Utangulizi
Huu ukurasa umeandikwa katika njia iliyokusudiwa habari za Isa (Yesu) kwa Waislam, kutokana na mtizamo wa Kikuran.Tafadhali angalia Kuran yako mwenyewe na ukathibitishe uamuzi ufuatao.
Katika Kuran Yesu siye Mungu, mwana wa Mungu au bwana aliyekufa msalabani. Yesu yuko katika Kuran kama nabii ambaye ujumbe wake Wayahudi waliukataa. Yeye anaitwa Masihi, lakini hii ina maanisha yeye ni mjumbe kutoka kwa Mungu (Kuran 4:171). Yeye alileta Injili (Kuran 57:27).
Ufafanuzi juu ya miujiza ya kuzaliwa kwa Yesu
Jambo la muhimu sana la tabia ya maisha ya Yesu ni kushikwa mimba na kuzaliwa kwake, inayopatikana katika Kuran 19:16-26. Kwa hivyo Yesu alizaliwa kimuujiza sababu ilitendeka pasipo nguvu za kiume. Muuijiza wa kuzaliwa kwa Yesu inaleta swali: Je Yesu ni binadamu au ni Mungu? Je Yesu alikuwa tu binadamu kwa sababu aliuumbwa kama Adamu? Ndiyo, kwa kweli, katika Kuran 3:59 tuna soma umoja kati ya kuzaliwa kwake Adamu na kuzaliwa kwake Yesu: Usawa wa Yesu mbele zake Mungu ni ile ya Adamu: alimuumba toka mavumbini, na akamwambia: ‘kuwa’ na akawa.
Walakini, Kuran inatuambia siyo tu kuhusu usawa, lakini kuhusu tofauti kati ya kuzaliwa kwa Adamu na kuzaliwa kwa Yesu:
- Adamu alizaliwa pasipo baba wala mama walio binadamu (Kuran 2:30; 15:28; 32:7).
- Yesu alizaliwa kutoka kwa bikira (Kuran 19:20-22).
- Adamu aliumbwa toka chini: kwa mavumbi tu, kwa hivyo ni wakidunia (Kuran 15:28; 32:7).
- Yesu aliumbwa katika Neno la Mungu, kwa hivyo ni wa mbinguni (Kuran 3:45).
- Yesu alipewa kwake Mariamu kama mtoto asiye na kosa toka kwake Mungu (Kuran 19:19).
Katika msingi wa mambo haya, tuna weza kusema kuna mambo ya kuangalia katika utofauti kati ya kuzaliwa kwake Adamu na Yesu. Adamu aliumbwa toka chini na Yesu aliumbwa toka juu. Sababu Yesu hakuwa na kosa lolote na akaumbwa kwa Neno la Mungu, Ilikuwa hazina iliyo juu sana. Tuna tofautisha Neno la Mungu (kalima) na maneno ya Mungu katika maandiko. Neno la Mungu na Roho lazima liwe la milele maana Mungu hangeweza kuwapo pasipo Neno na Roho. Kulingana na Kuran, Yesu maishani mwake hakuwa na makosa (Kuran 19:19), Huku Adamu akikosa kumtii Mungu maishani duniani (Kuran 2:36) Adamu hana tabia zinazofanana na Yesu, Neno la Mungu linasema.
Utambulisho wa Yesu
Kulingana na Kuran Yesu ana asili ya Roho. Lakini wakati Yesu asipo kuwa Neno la Mungu katika mwili, kama vile Wakristo wanavyoamini, na asipo kuwa mwili, basi utambulisho cha Yesu ni nini? Tunaweza kutamatisha hapa kwamba huu ndio uchunguzi kamilifu wa Yesu katika Kuran? Hii si kweli. Kuna mambo zaidi katika Kuran:
- Kuran ina hesabu nyingi ya majina muhimu ya Yesu kuliko mtu mwingine wowote.
- Yeye ni ’ishara’(Kuran 19:21; 21:91), ’rehema’ (Kuran 19:21) na ’Shahidi’ (Kuran 5:117).
- Yesu mara nyingi amenenwa katika Kuran kwa heshima.
- Hakuna ukosoaji wa Yesu katika Kuran.
- Katika Kuran Yesu ni mtume wa Mungu, Neno la Mungu (kalima) na Roho wa Mungu (ruh) (Kuran 4:71).
Neno la Kiarabu basher katika Kuran linamaanisha mwili, sio katika ulimwengu wa roho. Muhammad ni ule mwili kama kila mtu wowote awaye (Kuran 18:110, 41:6). Hii ni sawasawa na manabii wengine wote. Kwani kushangaza neno basher haliwezi kupatikana katika kumhusu Yesu. Hii ni thibitisho bora sana kwamba Yesu sio Mungu ila ni mwanadamu tu. Kwa hivyo yafaa tuliangalie hili jambo: Ina wezekana Yesu alikuwa zaidi ya nabii? Kumbuka yale Kuran ilivyosema juu ya Yesu:
- Yesu alizaliwa na bikira (Kuran 19:20-22).
