Tuesday, January 17, 2017

KWA NINI NAKATAA KUWA MUISLAMU?


Image may contain: text

Katika ulimwengu wa leo kuna njia nyingi za kutumaini. Furaha ya milele na Mbinguni vina hubiriwa kila mahali. Hata hivyo kuna dini na imani nyingi tofauti, filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo (furaha ya milele) vinatofautiana. Na kila mmoja katika tofauti hizo za dini au imani na filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo; anaamini ya kuwa amesimama katika ukweli.
ALLAH AMEKWISHA WAHUKUMU WAISLAM WOTE KUINGIA JEHANNAM:
Katika Surat Maryam, Quruan inasema kuwa (19) 71.72. wala hapana yoyote ila mwenye kuifikia Jehanamu, maana ni wajibu wa Mola wako umekwisha kuhukumiwa, nasi tutawaokoa wale wamchao na kuwaacha madharimu hali wamepiga magoti.
Quruan inakiri kuwan kila MUISLAM amekwisha hukumiwa kuingia Jehannam kwa maana huo ndio wajibu wa Allah kuwaingiza WAISLAM Jehannam. Allah anaendelea kusema kuwa, yeye atawaokoa Waislam baada kuingia Jehanam.
Je, haya madai ni kweli?
WAISLAM WOTE KUINGIA JEHANNAM:
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jehannamu wadhalilike.
Katika Surat Ghaafir Allah anaendelea kusema kuwa Waislam wote wataingia Jehannam. Mimi kama Mkristo siwezi kuipenda dini hii ambayo teyari Allah wake amesha toa hukumu ya kwenda Jehannam kwa wote wanao ufuata Uislam.
Zaidi ya hapo, katika Surat Maryam, Allah ameshindwa kutueleza ni kivipi atawatoa watu Jehannam, bali ameweka madai tu kuwa atakuja huko na kuwatoa Waislam.
ALLAH NA YEYE KUIJAZA JEHANNAM KWA MGUU:
Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 371
Imeletwa kwenu na Anas:
Nabii wa Allah alisema: Watu watatupwa katika Jihannam, na Jihannam itasema. "Je, hakuna watu zaidi wa kuingia huku Jehannam?" (50.30) Mpaka Allah atakapo weka Mguu wake Jehannam, na Jihannam itasema, Inatosha, inatosha (qat! qat!)
Katika Sahihi hadith hapo juu, tumesoma kuwa, naye Allah atauweka mguu wake Jihannam, kwasababu Jehannam bado ilikuwa inaita watu waingie huko na au labda ilikuwa bado haija jaa.
Je, wapi tumesoma kuwa Allah aliutoa Mguu wake Jehannan?
Wapi aya ambayo inatuambia kuwa Allah aliingia huko ili awatoe Waislam ambao teyari walisha hukumia kwenda Jehannam kutokana na Surat Maryam?
Ndugu wasomaji, Njia ya kwenda Mbinguni haipitii Jehannam kama ambavyo Allah anadai kwenye Surat tulizozisoma hapo juu. Jehannam haipo pembezoni mwa Mbinguni kama Allah anavyo wafundisha Waislam.
BIBLIA INAKUJIBU:
Biblia ina jibu swali hilo ikisema kamwe waliotumia njia ya motoni kutaka kutokea peponi kamwe hawataiona.
Luka 16:24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Hii aya ya Biblia inatuhakikishia kuwa, kuna sehemu mbili ambazo zitakuwa na au Walio mwabudu Mungu au wali mwabudu Shetani. Biblia haisemi kuwa wote wataingia Jehannam alafu Mungu atakuja huko Jehannam na kuchukua watu wake, la hasha.
Neno la Mungu linaendelea kusema kuwa: Mithali 16:25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Ndugu msomaji. Biblia imesha tufundisha kuwa mwisho wa njia ya Allah (Surat Maryam 72-73) ni Motoni ambako kumesemwa katika Mithali 16:25.
Ndugu zanguni, hii ni moja sababu nyingi zinazo nifanye niukatae Uislam, maana teyari umesha hukumu wafuasi wake na kuwasweka Jehannam.
Sasa, mimi kama Mkristo kwanini niupende Uislam ambayo unapeleka watu Jehannam?
Karibu kwa Yesu ambako kuna uzima wa Milele. Yohana 14: 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Na kwa mujibu wa Neno la Mungu, Yesu Kristo ndiye NJIA, Mtu hawezi kuja kwa BABA pasipo kupitia kwake (Yohana 14:6).
Kuna wengi hawajui kuwa Yesu Ndiye Hii Njia Nyembamba Iendayo Uzimani…
Hawa akili zao zimetiwa GIZA na Ibilisi (mungu wa dunia hii aka Allah) Ili Isiwazukie Nuru Ya Wokovu, wakamwamini Yesu aliye Utukufu wa Mungu na Sura Ya Mungu (2 Wakorintho 4:3-4).
Hatua ya pili mara baada ya kujua kwa Yesu Ni Njia Kweli Na Uzima na ya kuwa alikufa Msalabani kuchukua DHAMBI na Uovu Wako, lazima sasa UKUBALI ukweli huu moyoni mwako, UAMINI moyoni na kukiri waziwazi kwa kinywa chako ili uweze kupata Wokovu na pia khesabiwa haki (Warumi 10:9-10).
Tunapomwamini Yesu na kazi ya Msalaba, tunachukua SEHEMU YETU YA UKOMBOZI toka Msalabani, na kuimilki kisheria.
wako watu wengi wanaijua njia [Wametimiza Hatua Ya Kwanza] lakini kwa kweli hawaja chukua hatua ya KUYATOA maisha yao kwa Yesu, yaani kuingia kwenye Njia, yaani KUOKOKA!
Watu wengi tuliomo nao kwenye madhehebu na Dini zetu ni watu ambao wako hatua ya kwanza. Lakini lazima uchukue hatua ya pili, uingie kwenye Njia
“Yeye atakayenikiri mbele za watu nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye Mbinguni, bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye Mbinguni,” Mat. 10:32-33.
Yesu Kristo Mwana wa Mungu hakika ndiye, “Njia na Kweli na Uzima.” Hakuna atakaye okoka isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo. Kama ukimwamini Yesu leo na kumtii ujue ya kuwa furaha na amani na uzima vita kuwa vyako; sio katika ulimwengu huu tu, bali na katika ulimwengu ule ujao.
Hizi ndizo sababu chache kwanini nakataa kuwa Muislam.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries Org

KWANINI ALLAH ALIUMBA UCHAWI?

Image may contain: text
Nimenukuu Quran aya ya 2:102 na maelezo/ufafanuzi wake hapo chini kutoka tafsiri mbili za Quran (Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy na Tafsiri ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani). Aya hii na maelezo/ufafanuzi wake inaonesha mambo yafuatayo:
(a) Uchawi umeteremshwa na Malaika wa Allah
(b) Kuna wachawi wa Kiislam.
(c) Uchawi ni amali ya Ukafiri
Pia, kwa mujibu wa Sahih Bukhari juzuu ya 4, Kitabu cha 54, Hadithi namba 490 na Sahih Bukhari, juzuu ya 7, kitabu cha 71, hadithi namba 658; Muhammad alirogwa na akazurika na uchawi. Kisa cha mtume kurogwa na kuzurika na uchawi pia kinasimuliwa katika Quran Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy ukurasa wa 977 na 978.
Swali (a) Ikiwa uchawi ni ukafiri, Kuna uhusiano gani kati ya Allah na ukafiri mpaka atelemshe uchawi?
(b)Mtume Muhammad alirogwa na wachawi wa kiislam au wachawi wengine?
(c) Mtume Muhammad alirogwa na uchawi ulioteremshwa na malaika wa Allah au uchawi mwingine?
(d) Mtume au nabii gani mwingine alirogwa na akaathirika na uchawi?
Quran 2:102 inasema:
Wa Attaba`ū Mā Tatlū Ash-Shayāţīnu `Alá Mulki Sulaymāna Wa Mā Kafara Sulaymānu Wa Lakinna Ash-Shayāţīna Kafarū Yu`allimūna An-Nāsa As-Siĥra Wa Mā 'Unzila `Alá Al-Malakayni Bibābila Hārūta Wa Mārūta Wa Mā Yu`allimāni Min 'Aĥadin Ĥattá Yaqūlā 'Innamā Naĥnu Fitnatun Falā Takfur Fayata`allamūna Minhumā Mā Yufarriqūna Bihi Bayna Al-Mar'i Wa Zawjihi Wa Mā Hum Biđārrīna Bihi Min 'Aĥadin 'Illā Bi'idhni Al-Lahi Wa Yata`allamūna Mā Yađurruhum Wa Lā Yanfa`uhum Wa Laqad `Alimū Lamani Ashtarāhu Mā Lahu Fī Al-'Ākhirati Min Khalāqin Wa Labi'sa Mā Sharaw Bihi 'Anfusahum Law Kānū Ya`lamūna
Quran 2: 102(Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy) inasema: Wakafuata yale waliofuata mashetani wakadai kuwa yalikuwa katika ufalme wa (Nabii) Suleiman; na Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi (waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani na uchawi) ulioteremshwa kwa malaika wawili, Harut na Marut, katika (mji wa) Babil. Wala Malaika hao hawakumfundisha yoyote mpaka wamwambie: “ Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru.” Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo). Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa mambo hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza ambayo yatawazuru wala hayatawafaa Na kwa yakini wanajua kwamba aliyehiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za Akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya hivi). (Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy ukurasa 25-26)
Nanukuu Maelezo/ Ufafanuzi wa Quran 2: 102
Suleiman aliyetajwa hapa ni nabii, Mayahudi wanamwita Nabii Suleiman kuwa ni mfalme aliyepata ufalme kwa uchawi, si Mtume. Basi na hawa wachawi wa kiislam humnasibishia Nabii Suleiman hizo ilimu zao za uchawi. Basi Mwenyezi Mungu anamkanushia haya. Na aya hii yaonesha wazi kuwa (a) uchawi ni amali ya ukafiri na (b) kuwa mchawi hawezi kumdhuru mtu ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na (c) kuwa mchawi mwenyewe anadhurika kwa uchawi wake. Na anataja hapa Mwenyezi Mungu kuwa nyuma huko kabisa katika zama za mfalme
Quran 2:102.(Tafsiri ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani) Inasema:
Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.
SWALI LA KUJIULIZA:
HIVI KWANINI ALLAH ALIUMBA UCHAWI NA KUUTEREMSHA KWA BINADAMU?
MIMI SIWEZI KUMPENDA HUYU ALLAH AMBAYE AMEUMBA UCHAWI.
Karibuni kwa Yehova ambaye hakuumba UCHAWI.
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

Monday, January 16, 2017

ROHO, NAFSI NA MWILI

Image may contain: cloud, sky, text and outdoor
Ndugu msomaji,
Je, mwanadamu ni nani?
Kwa kifupi ninaweza kusema kuwa Mwanadamu ni Roho, ina Nafsi na inakaa ndani ya Mwili.
Ukisoma 1 Wathesalonike 5:23 Inatusaidia Kuona maeneo yote matatu ya mwanadam/mtu;
"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU Mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo"
Hapa unaona Nafsi, Roho na Mwili vimetajwa kwenye hiyo aya.
ROHO NI NINI?
Roho ambayo inahusisha mambo ya Mungu.
Ni ile sehemu ya mtu yenye ufahamu wa Mungu, ambayo hufanywa hai na hutiwa nguvu na Roho wa Mungu wakati wa Wokovu. Kabla ya mtu Kuokoka, sehemu hii, haifanyi kazi kwa utimilifu kabisa kwa sababu ya dhambi. Dhambi huifanya kuondolewa nguvu ya kutenda kazi sawa sawa, kwa Amani na Roho ya Mungu. Lakini kupitia Ubatizo wa Roho Mtakatifu, mwanadamu hupokea nguvu ya kiroho, inayomwezesha kuishi maisha ya Kristo.
Roho inahusika na:-
i) Maombi na Ibada na Mungu,
ii) Ushirika na Mungu,
iii) Mapokezi ya karama za Roho,
iv) Vita vya kiroho,
v) Kuunda Mawazo na Ndoto,
vi) Dhamira, Kupambanua,
vii) Udadisi, Kuuliza,
viii) Ufahamu, Kutafsiri,
ix) Shuhuda kwa Wanadamu
NAFSI NI NINI?

UTATA NDANI YA QURAN. "AYA ZA QURAN ZAPINGANA"

No automatic alt text available.


HUU NI MSIBA MKUBWA SANA KWA WAISLAM:
Sura Al-Baqara 2:109
Wengi wa watu wa kitabu, kutokana na wivu wao, wanatamani kuwarudisheni kwenye kutoamini baada ya kuwa mmeamini, pamoja na kwamba ukweli umeshadhihirishwa wazi mbele yao. Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake. Yeye ana nguvu juu ya kila kitu.
Quran pia inawaagiza Waislamu katika Sura Al Imran 3:20 kwamba:
... if they give no heed, then your only duty is to warn them.
Yaani:
... kama wasipowasikiliza, basi ninyi kazi yenu pekee ni kuwaonya tu.
Kwa hiyo, kutokana na aya hizi mbili, yaani Al-Baqara 2:109 na Al Imran 3:20, tunaona mambo yafuatayo:
1. Ni wajibu wa Waislamu kuhubiri dini yao lakini si wajibu wao kuwalazimisha watu kuamini dini yao.
2. Allah kwa wakati wake atawafunulia wale wasioamini ukweli wa mambo.
3. Ni wajibu wa Waislamu kutoa maonyo tu kwa wale wanaowahubiria.
LAKINI, HEBU TAZAMA AYA ZIFUATAZO UONE KIZUNGUMKUTI KWENYE HII DINI YA KUTENGENEZA:
Al-Nisa 4:101
Wale wasioamini ni maadui zenu wakubwa.
Vilevile inasema katika sura Al-Tawba 9:3
Tangazeni mapigo makuu (ya ole) kwa wasioamini.
Pia quran inasema katika sura Al-Anfal 8:39
Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.
MASWALI WANAYO YAKIMBIA WAISLAM:
1. Je, aliyempa Muhammad maneno ya Quran 2:109, Quran 3:20 na yale ya Quran 4:101, 9:3, 8:39 ni huyo huyo au ni wawili tofauti?
2. Iweje aseme kuwa usiwalazimishe watu kuamini bali waonyeni na kuwavumilia tu, kisha anageuka sehemu nyingine na kusema walazimisheni, tena kwa vita?
3. Je, hii si ishara ya tabia ya usahaulifu ambayo si tabia ya Mungu bali ni ya mwanadamu?
4. Kama ni huyo huyo, je, aya hizi zinafanana au zinapingana?
5. Kama zinafanana, ni kwa vipi?
6. Kama zinapingana, huu si ushahidi tayari kuwa quran haitoki kwa Mungu wa kweli kama ambavyo quran yenyewe imeweka kigezo cha kujua hilo? Maana Mungu wa kweli hawezi hata kidogo kusahau jambo alilolisema kabla halafu aje aseme kitu tofauti. Ni viumbe tu ndio wanaweza kusahau na kukosea.
Hakika Quran si kitabu cha Mungu. Waislam nawakaribisha kwa Mungu wa Biblia ambaye alimtuma Mwanawe kuja Duniani kwa ajili ya dhambi zetu.
Karibuni kwa Yesu.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba Minsitries Org.

KORAN YAKUFURU KUHUSU ROHO MTAKATIFU


JE, MUHAMMAD AU JIBRIL NI ROHO YA KWELI/ROHO MTAKATIFU?
Leo nitawajibu Waislam wote duniani kwa kutumia Biblia Takatifu kuwa Muhammad hakuwa Roho ya Kweli kama alivyo ahidiwa na Yesu Kristo ambaye ni Bwana na Mwokozi wetu.
Mara nyingi Waislam wanauliza, "Roho ya Kweli ni nani ambaye Yesu alimuhadi katika Yohana 16 aya ya 12 mpaka 14.
Nimekuwa nikiwauliza Waislam, hivi wao wanafikiri huyu Roho wa Kweli ni nani? Na wakanijibu kuwa huyo Roho wa Kweli ni Malaika Jibril.
Yohana 16:13 inasema: Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Zaidi ya hapo, Waislam wengi wanadai kuwa, Yesu alikuwa anamtabiri Muhammad, na wakati huo huo, wengine wanasema kuwa alikuwa anatabiriwa Jibril. KINYUME CHAKE, kama ilivyo shahidiwa katika Yohana 16 aya 13, Yesu alikuwa anamzungumzia Roho Mtakatifu. Tunafahamu hili kwasababu Yesu anamzungunzia Roho ambaye atawaongoza Wanafunzi wake kuanzia wakati huo na sio miaka mamia baadae.
Ukiisoma Biblia kwa makini kuanzia Yohana 16 aya ya 5 mpaka 15 utagundua hapo hapo kuwa Waislam wote pamoja na Allah wao ni waongo.
Lakini, kuna njia nyingi tunaweza kuzitumia kufahamu kama Waislam wako sahihi katika ufafanuzi wao kwa kuangalia na au soma kila wakati Yesu alipo sema "ROHO" katika Injili hiyo hiyo ya Yohana na tuone kama kweli alikuwa anamtabiri Muhammad wa Waislam katika aya mojawapo.
UTHIBITISHO WA KWANZA:
Yohana 1 aya ya 32 inasema: Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake "YESU".
Wote tunafahamu kuwa Muhammad hakuwa Mtakatifu na vile vile hakuwa anapaa kama ndege na alikuja miaka 600 baada ya Kristo, hivyo basi, ni dhahiri kuwa Roho Mtakatifu sio Muhammad ambaye alikuja miaka 600 baadae. Yohana hakuwai mwona Muhammad.
UTHIBITISHO WA PILI:
Yohana 1:33, [ Yohana Mbatizaji anaendelea kusema] "Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu."
Yohana anaweka kiuwazi zaidi aya hiyo hapo juu kuwa Yesu ndie atakaye kuwa anabatiza kwa Roho Mtakatifu.
Kwa kifupi Yesu atamtuma ROHO ambaye ni Mwenye Nguvu ya Mungu na ni Mungu.
Je, Muhammad ni huyo Roho? HAPANA KABISA, kwasababu Yesu aliwabatiza Wanafunzi wake na zaidi ya hapo, wafuasi wake walibatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. Mda mchache baada ya Yesu kupaa kwenda kwa Baba yake Mbinguni, hivyo basi, na narudia tena, hii ilifanyika Miaka mia sita 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa. Wanafunzi wa Yesu hawakubatizwa kwa kupitia Muhammad wala Waislam hawabatizi au batizwa.
UTHIBITISHO WA TATU:

LINI ALLAH ATAZUNGUMZA NA MUHAMMAD?

Image may contain: text
Ndugu zanguni,
Hili swali limeenda shule.
Leo ningependa tujikumbushe mambo machache ambayo labda hatukuyatilia maanani. Mitume wote na manabii wote wa Biblia waliwai ongea na Mungu. Lakini, Mtume wa Allah "Muhammad" hakuwai ongea na Mungu HATA MARA MOJA. Je, utume wake tutauamini vipi maana hakuwai ongea na aliye mtuma?
Lakini Mitume wote wa Biblia waliongea na Mungu.
1. Musa anoangea na Mungu: Kutoka 3:1-21
2. Elia anaongea na Mungu: 1 Wafalme 19- Soma yote
3. Paulo anaongea na Mungu: Matendo ya Mitume 18:9Wagalatia 1:1 Paulo, mtume, si mtume wa wanadamu aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu
Biblia ipo wazi kabisaa, kuwa Paulo alitumwa na Mungu, wakati Muhammad alitumwa na Jibril ambaye si Mungu. Koran inakiri kuwa Muhammad alikutana na Jibril na hakuwai kukutana na au ongea na Mungu hata mara moja. Lakini tunasoma katika Biblia kuwa, Paulo alipewa utume na Mungu mwenyewee.
Warumi 1:1 Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, ALIYEITWA KUWA MTUME na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu.
Hiyo ni mifano michache kutoka Biblia.
Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu aliye Mtuma? Maana ya neno Mtume kwa kifupi: Ni Mtu aliye tumwa.
HEBU TUANGALIE, HUYU MUHAMMAD ALIZALIWAJE?
1.KUZALIWA KWAKE,
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa "Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa na shetani tangu alipozaliwa, (Fat'hul Baary Juzuu ya 6 Uk. 389).
Je, kuna ushahid wowote ule kuwa Muhammad alitolewa Shetani? Kama upo Basi Waislam, tuleteeni tuuone.
2.BAADA YA KUTOKA PANGONI,
Basi Mtume akafanya khofu, akarejea kwa mkewe, akamhadithia, na pale pale homa kubwa kabisa, ikampanda, akataka afunikwe maguo, akawa anatetemeka kwa ngerema, na kuweweseka, na kusema, "Najikhofia nafsi yangu, kuchezewa na mashetani, na kuniharibu akili yangu na kunizuga"(Kitabu cha maisha ya Nabii Muhamaad s.a,uk.17 kilichoandikwa na Sheiky A.Farsy).
KUFUATANA KITABU CHA MAISHA YA NABII MUHAMMAD, tunajifunza kuwa Muhammad kwa mara ya kwanza kabisa alipata utume wake pangoni baada ya NAFSI YAKE KUCHEZEWA NA MASHETANI.
MASWALI:

ALLAH HAJUI SAYANSI YA DARASA LA TANO

Image may contain: 3 people, text
Ili kumpima Allah kama kweli aliumba kila kitu, leo tutamia Sayansi na tuone kama atapasi "Litmus Test". Maana ni rahisi sana kujua kama Uislam ni dini ya Mwenyezi Mungu au ulitengenezwa tu na Muhammad.
SOMA:
Surat Al Kahf 18:86 inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi ya maji yenye tope.
Unadhani hii ni sahihi. Jua lina joto la zaidi ya nyuzijoto 6000 kwenye uso wake. Lakini maji yakifika nyuzijoto 100 yanageuka mvuke. Je, maji yanayotajwa kwenye surat Al Kahf ni maji gani? Unadhani ni Mungu aliyeumba jua na maji ndiye anayesema haya?http://www.quranitukufu.net/018.html
SASA MUHAMMAD NA YEYE ANASEMA KUWA JUA LINAZAMA KWENYE CHEMCHEM YA MATOPE
Dhu al-Qarnaiyn [Zul Qarnain] "alishuhudia kuzama kwa jua kwenye sehemu yake ya kupumzikia kwenye bwawa lenye ute mweusi na wenye harufu mbaya sana." al-Tabari juzuu ya 5 uk.173-174 (Tazama Sura 18:82-97).
Katika Al Tabari hapo juu tumesoma kuwa jua hupumzika kwenye bwawa lenye ute mweusi. Unadhani hii ni sahihi. Jua lina joto la zaidi ya nyuzijoto 6000 kwenye uso wake. Lakini maji yakifika nyuzijoto 100 yanageuka mvuke. Je, maji yanayotajwa na Muhamamd kwenye hadith hii ni maji gani? Unadhani ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyeumba jua na maji ndiye anayesema haya?
MUHAMMAD ANASEMA KUWA ETI JUA LINAPOROMOKA TOKA KITI CHA ENZI MPAKA KWENYE BAHARI.
" [Muhammad] Aliendelea. Wakati jua linachomoza, linainuka juu ya kibandawazi (kinachokokotwa na farasi) toka kwenye moja ya chemchemi hizo likiwa pamoja na malaika 360 …. Wakati Mungu anataka kuvijaribu jua na mwezi, ili kuwaonyesha watumishi wake ishara na kwa njia hiyo kuwataka waache kutokumtii Yeye na kuanza kutii, jua huporomoka ghafla toka kwenye kibandawazi na kuanguka kwenye kina cha bahari, ambacho ni cha mduara.
Wakati Mungu anataka kuongeza umuhimu wa ishara kuwatisha zaidi watumishi wake, jua lote hunguka, na hapawi na sehemu yake yoyote inayobaki kwenye kibandawazi. Huko ndiko kupatwa kukamilifu kwa jua, wakati ambapo mchana hujiwa na giza na nyota hutokeza." al-Tabari juzuu ya1 uk.236.
Tunaendela na kumuumbua Allah na Muhammad: Kwenye hadith hapo juu, Muhammad anasema kuwa Jua linakokotwa na Farasi.
(i) Jua lina kipenyo cha (radius of the sun is) 432,450 miles (696,000 kilometers) na ukubwa wa 1.4 x 1027 cubic meters. Ikimaanisha kuwa ni sawa na dunia milioni moja na nukta tatu (About 1.3 million Earths could fit inside the sun.). Uzito wa jua ni sawa 1.989 x 10 kipeo cha 30. [Nisawa na uzito wa dunia mara 333,000]
(ii)Lakini Allah anadai eti hilo Jua lenye huo uzito na huo ukubwa linabebwa na farasi. Zaidi ya hapo, joto la jua peke yake litawaunguza hao Farasi na kuwa masizi.
(iii) Allah anaendelea kudai kuwa Jua hilo lina anguka kwenye kina cha Bahari. Hivi jua lenye ukubwa mara milioni moja nukta tatu zaidi ya dunia, linawezaje kuingia kwenye kina cha bahari ambayo ni sehemu tu ya dunia?
Ndugu msomaji, je, wewe bado unaendelea kumfuata huyu Allah amabye hajui hata sayansi ya kawaida tu?
Muislam anasema eti, Allah kaumba kila kitu, huku akishindwa vibaya sana sayansi ya kawaida tu, tena ya darasa la Tano.
HUU NI MSIBA MKUBWA SANA KWA WAISLAMU NA MUHAMMAD WAO.
ALLAH HAJUI SAYANSI NA HIVYO BASI HAWEZI KUWA MWENYEZI MUNGU ALIYE UMBA KILA KITU.
NDIO MAANA HUWA NASEMA, UISLAM NI DINI YA KUTENGENEZA TU NA HAUKUWEPO KABALA YA KUZALIWA MAREHEMU MUHAMMAD.
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries Org.

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA TATU)

Image may contain: one or more people and text
Je, Isa bin Mariamu ni Mwana wa Mungu?
Kama kuna jambo ambalo Allah mungu anayeabudiwa na Waislamu analikataa sana kupitia Quran basi jambo hilo si lingine bali ni YESU KUWA MWANA WA MUGU. Allah ansema hivi.
Sura 6:101 – Yeye ndiye muumba wa mbingu na ardhi, inamkinikaje awe na mwana, hali hana mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.
Quran 9:30 – Na Mayahudi wanasema ‘uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ na ‘wakristo wanasema Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale walilkufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa?
Hili ni agizo la kutisha kwamba Wakristo na Wayahudi tuangamizwe kwa kuwa tunaamini Mungu ana Mwana, au wana, lakini Wakristo tunaoamini hivyo kwa sababu Mungu wetu:-
- Yehova alifundisha kuhusu Bwana Yesu hivi:
Kutoka 4:22…Israeli ni Mwanangu Mimi……
Mathayo 17:5……Huyu ni Mwanangu Mpendwa wangu….
Malaika wa Mungu alisem hivi.Luka 1:30-31, 35 – Malaika akamwambia usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kuvuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.
Hivyo basi Isa wa kwenye Quran siyo Mwana wa Mungu lakini Yesu wa kwenye Biblia ni Mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.
Leo tumejifunza tena kuwa, katika Quran Allah kakiri kuwa yeye hana Mwana, lakini kwenye Biblia Yehovah anasema kuwa Yesu ni Mwana wake.
Mungu awabariki sana na fahamu kuwa Isa wa kwenye Quran sio Yesu wa kwenye Biblia.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Max Shimba Ministries

KUMBE ALIYEANDIKA QURAN ALIKUWA NA SHETANI?

Image may contain: 4 people


Mtu wa Awali, aliyejifundisha kusoma na kuandika katika Mji wa Makka alikuwa Bwana Harb bin Umayya-babu yake Bwana Muawiya. Alijifunza kwa watu wa Yaman, na yeye akaja kuwafundisha waliotaka katika mji wa Makka. Wakati Mtume alipopata utume walikuwako watu 6 tu katika Makka waliokuwa wakijiua kuandika. Wa 4 katika yao waliingia katika Uislamu, wakawa ndiyo waandikaji "Wahyi" (aya za Qur'an), watu hao walikuwa ni Sayyidna Abubakar. Sayydna Umar, Sayyidna Uthman na Sayyidna Ali.
Kitabu cha Maisha ya Nabii Muhammad uk. 8,na Sheiky A.Falsy)
SAYYIDNA ABUBAKAR,
Abubakar, Anasema: "Hakika mimi ninae shetani hunifikia mara kwa mara, basi wakati wowote atakaponifikia muniepuke" (Tabaqatul Kubra, J. 3 Uk. 212)
ETI KORAN IMETEREMSHWA NA ALLAH, THUBUTU
QURAN 2. SURA AL- BAQARA
97. Sema: Aliyekuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwaidhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na niuwongofu na bishara njema kwa Waumini.
SASA KAMA KILIANDIKWA NA MTU ALIYEKUWA NA SHETANI, KWANINI TUSIKUBALI KUWA NI AYA ZA SHETANI?
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

MUHAMMAD ALITAMKA AYA ZA SHETANI KWENYE QURAN

Image may contain: 1 person, meme and text
KWANINI MUHAMMAD ALISHINDWA KUTOFAUTISHA KATI YA ALLAH NA SHETANI?
KWANINI MUHAMMAD ALISHINDWA KUTOFAUTISHA KATI YA AYA ZA MASHETANI NA AYA ZA JIBRIL?
Moja ya matukio yenye kuaibisha zaidi kwenye maisha ya Muhammad lilitokea wakati Shetani alipoweka maneno yake kwenye mdomo wa Muhammad. Muhammad alisema maneno ya Shetani kama neno la Mungu. Tukio hili limethibitishwa kwa maandishi na waandishi kadhaa wa Kiislam wa kale na limeongelewa kwenye Hadithi na Kurani. Waislam wa miaka iliyofuata, kwa kujisikia aibu kuwa nabii wao aliyejitangaza mwenyewe amesema maneno ya Shetani, walikana kuwa tukio hili lilitokea. Visingizio na kukana kwingi vimekuwa vikitolewa na hawa Waislam wa miaka iliyofuata ili kulifunika kosa lenye kuhusisha dhambi la Muhammad.
Ni muhimu ikafahamika tena kuwa tukio la ‘Aya za Shetani’ si jambo ambalo limetungwa na watu wasiokuwa Waislam. Tukio hili limerekodiwa na vyazo vya kale zaidi vya Kiislam vilivyokuwepo wakati wa uhai wa Muhammad. Mtu yoyote asifikiri kuwa jambo hili ni hadithi iliyotungwa na watu wenye kuupinga Uislam. Ni kisa kinachopatikana moja kwa moja kwenye rekodi za kale za Kiislam.
Hili moja ya masomo yenye kubishaniwa zaidi kwenye Uislam. Shetani alimsababishia Muhammad kunena maneno yake (Shetani) kama maneno ya Mungu."
Je Kurani Ilisema Nini Mwanzoni?
Sura ya Nyota (Sura 53) mistari ya 19-20 inasema, "Je umemwona Lat, na ‘Uzza, Na mwingine, (mungu mke) wa tata, Manat?"

Allah alikuwa maarufu huko Arabia kabla ya kuja kwa uislam, kama mungu aliyekuwa na mabinti watatu: al-Lat, al-Uzza, na Manat. (Kumbuka kuwa al- inamaanisha ‘yule’, kwa Kiingereza "the".)
Waandishi wanne wa mwanzo wa maisha ya Muhammad waliandika kuwa awali aya hizi zilifuatwa na:
"Hawa ni mawinchi (wasuluhishi) ambao maombi yao yanapaswa kutumainiwa"
Tafsiri: Mabinti wa Allah walifikiriwa kuwa viumbe wa mbinguni wenye kuomba kwa ajili ya wengine. Mawinchi marefu ya Kinumidia ilikuwa ni sitiari yao. Maneno mbadala ya "inatakiwa kutumainiwa" (turtaja) ni "imekubaliwa kwa kuthibitishwa" (turtada). (Kutoka kwenye tafsiri ya Alfred Guillaume ya The Life of Mohammed, iliyoandikwa na Ibn Ishaq, uk.166.
Baadaye, kifungu hiki kiliondolewa na kifungu kifuatacho kiliwekwa badala yake:
"Nini! Kwako wewe mwenye jinsia ya kiume, Na kwake (mwanaume), mwanamke? Tazama, hakika mgawanyo huu hautakuwa wa haki kabisa." (aya za 53:21-22 leo)
Tafsiri: Wale wanaoamini kuwa Allah alikuwa na mabinti watatu hawakuntendea haki Allah, kwa sababu walipendelea watoto wa kiume ingawa walisema kuwa Allah alikuwa na wasichana tu.
Hizi ndizo ambazo zimeitwa "Aya za Shetani." Katika nyakati za sasa Salmon Rushdie alitumia msemo huu tu kwenye kichwa cha riwaya yake ya kubuniwa na isiyohusika na aya hizi, na andiko hili halikiongelei kisa hiki cha kisasa. Kwa upande wa Aya za Sheatani za asili, Muislam au mtu mwingine asiyekuwa Muislam mwenye kutazama jambo hil bila upendeleo anawezaje kujua aya ambazo zilikuwemo toka awali? Sehemu iliyobaki ya andiko hili inatoa ushahidi wa moja kwa moja na ule usio wa moja kwa moja kuwa Aya za Shetani zilikuwemo asilia, na mapingamizi tisa ya Kiislam.
Kama Muhammad alikuwa mtume wa Mungu, kwanini alishindwa kumtambua Shetani alipo weka aya zaje kwenye mdomo wa Muhammad?
Tutamwamini vipi Muhammad kuhusu aya zingine za Quran kuwa sio za Shetani?
Natanguliza pole kwa muhammadans kwa kuingizwa mjini na Muhammad na kulishwa aya za Shetani.
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Jesus demonstrated He is God

 

TRENDING NOW