Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” .
Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”,
Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an.(Qur’an is a post Bible book).
Hoja yetu kwa Waislamu ni hii nani aliyebadilisha jina Yasu’a kuwa Isa?. Jina Yasu’a linashabihiana zaidi na Jina Yehoshua ambalo hilo ni katika lugha ya Kiebrania, na katika Kiyunani lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya anaitwa Iesous (tamka Yesu) tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mwokozi.
Tunasoma hayo katika Math 1:21-23 “ Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa Nabii akisema Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”
Hoja yetu Je Isa a.s naye ni Mwokozi na Imanueli kama alivyo Yesu Kristo?.
Jambo jingine tunalopaswa kulizingatia tunapoangalia tofauti zao ni kuhusu mama zao. Mama yake Yesu Kristo ni Mariam anayetoka katika ukoo wa Yuda. Tunasoma hayo katika kitabu cha Mwanzo 49:10 “ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii”.
Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo.Tunasoma hayo katika Waebrania 7:14 “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani”
Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”.
fafanuzi unaoifafanua aya hii ya 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi “ This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)”
Tafsiri “Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam”
Kwa mujibu wa Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma hayo katika kitabu cha Hesabu 26:59 “Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao”
Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao: ISSA KAUMBWA. Qur’an Suratul Imran, 3:59 “ Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa”
Lakini tusomapo kumhusu YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU.
Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”
Mika 5:2 “ Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”
Yoh: 8:58 “ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”.
Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe
Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”
Kol 1:16-17 “ Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana ; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake”
2) (A) ISSA A.S : BAADA YA KUONDOKA KWAKE, (KAMA WAISLAMU WANAVYOAMINI), HAJAWAHI KUTOKEA KWA NAMNA YOYOTE ILE.