
Waraka wa 1 Yohana 3:4-10 unasema “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhiirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwuona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa ibilisi; kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.”
DHAMBI NI UASI
1 Yohana 3:4 inasema “ Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi."
Mtu yeyote anayefanya dhambi anaasi zidi ya Mungu. Yaani anamkosea Mungu. Ni kama vile Adamu na mkewe walivyoasi katika bustani, Mungu aliyowaweka, aliwaambia kwamba wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hawakutii kama Neno la Mungu linavyosema kwenye Mwanzo 2:16-17 “Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” Na kwa sababu hiyo dunia nzima wakaingia kwenye uasi wao kama Neno la Mungu linavyotuambia katika Warumi 5:12 “ Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Na Warumi 5:19a inasema “ Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya mwenye dhambi,..” Kwa sababu hiyo mtu yeyote ambaye hajaokoka kwa kumuamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake anaendelea kuwa muasi kwa Mungu. Na yeyote anayeendelea na dhambi yeyote anafanya dhambi na ni muasi. Yeyote asiyefuata Neno la Mungu, ni muasi pia na Yeyote anayeshikilia mafundisho ya dini yake badala ya mafundisho ya Neno la Mungu, naye ni muasi pia, Wapo wale wanaobatiza watoto wachanga na watu ambao hawajatubu dhambi zao, wote hao wanajumuisha kwenye kundi la waasi kama Neno la Mungu linavyosema kwenye Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa la moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
Nitaendelea tena siku nyingine endelea kufuatilia somo hili mpendwa rafiki yangu. Mungu akubariki sana.
JAMBO LA MUHIMU SANA KUFANYA


















