Sunday, January 24, 2016

ADAM, MUSA, IBRAHIM NA DAUDI HAWAKUWA WAISLAM

Ndugu msomaji,

Waumini wa dini ya Kiislam wamekuwa na tabia ya kusema kuwa, eti, Adam, Musa, Ibrahim na Daudi walikuwa ni Waislam. Madai haya ya Waislam yamekuwa yakisemwa katika mihadhara yao ya kidini bila ya kuwa na ushaidi yakinifu kusaidia madai yao.

Leo nitajibu madai haya kwa kutumia Biblia na Koran kama ifuatavyo:

ADAM, MUSA, IBRAHIM DAUDI HAKUWAI SEMA SHAHADA
Kufuatana na sharia za Kiislam, ili mtu awe Muislam lazima aseme na au afanye shahada. Adam, Musa, Ibrahim na Daudi hawakusema SHAHADA (La ilaha illallah) na hakuna ushaidi wa Kibiblia au Koran unao sema kuwa Adam, Musa, Ibrahim na Daudi walisema SHAHADA. Hivyo basi, Adam, Musa, Ibrahim na Daudi hawakuwa Muislam.

SASA NITAANZA KUHOJI UISLAM KWA KUPITIA QURAN, KAMA KWELI ADAM, MUSA, IBRAHIM NA DAUDI WALIKUWA WAISLAM:

ALLAH ANASEMA KILA UMMA AMEUPA KITABU NA MTUME:

Soma;
Quran 10: 47. Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.

Angalia hii aya pia

Quran 14: 4. Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

Dhana hii ya Allah kushusha Kitabu kwa kila lugha ni muhimu sana kwasababu imejirudia mara nyingi na ndio msingi wa hili somo.

Quran 16: 36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.




NABII ADAM::::::::::::::::::::
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA ADAM NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:

Kama kweli Allah aliteremsha Kitabu kwa kila Umma, na Adam ni Nabii wa Allah, basi ningependa mnijibu maswali yafuatayo:

1. ADAM alipewa kitabu gani, naomba mtuwekee nakala yake hapa na mtuambie jina la hicho Kitabu.

2. ADAM alikuwa Nabii wa Umma gani, wakati yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa? [Naomba mtutajie jina la Umma wa Nabii Adam]

3. Tuleteeni ushahidi wa aya kwenye hicho kitabu cha ADAM kuwa ADAM alisema shahada.

NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya hakupewa Adam.




NABII MUSA:
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA MUSA NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:

Allah anaendelea kusema kuwa aliteremsha Taurat kwa Nabii wake Musa.

Surat Al Baqara 136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.

Kama kweli Musa alipewa na au teremshiwa kitabu na Allah, basi naomba mnijibu maswali yafuatayo:

1. Kipo wapi na au ipo wapi NAKALA YA TAURAT ambayo Allah aliiteremsha kwa Musa kabla ya Quran?

2. MUSA alikuwa Nabii wa UMMAH gani? Naomba muutaje huo Ummah kwa jina.

3. Tuleteeni ushahidi wa aya kwenye hicho kitabu cha MUSA kuwa MUSA alisema shahada.

NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya sio Taurat ya Musa iliyo teremshwa kabla ya Quran.




NABII IBRAHIM:
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA IBRAHIM NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:

Quran 10: 47. Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.

Angalia hii aya pia

Quran 14: 4. Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

S. 3:67 Shakir: Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.

Allah amesema kila Umma ulipewa Nabii na ujumbe "Kitabu" na Ibrahima alikuwa Muislam, SASA BASI.

1. Waislam, Nitajieni jina la kitabu ambacho Ibrahim alipewa na Allah?

2. Nileteeni ushahid wa aya kutoka hicho kitabu kuwa Ibrahim alisema Shahada.

3. Nitajieni jina la Ummah ambao Ibrahim alikuwa Nabii wake?

4. Allah anasema kuwa Ibrahim hakuwa Yahudi wa Mkristo, kama hayo madai ni kweli, KWANINI WAISLAM WANASEMA KUWA UKRISTO ULIANZISHWA NA PAULO, huku ALLAH ANAKIRI KUWA HATA WAKATI WA IBRAHIM KULIKUWA NA UKRISTO?

NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya sio Kitabu ambacho Ibrahim aliteremshiwa kabla ya Quran.



NABII DAUDI:
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA DAUDI NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:

ALLAH ANASEMA "NA DAUDI TUKAMPA ZABURI :
Surat An Nissai aya 163, Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi. S. 4:163

Kama ni kweli Allah aliteremsha Zaburi kwa Daudi, basi maswali yafuatayo lazima yapewe majibu:

1. Daudi alikuwa Nabii wa Ummah upi, naomba Waislam muutaje huo ummah kwa jina.

2. Ipo wapi NAKALA YA ZABURI ambayo Allah aliiteremsha kwa Daudi kabla ya Quran?

3. Daudi alipokea hiyo Zaburi akiwa Mji gani?

4. Leteni aya kutoka Zamburi aliyo iteremsha Allah kabla ya Quran ambayo DAUDI anasema SHAHADA.


NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya sio ZABURI ambay iliteremshiwa kabla ya Quran.

MKINILETEA UTHIBISHO WA MASWALI YANGU HAPO JUU,

BASI LEO HII NITASILIMU NA KUWA MUISLAM

Katika huduma yake,

Max Shimba Ministries

Saturday, January 23, 2016

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA SABA)

Je, Yesu ni Mwana wa Mungu?
Je, Isa bin Mariam ni Mwana wa Mungu?

Biblia inasema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Katika hii mada, tuanze kwa kuangali, Je, Biblia inasema nini kuhusu Yesu? Kumbuka kuwa, Biblia ndio ilikuja kwanza kabla ya Quran. Ushahid unonyesha kuwa Biblia ilikuwepo miaka 632 kabla ya Quran kuandikwa na marafiki zake Muhammad.


YESU NI MWANA WA MUNGU

Tunaona hapa Biblia inatuambia YESU KRISTO ni Mwana wa Mungu (YOHANA 20:30-31) hapa Yesu mwenyewe anasema yeye ni Mwana wa Mungu ( MATHAYO 26:59-64; 16:13-17 ) , Neno Mwana linamzungumzia Yesu Mwana siyo kuwa Mungu anazaa la hasha

Yesu anaitwa mwana wa Mungu kwa sababu alizaliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Hata sisi tumezaliwa kwa mara ya pili kwa Roho tunapo mwamini Yesu Kristo hivyo tunahesabika kuwa ni wana wa Mungu.(WAFILIPI 2:14-15,YOHANA 1:12). Kwahiyo Yesu anapoitwa Mwana wa Mungu maana yake ni chapa ya Mungu (HUIOS) WAEBRANIA 1:1-3. Ndiyo maana hapa Yesu anawaambia wanafunzi wake, mumeniona mimi ; mumemuona Mungu, maana yake ndiyo hiyo (HUIOS) yaani chapa ya Mungu (YOHANA 14:7-9)

Tunaona hapa Yesu alisema Yeye ni Mwana wa Mungu (YOHANA 9:35-37)
Shetani naye anajua kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (MARKO 3:11,LUKA 4:41).
Malaika nao wanasema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (LUKA 1:30-35)
Mungu mwenyewe anasema kuwa Yesu ni Mwanangu mpendwa (MATHAYO 3:17,MATHAYO 17:5 )


ISA WA QURAN SIO MWANA WA MUNGU

Kama kuna jambo ambalo Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu analikataa sana kupitia Qurani basi jambo hilo si lingine bali ni uwana wa Mungu. Allah anasema hivi.
Quani 6:101 Suratul Al-An-am [Wanyama]
Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.
Qurani 9:30 Suratul At-Tawba [Kutubu]
Na mayahudi wanasema “uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;”na “Wakristo wanasema Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyenzi Mungu uwaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!

Allah anasema katika aya hizo hapo juu kuwa, yeye hana Mwana na kuwa Wakristo na Wayahudi wanamsingizia Allah kuwa na Mwana. Allah anasema kuwa, yeye hana Mwana kwasababu hana MKE. Ikiimanisha kuwa, Allah hana uwezo wa kuwa na Mwana bila ya kufanya tendo la ndo na Mwnamke. Huu ni ushahid tosha kuwa, Allah sio mjuzi wa yote, maana hawezi kuwa na mwana bila ya mke. 

Hebu tuangalie aya zingine za Biblia zinasema nini kuhusu Yesu.
1. Mathayo 17:5 ….Huyu ni mwanangu mpendwa wangu…
2. Malaika wa Mungu alisema hivi.
Luka 1:30-31,35
Malaika akamwambia usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.

Hivyo Isa siyo Mwana Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.

Leo tumejifuinza kwa mara nyingine tena kuwa Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia kwa kuwa Isa wa Quran yeye sio Mwana wa Mungu.
Katika huduma yake,

Max Shimba

Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2015

Wednesday, January 20, 2016

YESU NI MUNGU KUTOKANA NA QURAN (SEHEMU YA KWANZA)

Waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidini kupitia wahadhiri wao wa Dini wamekuwa wakipinga kuwa Yesu Kristo si Mungu kwa madai kuwa, Mungu hawezi kuzaliwa.
Ndugu msomaji, nakusihi ufuatilie somo hili kwa makini ili ujue ukweli kuhusu Umungu wa Yesu Kristo katika Koran:

Je Yesu anazo sifa za kipekee za Mungu kutokana na Quran?
Hebu tuanze utafiti wetu kwa kusoma Quran na tujionee wenyewe kama kweli Yesu ni Mungu au la.

MUNGU NI MFALME
Adhama ya Kwanza kutokana na Quran: Mungu ni Mfalme:
Koran inasema kuwa, sifa Moja ya Mungu ni “Mfalme”. Je, Yesu anayo hii sifa ya “Mfalme”? Haya tusome Quran kwanza.
Quran 59: 23
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.
Sasa tuangalie kama kweli Yesu anayo hii sifa ya Mfalme ambayo ni adhama ya Mungu pekee kutokana na Koran.

Biblia takatifi inasema yafuatayo kuhusu Yesu Kristo:
Ufunuo 17:14

Hawa watafanya vita na Mwana Kondoo na Mwana Kondoo atawashinda, kwamaana yeye ni Bwana wa Bwana na Mfalme wa Wafalme.

Katika aya hii tunasoma kuwa Yesu anaitwa “Mfalme wa Wafalme” ambayo ni adhama ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo shaidiwa na Koran Surah ya 59 na aya 23. Hivyo basi , Allah na Koran wamekiri kuwa Yesu ni Mungu kwasababu Biblia imetuthibitishia kuwa Yesu ni Mfalme wa Wafalme katika Ufunuo 17 na aya 14.

Tuendelee na ushaidi mwingine kutoka Koran ambao unatuhakikishia kuwa Yesu ni Mungu.

MUNGU NI MTAKATIFU
Adhama ya Pili kutokana na Quran: Mungu ni Mtakatifu:

Je, Yesu anayo hii sifa ya “Mtakatifu”? Tusome Quran kwanza:

Quran 59: 23 Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Katika Quran tumesoma kuwa, moja ya sifa za Mungu ni “Mtakatifu”, Je sifa hii ya utakatifu Yesu anayo?

Nenda kwenye hihiyo Kuran 19:19 Malaika akasema hakika mimi ni mjumbe ili nikupe Mwana Mtakatifu -Isa Bin Maryam.

Koran hiyo hiyo inatuhakikishia na kutujibu kuwa Yesu ambaye anajulikana kwa jina la Isa Bin Maryam katika Quran ni Mwana Mtakatifu. Hivyobasi, hii adhama ya Utakatifu ambayo ni ya Mungu pekee, tunasoma katika Quran iliyoteremshwa an Allah kuwa Yesu ameinyakua. Yesu anaitwa Mwana Mtakatifu.

BWANA NI MWENYEZI MUNGU
Adhama ya Tatu kutokana na Quran: Bwana ni Mwenyezi Mungu
Hebu tufungue Quran na tusome kuhusu Bwana:

Quran 3:39 Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni Bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema naye ni Nabii Isa.
Quran 39: 29

Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanao gombana, na wa mtu mwengine aliye khusika na Bwana Mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao?

Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui.
Quran 39:29 inasema kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana na hiyo ni sifa njema kwa Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hapo, Koran hiyo hiyo (Quran 3:39) inasema kuwa Isa Bin Maryam ni Neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu na ni Bwana. Koran imejibu kuwa, sifa ya Bwana ambayo ni ya Mungu pekee ni ya Yesu. Sasa tusome na Biblia kwa ushaidi zaidi kuhusu Yesu ni Bwana.
Ufunuo 17:14

Hawa watafanya vita na Mwana Kondoo na Mwana Kondoo atawashinda, kwamaana yeye ni Bwana wa MaBwana na Mfalme wa Wafalme.

Katika Ufunuo tunasoma kuwa Mwana Kondoo ambaye ni Yesu Kristo anaitwa Bwana wa Mabwana. Hivyobasi, hii adhama ya “Bwana” ambayo ni ya Mungu pekee tunasoma katika Quran iliyoteremshwa an Allah kuwa Yesu ni Bwana na ameinyakua, vilevile, katika Biblia Takatifu tumesoma kuwa Yesu anaitwa Bwana, ambayo ni Sifa ya Mungu Pekee kutokana na Quran.

Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni Mungu kwa kuwa Yesu anazo adhama zote na/au sifa zote za Mungu.

Katika huduma yake,

Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Saturday, January 16, 2016

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUKIRI KUWA YEYE SIO AKBAR

1. ALLAH AOMBA MSAADA KWA VIUMBE DHAIF
2. KUMBE ALLAH SIO AKBAR
Sura Al-Ankabut 29:6
Quran inasema:
Allah does not need his creatures’ help.
Yaani,
Allah hahitaji kusaidiwa na viumbe wake. (bila shaka ni katika kutekeleza makusudi na mipango yake).
LAKINI QURAN HIYO HIYO INAWAAMBIA WAISLAMU:
Sura Muhammad 47:7
If you help Allah, He will help you and make you strong.
Yaani,
Kama mkimsaidia Allah, yeye naye atawasaidia na kuwafanya kuwa imara.
Maswali:
1. Umesema huhitaji msaada, kisha unasema tena unahitaji msaada! Je, Mungu anaweza kufanya jambo kama hilo?
2. Aya hizi zinafanana au zinapingana?
3. Je, hii si ishara kuwa aya hizi zilisemwa tu ili kukidhi mahitaji ya wakati fulani, lakini msemaji alipoona anahitaji kuwafanya watu watende kinyume chake, akajikuta amesema tofauti na alivyosema siku za nyuma?
Na tena quran inasema katika sura Al-Baqara 2:244
Fight for the cause of Allah and bear in mind that He hears all and knows all.
Yaani:
Fanyeni vita kwa ajili ya Allah na mkumbuke kwamba anaona yote na anajua yote.
Maswali:
1. Kama kweli Allah hahitaji msaada wa viumbe wake; na kama kweli aliumba ulimwengu wote kwa NENO TU, iweje NENO hilo hilo lisiweze kuwabadilisha wanadamu hadi alazimike kuliingiza ndani yao kwa nguvu, kwa vitisho na kwa ukali namna hiyo?
(Ukristo unashinda na kufanikiwa kwa NENO tu. Maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu wetu. Yeye aliumba kwa Neno; na sisi watoto wake, tunaumba kwa Neno hilo hilo. Tunahubiri tu na watu wanaokolewa, wanaponywa, wanalindwa na kusimama na Mungu wa kweli. Huoni kwamba hii hasa ndiyo maana ya nguvu ya Mungu? Hatuhitaji kuchinja au kupiga watu ili wampende Mungu!! Unawezaje, hata tu wewe mwenyewe, kumfanya mwanao au mkeo akupende kwa njia ya vipigo na kulazimisha? yaani, ukitaka mwanao au mkeo akupende utamshikia rungu au panga au bunduki? Je, hiyo si ishara kwamba wewe huna nguvu ndiyo maana unalazimisha? je, huko si kujikanganya maana umetuambia kuwa wewe ni Mungu unayeweza yote?)
2. Je, Allah anapotaka wanadamu wanaomwamini wafanye vita ili kuwalazimisha wasioamini wamwamini, huko si kutaka msaada kwa viumbe wake?

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA KUWA AKHERA ITAJAA WATU WENYE CHUKI

Sura Al-Nahl 16:28
The angels will say to those whom they cause to die in purity, ‘Peace be on you.’ Come into paradise for what you did.
Yaani:
[Kuhusu wale wanaoingia mbinguni] – Malaika watasema kwa wale ambao watawafanya wafe katika usafi (utakatifu), ‘Amani na iwe juu yenu. Ingieni paradiso kutokana na matendo yenu.’
LAKINI, QURAN HIYO HIYO INASEMA:
Sura Al-Hijr 15:45-47
Indeed, the righteous will be within gardens and springs, [Having been told], "Enter it in peace, safe [and secure]." And We will remove whatever is in their breasts of resentment, [so they will be] brothers, on thrones facing each other.
Yaani:
Surat Al Hijir
45. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. 46. (Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani. 47. Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana.
Maswali:
1. Katika 16:28, inaonekana kwamba watakaiongia peponi ni watu walio safi kwa sababu malaika wamesababisha watu hao wafe wakiwa safi. Lakini 15:45-47 inaonyesha kuwa wataingia peponi wakiwa na chuki mioyoni mwao. Je, chuki ni sehemu ya usafi?
2. Je, aya hizi zimetoka kwa mtoaji yule yule?
3. Kama chuki ni mbaya kiasi cha kuhitajika kuondolewa mioyoni mwa Waislamu wanaoingia peponi, iweje wakiwa duniani wanaagizwa kuwachukia wale wasio Waislamu (kama tulivyoona kwenye 4:101)?

ALLAH ATEREMSHA AYA KWA MUHAMMAD NA KUSEMA UISLAM NI DINI YA VITA

1. KUMBE ALLAH NI KIGEUGEU
2. KUMBE MUHAMMAD NI KIGEUGEU
Sura Al-Kafirun 109:1-6
Say, "O unbelievers, I do not worship what you worship, nor do you worship what I worship. I shall never worship what you worship, nor will you worship what I worship. You have your own religion and I have mine."
Yaani,
Enyi msioamini, mimi siabudu mnachoabudu, wala ninyi hamuabudu ninachoabudu. Mimi kamwe sitaabudu kile mnachokiabudu, wala ninyi kuabudu kile ninachokiabudu. Ninyi mnayo dini yenu, nami nina yangu.
Pia, quran inasema katika sura Al-Baqara 2:256
There shall be no compulsion in religion.
Yaani:
Hakutakuwapo na kulazimishana katika dini.
LAKINI ALLAH HUYO HUYO ANASEMA:
Sura Al-Anfal 8:39
Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.
Yaani:
Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.
Maswali:
1. Aliyemwambia Muhammad asiwalazimishe wasioamini kuamini Uislamu ndiye huyo huyo aliyemwambia afanye vita?
2. Aliyesema kuwa “ninyi msioamini hamtaabudu ninachoabudu” ndiye huyo huyo anayesema ni vita tu hadi dini ya Allah itawale?
3. Na je, aliyesema kuwa hakuna kulazimishana katika masuala ya dini ndiye huyo huyo anayesema watu wake wapigane vita?
4. Huku si kujipinga mwenyewe?

ALLAH, MUHAMMAD NA UISLAM WASEMA NI MARUFUKU KWA MUISLAM KUWA RAFIKI NA MKRISTO

Ndugu msomaji,

Leo ningependa tujifunze kuhusu chuki iliyo ndani ya Allah na dini yake ya Uislam. Wengi wenu huwa mnadai na au fikiria kuwa Mungu wa Biblia aliye jaa upendo ni huyo huyo wa kwenye Quran ya Jibril. La hasha.

Allah ambaye ndie munguwa Waislam yeye amejaa chuki na anawataka na kuwaamrisha Waislam wote kufanye chuki iliyo ndani ya Quran.

Hebu anza moja kwa moja kusoma chuki za Allah:
ALLAH ANAWAAMBIA WAISLAM WOTE KUWA: NI MARUFUKU KUWA MARAFIKI NA WAKRISTO:

Surat Al Maida 51. Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. http://www.quranitukufu.net/005.html

SASA, kama Allah ni Yehovah wa Biblia, mbona hatusomi Mungu wa Biblia akisema muwachukie watu ambao sio wa imani yenu?

SOMA Luka 6:35 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

35 Bali, wapendeni adui zenu, watendeeni mema. Wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo mtapata zawadi kubwa nanyi mtakuwa wana wa Mungu Aliye Juu. Yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na watu waovu.

MUNGU WA BIBLIA ANSEMA Wapendini adui zenu, ni tofauti kabisa na Allah anaye sema WACHUKIENI WAKRISTO NA WAYAHUDI. Allah wa Quran sio Mungu wa Biblia.

ALLAH ANASEMA KUWA, WAISLAM HAWARUHUSIWI KUWAPENDA WAKRISTO HATA KAMA NI BABA ZAO AU MAMA ZAO AU NDUGU ZAO:

Suratul Al Mujaadalah 22. Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa. http://www.quranitukufu.net/058.html

HIVI, kweli bado unaamini kuwa Allah ni? Mbona sifa zake zote ni za SHETANI wa aliye semwa kwenye Biblia?

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA WAISLAM WASIWAFANYE WAKRISTO NA WAYAHUDI KUWA MARAFIKI ZAO.

Surat An Nisaai 144. Enyi mlio amini! Msiwafanye Wakristo na Mayahudi kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu? http://www.quranitukufu.net/004.html

Allah anaendelea kuonyesha sifa za Shetani. Leo anasema na kuwaamrisha Waislam kuwa, WASIWE NA URAFIKI NA WAKRISTO. Hivi Mungu gani huyu anaye penda kuchonganisha watu? Hii tabia ya chuki ni ya nani kama si SHETANI?

Hebu tumsome YESU WA KWENYE BIBLIA ANASEMA NINI?

‘Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. MWIVI HAJI ILA AIBE NA KUCHINJA NA KUHARIBU; MIMI NALIKUJA ILI WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. ‪#‎YOHANA‬ 10:7-15

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA WAISLAM NI MARUFUKU KUWA NA UMOJA NA WASIO WAISLAM

Surat Al Imran 118. Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.

Allah anaendelea kupanda chuki kubwa kubwa kwa Waislam, sasa anasema kuwa Waislam wasiwe na wasiri na watu ambao sio Waislam, hata kama huyo mtu ni Baba yao, mama yao nk. Hii chuki inapatika kwa SHETANI na sio Mungu wa kwenye Biblia.

ALLAH ATEREMSHA YA NA KUSEMA KUWA WAKRISTO NI MAADUI ZA WAISLAM.

Surat An Nisaai 101. Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.

ALLAH AWAAMRISHA WAISLAM KUWAKATAA WAKRISTO

Surat Al Mumtahinah 4 ...............Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake.

ALLAH AWAAMRISHA WAISLAM KUPIGANA NA KUWAUWA WAKRISTO.

Surat Tawba 123. Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mngu

Mwana wa Mungu siku zote Shetani kazi yake ni kuiba, kuua na kuharibu. Ndiyo kazi yake. Hajawahi kubadilika. Toka afukuzwe mbinguni hiyo ndo imekuwa kazi yake hapa duniani. Na Bwana Yesu amelisema hilo bila kumung’unya maneno. Bwana Yesu dhamira yake ni kutupa uzima tele.

Adui siku zote amekuwa ni muuaji tu. Kila sehemu anakopita yeye ni mharibifu. Huwa inafika mahala najiitisha kikao na kujiuliza sisi wanadamu tuna matatizo gani. Kwa nini kufanya urafiki na Shetani na kukubali kuwa mtumwa wake? Unapokubali kuwa mtenda dhambi maanake umekubali kufanya urafiki na Shetani maishani mwako.

Mwana wa Mungu Bwana Yesu anasema yeye amekuja ili wanadamu WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE.

Ikiwa adui amepora chochote ndani yako, ameua chochote ndani yako, amefanya uharibifu wowote ndani yako, ndani ya ndoa yako, au ndani ya familia yako, ndani ya kazi yako, ndani ya biashara yako, katika ukoo wako, kwa watoto wako, kwa wazazi wako, basi nakutangazia BWANA YESU ALIKUJA ILI UWE NA UZIMA, KISHA UWE NAO TELE. Ni ombi langu Bwana akupe uzima tele katika kila eneo adui alifanya uharibifu. Kama ilikuwa kwenye ndoa, kwenye biashara, kwenye kazi, kwenye kuutafuta uso wa Mungu. katika kupata watoto, kupata mume, kupata mke n.k Bwana akupe hitaji lako.

Shetani yuko chini ya miguu yako mpendwa, simama kurudisha chochote adui alikuwa amefanya uharibifu dhidi yako na usikubali kushindwa na Shetani. Yesu aliyemo ndani yako ni mkuu kuliko Shetani. Anataka akupe uzima tena uzima tele.
Barikiwa sana.

Yamkini unataka kuokoka? Basi wasiliana nasi tukusaidie
kuchukua uamuzi mwema wenye busara maishani mwako.

Yesu anakupenda.

Max Shimba Ministries

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW