Friday, May 25, 2018

MPINGENI SHETANI, NAYE ATAWAKIMBIA


Kama Wakristo, tunahitaji kufahamu ukweli wa kuwepo kwa uovu. Tunapojitahidi kusimama imara katika imani yetu, tunapaswa kutambua kwamba adui zetu sio tu mawazo ya kibinadamu, bali nguvu halisi zinazojitokeza na nguvu za giza. Biblia inasema, "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" (Waefeso 6:12).
1 Petro 5:8-9
“Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.”
Katika karne ya kwanza, kikundi cha watu waliofuata “mambo ya uganga” katika Efeso waliitikia ujumbe wa Kikristo kwa kuchoma hadharani vitabu vyao vya uganga. (Matendo 19:19) Thamani iliyokadiriwa ya vitabu hivyo ilikuwa vipande 50,000 vya fedha. Ikiwa masimulizi hayo ya Biblia yanarejezea dinari, sarafu ya fedha ya Warumi, basi thamani hiyo ingejumlika kuwa angalau dola 37,000!
Yakobo. 4:7-10 SUV
7Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 9Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. 10Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW