Thursday, January 14, 2016

MAJINI NI MAISLAM


MAJINI KATIKA DINI YA KIISLAM ( Q 72:1-14 )

1. QURAN INASEMA KUWA MAJINI YANAZALIANA NA KUFA KAMA BINADAMU 2. ALLAH AYARUHUSU MAJINI KUZAA NA BINADAMU 3. QURAN INAKIRI KUWA MAJINI NI MAISLAM NA YALISILIMU PALE QURAN ILIPO TEREMSHWA KWA MUHAMMAD. 4. MAJINI YANAMWABUDU ALLAH 5. KILA MUISLAM AMEPAGAWA NA MAJINI KATIKA MWILI WAKE


Leo ningependa tujifunze kidogo kuhusu Majini au Mashetani katika Uislam.

JINI NI NINI?

Katika lugha ya kiarabu, neno Jini linamaanisha kitu kilichofichwa au kisichoonekana QURAN 1:71 Neno hili hutumiwa na Waarabu kwa ajili ya kutaja jina fulani. Kwa Waarabu, Jini anayevaa sura ya kike humwita Jinivya, hivyo majini Ghul/Ghilan, nao hujifunua kwa sura ya kike.

Katika imani ya Kiislamu, wao huamni kwamba Majini hutofautiana na Mashetani. Majini waliosilimu wao huitwa majini mazuri na hawa wakiwa katika hali kujionyesha kwa wanadamu, hao huitwa AJINU na wale walioacha kusilimu mwaka 610 AD (Baada ya Kristo) katika safari ya mtume Muhamad alipotoka Taif , wao wanaitwa Mashetani . Hivyo, wao wanapokuwa katika hali ya kutoonekana huitwa ALBAHATWA lakini pia Majini wote wanapokuwa katika hali ya kutoonekana waweza kuitwa ALBAHATWA, yaani PEPO.

QURAN INASEMA KUWA MAJINI YANAZALIANA NA KUFA KAMA BINADAMU

Muislamu huamini kwamba kuna majini ya kike na kiume. Lakini pia , huamini kuwa Majini huoana na kuzaliana QURAN 55:56 na kuwa Majini huzaa sana kuliko binadamu na kwamba, Jini mmoja anaweza kuzaa watoto 300, na kuwa Jini huzaa watoto 3 hadi 4 kwa mkupuo. Somo QURAN 55:26-28 na kuwa Majini wanaweza kuishi miaka 400-1,000 kisha wanaweza kufa. Tofauti yao na binadamu ni kwamba wao wanaishi miaka mingi kuliko binadamu. Lakini pia, huamini kuwa wapo Majini wanaokula, wanaomeza, wanaokunywa, ila tofauti yao na wanadamu ni kwamba wao hula kwa kutumia mkono wa kushoto.

ALLAH AYARUHUSU MAJINI YANAZAA NA BINADAMU

Pia hiamini kuwa Majini wana uwezo wa kuzaa na Wanadamu. Soma QURAN 17:64. Waislamu huamini kwamba mtu anauwezo wa kuoa au kuolewa na Jini bila kujua, na mwanadamu anauwezo wa kumuua Jini. Soma QURAN 57:14-15

SURATULJINN
Ndani ya QURAN pia imo sura inayoitwa Suratuljinn (QURAN 72). Sura hiyo huitwa hivyo kwa sababu ni sura ya Majini (Mapepo).

Kwa nini wanatajwa Majini katika imani ya Kiislamu?

QURAN INAKIRI KUWA MAJINI NI MAISLAM NA YALISILIMU PALE QURAN ILIPO TEREMSHWA KWA MUHAMMAD.

Majini wanatajwa sana katika dini ya Kiislamu kwa kuwa ni waislam kwa kusilimu, kwa kuiamini Quran tukufu aliyopewa mtume Muhamad.

Majini walisilimu na kuwa Waislamu mwaka 610 AD(Baada ya Yesu) SOMA 72:1-14 QURAN. Hivyo basi, unapotumia neon jinni maana yake unatumia lugha ya Kiarabu ukimaanisha Pepo mchafu. Ni kama Spoon/kijiko, vyote ni kitu kimoja. Ndani ya Quran, neon “PEPO” limetumika kama Paradiso, mbinguni. Lakini pia, tunapata neon jingine liitwalo AKHERA ila neno hilo halimaanishi PARADISO, bali kwa lugha ya Kiarabu neno hili “AKHERA” lina maana ya KUZIMU.

Lakini pia ukiangalia ndani ya SURALJINN ( QURAN 72:1-2, 8-9, 12 ) Mapepo hawa wanajieleza waziwazi kabisa kuwa mwanzo waliishi Mbinguni, walipogeuka kwa kuasi, walitegwa na Mungu. Linganisha na maandiko haya katika Biblia ( UFUNUO WA YOHANA 12:7-9; YUDA 1:6-8; UFUNUO 20:10; UFUNUO 21:8 ). Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, hawa majini ( Mapepo ) waliotegwa na Mungu Mbinguni wakiwa Malaika huko na kutupwa Duniani baada ya kuasi huko, sasa, wakati wa mtume Muhamad katika safari yake ya kurudi Taif mwaka 620 AD (baada ya Yesu) wapo walioamini na kuona kuwa Quran ni ya ajabu ya kuwatangazia neema ya kuabudu. Katika vol 8-9, husema , wanapojaribu kwenda Mbinguni ( walikotoka zamani ), hukuta ile Mbingu imezungushiwa vimondo vya moto. Hivyo, hudai kuwa mbingu yao iko Akhera, yaani Kuzimu, maana Mbingu ya juu ina moto na hawana uwezo wa kwenda huko. SOMA (QURAN 72:9), Mbingu ina utisho wa moto ila Akhera ( kuzimu ) hakuna shida kwao.

MAJINI YANAMWABUDU ALLAH

Hivyo basi, kulingana na jinsi Allah asemavyo ndani ya Quran kuwa nimeumba binadamu na majini ili muniabudu ( QURAN 57:58 ; 51:56) na kuwa , mbinguni mwao Majini wanaabudu (Majini waliosilimu mwaka 620 AD) ,SOMA QURAN 72:14, ambao ni wema wanaosafiri na kurithi uzima wa milele upatikanao Akhera ( Kuzimu ). Lengo kubwa la Shetani na Majini ni kufanya urafiki na wanadamu wengi ili kwa wingi huo apate watu wengi wa kwenda nao JEHANAMU ( QURAN 6:128 ). Jambo la muhimu kujua hapa ni kwamba moto wa milele hakuwekewa Mwanadamu bali ni Shetani na malaika zake wote ( Majini au mapepo ). Hawa, hawana nafasi tena ya kuungama au kutubu.

