Wednesday, May 16, 2018

MWEZI RAMADHANI ULISHEREKEWA NA WAPAGANI WA MAKKA


Mwezi Ramadhan ulisherekewa na wapagani wa Makka huko Arabuni hata kabla ya Uislam kuwepo, rejea [Maisha ya nabii Muhamad uk 16, kifungu cha 3 sura ya 4 ama Al-bukhari vol 16 no. 28]
Mwezi huo ulikuwa mwezi wa mfungo kwa ibada ya miungu yao ya Kipagani hasa mungu mke Al-Uzza ambaye pia aliwekewa nyota hiyo.
Mwezi huo pia uliadhimishwa na wapagani wa Misri kwa kumtukuza mungu Remphan ama Remdan [Ra] kwa Kimisri na kiarabu ni Ramadan, ndo maana mwezi huo unaitwa mwezi wa Ramadan yaani wa mungu Remphan.
Ndio maana hizo nyota zimejaa misikitini pamoja na mwezi nusu ambao unamwakilisha mungu mke na uke wake mfano wa kipande cha mwezi. Mungu huyo anaitwa mungu wa uzazi na rutuba, ndo huyo anayeitwa Diana na Wagiriki, na Maddona kwa Warumi, na Ashtoresh kwa Kiebrania na Astarte kwa Wababel na Easter kwa Waingereza na al Uza kwa Waarabu. Mwezi na nyota ndo ishara ya dini ya Kislam.
Biblia inasema hivi "Nanyi mlichukua hema ya #Moleki, Na #nyota za mungu wenu #Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu;Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli. Matendo 7:43
MAKKA NI MJI WA KIPAGANI WENYE MIUNGU NA MASANAMU 360
Umeshawahi kujiuliza Makka ilikuwaje kabla Muhammad hajazaliwa?
Yaelekea ilikuwa sehemu ya kuvutia, kwani ilikuwa ni kituo cha biashara, mahali penye kusanyiko la tamaduni mbalimbali. Palikuwa na wafanya biashara wenye dini mbalimbali. Watu wa kabila la Kureshi wa Makka walimwabudu Hubal, Al-ilah na mabinti watatu wa Al- ilah. Mwamba mweusi kutoka mbinguni uliheshimiwa sana uliwekwa kwenye kona ya kaaba.
Kaaba ilikuwa ni kitovu cha kuabudia miungu/sanamu 360 kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 43 sura ya 33 na.658 uk. 396 na juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 47 na.583 uk. 406.
Ensaiklopidia ya Uislam (iliyohaririwa na Eliade) uk.303 na kuendelea inasema, watu, kabla ya Uislam, waliomba mara 5 wakielekeza nyuso zao Makka na kufunga nusu siku kwa muda wa mwezi mzima. Wakureshi walifunga siku ya 10 ya Myharram/Muharam. Hii nayo Muhammad aliagiza ifanyike, lakini baadaye ikawa hiari. (Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 25 na.172 uk.109), pia Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 24 na.31 uk. 25.
Waarabu kabla ya Uislam walifanya hija (Umrah) Maka. Fiqh us-Sunnah juzuu ya 5 uk.122, na Bukhari juzuu ya 2 kitabu 26 sura ya 33 na.635 uk.371-372 zinasema walidhani kutokufanya 'Umrah ikijuwa ni moja ya dhambi kubwa sana duniani. Walipofika Makka waliifunika kaaba kwa nguo ya Fiqh juzuu ya 5 uk.131, na walikuwa na mwezi mtakatifu uliohitaji kujitenga na vita kabla ya kuja kwa Uislam (Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 23 sura ya 96 na.482 uk.273.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW