BAADA ya shoga maarufu jijini Dar es Salaam, Ibrahimu Mohamed ‘Anti Suzy’ (25), kutoboa siri kwenye vyombo vya habari jinsi watoto wa kiume wanavyoharibiwa na wanaume na kueleza namna alivyobwagiwa mtoto wa mwaka amtunze, mwanamume aliyembwagia mtoto ameibuka na kumjeruhi kwa visu akitaka kumuua.
Mwanamume huyo mwenye mke, awali alikuwa akiishi na Anti Suzy kama mume na mke eneo la Jangwani, baada ya kumkimbia mkewe na alikorofishana na shoga huyo baada ya kumfanyia fujo na kumuibia.
Akizungumza na gazeti la Habari Leo jana nyumbani kwake, ‘Anti Suzy’ aliyejitangaza kuwa ni muathirika wa Virusi Vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 10 sasa, alisema mwanamume huyo alikuwa akimsumbua warudiane, lakini yeye alikataa na kumtaka aishi na mkewe na kutunza watoto badala ya kumng’ang’ania.
“Nilimwambia simtaki, vituko alivyonifanyia ukiacha kuniletea mtoto wa mwaka na nusu wa kike nimlee hapa nyumbani, alikuwa akinipiga, kunitukana na aliniibia vitu vyangu vyote. Kwanza nilishamwambia nimeathirika na Ukimwi ananifuata nini?” Alihoji shoga huyo.
“Jana (juzi) alinipigia simu akinitaka turidiane nikamwambia asinifuate kwanza nimeshaenda kwenye vyombo vya habari.”
Alisema alimwambia hivyo ili asimfuate, lakini baada ya kumweleza hayo, alimvamia nyumbani juzi kati ya saa nne na tano asubuhi akiwa na panga na visu akimtishia kumuua kama hawatarudiana na kama ataendelea kwenda kwenye vyombo vya habari kumuanika mambo yake.
“Nilikimbilia ndani na yeye akanifuata humo, akarusha panga anikate shingoni huku akisema ataniua, nikakwepa, lakini likanijeruhi shingo, kama haitoshi akachukua kisu alichokuwa nacho akanikata vidole.
“Damu ikaanza kutoka nyingi, alivyoona hivyo akanikaba kooni ili aninyonge, majirani waliposikia nakoroma, wakavunja mlango na kuniokoa,” alidai Anti Suzy.
Shoga huyo aliyeanza vitendo hivyo akiwa mkoani Mwanza, alisema aliamua yeye na mama mwenye nyumba kwenda Kituo Kidogo cha Polisi Jangwani kutoa taarifa na kupewa hati yenye namba MS/RB/10695/20....