Yesu Kristo anayetambuliwa na Waislam kama Mtume tu, hakuwa na urafiki wowote na Shetani wala Mapepo ( Majini ). Aliyaamuru Majini kutoka ndani ya watu waliokuwa wakiteswa nayo ( MATHAYO 8:29: MARKO 5 N,K )

Wakati Yesu anaondoka hapa duniani, alichukuliwa na wingu na kupaa kuelekea juu. Mbinguni ni juu kama Quran inavyothibitisha. Yesu aliweza kupaa na kuingia Mbinguni lakini Majini ( Mapepo ) walioslimu wakijaribu tu, wanakutana na moto mkali. Tumeona kuwa Majini ambao ni Waislamu kwa kusilimu, wanaishi AKHERA yaani Kuzimu. Je, Waislamu wengine unadhani wataishia wapi milele? Katika imani ya Kiislam huamini kuwa, Muislam akifa anakuwa na Majini wawili wa Kumlinda humo Kaburini.

KILA MUISLAM ANA JINI KATIKA MWILI WAKE

Majini wamepewa ruhusa ya kukaa katika mwili wa Muislam yeyote, hivyo kila Muislam ana Jini kuanzia moja na kuendelea. Vile vile Majini wameruhusiwa kukaa katika nyumba za Waislam. Katika nyumba yoyote ya Muumini wa dini hiyo, kuna Jini au Majini wanaokaa humo. Ni ukweli usiopingika kuwa bila Majini hakuna Uislamu kama vile pasipo Roho Mtakatifu hakuna Ukristo. Majini ndiyo yaliyomchukua mtume Muhamad kwa muda wa siku 40 akiwa Mabondeni walikompeleka na kuanza kumuagiza kuhusiana na kuanzisha imani hiyo ya Kiislamu.

USHAURI WANGU KWA WA WAKRISTO:

Ushauri wangu wa bure kwa Mkristo ni huu, USIMUACHE KAMWE KRISTO NA KUINGIA KATIKA IMANI ZA MASHETANI (1TIMOTHEO 4:1-2 ).

Majini au Mashetani ni kitui kimoja na wala hakuna tofauti yao. Wote hao Mashetani/Majini yalimpinga Mungu na kutupwa duniani. Biblia inasema kuwa Hakuna Msamaha kwa Majini maana wao walisha hukumiwa na wanacho subiri ni kutupwa Jehannam.

Shetani bado ni “mfalme wa nguvu za anga” (Waefeso 2:2). Hii inamaanisha kwamba Shetani na Malaika wengine walioasi wanaweza kushawishi mia zetu na mawazo yetu kupitia miziki, runinga, mijadala, nk. Tumeambiwa kujihadhari katika mawazo na nia zetu (2Wakorintho 10:3-5). 2Wakorintho 4:4 inatuambia kuwa mungu wa dunia hii amepofusha mawazo ya watu ili wasiamini.

Shetani ndiye yuko nyuma ya dini zote za uongo na dini za dunia. Shetani atafanya na kila kitu katika uwezo wake ili ampinge Mungu na wale wote wanaomfuata. Ingawa hatima ya Shetani imewekwa muhuri kuwa tanuru la moto milele (Ufunuo Wa Yohana 20:10).

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba Ministries Org.

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Wednesday, January 13, 2016

WAISLAM WANAULIZA: JE, ALIYE TAJWA KWENYE KUMBUKUMBU YA TORATI NI MUHAMMAD AU YESU?



Swali: Katika Kumbukumbu 18:17-18; 33:1-2, na 34:10-11, ni Muhammad aliyetabiriwa hapa, kama baadhi ya Waislam wanavyodai?Jibu: Kumbukumbu 18:15-18 inasema Mungu atamwinua nabii, kuwa watamsikia, kama Musa kutoka miongoni mwao, miongoni mwa ndugu zao.

Je Yesu alikuwa nabii?
Je Wayahudi walio wengi walimsikia Yesu?
Je Yesu alikuwa mmoja wa Wayahudi?
Je Yesu alikuwa Myahudi?

Waislam wanapaswa kutokuwa na shida kuafiki kuwa mistari hii inamfaa Yesu kuliko Muhammad. Kama angalizo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) pia alizungumzia jinsi ambavyo Kumbukumbu 18:15 isivyoweza kuwa inamwongelea mtu mwingine yoyote yule isipokuwa Yesu Kristo kwenye Disputation with Manes sura ya 43 uk.219.Yafuatayo ni maoni zaidi.

a. Kumbukumbu 33:1-2 inasema "Bwana", na Waislam hawamwiti Muhammad Bwana wao. (Waislam wa ‘Alawite na makundi mengine ya Ghulat wanamchukulia Muhammad kuwa Mungu, lakini maoni hayo siyo kawaida kwa Waislam.)

b. Kumbukumbu 34:10 kwamba "Wala hakuinuka tena katika Israeli nabii kama Musa." Wasifu huu uliandikwa, huenda na Yoshua, muda mrefu kabla Yesu hajaja.

c. Kumbukumbu 34:10 inasema "uso kwa uso", na Muhammad hajawahi kusema kuwa alipata maneno yake moja mwa moja kutoka kwa Mungu, bali kupitia malaika (Sura 2:97). Yesu aliwasiliana moja kwa moja na Mungu Baba kwa mujibu wa Yohana 1:18 na vifungu vingine.

d. Mstari unaofuatia, 34:11, unasema kuwa hakuna nabii mwingine yoyote aliyefanya miujiza hiyo mikubwa kama Musa.

Muhammad, kama ilivyoandikwa kwenye Kurani (Sura 17:90-93) hakuwahi kufanya miujiza kama hii, isipokuwa kusema Kurani. (Kurani inapingana na jinsi mapokeo ya baadaye ya Hadithi yanavyosema.)

e. Kwenye Kurani yenyewe, Sura 29:27 inasema unabii umekuja kupitia Isaka na Yakobo. Kwenye tafsiri ya Yusuf Ali ya Kurani, anasema, "Na tumewapa (Abraham) Isaka na Yakobo, na tumeagiza miongoni mwa wazao wake unabii na ufunuo . . ."

Wakati ambapo mabano kwenye jina la Abraham yapo kwenye tafsiri ya Yusuf Ali, neno lote "Abraham" halimo kwenye Kurani ya Kiarabu, na Yusuf Ali aliona haja ya kuongeza neno "Abraham" kwenye maandiko ambayo Waislam wanayaona kuwa ni neno la Mungu.

f. Mwisho, Petro, mtume wa Yesu, alisema andiko hili lilitimia kwa Yesu kwenye Matendo 3:22-26. Mtume Petro alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kujua jambo hili.

1. Ama, Yesu alifanya makosa ya kumruhusu mtu mwongo kama Petro kuwapotosha watu, kwa kwa karibu miaka 2,000, ambao wamekuwa wakijaribu kumfuata Mungu, na Mungu hakuinua kidole kuwaambia watu ukweli.
2. Au, Yesu alijua alichokuwa anafanya wakati alipomchagua Petro, na Mungu hakusahihisha kitu ambacho hakikihitaji masahihisho yoyote yale.
3. Vinginevyo, Petro hakusema hivyo, na kitabu cha Matendo ya Mitume kilipotoshwa kabla ya maelezo ya maneno hayo ya kwanza tuliyo nayo toka nje ya Biblia yanayoturejesha kwa Yesu, karibu mwaka 138 B.K.

Viongozi wa awali wa kanisa walisema kuwa mstari huu ulimwongelea Yesu. Baadhi yao ni
Justin Martyr 138-165 B.K.
Irenaeus 182-188 B.K.
Tertullian 220-220 B.K.
Origen 225-254 B.K.
Chrysostom 407 B.K.

Justin Martyr alizaliwa karibu mwaka 114 B.K., ingawa watu wengine hudhani mwaka 110 B.K. Apology yake ya kwanza iliandikwa kati ya mwaka 138 B.K. na mwaka 165 B.K. wakati wa kifo chake. Ni dhahiri kuwa alitakiwa kusoma unabii huu unaomwongelea Yesu kabla ya kuandika.

Muislam anaweza kusema kuwa Justin hakukosea tu bali pia manuscripts zote za Agano Jipya ziliunukuu usemi wa Petro kimakosa.

Pia, tafsiri kwenye lugha nyingine zilifanywa mapema sana; tarehe za hapo juu si za tafsiri za kwanza, bali ni tarehe za manuscripts za zamani zaidi ambazo zipo leo hii.
Hizi zinaaminika kwa sababu zimepita kwenye mtiririko huru ambao watu wanaweza kuutumia kuthibitisha manuscripts za Kiyunani.

Mtiririko wote wa manuscripts hizi, kutoka Afrika kwenda Asia, unaafiki kuwa Petro alisema hivi akimwongelea Yesu.

Tazama When Cultists Ask uk.43-44,45-46 na When Critics Ask uk.125-126, uk.131-132, na uk.133 kwa habari zaidi.Mungu awabariki sana

Max Shimba Ministries Org

KATIKA TAURAT, ZABURI, INJILI HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM

KATIKA TAURAT YA MUSA, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM
KATIKA INJIL YA YESU, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM
KATIKA ZABURI YA DAUDI, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM.

A. Kwanini Waislam wanadai eti Musa alikuwa Muislam, wakati Taurat iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?

B. Kwanini Waislam wanadai eti Yesu alikuwa Muislam, wakati Injili iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?

C. Kwanini Waislam wanadai eti Daudi alikuwa Muislam, wakati Zaburi iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?

Kama Waislam wanabisha, nionyesheni ipo wapi Taurat aliyo iteremsha Allah kwa Musa tuione? Na iwe na aya inayosema kuwa Musa alikuwa Muislam.

Quran inasema kuwa Allah ameitunza Taurat na Injil katika Surah 15 aya 9. Vile vile tunasoma kuwa Taurat na Injil vinasemwa kama kumbukumbu katika Surah 16:43, 21:7, 21:48, 21:105 na 40:53-54.
Kwahiyo, Surah 15:9 inakubali kuwa Taurat na Injil zimetunzwa na Allah. Kama ni kweli haya madai ya Quran:http://www.quranitukufu.net/005.html

1. Ipo wapi nakala ya Taurat ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
2. Ipo wapi nakala ya Injil ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
3. Ipo wapi nakala ya Zaburi ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?

Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyo teremshwa na Allah kabla ya Quran, na iwe na aya Adam anasema kuwa yeye ni Muislam.

Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyoteremshwa kabla ya Quran, na iwe na aya ambayo Ibrahim anasema kuwa yeye ni Muislam.

Waislam, ipo wapi Taurat ambayo mnadai kuwa Allah aliiteremsha kwa Musa? Mbona kila siku mnatuletea aya za Quran ambazo sio Taurat?

Kama kweli Allah aliteremsha Taurat kwa Musa, basi tuonyesheni wapi ilipo hiyo Taurat na sio aya dhaif za Quran. Hivi Quran sasa imekuwa Biblia - Mkusanyiko wa Vitabu?

Allah anadai kuwa aliteremsha Injil: Surat Al Maida 46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu. http://www.quranitukufu.net/005.html

Waislam, tuonyesheni wapi ilipo nakala ya Injil ambayo Allah anadai kuitunza katika Surat Al Hjr aya ya 9?

Hakika Allah hakuteremsha kitabu chochote kile zaidi ya maneno matupu yaliyo ndani ya Quran ya Jibril.

Allah sio Mungu. Musa hakuwa Muislam, Daudi Hakuwa Muislam, Ibrahim Hakuwa Muislam. Yesu hakuwa Muislam.

Kama kuna Muislam anao ushahid kuwa Musa, Daudi, Ibrahim, Yesu walikuwa Waislam, basi watuonyeshe wapi vilipo vitabu vyao ambavyo Allah anadai kuviteremsha. Waislam, sina muda na aya za Quran zilizo kuja miaka maelfu baadae.

Max Shimba Ministries.

Tuesday, January 12, 2016

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA KUWA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM



1. ALLAH ASEMA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM
2. MUHAMMAD AKIRI KUWA NA YEYE ATAINGIA JEHANNAM
3. ALLAH NA YEYE ANAINGIA JEHANNAM

Jamani huu ni Msiba katika taifa la Islam kwa kushindwa kusoma aya hii ambayo ipo wazi (Quran 40:60) http://www.quranitukufu.net/040.html .

Katika mada hii, nitawawekea aya kutoka Koran na simulizi za Muhammad ambazo zinatushuhudia kuwa, Waislam wote wataingia Jehanamu.

Hebu tumsome kwanza Allah katika aya aliyo iteremsha kwa Mtume wake Muhammad (Pbuh).
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike. http://www.quranitukufu.net/040.html
Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni ili wadhalilike”

Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana katika dini na taifa la Kiislam. Allah amesha toa hukumu kwa wamfuatao na inafahamika fika kuwa, Wale wote waingiao Jehannam, hao walikuwa hawafanyi Mapenzi ya Mungu wa Biblia. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Huu ushaidi ndio tulio usoma katika Quran 40:60. http://www.quranitukufu.net/040.html

Sasa tuwasikilize na maswahiba wa Mtume Muhammad.

Simulizi:Pia imesimuliwa na Ibn Jarir, iliyosimuliwa na Abu Kurayb, imesimuliwa na Ibn Yaman, imesimuliwa na Ibn Malik Maghul, imesimuliwa na Ibn Ishaq ambaye alisema, "Kila mara Abu Maysarah anapo kwenda kulala na akiwa kitandani kwake yeye husema, 'Mimi nasikia Uchungu kuzaliwa na Mama yangu. 'na kisha anaanza kulia kwa Machozi. Alipoulizwa kwa nini alikuwa akilia, alijibu yafuatayo,' Tuliambiwa na Mtume wa Allah kwamba SISI WAISLAMU tutaingia Jehannamu, LAKINI HATUKUAMBIWA kwamba TUTATOLEWAJE HUKO JEHANNAMU NA HATUKUAMBIWA NI KIVIPI TUTATOKA HUKO'"

Mfuasi huyu wa Muhammad anaoneka kupatwa na mshtuko mkubwa, pale alipo ambiwa kuwa, Waislam wote wataingia Jehannam. Mshtuko huu umemfanya ailaani siku ambayo alizaliwa. Kitu cha kujiuliza, kwanini Allah ambaye ni mungu wa Waislam anatoa ahadi ya Jehannam na si Akhera kama wafundishavyo Waislam?

MUHAMMAD NA YEYE AKIRI KUINGIA JEHANNAM"Wamegawanyika Mayahudi katika mapote 71, wakagawanyika Wakristo
katika mapote 72 na Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu)) [Ahmad, Abu Daawuud, atTirmidhiy na ad-Daarimiy]

Kama ushahid unavyo sema hapo juu kuwa Madhehebu yote ya Waislam yataingia Motoni, sasa, ni dhehebu lipi hilo ambalo halita ingia motoni?

JE, ALLAH NA YEYE ATAINGIA JEHANNA? AMINI USIAMINI, ALLAH NA YEYE ANAINGIA JEHANNAM KAMA VIUMBE
Sasa tusome Sahih Hadith: Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 371 Amehadithia Anas: Mtume wa Allah alisema, "watu watatupwa (Kuzimu) Jehannam na matokeo yake Jehannam itasema:" Je, kuna zaidi watu zaidi? (50.30) mpaka Allah atakapo weka mguu wake juu ya Kuzimu na Jehannam itasema, 'Qati! Qati! (Imetosha imetosha!) " Ushaidi zaidi: Bukhari :: Kitabu 9 :: Juzuu 93 :: Hadith 481, Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 373

Sasa tumefahamu siri kubwa hapa. Kumbe na Allah ataingia motoni. Jamani, hivi huu si ndio Msiba mkubwa sana kwa dini ya Muhammad? Allah nayeye anaingia motoni.

Katika Biblia tunasoma kuwa Shetani na yeye ataingi mtoni, tena atakuwa wa Mwisho kama Allah alivyo kuwa wa Mwsiho pale Jehannam ilipo itisha watu zaidi. Sasa rejea kwenye Biblia: Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. HAPO TUNASOMA KUWA IBILISI anaingia Motoni na kuwakuta wenzake humo, kama ambavyo Sahih Bukhari imesema kuwa Allah anaingia Jehannam na kuwakuta Waislam huko.

ALLAH ANAINGIA JEHANNAMAbu Huraira anasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):
“Pepo na Jahannam zilikuwa na mzozo, kila kimoja kikijaribu kuonyesha ule ubora wake juu ya kingine.” Basi Jahannam ikazungumza: “Mimi nimependelewa kwa kuwepo kwa wale watu wenye kiburi na nguvu ndani yangu.” Pepo ikajibu: “Mimi sijui ni kwa nini hakuna mtu isipokuwa wale dhaifu na wanyenyekevu ndio walioingizwa ndani yangu!”

Hivyo Mwenyezi Mungu akaiambia Pepo:
“Wewe ndiye Msamaha Wangu, na kupitia kwako ninatoa msamaha kwa yeyote kati ya waja Wangu.”
Halafu Yeye akazungumza na Jahannam:
“Wewe ndio ghadhabu Yangu, na kupitia kwako wewe ninamuadhibu yeyote nitakaye kumuadhibu. Kila mmoja wenu atajaa.”
“Bali Jahannam haitajaa, hivyo Mwenyezi Mungu ataingiza mguu Wake ndani yake.”
Kisha Jahannam itagutia:
“Tosha! Inatosha!”

Ndugu zanguni, ningependa mfahamu kuwa, utakapo ingia Jehannam, kutakuwa hakuna tena njia nyingine ya kutoka huko. Pale Jehannam ndio mwisho wa maisha ya walio tenda dhanb. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Je, kufanya mapenzi ya Allah ni sawa na kutenda dhanb? Je, Uislam ni dini ya haki, kama wanavyo sema wafundishaji wa dini hiyo? Jiulize tena, kwanini Allah anatoa ahadi ya Jehannam kwa wafuatayo mafundisho yake?

Lakini Yesu anasema haya:Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Ndugu zanguni, mwamini Yesu ili uwe na uzima wa milele. Yesu anakupenda. Yesu Ndie Njia Pekee. Yesu Ndie Uzima. Dini haita kupeleka kwa Baba aliye Mbingu, lakini Yesu anasema Yeye NDIE NJIA.

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba
For Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Monday, January 11, 2016

SIFA-ADHAMA SABA ZA ROHO MTAKATIFU

Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 17Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.

Yesu Kristo ametupa zawadi ya ajabu sana: Zawadi ya Roho Mtakatifu. Katika baadhi ya maeneo, zawadi hiyo inajulikana kama Roho Mtakatifu, na sehemu nyingine ametajwa kama Msaidizi (Msaidizi na Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu ni sehemu ya tatu ya Uungu, sehemu ya tatu ya Utatu wa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Yeye ni Msaidizi katumwa na Yesu, baada ya Msaidizi wetu kuja ambaye ni Roho Mtakatifu, Yesu alipaa tena mbinguni. Roho Mtakatifu hutolewa kwa wote ambao wamempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao

Kuna mambo saba ambayo tunahitaji kuelewa kuhusu Roho Mtakatifu. Tunajua kwamba, katika Biblia, saba ni namba ya kukamilika/ kukamilisha, au ukamilifu, na sifa saba zote tofauti za Roho Mtakatifu ni kweli kamili na kamilifu. Tunaweza kuzitegemea sifa hizi za ajabu za Roho Mtakatifu, wakati wote, katika kila hali na katika maisha yetu yote.

1. Roho Mtakatifu ni Msaidizi Mwenye Upendo. Tunapokabiliana na mateso katika maisha, mwongozo wa Roho Mtakatifu ni muhimu zaidi na ni faraja katika mioyo yetu: Roho Mtakatifu ni mtu ambaye ana upendo kwetu na anajua kila kitu kuhusu maisha yetu. Roho Mtakatifu alitupenda tangu kabla ya kuumbwa ulimwengu. Yeye alivyotupenda vizuri. Yeye anatupenda milele na anaendelea kutupenda milele yote. Roho Mtakatifu tu ndie mwenye uwezo wa kweli wa kutufariji mioyo yetu, kwa sababu hakuna mtu anaye tupenda sisi kama anavyotupenda Yeye Roho Mtakatifu.

Warumi 5: 5 wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo Lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

2. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwaminifu. Watu, hata wale ambao wana upendo kwetu, wakati mwingine wanaweza kushindwa kutusaidia. Wao (Ndugu na Marafiki) wakati mwingine si waaminifu. Na inaweza kuumiza sana nafsi yetu - rafiki anaweza kuwa mbaya kuliko jino la nyoka, na mchungu kupita nyongo. Huwa tunakata tamaa wakati mtu ambaye anatupenda anapobadirika wakati tunapokuwa na taabu, lakini, Mungu Roho Mtakatifu kamwe hawezi kufanya hivyo na kamwe hawezi kukuacha wakati wa taabu. Yeye anatupenda hata mwisho, kwani, Yeye peke yake ni Mwaminifu. Dhambi haiwezi kututenganisha na upendo wake, hakuna, kwa kweli, yeye alitupenda wakati sisi bado tulikuwa wafu katika dhambi zetu. Alitupenda huku qkijua jumla ya uovu wetu na dhambi zetu. Wema wetu wote kamwe haukumfanya yeye atupende zaidi, na zambi zetu zote hazimfanyi yeye Roho Mtakatifu asitupende au punguza upendo wake kwetu. Tunaweza kumwamini kikamilifu katika Yesu, kwa maana Yeye ni milele mwaminifu. Yeye kamwe hata tuacha, lakini atakuwa pamoja nasi mpaka mwisho wa maisha yetu hapa duniani.

Warumi 15: 13Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

3. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Asiechoka. Wakati mwingine sisi tukijaribu kumfariji rafiki yetu/ndugu yetu katika shida zao au dhiki, huwa tunachoka, pale tunapo ona kuwa shida ya tunaye mfariji inapo kuwa haiishi huwa mara nyingi tunaacha kufanya hivyo na au kata tamaa. Kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kufarijika na au kufarijiwa, infact, tunapo endelea kuwafariji, ndio wanazidi kuharibika na ua hali inazidi kuwa mbaya. Mara nyingi basi, sisi hufa moyo, na kuwaacha peke yao na matatizo yao. Roho Mtakatifu kamwe huwa hakati moyo/au choka kukusaidia, zaidi ya hapo, Yeye huwasaidia hata wale ambao wanafikiria kuwa hawawezi kusaidika. Yeye Roho Mtakatifu, huwa hachoki na au choshwa, si kwa dhambi zetu, si kwa manung'uniko yetu, hata kwa kukataa kwetu, Yeye bado anatupenda na anahuruma.

Yohana 14: 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

4. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwenye Busara. Sisi mara nyingi huzungukwa na watu ambao wanadhani wao wana busara, na bado hao watu hawana uwezo wa kuangalia ndani ya moyo wako na kusema nini ni chanzo cha magonjwa yetu/matatizo yetu ya kiroho. Kama marafiki wa Ayubu (Katika Biblia) walivyo toa mawazo yao potofu, ndivyo hivyo ambavyo hata marafiki zetu wanaweza kutupa mawazo ambayo si sahihi, zaidi ya hapo, hata Madaktari wanaweza kutupa dawa ambazo si sahihi au kwa makosa na zikashindwa kutibu magonjwa yetu na hata kusababisha madhara makubwa, au hata mauti. Ili kutabumbua ugonjwa wa Kiroho kwa usahihi, basi inahitaji hekima kamili. Hivyo basi, Roho Mtakatifu kwa kutumia hekima yake, anaweza kuingalia Roho/moyo wako na kutambua nini hasa kinakusumbua na au wapi lipo tatizo lako la Kiroho. Yeye anaona mzizi wa watatizo upo wapi, na ni nini kinasababisha ugonjwa wako wa kiroho. Yeye si anafahamu wapi lipo tatizo lako, lakini vile vile yeye anaweza kukutibu hilo tatizo lako. Hivyo basi, Roho Mtakatifu Mwenye Busara, ana uwezo wa kuponya magonjwa yetu yote na kutufanya tukubalike mbele za macho ya Mungu. 

1 Wakorintho 2: 10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

5. Yeye ni Msaidizi Alie Salama. Mara nyingi sana marafiki na familia hutoa ushauri salama wakati sisi tupo katikati ya majaribu na mateso. Ushauri wowote unao fuata maarifa ya ulimwengu huu ni ushauri salama. Kumbuka kwamba Shetani mwenyewe wakati mwingine huja kama mfariji wa uongo, anatuhakikishia kwamba mambo yote ni salama huku akifahamu kuwa si kweli, na huku akiweka shaka katika Neno la Mungu. Lakini faraja ya Roho Mtakatifu ni salama, na unaweza kutulia katika faraja na Imani Yake (Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu anajua moyo wa Mungu na mapenzi ya Mungu kwako, na faraja yake kamwe haiwezi kwenda kinyume na Matakwa ya Mungu.

1 Wakorintho 2: 13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

6. Yeye ni Msaidizi alie hai. Yeye (Roho Mtakatifu) huwa awafariji tu kwa maneno, lakini kwa matendo. Yeye anatuombea, kutukumbusha ahadi kubwa ya Mungu na neema yake. Yeye kamwe hatuachi au kutuacha, lakini badala yake anatuongoza katika mapenzi kamili ya Mungu Baba.
Warumi 8: 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 27. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

7. Yeye ni Msaidizi wetu wa sasa na hata milele. Hatuitaji kumtafuta, bali yeye yupo nasi daima. Yeye kamwe hatotuacha, wala kutuacha. Tunaweza kumwambia na au kumwita wakati wowote ule tunahitaji msaada wake, na tuna uhakika kuwa yeye yupo nasi na anaweza kutusaidia.

Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

Hivyo basi, ndugu msomaji, leo tumekumbushana sifa Saba za Roho Mtakatifu.
1. Roho Mtakatifu ni Msaidizi Mwenye Upendo.
2. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi mwaminifu.
3. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Asiechoka.
4. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwenye Busara.
5. Yeye ni Msaidizi Alie Salama.
6. Yeye ni Msaidizi alie hai.
7. Yeye ni Msaidizi wetu wa sasa na hata milele.

Nimategemeo yangu kuwa, baada ya kuzisoma hizo sifa Saba za Roho Mtakatifu, utaanza kumtegemea na kuongea naye kila siku. Kumbuka, Roho Mtakatifu ni Msaidizi wetu na yupo nasi kila siku kama ambavyo Biblia Takatifu inavyo sema.

Mtegemee Roho Mtakatifu katika Maisha yako yote. Mtegemee katika kazi zako. Mtegemee katika Masomo yako. Mtegemee katika Biashara zako. Mtegemee katika Ndoa yako. Mtegemee katika kila jambo. Hakika Yeye anakupenda na alikufahamu wewe hata kabla ya kualiwa kwao. Yeremia 1: 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries 

April 13, 2015 ©2015

JE UNAMFAHAMU ROHO MTAKATIFU?

Ndugu msomaji;
Je, unamfahamu Roho Mtakatifu?
Je, Roho Mtakatifu ni nani kwako?

Katika kijarida hiki kifupi, ningependa tumzungumzie Roho Mtakatifu kama alivyo semwa na kutajwa katika Biblia Takatifu.

Kuna utatanishi mkubwa sana na maelezo mengi sana kuhusu Roho Mtakatifu. Kuna imani zingine kama Mashahidi wa Yehova, wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Nguvu Fulani na au ni uwezo wa Mungu katika kufanya mambo. Wengine kama Waislamu, wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Malaika Gabriel. Wengine husema kuwa Roho Mtakatifu ni sehemu ya Nafsi ya Mungu. Lakini, Biblia inasema nini kuhusu Roho Mtakatifu. Ni vyema tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu kwa kutumia aya za Biblia na sio theologia na akili zetu.

ROHO MTAKATIFU NI MUNGUTuanze kwa ushaidi wa aya: Matendo ya Mitume 5:3-4. Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata? 4 Kabla hujauza hilo shamba lilikuwa mali yako. Na hata baada ya kuliuza, fedha ulizopata zilikuwa zako. Kwa nini basi umeamua moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”

Katika aya hizo hapo juu, Petro anapambana na anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na anasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali Mungu. Kwa maana nyingine, Petro alikuwa anamwambia Anania kuwa, kumdanganya Roho Mtakayifu ni sawa na kumdanganya Mungu. Huu ni uthibitisho wa kwanza kuwa, kumbe Roho Mtakatifu ni Mungu.

ROHO MTAKATIFU YUPO KILA MAHALIHebu tuangalie kama Roho Mtakatifu ana adhama za Mungu aliye hai. Sifa, moja ya Mungu ni kuwa, yeye yupo kila Mahali. Je, Roho Mtakatifu anayo hii sifa ya kuwa kila mahali? Fungua Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,”
Daudi anatuambia kwa kupitia Zaburi kuwa, huwezi kumkimbia Mungu. Daudi anamtaja Mungu na au anamwita Mungu kuwa ni Roho. Hii sifa ya kuwa kila mahali ni ya Mungu pekee, na katika Zaburi 139: 7-8, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu yupo kila mahali.

Tuendele na ushahidi zaidi wa kuwa kila mahali; katika Wakorintho wa Kwanza, hapa Mtume Paulo anasema yafuatayo 1 Wakorintho 2 aya ya 10 Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”

Kama Roho Mtakatifu anafahamu kila kitu kilicho ndani ya Binadamu, ambao wametapakaa Duniani kote, basi kitendo cha kuwa kila mahali kwa wakati mmoja ni Mungu pekee ndie aliye na huo uwezo.
Tuendelee kwa Ushihidi mwingine katika aya hiyo hiyo ya 10 ya Wakorintho wa kwanza Sura ya 2. Roho Mtakatifu ni Mungu kwasababu ana akili, hisia, na mapenzi yake.
Katika Wakorintho wa kwanza 2:10 tumesoma kuwa Roho Mtakatifu hufik
iria na hujua siri iliyo ndani yako. Hii sifa ya kufikiria na kujua, inavunja hoja ya Mashahidi wa Yehova kuwa Roho Mtakatifu ni “Nguvu”. Nguvu haina uwezo wa kufikiria wala kufanya maamuzi.

ROHO MTAKATIFU UHUZUNIKAKatika Waefeso 4:30 inasema “Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi”

Unaweza jiuliza, ni kivipi unaweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu? Kama Roho Mtakatifu angekuwa ni “Nguvu –Energy” kama anaitwa na Mashahidi wa Yehova, je, ni kivipi Nguvu ipate huzuni? Unapo tenda dhambi huku Roho Mtakatifu akiwa ndani yako kama alivyo fanya “Anania – Matendo ya Mitume 5:3-4” Unamhuzunisha Roho Mtakatifu maana yeye hujua yote na akuna siri ambayo haifahamu. Hii sifa ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu ina pinga madai ya Mashahidi wa Yehova na inapinga madai ya Waislam yanayo kama Uungu wa Roho Mtakatifu.

ROHO MTAKATIFU HUTUOMBEAWarumi 8:26-27 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno. 27 Na Mungu ambaye ana chunguza mioyo yetu anafahamu mawazo ya Roho kwa maana Roho huwaombea watakatifu kufuatana na mapenzi ya Mungu.

Katika aya hapo juu, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu anatuombea na kutusaidia katika udhaifu wetu. Hii sifa ya upendo usio na kipimo ni ya Mungu peke yake. Zaidi ya hapo, tunasoma kuwa, Mungu anachunguza mioyo yetu kwa kupitia Roho Mtakatifu. Kumbe basi, Roho Mtakatifu anafahamu mapenzi ya Mungu kwako. Hii sifa ya Roho Mtakatifu kuwa na uwezo wa kufahamu nini Mungu anawaza inamfanya Roho Mtakatifu na yeye awe Mungu. Hakuna mwenye uwezo wa kufahamu mawazo ya Mungu, isipokuwa Mungu.

ROHO MTAKATIFU HUFANYA MAAMUZI YAKERoho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11).
1 Wakorintho 12:7-11Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
7 Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote. 8 Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha. 11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.

Katika Wakorintho wa kwanza hapo juu, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu ndie anaye toa zawadi/karama ya hekima, ufahamu, imani, kuponya, miujiza, unabii, nk. Hii sifa ya kutoa hizi Karama ni ya Mungu, lakini hapa kwenye Wakorintho tumesoma na kugundua kuwa, Kumbe Roho Mtakatifu ndie anaye toa hizi karama za Mungu. Hivyo basi, kwa kuwa Roho Mtakatifu ndie anaye toa hizi karama za Mungu, hufanya hivyo kwa kuwa yeye ni Mungu na hizo karama ni zake.

ROHO MTAKATIFU ANAFAHAMU MAMBO YOTEKama ambavyo Mungu anafahamu mambo yote na anaweza yote, vivyohivyo Roho mtakatifu ni Mungu na anauwezo wa huohuo wa kufahamu yote. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26).
Yohana 14:26Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Katika Yohana hapo juu, tunajifunza kuwa, Roho Mtakatifu yupo nasi kila siku na anaishi ndani yetu. Huu uwezo wa kuishi ndani yetu na kuwa kila mahali, na kufahamu yote ambayo Yesu aliyo tuambia na kutukumbusha, huu uwezo ni wa Mungu na unamfanya Roho Mtakatifu kuwa Mungu.

HITIMISHORoho Mtakatifuni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye pia anayo nafsi na kwa hiari yake ameamua kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu kwa kuzingatia mgawanyo wa majukumu waliyokubaliana yaani nafsi ya Mungu Baba, Mungu Mwana(Yesu) na Mungu Roho Mtakatifu. Kazi/lengo kubwa la ujio wake ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu kwenye ulimwengu huu wa mwili, ili kumsaidia kuishi katika mapenzi ya Mungu.

Katika huduma yake

Max Shimba Ministries
@February 10, 2015
New York, NY 10019

TAFITI ZA KIMATAIFA ZAONYESHA KUWA UKRISTO WAFIKIA ASILIMIA 60 TANZANIA

UTAFITI UNAONYESHA KUWA WAKRISTO TANZANIA NI WASTANI WA ASILIMIA 60

Tafiti tatu zinaonyesha kuwa Ukristo unakua kwa kasi sana Tanzania, huku tafiti ya "INTERNATIONAL RELIGIOUS FREEDOM REPORThttp://www.state.gov/documents/organization/208416.pdf " ikionyesha kuwa Ukristo Tanzania ni asilimia 60.

Tafiti nyingine ya ACNUK inayonyesha kuwa Wakristo Tanzania ni asilimia 53.2 na Tafiti ya RE WORLD ORGhttp://www.refworld.org/pdfid/4d7621f72.pdf inaonyesha kuwa Wakristo Tanzania ni asilimia 62.
Tafiti kumi zinasema kuwa Uislam unakufa Tanzania, huku tafiti kumi zingine zinasema kuwa Ukristo umevuka asilimia 50.

Tuendelee kufanya kazi ya Bwana wetu Yesu, maana hata Tafiti za Kimataifa zinaonyesha kuwa Yesu anaendelea kuzoa malundo kwa malundo kila siku.

Tumsifu Yesu Kristo, mile na milele maana kazi yake ya Msalabani haikuwa ya bure. Matunda yake sasa yanaonekana Tanzania.

Mungu awabariki sana na kwa wale ambao hawajabahatika kuwa Wakristo, tunawakaribisha sana.

Max Shimba Ministries Org.

Sunday, January 10, 2016

WAISLAM WANADAI KUWA HII AYA INAPINGA UUNGU WA YESU - YOHANA 17:3

NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU, WAKUJUE WEWE ULIYE MUNGU WA PEKEE, WA KWELI NA YESU KRISTO ULIYE MTUMA -YOHANA 17:3

Ndugu wasomaji,
Leo nitaielezea aya ya Yohana 17: 3 ambayo Waislam wamekuwa wakiitumia mara nyingi sana kudai kuwa eti, Yesu amekana kuwa yeye ni Mungu. Waislam kwa kupitia mihadhara ya kidini na kwa kutumia vijarida mbali mbali wanatishia Umma wa Wakristo kuwa, Yesu ameukana Uungu. Je, hayo madai ya Waislam ni kweli? Je, hiyo aya ina la zaidi la kujifunza?

Ili uielewe Biblia vizuri, nilazima usome aya kadhaa ili upate kuelewa nini hasa Mungu anasema kupitia Neno lake. Hivyo basi, nimeweka aya ya 4 na ya 5 ili kufafanua nini hasa Yesu alikuwa anasema katika Yohana 17.

Ngoja niziweke aya zote hapa:Yohana 17: 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.4 Nimekutukuza Wewe duniani kwa kuitimizaile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.

Yesu katika aya ya 5 [Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako]

==> YESU anasema kuwa
1. Yeye aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo! Hapo panaanza kukupa mwanga halisi, wa nini Yesu alikuwa anasema na Yesu ni nani. Imani zote zinakiri kuwa aliye kuwepo kabla ya vitu vyote ni Mungu. Lakini katika aya ya 5, Yesu nae anadai kuwepo kabla ya uumbaji.

2. Yesu anaendelea kusema katika aya hiyo hiyo kuwa, yeye alikuwa na adhama ya Mungu -"UTUKUFU". Yesu anamwambia Mungu Baba kuwa, AMTUKUZE YESU KWA UTUKUFU ALIOKUWA NAO KABLA YA ULIMWENGU HAUJAKUWAKO. Sasa, kama Yesu, sio Mungu na alikuwa Binadamu wa kawaida, kwanini basi amwambie BABA YAKE AMTUKUZE? Yesu anatumia mamlaka gani hayo kudai Utukufu ambao sio wake bali ni wa Mungu pekee?

3. Kama Yesu sio Mungu. Je, alipo dai atukuzwe na Mungu Baba, huoni kuwa alikuwa anakufuru? Lakini Hatusomi kuwa YESU aliwai tenda dhambi yeyote ile. Hata dini ya Waislam, inakiri kuwa, Katika Binadamu wote ambao waliishi Duniani, ni Yesu pekee aliweza kuishi bila ya kutenda dhambi na kuwa na dhambi.

Ndugu wasomaji, madai ya Waislam kuwa Yohana 17:3 INAPINGA UUNGU WA YESU ni Batili kabisa, maana, leo tumejifunza katika Yohana hiyo hiyo kuwa Yesu aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo na Yesu anautukufu wa Mungu.

Aya ya 5 NUKUU: Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.

HOJA:1. Yesu anadai kuwa aliishi kabla ya ulimwengu kuumbwa.
2. Yesu anadai kuwa anautukufu kama wa Baba yake.

SASA BASI:1. Yesu ni nani mpaka adai utukufu kama wa Mungu tena kutoka kwa Mungu Baba?
2. Yesu ni nani mpaka aseme kuwa aliishi hata kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, tena namwambia Mungu Baba?

Ndugu zanguni,
Mada imekamilika na kujibu maswali ya Waislam kuwa Yesu aliukana uungu wake katika aya 3 ya Yohana 17.

Nawakaribisha wote Kwa Yesu Kristo aliye hai. Yeye ndie njia kweli na uziama. Njooni kwake ili mpate maisha ya milele na yenye uzima tele.

Katika Huduma yake,
Max Shimba.
Kwa Max Shimba Ministries

MTUME MUHAMMAD ALITUMIA NDUMBA

1. Mtume Muhammad alitumia Ndumba
2. Mtume Muhammad adai eti Nywele zake zinatibu jicho ovu.
3. Wapi katika Biblia tunasoma kuwa Manabii na Mitume wa Biblia walitumia Ndumba?
Ndugu Msomaji,

Leo ningependa tusome kuhusu Muhammad na Utumiaji wa NDUMBA katika Uislam,

MTUME MUHAMMAD ANATUMIA NDUMBAMuhammad alitumia ndumba [nguvu za kimazingaombwe] dhidi ya jicho ovu na wanyama jamii ya mjusi wenye sumu Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3525 uk.48.
Hivi wapi tunasoma katika Taurat au Zaburi au Injir kuwa Mitume na Manabii wa kwenye Biblia walitumia NDUMBA?
Hivi Allah hana uwezo wa kutibu jicho ovu au Sumu mpaka atumie NDUMBA?

MUHAMMAD SASA AMPA MKE WAKE AISHA NDUMBAMuhammad alimpa ‘Aisha ndumba ili kutibu jicho ovu. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na. 5445,5447-5450 uk.1196.
Hivi Ndumba ina tofauti gani na UCHAWI? Sasa hapo juu tumesoma kuwa Muhammad ametoa NDUMBA kwa mke wake kipenzi.
Wapi tunasoma kuwa Manabii wa Biblia walitumia NDUMBA?
Muhammad aliamini katika jicho ovu, na kulikuwa na hirizi dhidi yake al-Tabari juzuu ya 39 uk.134.
Sura mbili za mwisho (113 and 114) ziliandika juu ya ubaya wa jicho ovu kufuatana na Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3517 uk.41.
Hata hivyo, sura za 113 na 114 hazimo katika toleo la Ibin Mas’ud katika Korani (The Fihrist uk.57). Kuondolewa huko hakukuwa kwa bahati mbaya. Ilitaarifiwa kuwa Ibn Mas’ud alisema, "Hirizi mbili-Sura za [113, 114] si Kitabu cha Mungu."
Ibn Mas’ud alikuwa katibu muhtasi wa Muhammad. Muhammad aliwaambia watu wengine wajifunze kutoka kwa Ibn Mas’ud na wengine watatu. (Bukhari juzuu ys 6 kitabu cha 60 sehemu ya 8 na.521 uk.486-487).

MUHAMMAD ASEMA NDUMBA NANGAE HUTIBU JICHO OVUNdumba hutibu jicho ovu. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3510, 3511 uk.41; juzuu ya 5 na.3512 uk.42.
ALBADIRI NI NDUMBA
Albadiri inaruhusiwa dhidi ya jicho ovu na inge Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3513-3518 uk. 42-44.
Jicho ovu ni hali halisi. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sehemu ya 36 na.636 uk.427, juzuu ya 7 kitabu cha 71 sehemu ya 86 na.827 uk.538. Soma pia Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 55 sehemu ya 9 na.590 uk.386.
Jicho ovu ni kweli. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3506, 3507 uk.39.
"…Ushawishi wa jicho ovu ni hali halisi." Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5426 uk.1192. Soma pia Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5424-5427 uk.1192.
Amir bin Rabia alisemekana kuwa alitoa jicho ovu kwa mtu fulani. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3508 uk.40.
Hata hivyo nywele za Muhammadi zilikuwa tiba ya jicho ovu. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 72 sehemu ya 65 na.784 uk.518.
Wakati Muhammadi aliponyolewa nywele zake, wafuasi wake walitaka kudaka kila kipande cha unywele wake kwa ajili ya kukitunza. Muhammadi kwa ukarimu alisambaza nywele zake kwa watu. Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2991-2994 uk.656-657.

ETI MKIJUMUIKA TAREHE 17, 19, 21 YA KILA MWEZI NI TIBA. HII NAYO NI NDUMBA YA AINA YAKEMuhammad alisema pia kuwa ikiwa watu watajiumika tarehe ya 17, 19 au 21 ya mwezi itakuwa ni tiba kwa kila ugonjwa. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3852 uk.1084.
Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini alifanya
NDUMBA?
Kama Allah ni Mungu, kwanini anaruhusu kufanya NDUMBA?
Kama Uislam unatoka kwa Mungu, kwanini unaruhusu NDUMBA nangae?
Karibu kwa Yesu aliye hai na Mungu Mkuu,
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW