Wednesday, May 30, 2018

YESU ALIKUFA KWA AJILI YAKO

Related image
Yesu alikufa ili wanadamu waweze kusamehewa zambi zao na ili waweze kupata uzima wa milele. (Waroma 6:​23; Waefeso 1:7) Kifo cha Yesu kilionyesha wazi kuwa mwanadamu anaweza kubakia mwaminifu kwa Mungu hata kama anapata majaribu makali zaidi.—Waebrania 4:​15.
Yesu alikufa ili kila mutu mwenye anamuamini asiangamizwe lakini akuwe na uzima wa milele.​—Yohana 3:​16.
Ndio maana Yesu alikuja na kwa nini alikufa, kuwa dhabihu ya hakika na ya mwisho, dhabihu kamili kwa ajili ya dhambi zetu (Wakolosai 1:22, 1 Petro 1:19). Kwa njia yake, ahadi ya uzima wa milele na Mungu inakuwa yenye ufanisi kwa njia ya imani kwa wale wanaomwamini Yesu, "Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo" (Wagalatia 3:22) . Maneno haya mawili "imani" na "kuamini" ni muhimu kwa wokovu wetu. Ni kupitia kwa kuamini damu ya kumwaga ya Kristo kwa ajili ya dhambi zetu tunayopata uzima wa milele. "Kwa kuwa umeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani-na hii sio kutoka kwenu, ni zawadi ya Mungu-si kwa kazi, ili hakuna mtu anayeweza kujivunia" (Waefeso 2: 8-9).
Tunapata majibu kutoka kitabu cha “Isaya 53" - cha kushangaza yaliandikwa miaka miatano kabla ya kifo cha Yesu. Kama wakristo tunaamini hivyo na mistari mingine katika Biblia inavyosema, yote hii ilikuwa ni mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. Yesu alikufa juu ya msalaba kwa dhambi zetu, Mungu alimtuma Yesu mwanaye wa pekee ili afe na kuteseka ili sisI tusiteseke hivyo Alizipatanisha dhambi zetu.
"bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kupigwa kwake sisi tumepona sisi sote kama kondoo tumepotea kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote”. (Isaya 53:5-6 SUV)
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW