ‘YAHWE] wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

Friday, February 8, 2019

ASIYE NA DHAMBI AWE WA KWANZA KUTUPA JIWE

Image may contain: 1 person, text


Tuanze na kujifunza maana ya "Dhambi". Dhambi ni nini?

Dhambi ni tendo, hisia, au wazo lolote linalopingana na viwango vya Mungu. Inatia ndani kuvunja sheria za Mungu kwa kutenda mabaya, au ukosefu wa uadilifu, kwa maoni ya Mungu. (1 Yohana 3:4; 5:​17) Biblia pia inaeleza kuhusu dhambi ya kutofanya lililo sawa ingawa mtu anajua alipaswa kulifanya.​—Yakobo 4:​17.

Katika lugha za awali za Biblia, neno dhambi linamaanisha, “kukosa shabaha.” Kwa mfano, askari fulani katika Israeli la kale walikuwa na ustadi wa kutupa mawe kwa kombeo “bila kukosea.” Maneno hayo yanapotafsiriwa kihalisi yanamaanisha “bila kufanya dhambi.” (Waamuzi 20:16) Hivyo, kufanya dhambi ni kukosa shabaha ya viwango vikamilifu vya Mungu.

Kwa kuwa Mungu ndiye Muumba, ana haki ya kuwawekea wanadamu viwango. (Ufunuo 4:​11) Tunawajibika kwake kwa matendo yetu.​—Waroma 14:12.

Sasa tusome aya kutoka Biblia Takatifu Injili kutokana na Yohana Mlaongowa 8 aya ya 2 mpaka 11:

“2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha. 3 na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.”] (Yohana 8:2-11)

KWANINI MAFARISAYO WALIMLETEA HII KESI YESU KRISTO?

Kisa hiki ni maarufu sana katika Biblia. Hii ilikuwa ni mojawapo ya kesi ngumu iliyowasilishwa kwa Yesu ili kumjaribu wamwone atasemaje. Maandiko yanasema waziwazi ya kwamba nia ya washtaki wa mwanamke mzinzi kwenye kesi hii haikuwa nia njema ya kuzuia uvunjwaji wa sheria; bali waliitumia kesi hiyo kama kisingizio cha kumjaribu Yesu huku wakimtafutia “sababu ya kumshtaki Yesu”.

Yesu hali akijua hila zao, alinyamaza kimyaaaa. Tunasoma maandiko yakisema “nao walipozidi kumhoji”, yaani waliendelea kumshinikiza wakitaka atoe majibu kama anakubali sheria ichukue mkondo wake dhidi ya mwanamke mzinzi, au anapingana na sheria halali, ili wapate “sababu ya kumshtaki”. Mwishowe Yesu akatoa tamko lake akisema: “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe” kisha aliinama chini akaanza kuandika chini kwa kidole chake. Sasa hapa ndipo palipo na ujumbe kuhusu mada hii. Kwanini Yesu alisema yeye asiye na dhambi miongoni mwao awe wa kwanza kumtupia jiwe? Pili, alipoinama akaanza kuandika chini aliandika nini?

YESU ANAJUA YALIO NDANI YETU.

Kujibu swali la kwanza ni kwamba, Yesu kusema asiye na dhambi miongoni mwenu hakuwa na maana kwamba alikuwa anatafuta mtu asiye na dhambi kabisa miongoni mwao. Lugha asilia inasema Yesu aliwahoji kama kweli yupo mmoja kati yao ambaye “hajafanya dhambi yoyote iliyostahili hukumu ya kifo kama ya mwanamke mzinzi”. Yaani hakutaka wengi wasio na dhambi iliyostahili hukumu ya kifo, bali alitaka angalau hata mmoja tu kati yao asiyekuwa na dhambi inayostahili hukumu ya kifo!

Haya swali la pili, la alipoinama chini aliandika nini? Hakuna ushahidi wa kimaandiko ya kwamba aliandika nini chini. Lakini baadhi ya wataalamu wa tafsiri za maandiko ya kale wanasema alikuwa akiandika orodha ya dhambi zilizostahili hukumu ya kifo ambapo kila mmoja alisoma dhambi yake na kuamua kuondoka bila kuaga kuanzia mzee mpaka mtu wa mwisho.

ORODHA YA DHAMBI ZILIZOSTAHILI HUKUMU YA KIFO

Kimsingi, ni kweli ya kwamba katika Agano la Kale, ambalo lilikuwa na katiba (torati) iliyozingatia utawala wa sheria, lilidhibiti uhalifu na makosa ya jinai kwa adhabu kali kuanzia kupigwa viboko mpaka hukumu ya kifo cha kupigwa mawe.

Zilikuwepo zaidi ya sheria kumi na nne ambazo makosa yake yalistahili hukumu ya adhabu ya kifo. Baadhi yake ni kama hizi zifuatazo: Dhambi ya kuua kwa kukusudia ( Kutoka 21:12-14; Mambo ya Walawi 24:17,21), dhambi ya kushambulia au kulaani mzazi (Kutoka 21:15,17), Kutokutii wazazi (Kumbukumbu la Torati 21:18-21); biashara ya binadamu(Kutoka 21:16), mifugo ya wanyama ikishambulia na kuua watu na mwenye mifugo asizuie maafa hayo (Kutoka 21:28-29); dhambi ya uchawi (Kutoka 22:18; Mambo ya Walawi 20:27), Kutoa kafara binadamu (Mambo ya Walawi 20:2-5); Kufanya ngono na mnyama (Kutoka 22:19, Mambo ya Walawi 20:16), kufanya kazi siku ya Sabato (Kutoka 31:14; 35:2; Hesabu 15:32-36); Kuzini (Mambo ya Walawi 20:10; Kumbukumbu la Torati 22:22), ushoga na ulawiti (Mambo ya Walawi 20:13), Binti ya kuhani akifanya ukahaba (Law.21:9); Dhambi ya kukufuru (Mambo ya Walawi 24:14,16,23), dhambi ya kumwasi kuhani (Kumbukumbu la Torati 17:12).

WOTE SISI NI WATENDA DHAMBI

Haya tukirejea kwenye hoja ya msingi ya jibu la Yesu kwa waandishi na mafarisayo akiwataka kama yuko hata mmoja asiyekuwa na dhambi iliyostahili hukumu ya kifo sawa na ile waliyokuwa wakimshtakia yule mwanamke mzinzi; na wote wakaondoka bila kuaga, hiyo ikathibitisha waziwazi ya kwamba, hapakuwepo hata mmoja ambaye alistahili kumhukumu yule mwanamke mzinzi.

Kumbe wote walikuwa wamefanya dhambi mbali mbali zilizostahili nao wapigwe mawe kama yule mwanamke mzinzi. Inawezekana kweli hapakuwepo mzinzi kama yule mwanamke, lakini walikuwa na dhambi nyingine zinazostahili hukumu yenye uzito ule ule sawa na mwanamke mzinzi!

Biblia ndicho kitabu pekee chenye kuhukumu kwa haki bila upendeleo wala ubaguzi. Neno la Mungu katika Biblia halina unafiki wala hila ndani yake. Tunapolisoma na lenyewe linnatusoma na kutuhukumu dhamiri zetu hata kama tutajifanya hatuna hatia kwa nje. Biblia imeandika waziwazi ya kwamba: “Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;..” (Rum.3:23); na kisha imeandikwa ya kwamba: “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti;..” (Warumi 6:23)

KUKUBALI KOSA KABLA YA KUSAMEHEWA.

Mwanamke aliyefumaniwa uzinzi,alijikubali kwamba amefanya kosa,ndio maana tunaona hakujibu chochote cha kujitetea mbele za Yesu. Sababu kama asingekubali kosa lake angeliweza kujitetea,lakini alikaa kimya hata akasamehewa.

Mara nyingi sisi tunajihesabia haki penye makosa.

Yeye mwenye kujihesabia haki hali ni mdhambi,hawezi kupokea msamaha wa kweli. Kwa sababu kanuni ya kusamehewa ni lazima mmoja akubali makosa yake ndipo msamaha uachiliwe na msamaha wa namna hii uwa na nguvu sana.

YESU KRISTO ANAYO AMRI DUNIANI YA KUSAMEHE DHAMBI.

Imeandikwa;

“ Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako. “Luka 5:24

Hakuna mwanadamu anayepaswa kumuhukumu mwanadamu mwenzake kwa sababu ya dhambi aliyotenda sababu mwenye kuhukumu ni Mungu mwenyewe.

KAMA HAKUNA ALIYEKUHUMU HATA MIMI SIKUHUKUMU

Sasa tumefika kwenye kiini cha ujumbe wa leo. Baada ya washtaki wote kukimbia na mwanamke mzinzi kuachwa peke yake, ndipo Yesu alipomwuliza kama hakuna hata mmoja aliyejitokeza kumhukumu kuwa na hatia, na mwanamke akasema hakuna. Yesu akamwambia, “Wala mimi sikuhukumu”!

Kumbuka ya kwamba, kwa viwango vya kimaadili, ni Yesu peke yake ambaye hakuwa na dhambi hata moja. Kwa hiyo, kibinadamu Yesu ndiye aliyestahili kumhukumu huyu mwanamke mzinzi. Lakini pasipo kutarajia mwanamke mzinzi alishangazwa na kauli ya Yesu pale alipotamkiwa “uhuru wa kuishi” tena. “Wala mimi sikuhukumu”

Swali ni kwanini Yesu hakumhukumu mwanamke mzinzi wakati Yesu alisema alikuja kuitimiliza torati? Hivi kumwachia huru sio kuendeleza uzinzi badala ya kuudhibiti? Majibu ya maswali haya yapo ndani ya tafsiri ya jina la Yesu mwenyewe ambalo ndilo lilibeba utume wa kuja kwake duniani:

“Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.” (Yohana 3:17)

Bila shaka hapa unaweza kubaini ya kwamba, Yesu kutokumhukumu mwanamke mzinzi alikuwa akitekeleza utume aliotumwa na Baba yake. Kuokoa na sio kuhukumu! Kuokoa na sio kuhukumu! Hili lilitabiriwa na malaika Gabrieli kuhusu kazi ya jina la Yesu kama tusomavyo:

“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.” ( Mathayo 1:21)

ENENDA ZAKO USITENDE DHAMBI TENA

Kwa hiyo, maana ya “kutokuhumu” sio “kubariki maovu” yaendelee kushamiri pasipo udhibiti. “Kutokuhukumu” kwa mujibu wa Yesu maana yake ni kumpa nafasi nyingine (second chance) mwenye dhambi aweze kujirekebisha kitabia baada ya kufutiwa makosa yake bure na Yesu Kristo. Na ndivyo Yesu alivyofanya kwa yule mwanamke mzinzi: “Enenda zako; wala usitende dhambi tena.”

Kauli ya “usitende dhambi tena” ni kiashiria cha kufutiwa dhambi zilizokwisha kufanywa nyuma, na kwamba inawezekana kuishi pasipo kutenda dhambi tena baada ya kukutana na Yesu ana kwa ana kama mwanamke yule mzinzi!

Mpendwa msomaji wangu. Kabla hutujatoa hukumu dhidi ya wakosaji wengine miongoni mwetu, hebu tujihoji kwanza kama sisi wenyewe pia tuna hatia katika maisha yetu ya faragha. Ukijikuta nawe una hatia katika eneo lolote hata kama watu wengine hawajui ukweli wa dhambi zako za siri, basi uzuie ulimi wako kutoa hukumu dhidi ya dhambi za wengine.

Hii haina maana mtu akikosea asiambiwe ukweli wa makosa yake kwa nia ya kumshawishi ajirekebishe. Kinachokatazwa ni kumtakia hukumu ya adhabu ambayo ikikugeukia wewe hutaifurahia. Jifunze kusamehe bila masharti. Lakini kama dhamiri yako inakuhukumu kwa dhambi zako, ufumbuzi wake ni kumkaribisha Yesu Kristo katika maisha yako na kumwomba akujaze Roho Mtakatifu atakayekusaidia kuishi maisha mapya ya utakaso wa kweli.

Kama ujumbe huu umekugusa nijulishe kwa ku-like post hii, wajulishe marafiki zako kuhusu page hii pia. Mungu akulinde na kukubariki kwa wingi wa fadhili zake katika jina la Yesu, AMINA!!

Shalom

Thursday, February 7, 2019

MUNGU, MWANDISHI WA BIBLIA

No photo description available.


“kila andiko limeandikwa kwa upako wa Mungu”

Kama mtu anaweza kuangalia ukubwa wa mbingu ama ulimwegu atashangazwa na ubunifu na muundo msingi wa uumbaji. Kila upande wa jinsi dunia ilivyoumbwa ni ushahidi kimya kuwa yupo Muumbaji. Mbali na kitabu tunachojua kama Biblia, Binadamu atazidi kubaki mjinga na ashindwe kuelewa asili na hatima ya dunia. Biblia ndio ufunio wa Mungu kwa binadamu. Inaonyesha ukweli dhahiri kuhusu Mungu na binadamu. Inaonyesha kusudi kuu la uumbaji, asili ya dhambi na kifo, kuendelea na hatima ya mataifa na kisha ufalme wa Mungu unaokuja. Lakini Biblia pia ina dhamani ya kibinafsi. Na huwapa vijana na wazee matumaini. Inatuonyesha sababu halisi ya kuishi na pia kufunua ujinga ufuatao wa dunia ambayo imejitenga na Mungu na Uumbaji wake. Kwa kifupi,biblia inaweza kubadilisha maisha yetu.

Lengo la hili somo ni kuonyesha kwamba kuna Muumbaji mmoja mkuu ambaye aliongoza kuandikwa kwa Biblia ili kuonyesha tabia zake na kusudio lake kwa mwanadamu.


2 Timotheo 3:14-17; 2 Pet 1: 19-21

BIBLIA: UFUNUO WA MUNGU KWA BINADAMU

Ijapokuwa Biblia imegawanywa katika sehemu sitini na sita ina ujumbe mmoja dhabiti. Inadai kuwa Neno la Mungu. Kwa vitabu vitano vya kwanza imetajwa mara zaidi ya mia tano “Bwana akasema” au “Bwana akanena” tena kwa mara 300 inarudia maneno hayo kutoka kwa kitabu cha Yoshua hadi Wimbo wa Solomon. Vitabu za manabii zinarudia maneno hayo kwa mara 1200.

Waandishi wa Biblia walikua wanatimiza jukumu kama waalimu wa sheria wa Mungu aliyekua mwandishi Mkuu. Alionyesha mafunzo yake kupitia kwa wanadamu. Waliandika kutokana na upako wake (Hebrania:1:1-2; Nehemia 9:20) Aliwaelekeza jinsi watakavyosema ijapokua lugha waliotumia ilikua yao. Kwa kusudi hili Mungu aliwachagua wanaume kutoka kila tabaka la jamii. Wafalme, viongozi, makuhani, wasomi, wachungaji na pia wavuvi walikua kati ya waliochaguliwa. Aliwagawanya kulingana na hadhi, watkat na mahali walikotoka. Mwandishi mmoja akiwa Syria wa pili alikua Uarabuni, wa tatu Italia, wa nne Ugiriki, wa tano Babelli na wasita palestina. Hii inaaanisha walikumua na masasiliano machache sana. Musa ndiye aliyekua mwandishi wa kwanza na aliandika vitabu vitano nya kwanza vya BIblia miaka 1600 kable ya Yohana kuandika kumbukumbu ya ufunuo.

Licha ya tofauti hizi kubwa kuna uwiiano wa ajabu kwa yale yalionadikwa yanavyounganisha vitabu hivi vyote 66 na kuwa moja ili kufanya Biblia kitabu cha kipekee katika ulimwengu wa fasihi. Mungu amempa mwanadamu kitabu hiki ili kumpa matumaini (Warumi 15.4) Biblia pekee ndio inaweza onyesha njia ya wokovu (2Timotheo 3:15). Kukataa ujumbe huu ni kumaanisha kifo. (Kumbukumbu la Torati 30:17-20, Mithali 14:12.)

Kwa kawaida Biblia imegawanya katika sehemu mbili; Agano la kale (vitabu 39) na Agano jipya (vitabu 27). Mgao huu umefanywa na mwanadamu kwa sababu Biblia inastahili kuchukuliwa kama kitabu kimoja cha ufunuo wa Mungu kwa binadamu. Agano la kale lilikua limeandikwa kwa kiebrania na Agano jipya na Kigiriki. Mfumo wa kuandika Biblia na Kiingereza ulioidhinishwa na hutumika leo ulichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1611. Pia ilitafsiriwa na Kiswahili kama Biblia Muungano. Ilijulikana kama mfumo ulioidhinishwa kwa sababu mamlaka ya kutasfri kwa kizungu ilipewa Mfalme James wa Uingereza. Kutoka wakati huo tafsiri nyingi zimetolewa zingine zina manufaa na zingine zina manufaa kidogo sana. Nakala rasmi haina makosa lakini hakuna toleo lisilo na makosa. Kwa miaka iliyopita kumekua na makosa ya kutafsiri kwa waandishi kuiga nakala rasmi na kutafsiri kutoka kwa lugha asili kwa lugha nyingine. Lakini makosa haya ni kidoga na hayana umuhimu mkubwa kwa sababu kila toleo lina mafunzo muhimu ya Biblia yanayoeleweka.

BIBLIA: UPAKO NA UKWELI

Petro aliweka kanuni za msingi kwamba Biblia imechaguliwa (2 Petro 1:20-21). Alitangaza kwamba “ hakuna nabii wa andiko alikuwa na tafsiri ya kibinafsi; kwa sababu unabii wa kale haukuletwa na mapenzi ya binadamu bali ni wanaume watakatifu walioteuliwa na Mungu kuongeo kama wananvyoongozwa na Roho Mtakatifu.

Kwa hivyo ukweli unaweza patikana kwenya Biblia na hakuna yeyote anaweza kuonyesha uwongo kwenye matokeo ya kihistoria. Wanaopiga Biblia wamelazimika kukubali kwamba kuna ukweli ndani yake. Mashahidi wa manabii wanaonyesha kwamba kuna ukweli dhahiri kwamba Mungu ndiye Mwandishi kwani yeye pekee ndiye anaweza kutabiri siku zijazo. Utabiri wa kushangaza katika Biblia umetimia jinsi ulivyo tabiriwa. Mfano:

Ukuta wa Babelli bado ni vifusi (Isaya 13:19-21, Yeremia 51:37).
Ninevehe bado ni tupu na imejaa taka ((Nahumu 2:10).
Misri ni moja kati ya mataifa duni (Ezekiel 29:15).
Tiro iliyokua bandari imemezwa na bahari (Ezekiel 26:5).
Taifa la Israel limesambaa katika mataifa yote (Kumbukumbu la Torati 28:64) na sasa wanakusanywa tena Yeremia 30:11; Ezekiel 37:21-22)
Nguvu za Kaskazini zina uadui na taifa la Israel kama Urusi iliyoendelea.

MUNGU KATIKA BIBLIA

Biblia inaaza kwa kuongelelea mtu mmoja ambaye ni Mungu (Mwanzo 1:1). Na ufunuo unamalizia kwa kuonyesha jinsi Mtu huyu mmoja atakavyo wekwa wazi kwa viumba vyote. “Mungu awe yote katika wote” (1 Wakorintho 15:28). Inatuonyesha jinsi kila mmoja wetu anaweza kushiriki katika kukamilisha utukufu wa Mungu. Injili inatuita kila mmoja wetu tujitenge kutokana na wanaume na wanawake ambao wanajitengenezea njia ya kuelekea kuzimu milele. Mungu anachukua watu wake kutoka kwa Gentiles (Matendo. 15).

Jambo la kwanza muhimu ni kuelewa kwa usahihi Mungu ni nani (Yohana 17:3; Waebrania 11:6) lazima tukubali umoja wa Mungu.

TABIA ZA MUNGU

Kuna pande mbili katika tabia za Mungu tunapaswa kufikiria. Paulo alisema “ fikirieni kuhusu wema na ukali wa Mungu (Warumi 11:22. Pande hizi mbili za tabia ya mungu zilidhihirishwa na Musa katika Mlima Sinai(Kumbukumbu la Torati 34:6-7) na zote zilidhihirika katika uhusiano wake na mwanadamu. Kwa mfano kipindi kile Mungu alimtuma Musa kuwokomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Aliwaokoa kutoka kwa bahari ya Shamu lalini aliangamiza majeshi ya Faraoh. Yesu Bwana anakuja kuhukumu dunia kwa haki. Hii inammanisha kutakuwa na huruma na ukombozi wa wateule wake na pia kifo na uharibifu kwa wale waovu.

Sababu ya haya ni uasi wa binadamu” hata neema ionyeshwe walio waovu hawatajifunza haki (Isaya 26:10-11) Mungu anafunza binadamu kwa wema wake na wokovu wa milele.

Biblia Inatufundisha kwamba Mungu ni asiyebadilika kwa lengo lake (Mal. 3:6) Yeye ni mwenya kujua yote (Zaburi 139:1-6) Yupo kila mahali (vv.7-12); na ni mwenya nguvu (vv. 13-18).

Ni ukweli kwamba Mungu anayajua yote (Waebrania 4:13; Jeremia 23:24) na anaweza kutelekeza mapenzi yake ili kutuonyesha jinsi tunavyostahili kuishi mbele zake. Hata hivyo yeye hutawala kwa maenzi na wala sio woga. Madhumuni ya ufunuo wake ni kubadili tabia zetu ili tupate kuendana na njia zake, na tuwe tunafaa kiakili na kimaadili ili tuweze kupewa uzima wa milele na Kristo anarudi tena ( Wafilipi 3:20-21.).

KUSUDI LA MUNGU

Kusudi kuu la Mungu imeelezwa kwa kimsingi katika Hesabu 14:21- kama kweli ninavyoishi dunian yote itajazaa utukufu wa Bwana.” Hii inamaanisha nini? Dunia nzima itangaa kwa nguvu an utukufu wa Mungu lakini utukufu wa Mungu ni zaidi ya haya. Inagusia tabia zake. Wakati Musa alimwomba Mungu amwonyeshe utukufu wake, Kwa kumjibu Mungu alimwonyesha tabia zake, mwenye huruma, neema na mwingi wa rehema na ukweli. Kutoka 33:18; 34:6-7)

Utukufu wa Mungu utadhihirika kwa wote humu duniani wakati wanaume na wanawake watakoa uonyesha katika maisha na tabia zao. Yesu alituonyesha maisha yake ya "utukufu wa Baba yake" kwa kuwa alikuwa "amejaa neema na kweli" (Yohana 1:14).

Mungu anawaita wanaume na wanawake kwa lengo hili kama tunaweza kuelewa madhumuni ya Mungu na kuonyesha tabia ya Mungu katika maisha yetu, wakati Kristo atakaporudi, tutapewa asili ya Mungu (1 Petro 1:04.), Na kuonyesha tabia za Mungu katika ukamilifu wa uzima wa milele.

Wacha tuangalie Masomo yetu ya Biblia ili tuweze kupata “hekima na hata kupata wokovu” na ili tustahili kuingia katika ufalme wa mbiguni wakati Yesu ataporudi.

MASOMO KWETU

Ni kwa kusoma Biblia tu ndio tunaweza kujua hatima ya mwisho ya dunia na mwanadamu Mungu anataka tujue Ukweli Kumhusu Kusoma Biblia kunaweza kubadili maisha yetu Jinsi gani kijana kubali njia zake na kutii na kulifuata neon lako? (Zaburi 119:9).

Msimkatae yeyote anayeongea (Ebrania 12:25)
Hakikisheni kila jambo huku mkizingatia yaliyo mema. (1 Wathesalonike 5:21.).

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

Wednesday, February 6, 2019

JE, MCHEZO WA “KU-BETI” NI DHAMBI?

Image may contain: 1 person, sitting and indoor
Na Pastor Zakayo Nzogere
JE, MCHEZO WA “KU-BETI” NI DHAMBI?
Kati ya mambo mapya na yenye mvuto usio wa kawaida kwa watu wa rika zote, ni mchezo wa KU-BETI. Kuna makampuni mengi ambayo yanasimamia mchezo wa KU-BETI kama vile BetWay, Bet365, BetOnline, SportPesa, na mengine mengi.
Swali kubwa ambalo WAPENDWA wengi wanajiuliza ni kama mchezo huu ni halali kwa Mkristo kuucheza?
Mimi sina majibu ya moja kwa moja, ila nitatoa mtazamo wangu binafsi kwa kutumia Maandiko. Pia ninaomba na wengine muwe huru kutoa MITAZAMO yenu CHANYA ili kwamba tuweze kuwa na UELEWA mpana wa jambo hili.
MASWALI YA MSINGI YA KUJIULIZA:
• Dhambi ni nini?
• Kuna tofauti gani kati ya ku-beti, kamari, na bahati nasibu?
• Je, Biblia inasemaje kuhusu michezo ya bahati nasibu? & Je, ku-beti kunawezaje kuathiri maisha ya Mkristo?
1. DHAMBI NI NINI?
Biblia inafafanua dhambi kama uasi au kutotii maagizo ya Mungu. Adamu na Hawa walifanya dhambi ya kutotii maagizo ya Mungu, matokeo yake ni kwamba mahusiano yao na Mungu yakaharibika. Dhambi ikawatenga mbali na uso wa Mungu na nguvu ya mauti ikaanza kutawala (Mwanzo 3).
DHAMBI ni kitu kinachomtenga mwanadamu na Mungu. Hata hivyo Mungu hakupenda kuwaacha wanadamu waangamie katika dhambi yao; akamtuma Yesu Kristo aje kutukomboa (Yohana 3:16). Dawa ya dhambi ni KUMWAMINI BWANA YESU KRISTO.
2. KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KUBETI, KAMARI, NA BAHATI NASIBU?
Kwa mtazamo wangu, michezo hii yote ni michezo ya kubashiri au kutabiri nani atakae shinda au shindwa katika jambo fulani. Kwa hapa Tanzania, mchezo wa Ku-beti na Bahati Nasibu ni michezo ambayo imepewa vibali vya Serikali na ni michezo halali nchini. Kwa upande mwingine, KAMARI, ambayo kimsingi haina tofauti na hiyo mingine, yenyewe ni haramu kucheza. Kwangu mimi hii ni sawa na kuruhusu KONYAGI/WISKI na kukataza GONGO!!
3. JE, BIBLIA INASEMAJE KUHUSU MCHEZO WA KU-BETI AU BAHATI NASIBU; NA JE, INAWEZAJE KUATHIRI WOKOVU?
Biblia siyo kama MANUAL BOOK/KITABU CHA MAELEZO chenye mchanganuo wa kila kitu kinachohusu maisha ya wanadamu. Hata hivyo, Biblia kama Neno la Mungu, imejaa KANUNI ZA MSINGI (Principles) zinazoweza kutupa majibu na misimamo kuhusu mambo mbali mbali katika maisha yetu.
MFANO; hakuna mahali kwenye Biblia ambapo inakataza kuvuta sigara au kutumia madawa ya kulevya. Lakini Biblia inatoa kanuni ambayo imepelekea Kanisa kupiga marufuku matumizi ya vitu hivyo (1 Wakorintho 3:16-17; 6:19-20). Maandiko yanatuonyesha kuwa MIILI YETU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU, pia Mungu atamhukumu yeye atakayeuharibu mwili wake.
Kwa upande mwingine WANASAYANSI wametuonyesha kwamba vileo na vitu kama bangi, madawa ya kulevya na sigara vina madhara makubwa sana kwa mwili wa mwanadamu. Hivyo basi KANISA linatumia KANUNI za Neno la Mungu kukataza matumizi ya vitu hivyo.
Vile vile Biblia inatupa kanuni nyingi zinazotuonya kuhusu kupenda pesa, tamaa, na kujilimbikizia mali kwa njia ambazo si halali.
JE, KU-BETI KUNAWEZA KUATHIRI WOKOVU?
Hili swali ni gumu sana. Kwa mtazamo wangu, mchezo wa ku-beti unaweza usiwe dhambi lakini ni kitu ambacho mazingira yake yanaweza kupelekea mtu kuuchafua Ukristo/wokovu wake. Siwezi sema kwa kucheza mchezo huo Mkristo ataikosa Mbingu, lakini anaweza kuharibu ushuhuda na maisha ya kiroho kwa namna mbalimbali kama:
• Itamfanya Mkristo asiweze kutuliza mawazo yake katika kumtafakari Mungu na Neno lake, badala yake atakuwa anawaza ni timu gani itashinda.
• Inaweza chochea UVIVU miongoni mwa Wakristo na jamii kwa ujumla.
• Inaweza athiri huduma na vipawa kwa sababu mchezo wa Ku-beti unachukua muda mwingi wa mtu.
• Itaharibu hata MAOMBI YA MKRISTO…. Yeye atakuwa anaomba MUNGU Team aliyoiwekea pesa ishinde. Endapo wapendwa wamebeti timu mbili tofauti, basi mmoja atashangilia kwamba maombi yake yamejibiwa na mwingine atajiona kana kwamba Mungu hajajibu. Kimsingi wote watakua wakiomba MAOMBI BATILI.
TUFUATE USHAURI WA MTUME PAULO:
1 WAKORINTHO 6:12 (BHN); “Mtu anaweza kusema: “Kwangu mimi kila kitu ni halali.” Sawa; lakini si kila kitu kinafaa. Nakubali kwamba kila kitu ni halali kwangu lakini sitaki kutawaliwa na kitu chochote.”
WARUMI 14:21 (BHN); “Afadhali kuacha kula nyama, kunywa divai, au kufanya chochote ambacho chaweza kumsababisha ndugu yako aanguke.”
1 WAKORINTHO 8:9,13 (BHN); “Lakini, jihadharini: Huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi… Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi.”
NB: KU-BETI KUNAWEZA KUWA KAMA ULEVI (ADDICTION) NA KUMFANYA MTU KUWA MTUMWA.
Shalom,

CHAKULA CHA BWANA NI NINI?

Image may contain: one or more people and text
Chakula cha Bwana ni nini? Kwa nini kushiriki? Tushiriki mara ngapi? Haya ni maswali katika akili za wengi. Chakula cha Bwana kilianzishwa na Bwana mwenyewe kama kumbukumbu kwa ajili ya mateso yake kutokana na dhambi zetu (Mt. 26:26-29). Leo Wakristo wanaadhimisha jambo hili kukumbuka tukio kuu la vizazi vingi, kifo cha Kristo. Kushiriki katika hali ya kumpendeza Mungu, chakula hiki ni vema kiwe na vitu halali.
ASILI YA KIHISTORIA YA KARAMU YA BWANA
Injili ya Mathayo (26:26ff), Mariko (14:22ff) Na Luka (22:14ff) zinatoa habari kuhusu Karamu ya Mwisho ambayo Yesu alikula pamoja na wanafunzi wake usiku kabla ya kifo chake. Yote inaeleza Yesu kushukuru au kubariki mkate na kikombe, na kuwapa wanafunzi akisema kuwa mkate ni mwili na kikombe ni damu ya agano au agano jipya katika damu yake. Katika Luka 22:19 Yesu anasema, “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Injili ya Yohana haijatoa habari kuhusu kukula na kunywa bali mafundizo na matendo ambayo yalijawa kwenye jioni hiyo.
Yesu alisema: waliitekeleza karamu kama ukumbusho wa Yesu na kifo chake. Nyaraka za Paulo ndizo ushuhuda wa kwanza kabisa tulizo nazo na katika I Wakorintho 11:20 anamaanisha tukio katika uzima wa kanisa liitwalo “Karamu ya Bwana.” huitwa “Karamu ya Bwana.” kwa sababu ulianzishwa na kutawazwa na Bwana Yesu na aana yake halisi ni kusherehekea ukumbusho wa kifo cha Bwana. Paulo anasema kwenye I Wakorintho 11:23-24 “Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliowapa nanyi ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliyosalitiwa alitoa mkate, naye akisha kushukuru akaumega, akasema “Huu ndio mwili wangu uliyo kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” “Mimi nalipokea kwa Bwana . . . ” Pengine inamaanisha kwamba Bwana mwenyewe alimdhibitishia Paulo (ambaye hakuwa mmoja wa wanafunzi siku hiyo ya Pasaka) kwamba kile wengine waliripoti kuhusu Pasaka hakika kilitendeka.
Hivyo asili ya historia ya Karamu ya Bwana ni hicho chakula cha mwisho ambayo Yesu na wanafunzi walikula usiku kabla ya kusulubishwa. Maana na kitendo hiki kina shina kwa kile Yesu alisema na kufanya katika usiku huo wa mwisho. Yesu mwenyewe ndiye chimbuko cha chakula cha Bwana. Aliamuru kwamba kiendelee na yeye ndiye tegemeo na muhusika ndani yake.
Vitu Halali
Mkate na uzao wa mzabibu ndivyo vitu vya msingi. Ingawa si mwili na damu halisi, mkate ni ushirika wa mwili wa Kristo na kikombe ushirika wa damu yake (Lk. 22:12-20). Wakristo wanapoizingira meza hii mioyo yao inachochewa kwa uaminifu kutambua maisha yake yenye utukufu yalivyotolewa kafara na kifo chake msalabani kwa ajili ya ulimwengu mwovu.
WASHIRIKI WANACHOKIAMINI CHAKULA CHA BWANA
Chakula cha Bwana ni kitendo cha mkusanyiko wa familia ya walioamini Yesu, yaani Kanisa. Si kitendo cha wasioamini. Wasioamini wanaweza kuwepo—kwa kweli, tunawakaribisha—hakika hakuna kilichositirika kuhusu chakula cha Bwana.
Yesu alisema angekunywa kwa kikombe hiki pamoja na wale waliomo katika Ufalme wa Baba (Mt. 26:29) waamini waliobatizwa waliendelea kwa juhudi katika kumega mkate, (Mdo. 2:42).
Wanafunzi walikuja pamoja kukutanika Siku ya Kwanza ya juma kumega mkate (Mdo. 20:7).
Wale waliomo katika Kanisa la Bwana ndio watu halali wa kushiriki Chakula cha Bwana.
Lakini hakuna aliye na haki ya kukataza au kufunga ushirika huo kwa sababu Paulo alisema “Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe,” (1 Kor. 11:28).
KUSHIRIKI KATIKA DAMU NA MWILI WA KRISTO KIROHO KWA IMANI
Mawazo haya ya “Kushiriki mwili wa Kristo na damu . . . kiroho . . . kwa imani” yametoka wapi? Kifungu cha karibu zaidi kuhimiza haya ni katika sura inayotangulia: I Wakorintho 10:16-18 Ninapokisoma jiulize “Ni nini maana ya ‘kushiriki’?” “Kikombe cha baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo?
Naje ushirika huu una maana gani? Kushiriki, kugawana, na ushiririkiano yana maana gani? Nafikiri mstari wa 18 unatupa fikira kwa sababu unatumia neno sawa lakini analilenganisha na ninachotendeka katika dhabibu ya Wayahudi. “Waangalieni hao waisraeli: si wale wanaokula dhabibu Washirika ni kama kisawe kwenye madhabahu?” Nini maana ya washirika/washiriki, wanaoshiriki kwenye madhabahu? Ina maana kuwa wanashirikiana katika au wanafaidika kwa kile kinachoendelea katika madhabahuni. Wanafurahia, kwa mfano, msamaha na urejesho wa ushirika pamoja na Mungu.
Basi naichukua mstari wa 16 na 17 kumaanisha kwamba waumini wanapokula mkate na kunywea kikombe kimwili tunatenda aina nyingine ya kula na kunywa kiroho. Tunala na kunywa—yaani tunaingiza katika maisha yetu—Kilichotendeka kwa msalaba. Kwa Imani—kwa kutumaini ndani ya yote ambayo Mungu yu kwa ajili yetu ndani ya Yesu—tunajistawisha kwa fadhili ambazo Yesu aliyotupokeza kwetu alipotiririsha damu na kufa msalabani.
Hii ndiyo sababu tunawaongoza kwa mtazamo tofauti tofauti kwenye meza la Bwana kila mwezi (amani na Mungu, furaha kwa Yesu, tumaini la usoni, uhuru kutokana na uoga, usalama wakati wa mabaya, muelekeo wakati tumekwama, uponyaji wa magonjwa, ushindi wakati wa majiribio n. k). Kwa kuwa Yesu alipokufa damu yake iliyomwagika na mwili uliovunjika; uliotolewa kwenye kifo chake kwa niaba yetu, alizinunua kila ahadiza mungu.
Paulo anasema, “Maana ahadi zote za Mungu zilipo katika yeye ni ndiyo” (2 Wakorintho 1:20) kila kipawa cha Mungu na furaha ya ushirika wetu pamoja na Mungu, tuliupokea kwa damu ya Yesu. Paulo anaposema, “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuuegemeao si ushirika wa mwili wa Kristo? Anaamanisha: Je, si tunashiriki kwenye meza ya Bwana kiroho kupitia imani kila Baraka ya kiroho uliogharamiwa kwa mwili na damu ya Yesu? Hakuna asiyeamini awezaye kufanya hivyo. Shetani hawezi. Ni karama kwa familia. Tunaposherehekea meza ya Bwana, tunasheherekea kiroho kwa imani katika kila ahadi za Mungu zilizonunuliwa kwa damu ya Yesu.
Roho Inayostahili
Isipokuwa katika jicho lenye akili, “Kuupambanua mwili, anakula na kunywa hukumu ya nafsi yake,” (1 Kor. 11:29). Kwa sababu baadhi ya Wakorintho walishiriki Chakula cha Bwana katika hali isiyostahili na wala taadhima katika Roho, wakawa dhaifu na wasiojiweza (1 Kor. 11:30).
Katika kushiriki, afanye hivyo kwa kumbukumbu....... “Fanyeni hivi…kwa ukumbusho wangu” na kwa kujihoji, “lakini mtu ajihoji mwenyewe” na kwa matazamio, “mwitangaze mauti ya Bwana hata ajapo,” (1 Kor. 11:25, 26, 28).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

Tuesday, February 5, 2019

BIBLIA TAKATIFU MAANA YAKE NINI?

BIBLIA TAKATIFU MAANA YAKE NINI?
“Biblia Takatifu” maana yake nini?
Neno “Biblia limetoka katika neno la Kiyunani ‘biblos’ likiwa na maana “Kitabu”. “Takatifu” ni neno lenye maana ‘weka kando” au “tenga”, likiwa ni jambo lililowekwa kando au limeweka wakfu kwa ajili ya Mungu kwa hiyo kuitwa “Biblia Takatifu”hiki kitabu kiliitwa hivyo kwa sababu kilionekana kuwa ni neno la Mungu lililovuviwa, kilitengeka kabisa toka katika vitabu vingine vyote vilivyowahi kuandikwa.
Biblia iliandikwa lini?
Kwa kweli Biblia ni mkusanyiko wa vitabu au maandiko ambayo yaliandikwa kipindi kirefu takribani miaka 1600 na waandishi wengi tofauti. Vitabu vya kwanza viliandikwa na Musa karibu 1500 KK, ambapo cha mwisho kiliandikwa na Yohana Mtume kuelekea mwisho wa karne ya kwanza.
Kwa sababu gani Biblia imegawanyika katika Agano la Kale na Jipya?
Kama tukitazama orodha ya majina ya vitabu kabla ya dibaji tunaona kwamba Biblia ina vitabu 66. Waliofasiri waligawa hivi vitabu katika Agano la kale na Jipya miaka mingi baada ya kuwa vimeandikwa. Agano la Kale lina vitabu 39 vilivyoandikwa kwa kiebrania kabla ya kuzaliwa Kristo. Agano jipya lina vitabu 27 vilivyoandikwa katika lugha ya Kiyunani –Kigriki baada ya Kristo.
Mahali gani ilipoandikwa Biblia?
Palikuwa na watu wengi ambao Mungu aliwachagua kuiandika Biblia zaidi ya muda wa kipindi kirefu. Ingawa zaidi waliandika wakiwa katika nchi ya Israeli, walikuwepo baadhi kama Daniel na Ezekieli walioandika wakiwa Babeli na wengine kama Mitume walioandika wakiwa katika majimbo tofauti ya dola ya kirumi. Ukweli wa kushangaza ni kwamba ingawa Biblia iliandikwa kwa kipindi hicho kirefu, sehemu nyingi tofauti na waandishi wengi, ujumbe wake ni kwa kulingana sawa na umekuwa mmoja. Hali hii peke yake inaonyesha kwamba Mungu ndiye aliyekibuni.
Ni jinsi gani Mungu aliwafanya hawa watu waandike Biblia?
Kuna ushahidi mwingi katika Biblia unaotuambia namna Mungu alivyofanya ujumbe wake unakiliwe. Mtume Petro anaeleza jinsi hii” … hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu Fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu (2 Petro 1:20 –21).
Petro anaeleza ya kwamba Mungu aliteua watakatifu au watu wenye kumcha Mungu ambao kwao akawajulisha nia yake. Hawa watu waliandika ujumbe ambao walipokea toka kwa Mungu. Haya maandishi yaliyounganika yamekuwa kitabu tunachokifahamu kuwa ni Biblia.
Ni kwa sababu gani Biblia iliandikwa?
Swali hili linajibiwa na mtume Paulo namna hii. “Kila andiko, lenye pumzi Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki ili mtu wa Mungu uwe kamili, amekamilika apate kutenda kila tendo jema” / 2 Timotheo 3:16 – 17).
Kwa sababu hiyo Biblia ilitolewa ili kumfundisha mwanadamu kuhusu Mungu na kusudi lake, na kumwongoza katika njia ya maisha yampendezao Mungu na kuwapa thawabu wale wenye kumtii.
Ni jinsi gani tunaweza kuthibitisha ya kwamba Mungu yupo na kwa kweli Biblia ni Neno lake?
Hili ni swali lenye busara sana lakini jawabu halitatanishi wala si gumu kulifahamu, maana Mungu mwenyewe alitazamia, naye ametoa jawabu sehemu nyingi katika Biblia. Moja kati ya hili ni katika unabii wa Isaya:- Maana mimi ni Mungu wala hapana mwingine, mimi ni Mungu wala hapana aliye kama mimi, nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote” (Isaya 46: 9-10).
Tazama kadhia ambazo Mungu ametoa hapa:
Yeye peke yake ni Mungu wala hayupo mwingine. Ikiwa hii ni kweli basi Mungu wa Biblia peke yake ndiye Mungu wa ulimwengu, na kwa hiyo dini zote nyingine zenye kudai kumwabudu Mungu Mwingine sio za kweli.
Aweza kujulisha mambo yajayo. Tunafahamu kwa kuona kwamba hakuna mtu wa kumtegemea awezaye kujulisha yajayo. Katika Biblia Mungu anajulisha kabla matukio ambayo ni vigumu kubashiri, kunena kibinadamu lakini yametokea kwa usahihi kabisa.
Anauweza kutimiliza aliyoeleza habari zake kabla ya kutokea. Sio tu anauwezo wa kujulisha habari ya mambo yajayo, bali pia kuhakikisha yanatimia kwa wakati wake.
Kutokana na hili twaona kwamba Mungu ametoa njia iliyo rahisi sana ambayo kwayo mtafutaji halisi wa ile kweli aweza kupata jawabu la swali “Je! Yupo Mungu na Biblia ni neno lake? Hatutakiwi kuwa na akili nyingi mno au wenye elimu vizuri ili kutafuta jibu. Inategemea upande wetu kuwa wanyoofu katika kupima mambo kwa maneno ya akili ambayo yameonyeshwa katika Biblia. Unabii ulio katika Biblia unathibitisha kwa nguvu kadhia yake kuwa ni pumzi ya Mungu. Kwa kifupi tutaona baadhi ya unabii rahisi na kupima dai la Mungu kwamba aweza kujulisha yajayo.
Ukweli Mwingine wa kukumbuka
Biblia Agano la Kale ni dhahiri lilikamilika zaidi ya miaka 2000 kabla ya kuzaliwa Kristo. Septuagint (Tafsiri ya Kiyunani Agano la Kale) inatoa ushahidi wa kihistoria kuhusu jambo hili.
Gombo la Bahari ya Chumvi linasaidia katika kujua tarehe ya Agano la kale.
Ya kwamba Yesu Kristo aliwahi kuishi alihubiri Injili na kuuawa hayo yote yamesemwa dhahiri mbali na taarifa ya Biblia na wana historia walioishi kipindi kile kile yalipotokea.
Ukweli huu unaweza kuthibitishwa na Maktaba inayotegemewa na watu wote.
Katika ukweli huu uliothibitishwa kihistoria sasa tunaweza kupima iwapo Mungu aweza kujulisha hasa mambo kabla hayajatokea tukitambua kwamba utabiri uliofanywa katika Agano la kale umefanywa karibu miaka 250 kabla ya kutimi katika Agano jipya.
Unabii wa kusulubiwa Kristo
Ona kidogo maelezo yaliyoanza katika unabii ulio katika Zaburi 22 kuhusu kusulubiwa Kristo na jinsi kila maelezo yalivyotimia. Zaburi hii iliandikwa na Daudi miaka 1000 kabla ya kuja kutimia.
Zaburi 22 Tukio lilipotimilika
Mst 1 Maneno ambayo Kristo atanena akiwa msalabani Mathayo 27:46
Mst 7-8 Matendo na maneno ya Wayahudi wakiwa kando ya msalaba Math 27:39-43
Mst 16 Namna hasa ya kufa – kwa kusulubiwa. Math 27:35
Mst 18 Namna ambavyo nguo zake zitagwanywa Math 27:35; Yn 19:23-24
Ingekuwa vigumu kwa mwanadamu kubashiri matukio haya katika maelezo ya jinsi hii. Maelezo mengine yanatutaka tu kuamini ya kwamba Yesu mwenyewe, wakati wa Wayahudi waliokana dai lake kuwa ni Masihi, na askari wapagani wa kirumi wote walishirikiana kutekeleza kumsulubisha Yesu na hivyo kutimiza unabii wa Agano la Kale, tena wakaona wawadanganye watu waamini ya kwamba Biblia si neno la Mungu. Kamwe hili si wazo lenye akili wala ni lenye busara.
Sio tu Zaburi 22 ilibashiri kusulubiwa Kristo bali pia, katika aya ya 22, ufufuo wake.
Baadhi ya unabii kuhusu mataifa.
Nabii Isaya aliishi katika nchi ya Israeli kati ya mwaka760 – 700 KK katika siku zake dola kuu mbili zenye nguvu zilikuwa Ashuru iliyokuwa upande wa kaskazini na Misri upande wa Kusini.
Katika Sura yakeya 13 Mungu alifunuwa kupita kwake kuinuka na kuanguka kwa dola ya Babeli. Tunatakiwa kutambuwa kwamba utabiri wake wa kwamba Babeli itakuwa dola yenye nguvu ulifanyika si chini ya miaka 100 kabla ya tukio. Ingawa hivyo unabii wake sio tu unahusu kuinuka kwa Babeli bali pia kuangushwa kwake na Waajemi. Waajemi waliiangusha Babeli mnamo mwaka 536 KK, kwa hiyo utabiri huo uliafanyika karibu miaka 200 kabla ya kutokea.
Sio tu Isaya alinena kuharibiwa utawala wa Babeli, bali alisema ya kwamba mji hautakaliwa nao utakuwa jangwa. Huu ulikuwa ni utabiri wa ajabu kwa mji ambao katika siku zake ulikuwa ni mmojawapo wa maajabu ya ulimwengu wa kale (Isaya 13:17-22) .
Hata hivyo hayo sio yote! Tena Isaya alitaja jina la mfalme atakaye iangusha Babeli – Mtu aliyeitwa Koreshi (Isa 45: 1-2) kwa kuongelea hili, Isaya alieleza amri, atakayotoa Koreshi, ya kuwataka Wayahudi waliotawanyika katika dola yake warudi Yerusalemu na wajenge tena Hekalu ambalo liliharibiwa na Wakaldayo (Isaya 44:27-28: Ezra 1:1-4)
Unabii huu unakwenda mbali zaidi ya ubashiri awezao kuufanya mwanadamu. Ni Mungu tu awezaye kujulisha yajayo.
Ona unabii huu ulikuwa na maana gani katika ulimwengu wa leo. Ulikuwa na lazima.
Kutabiri taifa litakalokuwa likitawala ulimwengu miaka 100 tangu hapo
Tena likatabirika taifa litakalo angusha nguvu hii ya kwanza miaka 200 tangu hapo.
Ukataja mtawala wa taifa hili la pili.
Na kutaja amri ambayo atatoa alipofikia kuwa na mamlaka
Ni wazi hali hii haiwezekani kwa mtu kutabiri. Walakini, Mungu kupitia nabii wake Isaya alifanya hivi kikamilifu. Kwa hivi Mungu hawezi tu kutabiri yajayo, bali pia anaweza kutimiliza kwa usahili wa kushangaza.
Ajabu ya Unabii wa Danieli.
Daniel aliishi kati ya mwaka 600 – KK 534. Unabii wake ulitabiri;
Kuanguka kwa utawala wa Babeli (Daniel 5:25-31)
Kuinuka na kuanguka kwa utawala wa Waamedi na Waajemi (Dani 8:20)
Kuinuka na kuanguka utawala wa Uyunani (Dn 8:21)
Kuharibiwa mji wa Yerusalemu na Warumi mnamo 70 BK (Den 8:9-11)
Mwaka wa Kusulubiwa Yesu Kristo (Dan 9: 24 – 27).
Usahihi wa unabii wa Daniel umeshangaza watu ambao wamekuwa wakiichunguza ‘kweli’ kwa uhalisi, nao wameweka katika hali ngumu wenye mashaka na mafundisho ya dini na wasioamini kuwa yupo Mungu.No photo description available.
Mungu amejulisha nini yajayo?
Tunaweza kusoma Biblia kwa ujasiiri, tukijuwa ya kwamba kama Mungu ametimiza unabii wake wakati uliopita, kwa hakika atatimiza alichotabiri kwa wakati ujao.
Haya ni matukio kwa kifupi tuonayo kabla yake yaliyotabiriwa kipindi chetu.
Kutakuwa na hali ya kuanguka kwa uadilifu na heshima katika jamaii (Luka 17:26-30)
Wayahudi watarejea katika nchi ya Israeli, na Yerusalemu kuwa kitovu cha mivutano ya kimataifa (Zekaria 12: 2-3; Ezekieli 38: 8,12)
Yesu atarudi mwenyewe na wa kuonekana wazi duniani (Mdo 1: 9-11)
Mungu ataanzisha Ufalme wake duniani ambao utaingia mahali pa utawala wa binadamu (Daniel 2: 44)
Ufalme huu utatimiza sala ya Bwana “ Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe duniani, kama yalivyo mbinguni” (Mathayo 6: 9-10)
Yerusalemu utakuwa makao makuu ya huo ufalme (Yeremia 3:17)
Yesu Kristo atakuwa Mfalme kipindi hicho (Ufunuo 11: 15, 18)
Katika siku hiyo wakazi wa dunia kwa hiari watajifunza njia ya Mungu wala hakutawa na vita tena (Isaya 2:2-4)
Je! Kuna ujumbe binafsi katika Biblia ulio kwa ajili yetu?
Naama upo. Mungu anawapa wanaume na wanawake tumainila kushiriki ulimwengu huu mpya na Bwana Yesu Kristo ajapo. Huu ujumbe wenye tumaini unaitwa Injili, ambao unamaana habari njema za ufalme wa Mungu ujao, na wokovu toka dhambi na mauti kupitia Bwana Yesu Kristo . Huu ni ujumbe ambao Kristo na Wafuasi wake waliuhuribiri (Marko 16:15-16).
Muhutasari wa Maana
Biblia ni neno lenye pumzi ya Mungu, limetolewa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu / 2 Petro 1:20-21)
Ilitolewa ili binadamu aweze kufahamu mpango na kusudi la Mungu na aweze kuwelewa njia zake (2Timotheo 3:16-17)
Kutimia kwa usahili unabii wa Biblia unathibitisha ya kwamba Mungu yupo na kwamba Biblia ni neno lake lililovuviwa (Isaya 46:9-10)
Unabii ambao bado haujatimia unajulisha kwamba Yesu Kristo atarudi hivi karibuni hapa duniani kusimamisha ufalme wa Mungu duniani (Dan 2:44 Math, 6;9 – 10; Mdo 1:9-11)
SOMO LA 1 –Maswali.
1. Maneno “ Biblia Takatifu” Maana yake nini?
2. Kuna vitabu vingapi katika Biblia?
3. Ni jinsi gani Mungu alifanya Biblia hata ikaandikwa?
4. Ni kwa sababu gani Mungu akafanya Biblia ikaandikwa?
5. Ni kwa nini Unabii ni moja ya ushahidi mkubwa wa kwamba Biblia ni neno la Mungu?
6. Baadhi ya matukio gani ambayo Mungu alitabiri yatatokea ambayo bado kutimia?
Shalom,
Max Shimba Ministries

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW