1. Adamu na Hawa walifukuzwa kwenye Bustani ya Edeni kutokana na dhambi. Sisi pia tulio uzao wao ni wenye dhambi? Suluhisho la tatizo hili ni moja tu kulingana na Biblia – Yesu Kristo alikufa msalabani na kufanyika sadaka au dhabihu ili sisi tusiendelee kuchinja wanyama kila siku kwa ajili ya dhambi zetu kama torati inavyosema, badala yake tuamini TU katika sadaka ya Yesu na kupokea msamaha wa dhambi na wokovu wa Mungu bure.
Waislamu hamumwamini Yesu Kristo kama mwokozi aliyefia dhambi za wanadamu wote. Je, suluhisho la dhambi kwa mwanadamu ni nini? Kwa maana nyingine, ninyi Waislamu mtaponaje na jehanamu ya moto ilhali ni wazi kuwa ninyi, kama ilivyo kwa kila mwanadamu, mna dhambi ambazo ndizo hizohizo zilimtenga Adamu na Mungu?
2. Biblia inasema: Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:8-9). Kwa hiyo mimi Mkristo nikijikuta nimetenda dhambi nakwenda mwenyewe kwa Bwana Yesu na kumwambia, “Bwana wangu, nimesema uongo, nimeiba, nimetukana, nimetamani, … n.k. naomba unisamehe.” Sisubiri hadi mchungaji au mtu mwingine anikamate kwenye kosa kama polisi wanavyokamata wahalifu.
Ninyi Waislamu mnasema kuwa torati ndiyo njia sahihi ya maisha ya mwanadamu, kwamba mtu akifanya makosa ni lazima aadhibiwe kama vile kupigwa mawe, kuchapwa viboko, kukatwa mikono, n.k.
Swali ni kuwa, kwa nini hatusikii Waislamu wakijipeleka wenyewe kupokea adhabu hizo baada ya kufanya dhambi? Hatujawahi kusikia Mwislamu ameenda kusema, “Jamani nimezini kwa hiyo nimekuja mnipige mawe; Nimeiba, hivyo nimekuja mnikate mkono.” Kwa nini wanaoadhibiwa ni wale TU wanaokamatwa? Mnataka kutuambia kuwa wakosaji ni hao tu? Kama unaamini kuwa mzinzi ni lazima apigwe mawe, si uende ukaombe wakupige mawe baada ya kuzini. Kwa nini hamfanyi hivyo?