MUHAMMAD VS PAULO.
MUHAMMAD HANA UBAVU MBELE YA MTUME PAULO KULINGANA NA MAANDIKO.
TUWAPIME HAWA JAMAA WAWILI.
Waislam wanamlaumu na kumtukana sana
mtume Paulo kwa madai eti ni mtume wa uongo na mchafuzi wa maandiko, na kwamba ndiye aliyemwita Bwana Yesu Mungu na ndiye mwanzilishi wa Ukristo nk. Hizo hoja zote zitajibiwa kwa masomo haya. Yafuatayo ni mizani ya kuwapima Paulo na Muhamad nani wa uongo na nani wa kweli kupitia maandiko?
MIZANI YA KUWAPIMA HAWA MAJAA WAWILI NANI MTUME WA KWELI:
1)Kuzaliwa kwa Paulo na Muhamad
2)Elimu ya Paulo na Muhamad
3)Imani ya Paulo kidini na Muhamad
4)Jinsi Paulo na Muhamad walivyopata utume
5)Je kati ya Paulo na Muhamad nani alifanya mujiza?
6)Je Quran inajitosheleza kuwajua mitume na manabii?
7)Namna Paulo na Muhamad walivyopata maono(wahyi)
8)Hasara ya kumkataa mtume paulo
1)KUZALIWA KWA PAULO NA MUHAMMAD
1) Paulo alivyozaliwa
anasema katika Matendo 22:3… Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia….! Kiistoria mji wa Tarso ulikuwa chini ya dola ya Kirumi, ndiyo maana Paulo alisema yeye ni mrumi wa kuzaliwa, tazama Matendo 22:25-28. Paulo anasema alizaliwa Tarso, Tarso zamani ilijulikana km asia ndogo, kwa sasa ipo ktk nchi ya Uturuki, historia inaonesha kuwa Paulo alizaliwa mwaka wa 10 BK.
Mji wa Tarso ulikuwa maarufu kwa mambo makuu mawili..1} Elimu ya kiwango cha juu, na ina aminika wasomi wengi(mafilosofia) walitokea ktk mji huo, mf. Athenodorus ambaye alikuwa mwalimu wa Kaisari Agusto. 2} Mafundi wa ushonaji mahema, hiyo ni kazi ambayo pia Paulo aliijua na kuifanya na ilimsaidia kupata ridhiki na kupata kipato cha kusambaza injili ya Kristo bila kumlemea mtu yeyote, Matendo 18:1-3; 20:34, 2 thes 3:8. Ndiyo maana Paulo alisema yeye ni mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge, matend 21:39.
Paulo alizaliwa ktk kizazi bora.
Warumi 11:1…. Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benyamini. Hivyo ili kujua ubora wa kizazi hiki vyema kujua ibrahimu ni nani?
Mwanzo 14:13 Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania…Biblia inafundisha kuwa ibrahimu ni mwebrania na alipewa Baraka na kwa yeye na uzao wake mataifa yote yatabarikiwa mwanzo 12:1-4; 22:15-18
Paulo naye anatokea ktk uzao huo km anavyosema ktk wafilipi 3:4-5… Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi.Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo.
Waebrania ndio waisrael ambao ndio uzao uliopewa Torati na kufanywa wana na kupewa agano lililo bora, Tazama Warumi 9:4-5. Waebrania 7:22; 8:6. Na Benjamin ni moja wapo ya makabila 12 ya Israel.
2) Jinsi Muhamad alivyozaliwa
Muhamad amezaliwa mwaka 570 Baada ya kristo ktk mji wa Makka kusini Mashariki mwa Arabia, jina lake kamili ni Muhamad bin Abdullah bin Abd-Muttalib bin Hashim. Quran 41:44 inasimulia kuwa Muhamad ni Mwarabu, tena vitabu mbali mbali vya kiislamu vinasema kabila lake ni Mkureshi.
Muhamad katokea ktk kizazi kisichomjua Mungu wala kitabu
Quran 34:44 Wala (hawa waarabu) hatukuwapa vitabu(kabla ya kitabu hiki wakawa)wanavisoma. Wala hatukuwapelekea muonyaji kabla yako.
Allah Mungu kama wanavyoamini waislam hakuwapa waarabu kitabu kabla ya Quran. Hii ina maana kuwa muhamad tokea alipozaliwa hadi kufika miaka 40 hakujua hbr ya vitabu pamoja na waarabu wenzake wote hawakujua.
Tena ukisoma ufafanuzi wa Suratul al-Furqan aya 43 kuna maneno haya “ Waarabu kwa ujinga wao wa kuabudu chungu ya miungu walikuwa baadhi yao wakiona chochote kile kikawapendeza, hukiabudu hata Andazi lililokaa kwa sura nzuri.
Hivyo tumeona kuwa Paulo amezaliwa ktk kizazi cha watu bora wanaomjua Mungu, lkn Muhamad amezaliwa ktk kizazi kisichomjua Mungu wala kitabu.
ELIMU YA PAULO NA MUHAMMAD
1)Elimu ya Paulo:
Matendo 22:3 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Je Gamaliel alikuwa ana sifa gani ktk Israel..matendo 5:34 Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza,
Na Paulo alihitimu kwa kiwango cha juu chini ya mwalimu huyo mashuuri wa torati, Wagalatia 1:14 Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. Ndo mana kwa maarifa hayo Paulo aliweza kuandika vitabu 13 kwa nguvu za R. Mtakatifu wagalatia 6:11. Mashuhuda wa Elimu yake ni mtume Petro na Liwali Festo, 2 petro 3:15-17; matend 26:24,25.
2) Elimu ya Muhamad
Quran 7:157 inasema. Ambao wanamfuata Mtume, Nabii, aliye ummy (asiye jua kusoma wala kuandika) na juu ya hivi atafundisha mafundisho haya ya uislamu.
Quran 62:2 inasema Yeye ndiye aliyemleta mtume kwa ktk watu wasio jua kusoma anayetokana na wao na Quran 75:16 ktk ufafanuzi wake inasema mtume alivyo kuwa hajui kusoma wala kilichoandikwa .
Ktk kitabu cha maisha ya muhamad kilichoandikwa na sheikh Farsy kwenye ukurasa wa 8, kuna maneno haya.
Mtume aliondokea km Makureshi wengine bila kujua kuandika wala kusoma kilichoandikwa. Hajakuwepo Kureshi yeyote aliyekuwa akijua kusoma wala kuandika.
Kutokuwa na Elimu kwa muhamad ndo maana aliwafundisha waislam, wakikosa maji ya kutawaza watumie mchanga(vumbi) tazama Quran 5:6. Fundisho lingine la ajabu alilofundisha muhamad linapatikana ktk hadithi ya Mishikat Al-Masabih vol 11 uk 152. Pana maneno haya…..Mjumbe wa Allah mtume(saw) alisema: “ Inzi akianguka ktk bakuli la mmoja wenu, mwingize kabisa kwa sababu kuna ugonjwa ktk bawa lake moja na madawa ktk bawa lake la pili.” Na pia kwa sababu anaingiza bawa lenye ugonjwa kwanza kwa hiyo mzamishe kabisa.
Biblia haikubaliana na ujinga huo tazama… Ezekieli 13:3 Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lo lote!
4) IMANI YA PAULO NA MUHAMMAD
1) Paulo:
Alikuwa ktk dini ya kiyahudi yenye kushika Torati na mafundisho yote ya manabii kabla hajakuwa mkristo. Wagalatia 1:13; matnd 26:4-5. Na hata alivyokuwa mkristo aliendelea kufundisha kupitia torati na manabii…Matendo 28:23 Wakiisha kuagana naye siku, wakamjia katika nyumba aliyokaa, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hata jioni.
2) Muhamad:
Alikuwa mpagani wa kikureshi wenye kuabudu miungu 360 pamoja na jiwe jeusi kwenye al-kaaba kabla hajakuwa muislam, miungu hiyo ni pamoja na lata, Uzza na manata Quran 53:16-23 , tazama pia Kitabu cha maisha ya muhamad uk 8.
5) JINSI PAULO NA MUHAMMAD WALIVYOPATA UTUME
1)Paulo alivyopata utume:
Alipewa utume na Yesu mwenyewe wkt akiwa ktk safari yake ya kwenda Dameski, Yesu alimtokea na kumwagiza yapasayo kufanya Matnd 9:1-8. Na utume wake, Bwana Yesu akauthibitisha kupitia mwanafunzi wake Anania kwa kumwambia anania yafuatayo katika maono matendo 9:11-15 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Na pia Anania ndiye aliyembatiza Paulo, matnd 9:18.
Na Paulo naye akiitikia wito wa kitume aliopewa na Bwana Yesu…akisema yafuatayo ktk warumi 1:1 Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu;
Je kweli Paulo alitimiza utume huo wa kupeleka injili kwa mataifa na kisimama mbele ya wafalme na wana wa Israel? Jibu ni ndiyo…zifuatazo ni nchi Paulo alizo hubiri Uarabuni, Athene-ugiriki, Dameski-syria, Roma-italy, Yerusalemu-israel, Spain, Efeso, Galatia, korintho,filipi, Thesaloniki. Krete nk, na kote huko alikutana na changamoto zilizompelekea kusimamishwa mbele ya wafalme na maliwali na mbele ya wana wa Israeli. Tazama (Galatia 1:17; matendo 9:19,20,26-29; 17:16-22; 18:19;19:35; 28:16-30; warumi 15:24:28 na kuhusu kusimama mbele ya wafalme na wayahudi tazama matendo kuanzia sura ya 21-28).
2) Muhamadi alivyopata Utume
Ktk kitabu cha maisha ya nabii muhamad kilichoandikwa Sheikh abdalah Farsy uk 11-13,81 kina maelezo yafuatayo….
Hata siku moja ktk mwezi wa ramadhan tarehe 17 jumatatu, muhamad akiwa ana miaka 40 unusu wa umri wake, Mtume alimwona mtu kasimama mbele yake bila ya kumwona wp katokea, akamwambia soma mtume akamwambia sijui kusoma kwn sijapata kujifundisha kusoma. Yule mtu akaja akamkamata akambana akamwambia soma mtume akamwambia jawabu lake lilelile, ht mara ya tatu akamwambia soma iqra bismi rabbika akamsomea sura ya 96 mpaka kati yake, kasha mtume akamsomea kama alivyosomewa. Mara Yule mtu akatoweka mbele yake asimwone kaenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake kwa hofu imemshika, na alipofika nyumbani bibi khadija alidhani anahoma akamfunika maguo gubigubi na akakaa mbele yake akimsikiliza anavyoweweseka, hata homa ilivyomwachia alimweleza bibi khadija yaliyomtokea. Na bibi khadija akamtuliza moyo wk akamyakinisha ya kuwa hpn lolote baya litakalomzukia, mara bibi khadija akaenda kwa jamaa yake bwana waraqa bin Naufal akampa hbr yote, iliyompata mumewe naye akamwamrisha amwite mumewe na mtume akaenda akamweleza hbr yote,bwana Waraqa akamwambia huyo ndiye Gibril aliyemshukia nabii Musa na Nabii Issa. Basi jibashirie kuwa ww ni mtume kwa umma huu, name natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako inshallah ntakuwa mkono wk wa kulia. Ilikuwa December 610, hivyo utume wake alibashiriwa na Waraga mbele ya bi khadija.
Na ukisoma kitabu kiitwacho wakeze mtume wakubwa na wanawe kina maelezo yafuatayo
Kwa ufupi: muhamad alivyotoka pangoni kuelekea kwake baada ya kubanwa na Yule mtu hasiye julikana katoka wapi, homa ilimpanda akataka afunikwe maguo mara akawa anatetemeka kwa nderema na kuweweseka na kusema najiofia nafsi yangu kuchezewa na mashetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga, bibi khadija pale pale alimdakiza na kumtia moyo kwamba sivyo hivyo ……………. na kumwambia mm naona ushakuwa mtume. Na baada ya muhamad kusinzia bi khadija alitoka na kwenda kwa waraqa bin naufal padre wa kinasara na akamjuvya na Yule padre akamwambia utume huo kashapata mumeo bahati yako. Upesi khadija akarejea nyumbani na kumkuta muhamad kashaamka
akamwambia twende kwa waraqa ili umsimulie yaliyokufika, wakaondoka mguu kwa mguu mpaka kwa huyo bwana mkubwa, mtume akamwadithia yote. Na bwana waraqa akamwambia nakubashiria muhamad huo ndio utume uliomwendea nabii musa na nabii issa na wengineo na krb hv utapewa amri ya kufundishwa dini ya haki, nikiwa hai ntakuwa mkono wk wa kulia nikusaidie kila namna na ni kupiganie.
Kwa ufupi utume wa Muhammad ni wa kubashiriwa na bwana Waraqa pamoja na bi khadija, na waraka akimwahidi muhamad kuwa mkono wake wa kulia. Maana ya mkono wa kulia ni utendaji mkubwa, km vile Yesu alivyofufuka na kupaa kwenda mbinguni ni kuketi ktk mkono wa kuume(kuume) wa Mungu BABA, yaani inamanisha Yesu ni mtendaji mkuu wa wokovu wetu. Kwa hiyo bwana waraka ni mtendaji mkuu wa muhamad na uislam maana isingekuwa yy muhamad asingekuwa mtume.
Mashaka ya utume wa muhamad
Alibanwa na mtu asiyejulikana
Muhammad akiri ni mashetani yalimchezea na kumwaribu akili yk na kumzuga. Hata baada ya kuusimamisha uislam Muhamad aliendelea kukazia kwa wafuasi wake kuwa anatumia nguvu za majini na kila muislam amepewa nguvu za majini. Muhammad anasema katika Sahih muslim Juzuu 4 hadithi na 2814 kasema;(“Wala hakuna yeyote katika ninyi isipokuwa amepewa nguvu zinazotokana na majini. Wakasema (maswahaba) hata wewe mtume wa Allah? Akasema hata mimi isipokuwa Allah hunirahisishia juu yake hunyenyekea wala hayaniamrishi ila yaliyo mazuri)
Alibashiriwa utume na mke wake pamoja na padre wa kikatoliki waraqa bin naufal, kwa hiyo bila watu hao hamna utume kwa muhamad.
Na ukisoma Quran 4:79 inasema Wema uliokufika umetoka kwa mwenyezi mungu na ubaya uliokufika umetoka nafsini mwako mwenyewe umefanya mambo hata yakakufika hayo. Nasi tumekupeleka kwa watu kuwa mtume na Mungu ni shahidi wa kutosha hapahitajiki shahidi mwingine.
Hii aya inatuahakikishia zaid utume wa muhamad alibashiriwa na kupelekwa kuwa mtume na Waraqa bin naufal na khadija na Mungu hakuhusika bali alikuwa shahidi tu.
2) Ukisoma biblia Mungu anakataza kubashiri…tazama yafuatayo Kumbukumbu la Torati 18:10,12 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye KUBASHIRI, wala msihiri,………. Kwa maana mtu atendaye hayo ni CHUKIZO kwa Bwana
) JE, KATI YA PAULO NA MUHAMMAD, NANI ALIFANYA MIUJIZA ?
Paulo alifanya miujiza
Matendo 19:11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka, viwete wakapona.
Muhamad hakufanya mujiza bali yeye mwenyewe aliathiriwa na uchawi(kulogwa)
Quran 29:50 Na walisema mbona hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa mola wake? Sema miujiza iko kwake mwenyezi mungu tu akitaka atakuteremshieni na kama hataki basi nami hakika ni muonyaji mbainishaji (dhahiri tu)
Kuhusu kuathiliwa na uchawi soma vitabu vifuatavyo: Bhukari, Sahihi muslim na Nafai ibn majah.
7) NAMNA MTUME PAULO NA MUHAMMAD WALIVYOPATA MAONO (wahyi)
Paulo:
Matendo ya Mitume 16:10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
Matendo ya Mitume 18:9 Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,
Matendo ya Mitume 26:19 Kwa hiyo, Ee Mfalme Agripa, sikuyaasi yale maono ya mbinguni,
Muhammad:
Kitabu cha mkweli mwaminifu juzuu ya 1-2
Aliulizwa mtume(saw) vp unakuteremkiaje wahyi(maono) akasema..Baadhi ya wakati unanijia km jumla ya makengele yanalia kwa makelele makali sana na hivyo ndivyo shida kwangu, basi mpaka kuziba masikio yangu na mara nikafahamu niliyoambiwa…
8) HASARA YA KUMTUKANA MTUME PAULO
2PETRO 3:15-18 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe. Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msijemkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
Warumi 2:16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
HITIMISHO
Wanao mkataa mtume Paulo na injili aliyohubiri biblia inawaita wahalifu, wakosaji, watu wasio imara, wapotoshaji wa maandiko na mwisho wao ni kuhukumiwa.
Karibuni kwa YESU nyote.
MUHAMMAD HANA LOLOTE MBELE YA PAULO
NI MBWEMBWE TU.
Shalom
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?
Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment