Tuesday, August 22, 2017

KAMA ALLAH SIO MUNGU WA KIPAGANI, KWANINI BABA YAKE MUHAMMAD AMBAYE ALIKUWA MPAGANI ALIITWA ABDULLAH?

Image may contain: one or more people, crowd and text
(Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.
Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?
Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozo wetu.

KAMA UNAMPENDA RAFIKI YAKO, MWAMBIE UKWELI AMBAO NI MCHUNGU

Image may contain: one or more people and text
Wengi tumejikuta tukiona ni vyema tukaambiwa yasiyo na ukweli maishani mwetu na kudanganywa ilimradi tu yanaturidhisha wakati huo lakini ajabu tunachukia na kutopenda ukweli ambao hata kama unaumiza lakini faida yake ni kubwa sasa na pia mbele twendako.
MITHALI 27: 5 Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika. 
6 Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
7 Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
Huwa natumiwa lawama kila siku, kwanini natoa mada chungu kwa Waislam kila siku?
Leo nimewajibu wale wote wanao ulizo hilo swali kwa kutumia aya.
Ukweli unaweza kukumiza lakini, kwa kusema uongo unaweza kuumia milele,Ni wazi kuwa watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, na wakati mwingi baadhi ya watu husema uongo huku wakifikiri kufanya hivyo ni kujipa matumaini katika jambo fulani, lakini ukikaa na kufikiria unaposema uongo au unapokataa ukweli ujue unajidanganya mwenyewe na siku zote utabaki kuwa na maumivu moyoni mwako kutokana na kuishi na uongo ndani ya moyo wako.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

MUHAMMAD ALIPEWA UTUME NA MKEWE KHADIJA

Image may contain: 1 person, smiling, text
Alipokuwa pangoni alichezewa na Shetani: Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya:
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
Katika tukio hili lililompata Muhammad akiwa pangoni , ndipo Waislamu wote ulimwenguni wanapolieleza kuwa hapo ndipo Muhammad s.a.w alipoletewa wahyi (ufunuo) na kupewa unabii na utume. Lakini unapotafakari juu ya ujumbe huo utaona kuwa hata yeye mwenyewe hajui nini kilichokuwa kimemtokea kule pangoni.
Ndiyo maana tunasoma kuwa alipofika nyumbani kwake mkewe Bi. Khadija alimfunika nguo mumewe akidhani ana homa. Muhammad alimweleza mkewe kilichomtokea kuwa ni “Shetani” hakumsema malaika yeyote kama Waislamu wanavyotaka kutuaminisha leo. Kwa sababu kama angekuwa ni malaika kama tunavyosoma ndani ya Biblia, asingesita kujitambulisha kwa Muhammad kuwa yeye ni nani. Hii ni hoja ya kwanza.
Mwisho wake Bi Khadija akamsimika UTUME Mume wake Muhammad.
Leo umejifunza kuwa Muhammad alipewa utume na Mkewe.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
www.maxshimbaministries Org

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: text
Ibn Isaq/Ishaq (aliyekufa mwaka 145/767 au 151/773 BK) alikuwa Msuni wa mlengo wa Kishafi ambaye baadaye alianzisha shule yake mwenyewe iliyodumu kwa muda mfupi. Aliandika kitabu kiitwacho Sirat Rasullallah (Maisha ya Nabii wa Allah). "[Wahamiaji] walibakia sehemu ileile waliyokuwepo [Ethiopia] hadi waliposikia kuwa watu wa Maka wameukubali Uislam na wamejinyenyekeza. Hii ilikuwa ni kwa sababu sura ya Nyota [Sura 53] ilikuwa imetumwa kwa Muhammad na mtume aliinena. Mtu mmoja Muislam na mwenye kuamini miungu wengi alisikiliza kimya hadi alisema maneno haya ‘Je umemwona al-Lat na al-uzza?’ Walimsikiliza kwa uangalifu sana wakati waumini walimwamini [nabii wao]. Baadhi yao waliiasi imani yao walipoisikia ‘saj’ ya Shetani na kusema, ‘Kwa uwezo wa Allah tutawatumikia (mawinchi) ili kwamba watulete karibu na Allah.’ Shetani alifundisha aya hizi mbili kwa kila mtu aliyekuwa anaamini miungu wengi na ndimi zao zilizielewa kwa urahisi. Jambo hili lilimsunbua Mtume hadi Gabriel alipokuja kwake na kulalamika …." (Anaelezea mlolongo wa kuenea kuwa Yazid bin Ziyad-> Muhammad bin Ishaq -> Salama -> Ibn Hamid -> ibn Isaq
Ibn Jarir al-Tabari (aliyekufa mwaka 923 BK) alikuwa Msuni wa mlengo wa Kishati aliyeandika kitabu chenye juzuu 38 cha Kiislam cha Historia ya ulimwengu hadi mwaka 915 BK. Alipewa jina la "shehe wa wafafanuaji." Anaandika kwenye juzuu ya 6 uk.108-110, "Mjumbe wa Mungu alipoona jinsi kabila lake lilivyomkataa na kuhuzunishwa alipowaona wanauacha ujumbe aliowaletea toka kwa Mungu, alitamani moyoni mwake kuwa kitu chochote kimjie toka kwa Mungu ambacho kitampatanisha na kabila lake …. Na alipoyafikia maneno: ‘Je umewafikiria al-Lat na al-Uzza na Manat, wa tatu, Yule mwingine?’ Shetani alimlaumu, kwa sababu ya midahalo yake ya ndani na vitu alivyokusudia kupeleka kwa watu wake, maneno: ‘Haya ni mawinchi yanayopaa juu zaidi; hakika maombezi yao hupokelwa kwa kuthibitishwa [kwa mpokezano: kuhitajiwa au kutegemea].’ Waquraysh waliposikia hili, walifurahi sana na kupendezwa na namna alivyosema kuhusu muingu yao, na walimsikiliza, wakati Waislam, wakiwa wanamwamini kabisa nabii wao kuhusu ujumbe aliouleta kutoka kwa mungu, hawakumshuku kuwa amepotoka, anaota, au kafanya makosa. … Kisha [baadaye] Gabriel alikuja kwa Mjumbe wa Mungu na kusema, ‘Muhammad, umefanya nini? Umenena kwa watu kitu ambacho sikukuletea toka kwa Mungu …’"
Wanazuoni wa Kiislam wa miaka ya mbele waliosema jambo hili:
Abu Ma’shar kutoka Chorassan (787-885 BH)
Ibn Abi Hatim
Ibn al-Mundhir
Ibn Hajar from Asqalaan (773-852 BH)
Ibn Mardauyah
Musa ibn ‘Uqba
Ufafanuzi mashuhuri sana wa Zamakhshari wa Sura 22:52. (1070-1143 BH)
Wanazuoni sita ni kwa mujibu wa kitabu kiitwacho The Book of the Major Classes, kilichotafsiriwa na S. Moinul ‘Haq.
Ushahidi usiokuwa wa moja kwa moja wa Aya za Shetani:
Kurani na Hadithi
Bukhari alikufa karibu na mwaka 870 BK (hata miaka mitatu baada ya vyanzo vitatu kati ya vinne vilivyoorodheshwa.) Wakati Muhammad alipoisema Sura ya Nyota, wapagani na Waislam walisujudu. (Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 19 na.173, uk.100 juzuu ya 3 kitabu cha 19, na.176, uk.101; juzuu ya 6 kitabu cha 60 na.385-386 uk.364-365; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 481 na.1401, uk.369). Wapagani hawasemekani kusujudu kwa ajili ya Muhammad kusema maneno mengine yoyote, ni kwa nini wakubaliane kiasi hiki na sura hii, hasa kwa vile Bukhari na Abu Dawud hawasemi kuwa hao wapagani waliwahi kuwa Waislam, na hii ilikuwa kabla ya vita na hawa wapagani wa Maka!
Pia, Sura 22:52 inasema, "Hatukuwahi kumtuma mtume au nabii Kabla yako, lakini, alipoumba nia, Shetani alimtupia (ubatili) kiasi kwenye nia yake: lakini Mungu atafuta kitu chochote (batili) ambacho Shetani anatupia ndani, na Mungu atafanya dhahiri (na kuthibitisha) Ishara Zake…"
Sura 17:73-75 inasema, "Na lengo lao lilikuwa kukujaribu na kukupeleka mbali na jambo tulilolifunua kwako, kuweka badala yake kitu tofauti kabisa kwa kutumia jina letu: (Kwa ajili hiyo), tazama! Watakuwa wamekufanya kuwa rafiki (yao)! Na je hatujakupa wewe, ungeweza kuelekea upande wao kiasi. Katika hali hiyo tulipaswa kukufanya uonje mara mbili (ya adhabu) kwenye maisha haya, na kiasi kama hichohicho mautini: na zaidi ya hapo usingepata mtu wa kukusaidia dhidi yetu!"
Kumbuka kwamba ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa Sura 17:73-75 ilifunuliwa wakati wa "Kupaa kwa Nabii", Tabari na Ibn Sa’d waliandika kuwa Sura 17:73-75 ilifunuliwa karibu na wakati wa aya za Shetani. Waislam hata wana neno maalum la kunong’oneza kwa Shetani, ambalo matamshi yake yanafanana na "wiswas".
USIKOSE SEHEMU YA TATU
Shalom