- Yesu hakuwa na kosa (Kuran 19:19).
- Yesu alikuwa mponyaji mkubwa wa wagonjwa (Kuran 3:49; 5:110).
- Yesu alipelekwa Mbinguni na Mungu (Kuran 4:158).
- Yesu ata rudi tena (Kuran 3:45; 43:61).
Yamkini hii sio yote: yapo mambo zaidi katika Kuran kuhusu Yesu. Kuran inakubali kuna tofauti maalumu kati ya watumshi wa Mungu (Kuran 2:253) Yesu ana nafasi maalumu katika Kuran. Yesu ni ishara ya Mungu kuthibitisha (Kuran 2:253, 43:63) na Yesu alipata usaidizi wa Mungu kwa Roho Mtakatifu (Kuran 2:253) Yesu ni mtu wa heshima kuu katika ulimwengu huu na ujao (Kuran 3:45) Vitabu vyote vya fafunuzi vinakubaliana na jambo kwamba vyote utakatifu kama baraka[5]
Ni Yesu peke yake anayeweza ‘kuumba’ na ‘kutoa uzima’ (Kuran 3:49). Hakuna nabii katika Kuran amewahi kutenda matendo haya. Kwakuwa nafasi ya Yesu iko juu ya watu wote na ameinuliwa katika kiwango hakuna mwanadamu aliwahi kuifikia. Je unafikiri nini kumhusu Yesu? Je unaweza kusema yeye ni nabii tu mwingine?
Kujisomea zaidi
Waislamu wengi wanaamini hadithi ya kwamba wao ndio wana kibali cha kusoma Kuran kama tafasiri ya mwisho ya maandiko ya Mungu. Wanafikiri kwamba Bibilia (ikiwa na Taurah - Vitabu vitano vya Musa, Zaburi na Injil) kwamba siyo ya kupendeza. Lakini hivi sivyo kulingana na Kuran. Kwa nini? Sababu ni kwamba kulingana na Kuran 3:61 na 3:64 Waislam wana karibishwa wawe na mjadala na watu wa Kitabu (Bibilia) na kukaribisha kuchunguza njia za kweli. Tabari (alikufa katika mwaka 923 AD), Alikuwa mmoja wa wasomi wa Kiislam. Ameandika vitabu vingi vya ufafanuzi wa Kuran. Kama katika Kuran 28:82. Tabari anauliza: Makosa ya Ibrahimu yalikuwa yapi? Anajumuisha uongo aina tatu kuhusu Ibrahimu:
- Kwa kusema ’Mimi ni mgonjwa’ kuepuka kuabudu sanamu (Kuran 37:89). Je huu si uongo mweupe?
- Alipokataa kwamba aliharibu minara ya sanamu, maana alisema Mungu ndiye aliye fanya (Kuran 21:63). Tena ni uongo usio na hatia.
- Aliposema kwamba Sarai hakuwa mkewe ila dada yake.
Hautapata tukio la nambari ya tatu katika Kuran. Ni katika Bibilia, katika Mwanzo 12:11-13.
Yule msomi wa Kiislam alikuwa anasoma katika Bibilia kujibu hayo maswali!
Kama Tabari Waislam wengi husoma Bibilia, sababu inatoa elimu kamili. Maana kuna usemi kwamba Kuran inadai kutoa ukweli kamili juu yake Yesu, hadithi yote ya maisha yake, au wito katika Kuran kuchunguza na kufungua mlango wa kutumia Injili kama chanzo, hata tangazo linalojieleza (Kuran 2:256) Ndiyo, kabisa, Kuran inatoa semi za imani kuhusu Yesu, ikiwa na makusudi ya kuchochea masomo ya mwanadamu, ili asitoe jawabu la mwisho. Katika maneno mengine; Kila Muislam lazima akadariye zaidi ya uwezo kwa kusema ana kweli kamili kuhusu Yesu. Hata Muhammed aliagizwa kuongozwa na wale walio pokea Maandiko Matakatifu kabla ya Yeye:Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka (Kuran 10:94).
Itakuwa kujikinai kwa Waislam kuamini ya kwamba hawajui tu ukweli ila wana ukweli kamili kuhusu Yesu, na kukataa kutafuta njia iliyo wazi kwa Kuran katika kutafuta ushihidi mwingine [6]
Kuran inathibitisha Injili na inaelekeza habari zaidi kwake.
No comments:
Post a Comment