Biblia inatueleza kuhusu hii dhambi kuwa ni kitu gani. Inafafanua kuwa dhambi ni “uasi au kuvunja sheria” (1Yohana 3:4). Dhambi ni msukumo wenye nguvu ambao unatufanya sisi tupende kuziendea njia ambazo ni kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo, badala ya kubarikiwa kwa kuyafuata mapenzi ya Mungu, tunaadhibiwa kama tutaishi kwa kuzifuata na kuishi kwa kufuata tamaa za Shetani, ambazo ndizo dhambi. Njia na matendo ya Shetani ni kinyume kabisa na zile za Mungu. Mungu anazichukia dhambi (Mithali 6:16-19). atendaye dhambi ni wa Ibilisi; (au Shetani) kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. (1Yohana 3:8).
Mkristo anakailiwa na mapambano yasiyo na mwisho kwenye maisha yake ya kila siku katika kukabiliana na kuzishinda dhambi. Inatupasa kuwa washindi kama tutaweza kujipatia ukamilifu wa tabia na mwenendo mtakatifu na wa haki. Shetani anapenda na kututaka sisi kuidharau Torati au Sheria za Mungu. Kwa hiyo, kama tutashindwa na kukata tamaa kwenye harakati zetu za kupambana na dhambi, basi Shetani atashinda.
Je, kuna dhambi nyingine zilizo kubwa kuliko nyingine?
Baadhi ya makanisa yanayojiita yenyewe kuwa ya Kikristo yanafundisha kwamba kuna dhambi za mauti na zisizo za mauti. Wanasema kwamba baadhi ya dhambi ni mbaya au kubwa zaidi ya nyingine na kwa hiyo wazitendao wanastahili kuadhibiwa kwa adhabu kali zaidi. Wanasema kuwa dhambi za mauti ndizo zinawapelekea kwenda jehanamu na dhambi nyingine za kawaida zinasameheka kirahisi na huenda baada ya muda mfupi akiwa huko Pargatory mtu azitendaye dhambi hizi zisizo za mauti anaweza kusamehewa na kwenda Mbinguni. Dhana hii inatokana na neno lililotumiwa na mtume Paulo kuhusu ukweli kwamba kuna dhambi ambazo zinampelekea mtu kuingia mautini. Hata hivyo, dhana au wazo ama fundisho la mtu kwenda Mbinguni na Kuzimuni akiwa na roho isiyokufa anapokufa mauti sio fundisho la Kikristo.
Dhana na fundisho la watu kwenda ama Mbinguni au Jehanamu wanapokufa linatokana na mafundisho ya imani za kipagani. Neno litumikalo kuelezea Kuzimuni ni Sheol, na linamaanisha kaburini ambako wafu huzikiwa. Hades lilikuwa ni neno la Kiyunani lililotumiwa kwa Kiebrania, ambalo pia linamaanisha kaburi. Neno la tatu lililotafsiriwa kama kuzimu kwenye Biblia ni Jehanamu [Gehenna], ambayo ilikuwa ni shimo la takataka au jalala lililokuwa nje ya mji wa Yerusalemu ambapo walipatumia kwa matumizi ya kuwachomea au kuwateketeza mbwa na takataka nyingine. Neno linguine lililotumika kwenye Biblia ni tartaros au tartaroo, ambalo lilikuwa ni shimo lililobakizwa kwa ajili ya malaika wakati watakapofungwa humo. Hakuna kitu kama hicho kwenye maandiko kijulikanacho kama kuchomwa na kuunguzwa moto milele kwenye Jehenamu.
Mtume Yohana anasema hapa kuwa kuna dhambi zisizo za mauti. Hii inamaanisha tu kwamba ni dhambi tunazozitenda au tunazokabiliana nazo wakati tunaposhughulika na shughuli zetu za kila siku. Hata hivyo, kwa njia ya toba tunawekwa huru kutokana na dhambi hizi na tunaruhusiwa kubakia kwenye Mwili wa Kristo na kwenye Ufufuo wa Kwanza wa Wafu ulioelezwa kwenye Ufunuo 20. Wale wanaotenda dhambi kwa makusudi watakwenda kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu. Hata hivyo, kila aliyezaliwa na Mungu hawezi kutenda dhambi (1Yohana 3:9).
Dhambi ya Lusifa
Wakati Mungu alipoumba viumbe wa kiroho aliwaumba wakiwa wakamilifu. Sheria au Torati ya Mungu pia ailikuwpo tangu mwanzoni. Lakini ni kama tunavyoweza kufanya maamuzi mema na mabaya na ndivyo ilivyo hata kwa hawa viumbe wa kiroho nao hufana vivyohivyo. Mungu hahitaji wanadamu au viumbe hawa wa kiroho wanaoendelesha na kufanya mambo yao kama maroboti. Bali Mungu anawataka viumbe hawa wote wawili, yaani wa kiroho na wa kimwili wanaopenda kutii Sheria na amri zake kutoka mioyoni mwao na sio tu kwa sababu wanalazimishwa kufana hivyo.
.jpg)


