Saturday, February 15, 2014

FIKRA NGUMU KUHUSU YESU: JE, YESU NI NANI?

Hivi katika Biblia, Yesu alijiita nani na alisema nini kuhusu yeye mwenyewe? 

Ndugu wasomaji, leo ningependa tujifunze kidogo kuhusu huyu Yesu wa Biblia ambaye hakuwa mtu wa kawaida. 

Watu ulimwenguni pote wamesikia kuhusu Yesu Kristo, ingawa aliishi duniani miaka 2,000 hivi iliyopita. Hata hivyo, wengi hawajui kwa kweli Yesu alikuwa nani. Baadhi yao husema kwamba alikuwa mtu mzuri tu. Wengine wanadai kwamba alikuwa nabii tu. Na wengine wanaamini kwamba Yesu ni Mungu na anapaswa kuabudiwa.

Ni muhimu ujue ukweli kuhusu Yesu. Kwa nini? Kwa sababu Biblia inasema:

Biblia inafundisha kwamba Yesu aliishi mbinguni kabla ya kuja duniani. Mika alitabiri kwamba Masihi angezaliwa Bethlehemu na alisema pia kwamba asili Yake “ni kutoka nyakati za kale.” (Mika 5:2) Mara nyingi, Yesu mwenyewe alisema kwamba aliishi mbinguni kabla ya kuwa mwanadamu. (Yohana 3:13; 6:38, 62; 17:4, 5) Akiwa kiumbe wa roho mbinguni, Yesu alikuwa na uhusiano wa pekee pamoja na Baba Yake ambaye ni Mungu.
Yohana 17: 5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

Neno “UTUKUFU” maana yake ni heshima, uweza, uzuri, umaarufu, nguvu, sifa na mamlaka. Mambo hayo yote Yesu alikuwa nayo kabla hata ulimwengu haujaumbwa. Yesu Kristo alikuwapo hata kabla ya kuzaliwa na Mariamu; jambo hili pia Yesu Kristo kwa kinywa Chake Yeye mwenyewe ametuthibitishia alipokuwa akiwaambia Wayahudi kwamba:

“Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?

Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini Mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima Yangu. Wala mimi siutafuti utukufu Wangu; Yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akuilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba Yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
Fikiria mifano miwili tu. Kwanza, zaidi ya miaka 700 mapema, nabii Mika alitabiri kwamba Yule aliyeahidiwa angezaliwa Bethlehemu, mji mdogo katika Yuda. (Mika 5:2) Yesu alizaliwa wapi hasa? Katika mji huohuo! (Mathayo 2:1, 3-9) Pili, karne nyingi mapema, unabii ulio katika Danieli 9:25 ulionyesha mwaka hususa ambao Masihi angetokea, yaani, 29 W.K.* Kutimia kwa unabii huo na unabii mwingine mbalimbali kunathibitisha kwamba Yesu alikuwa Masihi aliyeahidiwa.

Yesu alitimiza nini kwa kuendelea kuwa mwaminifu mpaka kifo? Kifo cha Yesu kinatuwezesha kupata uzima wa milele katika dunia itakayokuwa paradiso kama vile Mungu alivyokusudia mwanzoni.

Upo ushahidi mwingi sana ndani ya Biblia Takatifu unaotuthibitishia kuwa Yesu alikuwepo hata kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile; kwani nao manabii pia walitabiri ujio wa Yesu ambaye alikuwepo tangu milele yote, na tena manabii hao walisema wazi wazi kuwa huyu Yesu ni Mungu.

MASWALI YA FUNZO
1, 2. (a) Kwa nini kujua jina la mtu mashuhuri hakumaanishi kwambaunamjua vizuri? (b) Watu wana maoni gani yanayotofautiana kumhusu Yesu?

3. Kwa nini ni muhimu ujue ukweli kumhusu Yesu?
Nimategemeo yangu kuwa utaendelea wewe mwenyewe kufanya utafiti kuhusu huyu Yesu aliye ishi kabla ya Dunia kuumbwa.

Mungu awabariki sana.

Katika huduma yake,

Max Shimba Ministries

For Max Shimba Worldwide Missions
02/15/2014

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW