Wednesday, October 30, 2013

YESU NDIE NJIA NA KWELI NA UZIMA. Kumbe Dini sio Njia

Katika Biblia tunasoma kuwa Yesu anasema yeye ndie "KWELI" na anaendelea kusema kuwa KWELI ndiyo itakuweka HURU. Hebu rejea kwenye hii aya: 

Yohana 14:6 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

Kufuatana na aya hapo juu, Mtu yeyote yule hawezi kwenda kwa Baba na/au Mbiguni bila ya kupitia "KWELI" ambayo ni YESU. Kumbe basi dini haiwezi kukupeleka popote pale. Kumbe, NJIA PEKEE ya Uzima wa Milele ni YESU na SI DINI.

Kumfahamu Yesu ambaye ni KWELI kutakufanya umwelewe Mungu wa UKWELI!! Kumbe basi, Yesu ndie mwenye uwezo wa kukufanya uelewe KWELI ya Mungu.

Yohana 8:31-32 Kwa hiyo Yesu akawaambia wale waliomwamini, “Kama mkiendelea kutii maneno yangu mtakuwa wanafunzi wangu halisi. 32 Mtaelewa yaliyo kweli kumhusu Mungu na ukweli huu utawafanya muwe watu huru.

Kufuatana na aya hapo juu, inatuhakikishia kuwa mafundisho ya YESU PEKEE ndiyo yatakufanya uelewe KWELI na kumfahamu Mungu wa KWELI. Zaidi ya hapo, kuwa Mwanafunzi wa Yesu(Ukristo) ndio njia pekee ya kufahamu kweli.

Yesu Ndie Njia ya Kweli na Uzima.

Mwamini leo ili upate uzima wa milele.

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW