
Je Muhamad hakunywa pombe au Quran imekataza pombe hilo ndo swali la kujiuliza. Ukipitia aya za Quran na hadithi za Muhamad utakuta mtume saw alikunywa pombe na pia Quran inaunga mkono na kuruhusu jambo hilo. Bila shaka kuna baadhi ya watu watapinga na kutoa maneno ya kashfa pamoja na matusi lakin lazima ukweli uwekwe wazi. Ingawa baadhi ya madhehebu ya kikristo yanaruhusu pombe lkn leo tutaangalia khs ngd zetu waislam ambao mda mwingi wanawarahumu wakristo eti wanaruhusu pombe.
Kabla ya yote ebu tutazame aya zinazokataza pombe ktk Quran
Quran 2:219. Wanakuuliza juu ya ULEVI na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa namanufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Nawanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri.
Hilo neno dhambi katika baadhi ya tafasiri za kiingereza limetumika Harm km ifuatavyo na ktk tafasiri ya kiarabu hamna neno dhambi ktk aya hiyo …….
Kwahiyo katika aya hii hakuna amri ya kukataza pombe moja kwa moja, huko mbele tutaona zaidi, ingawa hiyo aya ilikuwepa waislam na muhamad bd waliendelae kunywa pombe.
Quran 4 :43. Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali MMELEWA,………
Hii aya haikatazi pombe bali inatoa ushauri juu ya waislam ambao walikuwa wana Sali huku wamelewa.
Aya zinazoruhusu pombe ktk Quran
Quran 16: 67. Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ULEVI na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanao tumia akili
Quran 47:15. Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya ULEVI yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?