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA NNE)

No automatic alt text available.
YOSEFU ALIUKIMBIA UASHERATI
Yosefu alishawishiwa jinsi gani, naye alifanya nini?
Yosefu, ndugu-nusu ya Dina, aliyekuwa kijana mzuri aliyempenda Mungu, aliukimbia uasherati. (Mwanzo 30:20-24) Alipokuwa mtoto, Yosefu aliona matokeo mabaya ya upumbavu wa dada yake. Inaonekana kukumbuka mambo hayo, na vilevile kutamani kukaa katika upendo wa Mungu, kulimlinda Yosefu miaka mingi baadaye huko Misri wakati mke wa bwana wake alipokuwa akijaribu kumshawishi “siku baada ya siku.” Bila shaka, kwa sababu Yosefu alikuwa mtumwa, hangeweza kuacha kazi na kuondoka! Ilimbidi ashughulikie hali hiyo kwa hekima na uhodari. Alifanya hivyo kwa kukataa tena na tena vishawishi vya mke wa Potifa, na mwishowe, kwa kumkimbia.—Mwanzo 39:7-12.
Fikiria hili: Ikiwa Yosefu angetumia muda mwingi akiwaza kuhusu mwanamke huyo au kuwaza-waza juu ya ngono, je, angeendelea kuwa mtimilifu? Haielekei angeweza. Badala ya kuwazia daima mambo yasiyofaa, Yosefu alithamini uhusiano wake pamoja na Yehova, jambo ambalo lilionekana wazi katika maneno ambayo alimwambia mke wa Potifa. Alisema: “Bwana wangu . . . hakunizuilia chochote ila wewe, kwa sababu wewe ni mke wake. Basi ninawezaje kufanya ubaya huu mkubwa na kwa kweli nimtendee Mungu dhambi?”—Mwanzo 39:8, 9.
Mungu alielekeza mambo jinsi gani katika kisa cha Yosefu?
Wazia shangwe ambayo Mungu alikuwa nayo alipomwona kijana Yosefu akiendelea kuwa mtimilifu siku baada ya siku, ingawa alikuwa mbali na familia yao. (Methali 27:11) Baadaye Mungu alielekeza mambo ili Yosefu afunguliwe kutoka gerezani na vilevile kuwa waziri mkuu wa Misri na msimamizi wa chakula! (Mwanzo 41:39-49) Jinsi yalivyo kweli maneno haya ya Zaburi 97:10: “Enyi mnaompenda Mungu, chukieni yaliyo mabaya. Yeye anazilinda nafsi za washikamanifu wake; huwakomboa kutoka katika mkono wa waovu”!
USIKOSE SEHEMU YA TANO
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

YESU NI MUNGU MUUMBAJI

Image may contain: text
Sifa ya kuumba niya Mungu peke-yake (Yohana 1:3,14) “vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. Naye Neno alifanyika mwili; nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli”.
Yesu anaitwa Neno la Mungu (Ufunuo 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(Yohana 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote. Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine.
Katika yeye (Yesu) vitu vyote viliumbwa (Wakolosai 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana; vya Mbinguni na vya duniani.
Maandiko yako wazi kabisa, na kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi kuwa Yesu ni Mungu.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

MAMLAKA ULIYONAYO UNAPOLITUMIA JINA LA YESU KRISTO!

Image may contain: text
“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” (Wafilipi 2:9-11)
Kwa mistari hii michache tunaona ya kuwa jina la Yesu kristo lina mamlaka MBINGUNI, DUNIANI na CHINI YA NCHI au KUZIMU.
“Kwa jina la Yesu kila goti lipigwe” maana yake jina la Yesu lipate heshima linavyostahili kila mahali.Likiwa mojawapo ya funguo za ufalme wa mbinguni, jina la Yesu linatupa MAMLAKA mbinguni, duniani na chini ya nchi.
Kwa mfano: tunaokolewa kwa jina la Yesu (matendo ya mitume 4:12). Tunazaliwa mara ya pili kwa jina la Yesu (Yohana 1:12). Kwa maneno mengine kwa sababu ya jina lake, Yesu alisema; “Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu” (Yohana 16:23-24)
Mtu anapata furaha iliyo timilifu anapoomba kwa jina la Yesu Kristo! Kwa nini? Kwa sababu akiomba kwa jina la Yesu Kristo – anapata kile alichoomba. Heshima yote hii ya kujibiwa maombi yetu na Mungu Baba inatokana na Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na mwokozi wetu. Yesu Kristo alisema, “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.” (Yohana 12:26)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu

KORAN NI SAWA NA TANGAZO LA VITA

Image may contain: one or more people and text
Dhana ya Kiislamu ya Amani, kwa maana ya kufanya ulimwengu kuwa wa Kiislamu, ni mipango ya kishetani kwa ajili ya kufanya vita na kumwaga damu. Ilikuwa si jambo la kufikirika kuwa siku moja Ugaidi wa Kishetani utaweza ingia kwenye Nchi za Kistaarabu, kwa kupitia njia ya "dini" ya amani, nikimaanisha Uislam. Maantiki ya fikra yakinifu katika Uislamu ni tofauti na ile ya Wastani wa Mtu ..., nikimaanisha, katika Uislam, kuuwa kwao ndio amani wanayo itangaza.
Mtu KAMWE hawezi kuuacha Uislamu, unajua, wale ambao waliiuacha Uislam na kujiunga na Imani zingine, wale hawakupigwa Muhuri wa kwenda Jehanamu. Maana Allah ameahidi Jehanamu kwa Waislamu wote Soma: Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike. Kuukacha Uislam na kuingia kwenye hekima hilo ni kosa la kifo katika dini ya amani/Islam. Hapo ndipo panaanza kufanya mtu afikirie, Je, kweli Koran ni kitabu cha Mungu? Mbona kuna kulazimishana kwenye hii dini?
Hivyo, hii ni sehemu ya mantiki hiyo hiyo ya kuwa, Mtu ambaye anabadili dini na au shirika kama vile Al Shabaab au Uislamu ni tu kama nilivyoeleza, mtu wa namna hiyo hakupigwa Muhuru wa kwenda Jehannam na Allah, anyway. Hivyobasi, huyu mtu ni Msaliti na akikamatwa basi aelewe kuwa kifo kipo mkonini mwake, kwa kuikacha dini ha Amani/Islam.
Mwenye akili lazima ataelewa kuwa amani ya Allah na Muhammad ni vita na umwagaji damu. Hakuna jema kwenye hii dini ya Jibril zaidi ya kutangaza kifo kwa makafiri.
Shalom,

USIOGOPE, SIMAMA IMARA KWENYE MWAMBA WA MILELE

Image may contain: one or more people, sky, text, outdoor and nature
Isaya 26: 4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.
Simama imara maana Yesu Mungu Mkuu ni MWAMBA WAKO na hakuna "Mapepo au Majini au Mashetani au Nguvu za giza" zinakazo kutetemesha.
Kumbuka, Mwamba ni Yesu na upo juu yako.
Barikiwa sana ndugu.
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

KAA NDANI YA YESU, NAYE ATAKAA NDANI YAKO

Image may contain: food
Je, wewe ni tawi la Mzabibu unao zaa?
Watu tuliookolewa, ni matawi ya Mzabibu wa Kweli. Yesu Kristo ndiye mizizi na shina. Kutoka kwake tunapata uzima. Chakula, maji na madini mengine hutoka chini kwenye mizizi na kupanda juu kwenye matawi. Uzima au uhai wetu unatokana na Yesu. Wokovu wetu hutoka kwake. Ikiwa tawi linaonekana kijani kibichi linapendeza, kupendeza huko hutokana na mizizi.
Yohana 15:1-8:
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.
Mtu yeyote anayedai kwamba ameokoka, lakini hazai matunda tuliyojifunza; huyu ni tawi lisilozaa. Hukatwa na kuondolewa, na kutupwa motoni. Ili tupate uzima wa milele, hatuna budi kuishi wakati wote maisha yanayoonyesha matunda.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

Why is the wife of Adam not mentioned by name in the Quran?

Why is the wife of Adam not mentioned by name in the Quran? Provocative Questions on Adam’s Wife and the Quran’s Omissions Why does the Qura...

TRENDING NOW