Monday, April 13, 2015

SIFA SABA ZA ROHO MTAKATIFU


Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 17Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.


Yesu Kristo ametupa zawadi ya ajabu sana: Zawadi ya Roho Mtakatifu. Katika baadhi ya maeneo, zawadi hiyo inajulikana kama Roho Mtakatifu, na sehemu nyingine ametajwa kama Msaidizi (Msaidizi na Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu ni sehemu ya tatu ya Uungu, sehemu ya tatu ya Utatu wa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Yeye ni Msaidizi katumwa na Yesu, baada ya Msaidizi wetu kuja ambaye ni Roho Mtakatifu, Yesu alipaa tena mbinguni. Roho Mtakatifu hutolewa kwa wote ambao wamempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao

Kuna mambo saba ambayo tunahitaji kuelewa kuhusu Roho Mtakatifu. Tunajua kwamba, katika Biblia, saba ni namba ya kukamilika/ kukamilisha, au ukamilifu, na sifa saba zote tofauti za Roho Mtakatifu ni kweli kamili na kamilifu. Tunaweza kuzitegemea sifa hizi za ajabu za Roho Mtakatifu, wakati wote, katika kila hali na katika maisha yetu yote.

1. Roho Mtakatifu ni Msaidizi Mwenye Upendo. Tunapokabiliana na mateso katika maisha, mwongozo wa Roho Mtakatifu ni muhimu zaidi na ni faraja katika mioyo yetu: Roho Mtakatifu ni mtu ambaye ana upendo kwetu na anajua kila kitu kuhusu maisha yetu. Roho Mtakatifu alitupenda tangu kabla ya kuumbwa ulimwengu. Yeye alivyotupenda vizuri. Yeye anatupenda milele na anaendelea kutupenda milele yote. Roho Mtakatifu tu ndie mwenye uwezo wa kweli wa kutufariji mioyo yetu, kwa sababu hakuna mtu anaye tupenda sisi kama anavyotupenda Yeye Roho Mtakatifu.
 
Warumi 5: 5 wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo Lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

2. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwaminifu. Watu, hata wale ambao wana upendo kwetu, wakati mwingine wanaweza kushindwa kutusaidia. Wao (Ndugu na Marafiki) wakati mwingine si waaminifu. Na inaweza kuumiza sana nafsi yetu - rafiki anaweza kuwa mbaya kuliko jino la nyoka, na mchungu kupita nyongo. Huwa tunakata tamaa wakati mtu ambaye anatupenda anapobadirika wakati tunapokuwa na taabu, lakini, Mungu Roho Mtakatifu kamwe hawezi kufanya hivyo na kamwe hawezi kukuacha wakati wa taabu. Yeye anatupenda hata mwisho, kwani, Yeye peke yake ni Mwaminifu. Dhambi haiwezi kututenganisha na upendo wake, hakuna, kwa kweli, yeye alitupenda wakati sisi bado tulikuwa wafu katika dhambi zetu. Alitupenda huku qkijua jumla ya uovu wetu na dhambi zetu. Wema wetu wote kamwe haukumfanya yeye atupende zaidi, na zambi zetu zote hazimfanyi yeye Roho Mtakatifu asitupende au punguza upendo wake kwetu. Tunaweza kumwamini kikamilifu katika Yesu, kwa maana Yeye ni milele mwaminifu. Yeye kamwe hata tuacha, lakini atakuwa pamoja nasi mpaka mwisho wa maisha yetu hapa duniani.

Warumi 15: 13Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

3. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Asiechoka. Wakati mwingine sisi tukijaribu kumfariji rafiki yetu/ndugu yetu katika shida zao au dhiki, huwa tunachoka, pale tunapo ona kuwa shida ya tunaye mfariji inapo kuwa haiishi huwa mara nyingi tunaacha kufanya hivyo na au kata tamaa. Kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kufarijika  na au kufarijiwa, infact, tunapo endelea kuwafariji, ndio wanazidi kuharibika na ua hali inazidi kuwa mbaya. Mara nyingi basi, sisi hufa moyo, na kuwaacha peke yao na matatizo yao. Roho Mtakatifu kamwe huwa hakati moyo/au choka kukusaidia, zaidi ya hapo, Yeye huwasaidia hata wale ambao wanafikiria kuwa hawawezi kusaidika. Yeye Roho Mtakatifu, huwa hachoki na au choshwa, si kwa dhambi zetu, si kwa manung'uniko yetu, hata kwa kukataa kwetu, Yeye bado anatupenda na anahuruma.
 
Yohana 14: 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 

4. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwenye Busara. Sisi mara nyingi huzungukwa na watu ambao wanadhani wao wana busara, na bado hao watu hawana uwezo wa kuangalia ndani ya moyo wako na kusema nini ni chanzo cha magonjwa yetu/matatizo yetu ya kiroho. Kama marafiki wa Ayubu (Katika Biblia) walivyo toa mawazo yao potofu, ndivyo hivyo ambavyo hata marafiki zetu wanaweza kutupa mawazo ambayo si sahihi, zaidi ya hapo, hata Madaktari wanaweza kutupa dawa ambazo si sahihi au kwa makosa na zikashindwa kutibu magonjwa yetu na hata kusababisha madhara makubwa, au hata mauti. Ili kutabumbua ugonjwa wa Kiroho kwa usahihi, basi inahitaji hekima kamili. Hivyo basi, Roho Mtakatifu kwa kutumia hekima yake, anaweza kuingalia Roho/moyo wako na kutambua nini hasa kinakusumbua na au wapi lipo tatizo lako la Kiroho. Yeye anaona mzizi wa watatizo upo wapi, na ni nini kinasababisha ugonjwa wako wa kiroho. Yeye si anafahamu wapi lipo tatizo lako, lakini vile vile yeye anaweza kukutibu hilo tatizo lako. Hivyo basi, Roho Mtakatifu Mwenye Busara, ana uwezo wa kuponya magonjwa yetu yote na kutufanya tukubalike mbele za macho ya Mungu. 
1 Wakorintho 2: 10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 

5. Yeye ni Msaidizi Alie Salama. Mara nyingi sana marafiki na familia hutoa ushauri salama wakati sisi tupo katikati ya majaribu na mateso. Ushauri wowote unao fuata maarifa ya ulimwengu huu ni ushauri salama. Kumbuka kwamba Shetani mwenyewe wakati mwingine huja kama mfariji wa uongo, anatuhakikishia kwamba mambo yote ni salama huku akifahamu kuwa si kweli, na huku akiweka shaka katika Neno la Mungu. Lakini faraja ya Roho Mtakatifu ni salama, na unaweza kutulia katika faraja na Imani Yake (Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu anajua moyo wa Mungu na mapenzi ya Mungu kwako, na faraja yake kamwe haiwezi kwenda kinyume na Matakwa ya Mungu.

1 Wakorintho 2: 13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. 

6. Yeye ni Msaidizi alie hai. Yeye (Roho Mtakatifu) huwa awafariji tu kwa maneno, lakini kwa matendo. Yeye anatuombea, kutukumbusha ahadi kubwa ya Mungu na neema yake. Yeye kamwe hatuachi au kutuacha, lakini badala yake anatuongoza katika mapenzi kamili ya Mungu Baba.

Warumi 8: 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 27. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. 

7. Yeye ni Msaidizi wetu wa sasa na hata milele. Hatuitaji kumtafuta, bali yeye yupo nasi daima. Yeye kamwe hatotuacha, wala kutuacha. Tunaweza kumwambia na au kumwita wakati wowote ule tunahitaji msaada wake, na tuna uhakika kuwa yeye yupo nasi na anaweza kutusaidia.

Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 

Hivyo basi, ndugu msomaji, leo tumekumbushana sifa Saba za Roho Mtakatifu.
1. Roho Mtakatifu ni Msaidizi Mwenye Upendo.
2. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi mwaminifu.
3. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Asiechoka.
4. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwenye Busara.
5. Yeye ni Msaidizi Alie Salama.
6. Yeye ni Msaidizi alie hai.
7. Yeye ni Msaidizi wetu wa sasa na hata milele.

Nimategemeo yangu kuwa, baada ya kuzisoma hizo sifa Saba za Roho Mtakatifu, utaanza kumtegemea na kuongea naye kila siku. Kumbuka, Roho Mtakatifu ni Msaidizi wetu na yupo nasi kila siku kama ambavyo Biblia Takatifu inavyo sema.

Mtegemee Roho Mtakatifu katika Maisha yako yote. Mtegemee katika kazi zako. Mtegemee katika Masomo yako. Mtegemee katika Biashara zako. Mtegemee katika Ndoa yako. Mtegemee katika kila jambo. Hakika Yeye anakupenda na alikufahamu wewe hata kabla ya kualiwa kwao. Yeremia 1: 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. 

Katika Huduma Yake,

Max Shimba
For Max Shimba Ministries

April 13, 2015 ©2015

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW