UTATA MKUBWA KATIKA KORAN
NANI ALIKUWA MUISLAM WA KWANZA?
Ndugu zanguni:
Leo ningependa tuangalie kiundani kidogo kuhusu, “nani
alikuwa Muislam wa Kwanza” kutokana na Koran iliyo teremshwa na Allah.
Kwa mujibu wa vifungu kadhaa katika Quran, Muhammad
ni Muislamu kwanza :
Quran 6: 14. Sema: Je, nimchukue rafiki
mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye
ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa
wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. 161. Sema:
Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini
iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala
hakuwa miongoni mwa washirikina. 162. Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na
kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. 163. Hana
mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. (Wa ' Ana '
Awwalu Al- Muslimin ). S. 6:161-163
Sema (Ewe Muhammad): Hakika Mimi nimeamrishwa
nimuabudu Mwenyezi Mungu, kwa kumsafishia Dini Yeye ( tu ). Na nimeamrishwa
niwe wa kwanza wa wale ambao ni Waislamu ( kujisalimisha kwake ). S. 39:11-12
Pickthall
Sura hizo hapo juu na aya hizo ulizo zisoma
zinapingana vibaya sana na sura zingine katika Koran hiyo hiyo ambazo
ziliteremshwa na Allah huyo huyo na kusema Manabii walio tangulia kabla ya
Muhammad ndio walikuwa Waislam wa Kwanza.
Kuran inadai kwamba Adam, Ibrahim, Nuhu, mababu,
makabila kumi na mawili ya Israeli, Musa, Yesu nk, hao wote walikuwa waumini wa
Allah na walikuwa Waislam, kumbuka hao wote waliishi kabla ya Muhammad ambaye
anadai kuwa yeye ni Muislam wa Kwanza:
S.
02:30 , 34-35 , 37
30. Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia
Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo
atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa
zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo
yajua. 34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote
isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri. 35. Na
tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa
popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio
dhulumu. 37. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola
wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi
wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. S. 02:30 , 34-35 , 37
163. Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe
kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na
tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na
Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi. S. 4:163
84. Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na
Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi
chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi
ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema: S. 6:84
127. Na
kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe
Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi. 128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe
ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu
kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 129. Ewe
Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na
awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu,
Mwenye hikima. 130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia
nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na
hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema 131.
Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea
kwa Mola wa walimwengu wote. 132. Na
Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu
amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. 133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub
mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu
Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu,
na sisi tunasilimu kwake. S. 2:127-133 Shakir




