Una njaa? Si njaa ya chakula, lakini je, una njaa ya kitu Fulani zaidi maishani? Je, kuna hali Fulani ya kutotosheka ndani yako? Ikiwa iko basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mkate wa kweli. Kila ajaye kwangu hatahisi njaa na aniaminiye hataona kiu” (Yohana 6:35).
Je, umechanganyikiwa? Je, huoni mbele ya maishani mwako? Je, unajihisi kama umeachwa kwenye giza na huoni pa kutokea? Ikiwa hali yako ni kama hiyo basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu. Anifuataye hatatembea gizani, bali atakuwa na nuru ya uzima” (Yohana 8:12).
Je, unajisikia kama umefungiwa nje ya maisha yako? Je, umejaribu njia nyingi na kutambua ya kwamba kile ulichokitarajia hakipo ndani yake? Je, unatafuta njia ya kufikia maisha makamilifu? Ikiwa haya ndiyo uyatafutayo, Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mlango wa kondoo; aingiaye kupitia mimi ataokolewa. Ataingia na kutoka na kupata malisho” (Yohana 10:9).
Je, watu wengine husababisha kushindwa kwako? Je, uhusiano wako nao umekuwa si wa kina na bila muelekeo? Je, ni kama watu wanakutumia tu kwa manufaa yao? Ikiwa ndiyo hali unayopitia Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema hutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo……. Mimi ndimi mchungaji mwema; Ninajua kondoo wangu na kondoo wangu wananijua” (Yohana 10: 11,14).
Je, unashangazwa na kinachotendeka baada ya maisha haya? Je, umechoshwa na maisha ya kupigania tu vitu vinavyooza na kushika kutu? Je, wakati mwingine maana ya maisha yako huionea shaka? Je, unataka kuishi hata baadaya kufa? Ikiwa haya ndiyo uliyonayo basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Aniaminiye ataishi, hata ajapokufa; na aishiye na kuniamini hata kufa kamwe” (Yohana11:25-26).
Njia ni nini? Ukweli ni nini? Uzima ni nini? Yesu akajibu, “Mimi ndimi njia kweli na uzima.Hakuna afikaye kwa baba bila kupitia kwangu” (Yohana 14:6).
.jpg)