Friday, October 23, 2020

DUNIA INA UMRI GANI KIBIBLIA?

 Kulingana na hesabu ya vizazi na miaka yao waliyoishi katika biblia, inakadiriwa tangu Edeni mpaka wakati wa Gharika, ni miaka elfu 2, na tangu wakati wa gharika mpaka kuzaliwa kwa Bwana Yesu ilipita miaka elfu 2 hivi, na tangu kipindi cha Bwana wetu Yesu hata leo nacho pia ni kipindi cha miaka elfu 2 kimepita. Kwahiyo jumla yake tangu Edeni mpaka sasa ni miaka kama elfu 6 hivi, au imezidi kidogo au imepungua kidogo..Sasa kumbuka huo ulikuwa ni mwanzo wa Edeni, lakini haukuwa mwanzo wa Dunia..dunia ilikuwepo kabla ya Edeni..Tunasoma.

 
Mwanzo 1:1 “hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”
 
…hapa hajasema huo mwanzo ulikuwa ni wa miaka mingapi iliyopita inaweza ikawa ni miaka elfu kumi,milioni kumi au vinginevyo…
 
lakini mstari wa pili unasema nayo nchi ilikuwa ukiwa na utupu inamaanisha kuwa kuna jambo lilitokea likaifanya hiyo nchi kuwa ukiwa baada ya Mungu kuziumba mbingu na nchi na hapa si mwingine zaidi ya shetani ndiye aliyeiharibu na kuifanya ukiwa (kama anavyoendelea kuiharibu sasa hivi) maana Mungu hakuiumba ukiwa yaani dunia iwe ukiwa bali ikaliwe na watu,
 
Isaya 48:18 inasema
 
18 Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine. “.
 
Lakini baada ya dunia kuharibiwa kwa viwango vya hali ya juu, ikapoteza umbo lake ikawa kama moja ya sayari nyingine, na ndio tunaona Mungu akaanza kufanya uumbaji upya baada ya nchi kukaa muda mrefu katika hali ya ukiwa, hapo mbingu na nchi zilikuwa tayari zimeshaumbwa muda mrefu nyuma.
 
Kwahiyo mwanadamu na viumbe vyote inakadiriwa viliumbwa takribani miaka  6000 iliyopita lakini dunia iliumbwa kabla ya hapo na shetani alikuwepo duniani kabla ya mwanadamu kuumbwa, kwasababu tunamuona alionekana katika bustani ya Edeni na biblia inamwita shetani kama yule nyoka wa zamani
 
Ufunuo 20:2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;,
 
kwahiyo inamaanisha alikuwepo toka zamani kabla hata ya mwanadamu kuumbwa, ambapo tunaona alitupwa huku duniani baada ya kuasi mbinguni pamoja na malaika zake.

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW