JE, KULA NYAMA YA NGURUWE NI DHAMBI?
1. Je, kuna aya yeyote ile katika Agano Jipya inayo mkataza Mkristo kula nyama ya Nguruwe?
2. Je, kuna sheria yeyote ile kwenye Agano Jipya inayo kataza kula nyama ya Nguruwe?
3. Je, Yesu alisema au waamrisha Wafuasi wake wasile Nyama ya Nguruwe?
4. Je, Yesu alipo vitakasa vyakula vyote [Marko 7 :15-19] kunapingana na sheria ya hapo mwanzo kwenye Mambo ya Walawi?
Ndugu msomaji,
Katika hili somo, tutajifunza kuhusu ulaji wa Nyama ya Nguruwe na kwanini Wakristo wanakula Nyama ya Nguruwe.
Tuanze moja kwa moja kwa kusoma aya za Biblia:
"Bwana Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawambia Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, kila mnyama wa katika nchi watawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani pamoja na viti vyote vilivyojaa katika ardhi,na samaki wote wa baharini vimetiwa mikononi mwenu, kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani ,kadhalika hivi vyote ,balo nyama pamoja na uhai ,yaani damu yake msile" {Mwanzo 9:1-4}
Ndugu msomaji wangu maandiko yamefunua wazi kwamba Mungu alitoa wanyama wote kuliwa baada ya mboga za majani walakini hatuoni Mungu akitoa sheria ama akiwabagulia wanyama wa kuliwa yaani walio safi na wasio safi, bali maandiko yametuonyesha kuwa Mungu alitoa wanyama wote kuwa chakula kwa wanadamu kama ilivyo shuhudiwa katika Mwanzo Mlango wa 9 aya ya 1-4.
Je sheria inayohusiana na wanyama safi na wasio safi ilitolewa wapi?
Ndugu msomaji kama ambavyo nilivyokwisha kutangulia kusema kuwa sheria hii inayohusiana na vyakula haikutolewa tangu mwanzo kwa ushaidi wa andiko ambalo nimekupa limeonyesha hivyo, swali la lini sheria hii ambayo ilihusiana na vyakula ilitolewa maandiko yapo wazi kabisa eneo ilo ni baada ya wana Israel kutolewa utumwani Misri ndipo tunaona katika biblia sheria inayohusiana na wanyama walio safi na wasio safi kwaiyo kabla ya hapo wanyama wote walikuwa chakula {Mambo ya Walawi 11 :1-7} kupitia fungu ili la biblia tunaona kuwa Mungu anatoa sheria inayohusiana na wanyama wanaopaswa kuliwa na wasiopaswa kuliwa?
Ni kweli kabisa Mungu alitoa hiyo kuwa ni sheria kwao wana wa Israel walakini tusiishie tu hapo katika kuangalia sheria kuwa ni sheria tusafiri pamoja kifikra,utakumbuka kuwa watu ambao kiasili sio wayahudi walikuwa hawana desturi za usomaji wa torati?
Je hii sheria iliyohusiana na wanyama safi na wasio safi ilifahamika kwao?
Bila shaka jibu ni hapana labda utajiuliza kwanini?
Napenda tujifunze ili jambo na kutokuacha historia ya vizazi pia na chanzo cha kusambaa kwa wanadamu duniani kote
Theolojia inatueleza kwamba vizazi vya ulimwengu huu vimetokana na wana watatu wa Nuhu ambao ni Shemu, Hamu, na Yafethi sasa katika historia ya chanzo cha mataifa mbalimbali kama inavyoelezwa kwamba wanadamu yaani mataifa yote yaliotokana na watoto wa Nuhu walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa na lugha moja na usemi mmoja na waliishi pamoja, wanadamu hawa ikumbukwe kwamba hawakupewa sheria yoyote inayohusiana na wanyama wapasao kuliwa na wasiopaswa hawakupewa na hapa tunaelezwa ndio chanzo cha mataifa mbalimbali maana baada ya Mungu kuwachafulia lugha walisambaa kila mmoja mahali pake (Mwanzo 11:1-9}
Sasa swali la kujiuliza je wanadamu hawa waliondoka na ufahamu upi kuhusiana na vyakula, kwamba Nguruwe haramu ama?
Maana ifahamike kuwa kwao walipewa wanyama wote kuwa chakula kwa sababu hawakuwa na sheria inayohusiana na vyakula safi na visivyo safi kwao wanyama wote ni safi tu waliondoka na imani hiyo kama walivyopokea huu ndio ukawa mwanzo wa mpishano wa vyakula baina ya watu walioitwa wa mataifa na wayahudi baada ya wao kupewa sheria iliyohusiana na wanyama walio safi na waschakula.
Wayahudi walipata tabu sana kushiriki katika kalamu za watu ambao kiasili hawakuwa wasomaji wa torati na kuishi katika nchi zao, kwa sababu walipishana katika desturi za vyakula ,wayahudi hata wale ambao walikuja kuwa wafuasi wa Kristo walipata ugumu mno katika eneo ilo,sababu wao wayahudi walipewa sheria kuhusiana na wanyama safi na wasio safi ila mataifa kwao wanyama wote walikuwa safi sasa mtume Paulo hali akiwa na ufunuo wa Kimungu aliwaeleza wale wayahudi waliokuwa wakristo zama zile na walikuwa wakiambatana na mitume katika uinjilisti alisema maneno haya
" Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila ya kuuliza uliza kwa ajiri ya dhamiri ,maana ,dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo, mtu asiyeamini akiwaalika ninyi mnataka kwenda ,kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila ya kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri" {1 Wakorintho 10:25-28}
Kwanini mtume Paulo awaagize wale kila kitu ikiwa wapo wanyama waliozuiliwa je alikuwa anapingana na Mungu? Lah hasha! hakuwa akipingana na Mungu, bali Mtume Paulo alifahamu kesi kuhusiana na vyakula, Yesu aliye kielelezo cha imani yetu aliitatua kupitia Marko 7 :15-19 pale alivyovitakasa vyakula vyote, akamaliza utata huo, hivyo baada ya hapo kila chakula kilikuwa halali kuliwa rejea tena kusoma Mwanzo 9:1-4
" Akawaambia hivi hata ninyi hamna akili ?
Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia mtu unajisi , kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni kisha chatoka kwenda chooni?
Kwa kusema hivi ali itakasa vyakula vyote ,akasema kimtokacho mtu ndicho kimtiacho mtu unajisi ,kwa maaana ndani ya mioyo watu hutoka mawazo mabaya ,uasherati,wivi uuaji,uzinzi, tamaa mbaya"
Kwa sababu Yesu alivitakasa vyakula vyote ndio maana tunaona agizo lake kwa Wayahudi aliokuwa akiambatana nao kwa ajili ya kueneza ujumbe wa Mungu kuwa wakialikwa katika majumba ya wasio amini na wakawapikia nyama ambazo mmezuiliwa msile na torati kuleni kwa sababu unajisi haupo ndani ya nguruwe wala ngamia ila unajisi upo mioyoni mwa watu
Ndugu pamekuwa na hoja juu ya nguruwe kuwa na madhara jamani kwani ni nguruwe tu ana madhara?
Je Ng'ombe hawa wa leo nyama zao hazina madhara?
Je Kuku wa kizungu na mayai yake hawa madhara kiafya?
Je chumvi za viwandani na mafuta pamoja na mavinywaji havina madhara?
Watu wa Mungu kimsingi kupitia Agano Jipya, Wakristo, hatuna sheria yoyote inayotuagiza kutokula Nguruwe hivyo basi sio dhambi kula Nguruwe ,dhambi katika tasfiri ya Biblia ya Union Version kupitia 1 Yohana 3:4 imetafsiriwa kuwa " dhambi ni uhasi wa sheria" kwaiyo ili dhambi iwepo lazima pawepo na uvunjifu wa sheria je katika agano jipya Wakristo tumepewa sheria inayotutaka kutokula Nguruwe ama ngamia kwa wanaokula?
Kama hakuna basi kula Nguruwe ama Ngamia sio dhambi?
Mungu tangia mwanzo alipotoa agizo la wanadamu kula nyama, alitoa wanyama wote kuwa chakula itakuwaje dhambi kwao?
Maana hakuwapa sheria iliyowabagulia wanyama wa kuliwa na wasio paswa kuliwa kwao wanyama wote walikuwa chakula sawa kama ambavyo Mungu ametoa wanyama wote kuwa chakula kwao, kama kweli alitaka wasiliwe nguruwe angewataza wasiliwe kabla hakuwapa wanadamu wanyama wote
Biblia inasema kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna kiumbe cha kukataliwa ,kama kitapokelewa kwa shukrani ,kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba {1Timotheo 4:4-5}
Kama hakuna kiumbe cha kukataliwa maana viumbe wote ni vizuri sasa ubaya wa Nguruwe ni nini?
Kama hacheuwi hii ndio sababu ndio Mungu ametaka awe hivyo!!!!!!! Ukianzia mistari ya juu utaona anaonya watu ambao wanawazuia wengine na baadhi ya vyakula kwa kisingizio cha wanyama wazuri na wabaya, sasa hawa leo ambao wanawataka watu kujitenga na baadhi ya vyakula tunawaweka kundi gani?
Biblia inasema viumbe vyote ni safi unganisha na Mwanzo 9:1-4 upate maana halisi, hivyo kula nguruwe sio dhambi ni halali kabisa
Sio vyakula ambavyo vinatuudhurisha mbele za Mungu tunakula kwa ajili ya miili yetu sio kwa ajili ya Mungu (Warumi 15:17 na Marko 7:15-19)
Hakuna kosa kula Nguruwe kwa mujibu wa Agano Jipya asanteni mbarikiwe nyote.
Mungu awabariki sana.
By permission: Pastor Samuel J. M, Christ Nations Org, Max Shimba Ministries Org, NKJV, Gideon Bible 1960, Green Island Tabernacle
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 25, 2016