UTANGULIZI
Imekuwa ni kawaida sasa kwa
miaka zaidi ya ishirini hivi, kusikia katika mihadhara inayoendeshwa na
wahadhiri wa dini ya Uislamu, ambayo imeenea sehemu mbalimbali Duniani na haswa
katika nchi za Africa Mashariki na Kati,(East and Central Africa). Wahadhiri
hao hufundisha jamii kupitia Qurani na Biblia kwa kusema kuwa Mungu ni Mmoja
tu. Wasema Mungu kwa Kiebrania anaitwa Yehova , kwa Kiarabu Allah, kwa
Kiingereza God na kwa Kiswahili ni Mungu. Kwa hivyo wasema Mungu Allah kama
Qurani inavyofundisha, ndiye Yehova kama Biblia inavyofundisha. Mihadhara hiyo
inayoendeshwa na Waislamu imeenea sana, mfano Nchini Tanzania kuna vikundi
vingi na kimoja wapo kinaitwa Al-Marid International Propagation Center. Hawa
wameandika katika bango lao kwa kunukuu katika Biblia maneno aliyoandika Mtume
Paulo katika Waefeso 4:4-6. Maneno waliyoyanukuu yanasema hivi “Bwana mmoja ,
Imani moja ….., Mungu mmoja , naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote.
Nilipotembelea mkoa wa Morogoro pale mjini, eneo la kiwanja cha ndege nikaona
Msikiti mmoja umeandikwa maneno haya ya Waefeso 4:4-6. Na nilipotembelea mji wa
Nairobi Nchini Kenya pia nikaona kuna vikundi vingi vinavyoendesha mihadhara na
kikundi kimoja wapo kinaitwa Kibera Islamic Propagation Centre. Hawa nao katika
bango lao wameandika ujumbe unaosema hivi “Acha Biblia Ijisemee na kunukuu
injili aya hii” Yohana 8:32 Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka
huru.
Kwa hivyo utaona kuwa
wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia
na kusema Allah Sub-Hana Wataala ndiye YEHOVA. Fundisho hili wanalieneza kwa
kupitia Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na
Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika
Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingawa hawajabadili dini
wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila mkristo, je, ni kweli
Mungu Allah kama inavyotuhadithia Qurani ndiye Yehova kama Biblia
inavyotufundisha? Nakusihi fuatilia somo hili kwa makini ili kujua Ukweli……
SEHEMU KUU ZA SOMO HILI NI
HIZI……
1. Hoja za waislamu kusema
Allah ndiye Yehova.
2. Je, jina la Mungu kadiri
ya Qurani na Biblia ni moja?
3. Je, Malaika mkuu wa
Allah ndiye wa Yehova?
4. Je, ni nani muumba,Allah
au Yehova?
5. Mji aliochagua Allah je,
ni sawa na wa Yehova?
6. Allah anavyofundisha
kuhusu kujitakasa nafsi je, ni sawa na Yehova?
7. Je, mbingu ya Yehova ni
sawa na ya Allah?
8. Mwisho wa wanaomwabudu
Allah ni wapi?
1. Hoja za waislamu kusema
Allah ndiye Yehova
Wahadhiri wa Dini ya
Uislamu wanasema Mungu Allah ndiye Yehova kwa sababu Manabii wa Mungu kadiri ya
Biblia na Qurani walifundisha kwa kusema Mungu ni mmoja tu. Na wanasoma aya
hizi…
Nabii Musa alivyosema
Kumbukumbu la Torati 6:4
Sikiza ee Israeli; BWANA
Mungu wetu BWANA ndiye mmoja.
Nabii Isaya alisema hivi
Isaya 45:18,21
Maana BWANA , aliyeumba
mbingu, asema hivi, yeye ni Mungu ,ndiye aliyeumba Dunia na kuifanya ….. si
mimi BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi. Mungu mwenye haki , mwokozi hapana
mwingine zaidi ya mimi.
Nabii Daudi Alisema
Zaburi 86:10
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,
wewe ndiwe mfanya miujiza , ndiwe Mungu peke yako.