Wednesday, May 16, 2018

MAJI YA BAHARI MBILI KUTO KUCHANGANYIKA. JE, HII NI MIUJIZA YA ALLAH AU NI UKOSEFU WA ELIMU?


MAJI YA BAHARI MBILI KUTO KUCHANGANYIKA.

JE, HII NI MIUJIZA YA ALLAH AU NI UKOSEFU WA ELIMU?

Leo nitajibu hoja dhaifu ya Waislam kuhusu madai ya maji ya Bahari mbili kuto kuchanganyika. Je, hii ni miujiza au ni ukosefu wa elimu ya fizikia?

Ili kufahamu nini kilitokea kuhusu kuto changanyika kwa maji, ni vema kwanza tujifunze Fizikia ya darasa la Nne kuhusu Densiti.

ALLAH katika Qurani Sura ya 18 aya 60 mpaka 82
"Nakumbukeni Musa alipomwambia kijana wake wake nitaendelea na safari mpaka nifike katika ya maungano ya bahari mbili au niendele karne na karne mpaka nikutane na huyo ninayetaka kukutana naye."

Basi, Waislam walipo ona picha ya ya bahari mbili (madai yao), wakaunganisha na hii aya kuwa ni miujiza ya Allah. Kwa bahati nzuri, hapa katika huduma ya Max Shimba Ministries, tunawasomi walio bobea wa Sayansi, Hisabati na Biologia. Hivyo leo tunawajibu Waislam kwa kutumia sayansi.

Tuanze na kanuni ya Densiti:

DENSITI NI NINI?

DENSITI = MASI/MJAO

DENSITI
Densiti ni kipimo cha kulinganisha masi na mjao wa gimba fulani. Alama yake ya kifizikia huwa ni ρ (rho).

Gimba lenye densiti kubwa huwa na mada nyingi katika mjao fulani. Gimba lenye densiti ndogo huwa na mada kidogo katika mjao uleule. Densiti kubwa husababisha ya kwamba sisi tunaita kitu "kizito".

Vipimo kwa kawaida vya densiti huwa ni g/cm3 na kg/m3.

Kwa kutumia maantiki:
Maji yasiyo na chumvi ndani yake huwa na densiti 1. Lita 1 huwa na masi ya kilogramu 1.

MASI NI NINI?
Masi katika elimu ya fizikia ni tabia ya mata, na kwa njia hii pia tabia ya gimba au dutu.

Kipimo sanifu cha kimataifa cha masi ni kilogramu. Alama yake katika fomula kwa kawaida ni {m}.

MJAO NI NINI?
Mjao (kwa Kiingereza volume) unaeleza ukubwa wa gimba la hisabati (mchemraba, tufe, mcheduara) kwa kupima nafasi ya yaliyomo yake.

Hupimwa katika vizio vya ujazo kama mita ujazo (m³) au sentimita ujazo (cm³).

Kila gimba lenye urefu, upana na kimo huwa na mjao.


MAJI YA CHUMVI:
Maji ya chumvi ni maji yenye kiasi cha myeyusho wa chumvi ndani yake. Kwa kawaida kila aina ya maji huwa na kiwango cha chumvi iliyoyeyushwa.

Kwa wastani, maji katika bahari ya dunia yana chumvi kwa karibu 3.5% (35 g / L, 599 mM). Hii ina maana kwamba kila kilo (takriban lita moja na kiasi) ya maji ya bahari ina takriban 35 gramu (1.2 oz) ya chumvi zilizoharibiwa (Zaidi ya sodiamu (Na+) Na kloridi (Cl-) Ions). Wastani wa wiani juu ya uso ni 1.025 kg / L.

Maji ya bahari ni denser/mazito kuliko maji safi na maji safi yana (wiani 1.0 kg / L saa 4 ° C (39 ° F)) kwa sababu chumvi zilizoharibiwa huongeza wingi kwa kiasi kikubwa. Sehemu ya kufungia ya maji ya bahari inapungua kama ongezeko la chumvi linapo ongezeka. Katika salinity ya kawaida, inafungia nyuzi 2 ° C (28 ° F). Maji ya bahari ya baridi (katika hali ya kioevu) ilikuwa mwaka 2010, katika mkondo chini ya glacier ya Antarctic, na kipimo cha -2.6 ° C (27.3 ° F). Maji ya bahari ya pH ni kawaida kwa kiwango cha kati ya 7.5 na 8.4. Hata hivyo, hakuna kiwango cha pH kinachokubaliwa kwa kiwango kikubwa kwa maji ya bahari na tofauti kati ya vipimo kulingana na mizani tofauti ya kumbukumbu inaweza kuwa hadi vipimo 0.14.

MAJI MATAMU:
Maji matamu ni maji yasiyo na chumvi nyingi ndani yake.

Kwa kawaida maji ya mvua, ya mtoni au ziwani huitwa "maji matamu" maana yake ya kwamba kimsingi inafaa kwa kunywa au kumwagilia mimea hata kama mara nyingi inaweza kupatikana na matope au machafuko ndani yake. Kinyume chake ni maji ya chumvi jinsi inavyopatikana baharini au katika maziwa kadhaa.

Kitaalamu maji huitwa "matamu" kama kiwango cha chumvi ndani yake ni chini ya asilimia 1 au gramu moja ya chumvi katika lita ya maji. Sehemu kubwa ya maji matamu yanayopatikana duniani ni theluji na barafu ambayo ni hasa mvua iliyowahi kuganda katika hali ya hewa baridi

SASA NITAELEZA KWA LUGHA YA KAWAIDA ILI WOTE WAELEWE KWANINI MAJI HAYA HAYACHANGANYI KWA HARAKA.

Kwanza ningependa mfahamu kuwa, SIO bahari mbili zinakutana. Hili dai la Waislam ni uongo na ukosefu wa elimu. Hii picha inayo tumiwa ni kukutana kwa "glacial melt water" na "off shore waters" ya ghuba ya Alaska.

Sababu ya tukio hili la ajabu ni TOFAUTI ya DENSITI YA MAJI, Joto la maji, ujazo wa chumvi katika hayo maji yaliyo yeyuka kutoka Barafu, na maji ya ghuba ya Alaska, yanashindwa kuchanganyika kwa sababu ya tofauti ya densiti yao.

Maji ya bahari huwa na kiwango cha chumvi cha asilimia 3.5 iliyoyeyushwa ndani yake. Wataalamu mara nyingi hutaja kiwango cha 0.1 % kuwa maji matamu.

Kwasababu maji haya yote ni ya baridi "temperature" sana kinacho tokea ki kwamba, mchangayiko wake unachukua muda.

Mmumunyo au myeyusho (kwa Kiingereza solution) ni tokeo la kuchanganya kabisa dutu mbili hadi kupata mchanganyiko wa aina moja usioonyesha sehemu zake. MFANO RAHISI: ni kukoroga sukari katika maji. Hapo sukari haionekani tena imechanganika kabisa na maji. Ikiwa maji ni baridi, sukari itachukua mda mrefu sana kuchanganyaki kulinganisha na maji ya moto au vuguvugu.

Hivi ndivyo inatokea katika ghuba kule Alaska ambapo maji yote ni baridi na majimyeyuko kutoka barafu yenye chumvi ndogo sana inachukua muda mrefu sana kuchanganyika na maji ya ghuba yenye chumvi ya asilimia mpaka 3.5

Je, huu ni muujiza au ni sayansi ya kawaida tu?

Ndio maana naendelea kusema Allah sio Mungu.

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW