TUNAZIDI KUCHAMBUA HOJA ZA MIHADHARA YA KIISLAMU;
LEO TUANGALIE JUHUDI ZA WAHADHIRI KUTAFUTA UTABIRI WA MUHAMMAD MWANA WA ABDALAH KWENYE BIBLIA:
Nabii Isaya ameandika kwamba: Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi (Isaya 29:12).
Waislamu walipoona andiko hili wakadhani kuwa tayari wameshapata ushahidi kuwa Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia kwa kuwa Muhammad alikuwa ni mtu ambaye hakuwa amesoma.
Ukifuatilia sura nzima ya 29 na mantiki iliyozaa mstari huu wa 12, unaweza kuishia kucheka tu, ingawaje hili si jambo la kucheka.
Wanachofanya Waislamu ni upotovu mkubwa ambao unaangamiza mamilioni ya watu wa Mungu milele katika jehanamu ya moto. Watu wanaaminishwa uongo na wao wanaukumbatia kana kwamba ni ukweli.
Kwa ujumla, ukisoma sura ya 29 ni sura ambayo inatamka hukumu juu ya Ariel (Yerusalemu) kutokana na uasi wao juu ya sheria na maagizo ya Mungu, Yehova. Hebu tusome sura hiyo kwa Taratibu:
1 Ole wa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi alifanya kituo chake ndani yake; ongezeni mwaka baada ya mwaka; sikukuu na zirudi wakati wake,
2 ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli.
3 Nami nitapiga kimo juu yako pande zote, nitakuhusuru kwa ngome, nami nitajenga maboma yakuzunguke.
4 Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong'ona toka mavumbini.
5 Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula.
6 Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.
7 Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, nao wamwudhio, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.