Saturday, May 12, 2018

ALLAH AMEKIRI KWA AYA KUWA YESU NI MWEZA WA YOTE NA ANAWEZA KUPITISHA NGAMIA KWENYE TUNDU LA SINDANO




Hebu tuanze kwa kusoma aya kutoka Quran.
Suratul Al Araaf 40. Hakika wale wanao zikanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya sindano. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wakosefu......Allah Amesema!!!.
Ndugu zanguni, Allah anasema hakika wanao pinga ishara zake kamwe hawataingia peponi, mpaka siku ambayo Ngamia ataweza kupita katika tudu la sindano. Allah anawahakikishia wabaya wake kuwa, kamwe hawata iona pepo yake maana Ngamia kamwe hato weza kupita katika tundu la sindano. Je, haya yanawezekana kwa Yesu Mungu Mkuu. Tito 2:13?
Je, Yesu anaweza kupitisha Ngamia kwenye tundu la sindano ambalo Allah ameshindwa vibaya sana katika Suratul Al Araaf 40?
Yesu Mungu Mkuu anakujibu kama ifuatavyo?
Marko 10:25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Luka 18:25 Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Mathayo 19:24 Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Baada ya kumsoma Yesu anaye pitisha Ngamia kwenye tundu la Sindano, na Allah anaye shindwa kupitisha Ngamia kwenye tundu la Sindano, wewe utafuata ishara za nani?
Marko 10 :27, Yesu akawakazi macho akasema, « kwa
wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo, maana yote yanawezekana kwa Mungu ». hakuna jambo liwalo lote lile ambalo Mungu linamshinda. Hakuna.
Yesu amekujibu kuwa, Allah sio Mungu bali ni kama mwanadamu ndio maana anashindwa kupitisha Ngamia kwenye tundu la sindano.
Waefeso 3 :20, Neno la Mungu linasema, Basi, atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.
Yesu Mungu Mkuu anao uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu kuliko yale tuliyowahi kuyaona, kuyaomba au kuyawaza. Mungu aweza kufanya mambo makubwa sana na ya ajabu LAKINI Allah yeye hana uwezo huo kama tulivyo soma kweye Suratul Al Araaf 40.
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW