Friday, May 11, 2018

ALLAH HAKUMUUMBA IBILISI BALI YEYE NI IBILISI


Tuanze na madai ya Allah ya kumhukumu Ibilisi kuhusu kumsujudia Adam.
Surat Al Baqara 34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Ibilis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.
Allah anadai kuwa Ibilisi alipo ambiwa amsujudie Adam alikataa. Je, Ibilisi alikosea kukataa kumsujudia Adam? Je, Ibilisi ni Malaika kutokana na Quran?
Kumbuka Allah kawaamrisha Malaika wamsujudie Adam.
Surat Al Araaf 11. Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.
12. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.
Ibilisi anamjibu Allah kuwa mimi umeniumba kwa moto, ndio maana sikumsujudia Adam. Je, Malaika waliumbwa kwa moto kama Ibilisi?
Uislam unadai kuwa: Malaika waliumbwa kwa mwanga.
Nabii wa Allah alisema: Malaika waliumbwa kutoka mwanga, kama ambavyo majini yaliumbwa kutoka moto usio na moshi na binadamu aliumbwa kama mlivyo fundishwa. Sahih Muslim
MASWALI:
1. Kwanini Allah alimhukumu Ibilisi huku akijua kuwa alio waamrisha wamsujudie Adam ni Malaika?
2. Je, Ibilisi sasa ni Malaika na aliumbwa kwa mwanga?
3. Kama Allah ni Mungu, kwanini asahau kuwa Ibilisi sio Malaika?
HAKIKA ALLAH SIO MUNGU
Imesimuliwa na Anas Ibn Malik, "Nilimsikia Nabii wa Allah akisema: Allah ni Shaitwan aliye katika umbo la Malaika na alinifunulia aya zake na kitabu chake ni Quran, na mimi ni mtume wake. ( Umdah Al - Ahkaam : Volume 3, Page 460 )
رواه أنس ابن مالك : " سمعت من رسول الله صلى الله عليه وسلم أنه قال " كان الله هو شيطان في شكل ملاك كشف لي الآيات وكتابه القرآن وأنا نبي له . (عمدة الأحكام المجلد 3، الصفحة 460)
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kriso Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW