Wednesday, May 16, 2018

JE, UNABII KUHUSU MJI MTAKATIFU WA YERUSALEM UNATIMIA BAADA YA MAREKANI KUWEKA UBALOZI WAKE YERUSALEM, MJI MKUU WA ISRAEL?

Image may contain: text


Kwanza tuanze na mwaka wa 1948 May 14 ambao Israel ilitanganzwa kuwa taifa. Ukiangalia haraka haraka utagundua kuwa tarehe 14 Mwezi May 1948 na tarehe 14 Mwezi May 2018 siku ambayo Marekani imefungua Ubalozi wake Jerusalem ni miaka 70 [2018-1948 = 70].
Je, miaka 70 maana yake nini Kibilia?
NAMBA 7
Biblia ina mifano mingi ambapo namba saba imetumiwa kwa njia hiyohiyo. (Mambo ya Walawi 4:6; 25:8; 26:18; Zaburi 119:164; Ufunuo 1:20; 13:1; 17:10) Yesu alipomwambia Petro kwamba amsamehe ndugu yake “si, Mpaka mara 7, bali, Mpaka mara 70,” kurudia namba 7 kulionyesha kwamba alipaswa kuendelea kusamehe “bila kuacha”.—Mathayo 18:21, 22.
Namba 7 inatumika sana kwenye Biblia katika maana ya Ukamilifu wa Ki Mungu. Ukiomba kitu chochote katika Mungu mara 7 hakika Mungu atakupa jibu. Kwa mfano Ukuta wa Babeli ulidondoka baada waisrael kusunguka mara 6 na mara 7 ukuta kukadondoka. Naamani aliambiwa akajichofye mara saba na baada ya hapo ukoma ukapona kabisa.
NAMBA 10
Namba 10 ni sawa na namba 1 inaweza kuwa 10, 100, 1000, 10000…. Nk. Namba 10 ina maanisha Ukamilifu kamili. Biblia inasema kuhusu sarafu 10 (Luka 15:8), Kondoo 100 (luka 15:4) miaka 1,000 (2Petro 3:8),Vizazi 1000 (Kumbukumbu la Torati 7:9) n.k kwa hiyo kama namba 10 ni alama ya jambo fulani au ina maana fulani kiroho basi ni Ukamilifu. 10 Namba hii inaweza kuwakilisha jumla ya kitu, au kukusanya pamoja.—Kutoka 34:28; Luka 19:13; Ufunuo 2:10.
Hivyobasi, Miaka 70 [7 x 10] inamaana ni ukamili usio kuwa na mwisho. Ikimaanisha Yerusalem ni Mji Mkuu wa Israel milele yote.
UNABII WA KWANZA:
“Kwa sababu [Waisraeli] hamkuyatii maneno yangu [Mungu], tazama, ninatuma . . . Nebukadreza mfalme wa Babiloni, . . . , nami nitawaleta wao [Wababiloni] juu ya nchi hii na juu ya wakaaji wake . . . Na nchi hii yote itakuwa mahali palipoharibiwa, kitu cha kushangaza, na mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babiloni miaka 70.”—Yeremia 25:8-11.
UTIMIZO:
Baada ya kulizingira jiji hilo kwa muda mrefu, Nebukadneza alilipora na kuliharibu Yerusalemu katika mwaka 607 K.W.K. Pia aliyashinda majiji mengine ya Yudea, kutia ndani Lakishi na Azeka. (Yeremia 34:6, 7) Aliwahamisha waokokaji wengi na kuwapeleka Babiloni ambako walikaa wakiwa mateka kwa miaka 70.
Historia inafunua nini?
● Biblia inaonyesha kwamba Nebukadneza ndiye aliyekuwa mfalme wa Babiloni karibu na wakati ambapo Yerusalemu liliharibiwa. Vitu vya kale vilivyochimbuliwa vinaunga mkono kile ambacho Biblia inasema kuhusu kuwapo kwake. Jiwe fulani la shohamu lililo na mchongo limewekwa huko Florence, Italia. Sehemu fulani ya maandishi yaliyo juu ya jiwe hilo yanasema hivi: “Kwa heshima ya Merodaki, bwana wake, Nebukadneza, mfalme wa Babiloni, alipokuwa hai aliagiza hili lijengwe.” Nebukadneza alitawala kuanzia mwaka wa 624 hadi 582 K.W.K.
● Kitabu The Bible and Archaeology kinasema kwamba mambo yafuatayo yamethibitishwa baada ya eneo la Lakishi kuchimbuliwa na kufanyiwa uchunguzi: “Uharibifu wa mwisho ulikuwa wenye jeuri, na moto ulioharibu jiji [Lakishi] ulikuwa mkali sana hivi kwamba mawe ya chokaa yaligeuzwa kuwa ungaunga wa chokaa.”
UNABII WA PILI:
“Kupatana na kutimia kwa miaka 70 katika Babiloni [mimi Mungu] nitawakazia ninyi fikira [Wayahudi walio uhamishoni], nami nitawatimizia neno langu jema kwa kuwarudisha tena mahali hapa [nchi ya Yuda].”—Yeremia 29:10.
UTIMIZO:
Baada ya miaka 70 ya uhamisho, kuanzia 607 hadi 537 K.W.K., Mfalme Koreshi wa Uajemi aliwaachilia Wayahudi waliokuwa utekwani na kuwaruhusu warudi nyumbani kwao ili wakajenge upya hekalu huko Yerusalemu.—Ezra 1:2-4.
Historia inafunua nini?
● Je, Waisraeli waliendelea kuwa mateka Babiloni kwa miaka 70 kama Biblia ilivyotabiri? Hebu ona maelezo ya Ephraim Stern, ambaye ni mmoja wa wataalamu wakuu wa wachimbuaji wa vitu vya kale nchini Israel. “Kuanzia mwaka wa 604 K.W.K. hadi 538 K.W.K.—hakuna uthibitisho unaoonyesha kuwa kuna mtu aliyeishi nchini Israeli. Wakati huo, hakuna hata mji mmoja ulioharibiwa na Wababiloni unaoonekana kuwa ulikuwa na watu.” Kipindi hicho ambacho hakukuwa na mtu katika eneo lililoshindwa kinapatana sana na uhamisho wa Waisraeli kupelekwa Babiloni kuanzia 607 hadi 537 K.W.K.—2 Mambo ya Nyakati 36:20, 21.
Baada ya utawala wa Sulemani, taifa la Israeli likagawanyika sehemu mbili. Makabila kumi ya kaskazini waliitwa "Israel," na wao walidumu miaka 200 kabla ya hukumu ya Mungu kwa ajili ya ibada yao. Asiria ikatwaa Israeli kama watumwa karibu 721 BC. Makabila mawili katika kusini yaliitwa "Yuda," na wao walidumu muda mrefu kidogo, lakini hatimaye, pia, wakageuka kutoka kwa Mungu. Babeli aliwachukua mateka 600 BC
Miaka 70 baadaye, Mungu kwa neema aliwaleta mabaki ya wafungwa nyumbani kwa nchi yao wenyewe. Yerusalemu, mji mkuu, ulijengwa upya karibu 444 BC, na Israeli kwa mara nyingine tena ikawa na urahia wa taifa.
Kubomolewa kwa hekalu: Yesu alisema katika Mathayo 24:2, "...amin, amin nawaambieni, halitasalia hapa jiwe ambalo halitabomoshwa". Hii ni baada ya wanafunzi wake kumuonesha mawe ya hekalu na misingi yake ilivyo imara. Hekalu lilikuja kubomolewa miaka 70 AD. Na sasa eneo hilo lilipokuwepo hekalu limejengwa msikiti.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW