Sunday, December 27, 2020

KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25?

 TEREHE 25 DISEMBA IMETAJWA KWENYE BIBLIA


KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25?

Tuanze na kumsikiliza Yesu akiitumia aya inayo husisha tarehe 25 na alikuja kufanya nini:

Luka 4: 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.

KATIKA AYA YA 18 KWENYE LUKA 4 YESU ANASEMA AMEKUJA KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO. HII NDIO KAZI YESU ALIKUJA KUFANYA. KUTUWEKA HURU WAFUNGWA WOTE.

Yesu alifahamu fika kuwa tarehe sahihi ambayo wafungwa walifunguliwa ni Disemba 25 na ndio taerehe hiyo leo hii tunasherekea kuja kwake.

Yesu alikuja kuwatangazia Wafungwa wote duniani kufunguliwa kwao. Uthibitisho sahihi wa wafungwa kufunguliwa umenukuliwa kitarehe kama ilivyo shahadiwa hapa chini.

Yeremia 52: 29 katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza aliwachukua toka Yerusalemu watu mia nane na thelathini na wawili;
30 katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadreza, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arobaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita.
31 Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, AKAMTOA GEREZANI.
32 Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake juu ya viti vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli.

TUNAJIFUNZA KATIKA YEREMIA 52 AYA YA 31 KUWA TAREHE 25 DISEMBA NI TAREHE AMBAYO WAFUNGWA WALICHWA HURU, JE YESU ALIKUJA DUNIANI KUFANYA NINI?

Luka 4: 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

“Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.” Isaya 61:1

UTANGULIZI

Roho yake Bwana i juu yangu leo ili nikuhubirie wewe mnyenyekevu habari njema, na kuwafungua walio fungwa na kuwaweka huru mateka. Nawatangazia mateka uhuru wao, kutoka mashimoni, kwenye magereza ya kifo, la mauti, la magonjwa ili watoke kwenye magereza hayo kwa maana muda wa kufunguliwa kwao umefika. Unaweza ukawa umefunguliwa muda mrefu lakini bado umekaa kwenye hali hiyo kwa kuwa ulikosa wa kukuambia ya kwamba umefunguliwa somo hili litakuwa tangazo na habari njema ya kufunguliwa kwako kwa jina la Yesu.

Yesu alipowatangazia wale wote waliokaa kwenye Sinagogi na wengine kuwekwa huru na kufunguliwa kwao, wao walikataa na kusema ‘sisi si wafungwa, si mateka, sisi ni watoto wa Ibrahimu’. Yesu akajibu akawaambia “kama mngekuwa ni watoto wa Ibrahimu msingenikataa.” Yupo mtu amefungwa sana lakini anasema mimi sijafungwa, siuumwi, nimekamilika. unasema hayo kwakuwa hujuhi kama wale wengine.

“Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” Luka 4:16-21

Watu wengi wamechukuliwa mateka, wamenaswa kwenye mashimo, na yule aliyetumwa kuwateka mateka hana mpango wa kuwaachilia mateka, ndipo Yesu akaja mwenyewe kuwatangazia uhuru watu wajue kuwa uhuru wao huu tayari. Maana unaweza ukawa ulifungwa na vifungo vikalegezwa, lakini ukaendelea kukaa kwenye kifungo hicho bila kujua. Unaweza ukawa umeponywa lakini bado ukajiona mgonjwa kwakuwa ulikosa wa kukutangazia uhuru wako.

Ni vizuri ujue aliyesema maneno haya ni nani? Na aliyewafunga watu ni nani? Aliyeyasema maneno haya ni nabii Isaya, yeye alimuongelea mtu aliyewafunga watu na kuwaweka mateka asiwaruhusu kutoka kwenye vifungo hivyo. Sifa nyingine ya anayewafunga watu ni kuangusha mataifa, kuangusha kazi zao, biashara zao, ndoa zao, n.k. Na anaye wafunga watu ni Shetani, yeye alikuwa malaika wa ngazi ya kerebu, alivyohasi akatupwa chini hata mwisho wa shimo ndiye mwenye sifa ya kukamata watu na kuwateka na kuwafunga magerezani.

“Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?” Isaya 14:12-17
Kwa kawaida katika nchi yetu watu wakivunja sheria hufungwa kulingana na makosa yao, wengine wiki, siku, mwezi au mwaka na wengine maisha. Lakini huyu [shetani] yeye alikuwa anawafunga watu maisha, ndipo Yesu akaja kuwafungua waliofungwa na shetani na kuwatangazia uhuru wao kutoka kwenye magareza.

Magereza yanayo ongelewa hapa si magereza ya kawaida bali ya ulimwengu wa roho, unaweza ukawa mzima kabisa lakini kazi yako imefungwa, unaweza ukawa na kazi njema lakini umefungwa kwenye gereza la magonjwa, ulikuwa unaona vizuri lakini macho yako yamefungiwa. Leo Bwana amekuja kuyafungua ili yarudi mahali pake, ili uone kazi, uone fursa na kila kitu kwa jina la Yesu.
Aliyewafanya watu mateka hapendi wala hafikirii au hana mpango wala hawazi kuwaachia huru, yeye kazi yake ni kufunga. Lakini akiona mtu anakuja kumfungua anakuwa makali sana, hapendi mtu atoke kwenye gereza, akiona mtu ametumwa na Bwana akufungue anasababisha matatizo ili usifunguliwe. Ni mkali mno na asiyetaka kuwafungua watu, wasirudi kwao.

Kwao ni wapi? Ulikuwa na ndoa yenye furaha, mara ukahamishwa kutoka kwenye furaha kuingia kwenye ngumi, kila siku ni ugomvi kati yako na mumewe. Ukiomba mswaki asubuhi kwa mkeo mara unapewa ngumi. Lakini leo Bwana anataka kukurudisha kwenye furaha yako kwa jina la Yesu.

Yesu aliwatuma wanafunzi wake katika malango ya mji njia panda kuwafungua kondoo wawili mtoto na mkubwa. Walifungwa kuingia kwenye kazi, kwenye biashara, kwenye ndoa n.k wamekosa uamuzi wamekaa katika njia panda, Yawezekana nawe umefungwa njia panda umeshindwa kufanya lolote, umeshindwa cha kuamua, leo Bwana amekuja kukufungua kutoka kwenye vifungo vyako ili uwe kufanya maamuzi, uanze kazi, biashara n.k.

“Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia, Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwanapunda pamoja naye; wafungueni mniletee.” Mathayo 21:1-2

Wachawi wakikufunga wanakaa karibu sana nawe kuliko nguo ulizo vaa; aliyekufunga anaweza kuwa jirani, rafiki au ndugu. Anaweza akawa anakusomesha shule kumbe ndani ya masomo kuna mtego ndani yake, yuleyule anayekusaidi ndie aliyekufunga, Amekuweka njia panda usiweze kuamua kwamba ujenge nyumba au uanze biashara au uanze kazi.

Yesu aliwaambia wanafunzi wale aliowatuma, mkifika mahali pale mtu akiwauliza nani kawatuma kuwafungua kondoo? mjibuni Bwana anahaja nao. Watu waliokufunga hawataki uendelee, ufanikiwe, wakiona duka linaongezeka wanakuwa wakali sana, wanazuia, wanapinga usifanikiwe. Lakini Bwana amekuja kukufungua kwa kuwa anahaja nawe.

“Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.” Mathayo 21:3

Kuna mtu yuko mahali amefungwa, kila akipata kazi anafukuzwa, mwingine upo kanisani lakini roho yako imefungwa kwenye shamba la mtu au kwenye duka la mtu, yeye anapata faida kupitia wewe lakini wewe unazid kudidimia. kupata chakula kwako imekuwa shida, hujapata kazi upo kama ulivyo. Mtekaji hataki utoke kwenye kifungo hicho amewekuwekea walinzi wanakulinda usitoke. Ikiwa kwenye magereza ya kimwili kuna walinzi wanawalinda waliofungwa ndivyo waliokufunga wankulinda ubaki kwenye kifungo chako.

Nimesoma habari jana mchungaji mmoja amechinja mke wake ambaye ni mwalimu wa chuo kikuu, usiwaze kuwa ni msongo wa mawazo huo au makosa ya mke, ni bwana jera wa rohoni analinda hadi mtu anaamua kumchinja mke wake. Ndipo Yesu akasema pale njia panda kuna wafungwa wawili wamefungwa na waliomfunga wapo karibu lakini wakiwauliza waambie Bwana anahaja nao.

Ndoa yako ipo mashakani, huwezi kuamua; nikupe mfano wa kibinadamu, wafungwa sio kwamba hawapendi kuvaa tai, wanapenda lakini baada ya kuingia magereza wanapewa sale ya njano na kaptura, chakula cha kupangiwa. Unawaza ‘mimi sijafungwa’, rafiki yangu Mungu anatamani ujue kuwa heshima ya kidunia inaambana na mambo matatu, unakula nini unavaa nini na unakaa wapi, kuna mtu unatamani ungenda na gari kazini lakini umefungwa unatembea kwa miguu.

Shetani hakuwa ndani ya Yoshua kuhani mkuu bali alikuwa nje ili amzuie. Mungu anataka uhamie kwako, uingie kwenye ufalme wako, zamani wewe ulikuwa una duka kubwa lakini siku hizi unanunua kwa watu, umetengenezewa kifungo usifanye mambo fulani.

Ulikuwa unalala vizuri zamani lakini wachawi wanajua kuwa mtu huyu akilala ataongea na Mungu, ikifika saa tatu usingizi unakata ikifika saa mbili inabii uende kazini usingizi unarudi hatari. Hali imebadilishwa ya mwili ili ushindwe, ukose kazi.n.k

Kuna wakati watu wamekaa magereza hadi wamezoea, unasikia mtu anasema ule ugonjwa 'wangu' umeaanza tena, ile presha 'yangu' imepanda tena.. Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri Farao akaamua kuwatendea kwa akili ili waendelea kuwa hapo, wakawa wanakula chakula, mikate, pilau mpaka walipotolewa wakatamani kurudi misrii. Hivyo shetani anaweza kukulinda matekani hadi wewe ukakubari kukaa kifungoni, anakutengenezea mazingira uyapende mazingira ya utumwani.

Mtu anaweza kufungwa na kila analojaribu likawa haliwezekani, unaweza ukawa mtumishi wa Bwana lakini ukawa ni mzinzi , umetekwa; unaweza kumtumikia Mungu lakini bado ni mmbea. Ukisikia Tangazo hili toka shimoni kwa sababu wao hawapendi kuwafungua watu warudi kwao, dunia haiwezi kukufungua, shetani si rafiki yako ni adui anatengeneza mipango ili tu ubaki kwenye kifungo.

Mtu anaweza kufungwa na kuwekwa shimoni, kisha ukaona moyo wake umebadilika, ukaona tabia yake imeharibika. Unaweza kumuona mtu anaumwa macho hadi anabadilishiwa miwani kila mwezi. Kuna binti mmoja alikuja kanisani na miwani, nikamuombea akapona kabisa. Kuna wakati mwingine unamwona mtu miguu inamuuma unamuombea unamwambia simama uende lakini anaendelea kuwa hivyo kwa kuwa yule aliyemfunga hataki kuwaachia.

Bwana anasema ‘nimekuita kwa haki na nimekushika kwa mkono na kukulinda, ili uwe na agano kwa ajili ya watu na nuru ya mataifa. Ili uyafunue macho ya vipofu na waliokuwa katika nyumba ya utumwa. Ukiwa gerezani huwezi jua nini kinaendelea katika ulimwengu wa kawaida, huwezi kuona maendeleo, huwezi kuona uzao wako unaenda vibaya au la. Sera ya kumpeleka mtu shimoni jambo la kwanza nikumfanya mtu awe kipofu, mtu akitiwa upofu hata ukimwambia mtu njoo kanisani anakuwa na maneno, ukimwambia acha dhambi analeta mzaa kwa kuwa amekuwa kipofu hauoni tena, haoni kama amechukuliwa msukule.

“Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.” Isaya 42:7

Ukitekwa na kuwekwa kifungoni akili zinakuwa haifanyi kazi na macho hayaoni. Ndio maana unaweza mkuta yupo jalalani unamwambia toka hapa, anajibu anasema niko ‘Marekani nakula raha usinisumbue.’ Si yeye anayesema ndani yake bali pepo wamekaa kumzuia asitoke kifungoni. Jambo la ajabu wale wanaotoa matangazo ya ajabu au ya madhara ni watu wanaoonekana wamevaa vizuri, ili wawavutie watu waingie dhambini. Unashangaa mtu anaenda kukutana na mtu gesti anazini naye bila kumfahamu, si kwa akili zake bali amepofushwa macho.

Mkristo anapaswa kulipokea neno la Mungu kwa unyenyekevu. Kinachokufanya ukwame mahali ni kwa sababu haunyenyekei kwenye neno la Mungu, Neno la Bwana likitoka lazima ulishike na upige nalo likupeleke mahali. Je wewe unanyenyekea kwenye neno la Mungu,? Wahubiri hawapo hapa kuchekesha, kamata kila Neno linalotoka kwenye vinywa vyao libebe litumie kwenye maisha yako. Musa aliwaambia watu maneno mengi aliyo ambiwa na Mungu, ndipo Yethro akasema maneno yote uliyoyasema tunayo na tutayatumia. Biblia inasemaMtu yule anayesikia neno la Mungu asilitendee kazi anafananaishwa na mtu anayejiangalia kwenye kioo kisha anajisahau. Mtu anayeshika neno nakulitenda anafananishwa na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba, mafuriko, upepo uje lakini yeye atasimama. Bwana akusimamishe tena ujenge nyumba kwenye mwamba kwa jina la Yesu.

Kuna vipofu maprofesa, wafanyabiashara, mawaziri. Yupo mtu amekomaa na bagia tu, chapati tu, unga tu hana biashara ya zaidi kumuingizia kipato. Kifungo cha mtu kinaanzia kwenye ukipofu, ukipata upofu unawekwa gerezani na mtu aliyeshimoni amefungwa macho anaona ni pazuri kumbe yupo kwenye mlima, kwenye mapori, kwenye misitu kwakuwa amepigwa upofu hawezi kufikiria lolote. Unamkuta unamwambia mtu tukatafute kazi lakini hataki kwakuwa yupo kifungoni,. leo Bwana akuamshe mahali ulipolala kwa jina la Yesu.

Nyumba za giza zimejaa watu, nyota za watu, zimejaa misukule, zimejaa ndoa za watu, kazi za watu, zimejaa miguu na mali za watu. Uonapo maisha yako ni giza au uelewi kesho yako itakuwaje ni kwasababu umefungwa na kuwekwa kwenye nyumba ya giza na umetiwa upofu usiweze kuona tena.

Tangazo la Yesu limekwisha kutoka, ukisikia Tangazo hili utoke kwenye kila kifungo ulichofungiwa, utoke kwenye jela ya kushindwa kwenye kazi; jela ya ndoa, utoke kwenye jela ya ndoa. Ni wakati wako wa kutoka kwenye jela hilo, usisubiri ufuatwe mahali ulipo, ukisikia Tangazo unatoka kifungoni unaenda mahali pako kwa jina la Yesu. Leo Bwana akutoe kifungoni, ulipozuiliwa naagiza moto wa Mungu ukutoe kwa jina la Yesu.

Shetani aliwahi kushindana na Yesu alipotoa Tangazo la kuwatoa watu mashimoni, nakuwafungua watu kwenye vifungo vyao. Wakamkokota wakataka wamtupe kwenye bonde lakini Yesu akapita katikati yao. Huu ni wakati wa kukimbilia nyumbani mwa Bwana, kumwambia kama unanibariki au la, si wakati wa kukaa bila kazi, bila ndoa umekaa kwenye nyumba ya giza. Leo upite katikati ya wanaokuzuia kwa jina la Yesu.

Usikubali kubaki kama ulivyo, kama ukianza kazi usikubali kubaki ulivyo, usikubali kubaki kwenye ndoa ya mateso,usikubali kubaki kwenye mtaji wa ndizi kumi. Inabidi uongezeke, ukiolewa basi uzae, ukifanya kazi basi ujenge ukianza biashara ufanikiwe, ukikaa kwenye kazi ufanikiwe, lakini wachawi wanafurahi sana ubaki kwenye taabu. Wana wa Israeli walipotanagaziwa kutoka kwenye utumwa walipita kwenye nyumba za wamisri wakichukua mali wakaondoka nazo, nawe Bwana akutoe na kazi, biashara na elimu yako kwa jina la Yesu.

“ kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza, Jionyesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho. Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza. Nami nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na njia kuu zangu zitatukuzwa zote.” Isaya 49:9-11

Mchawi anaweza kukufunga wewe kwakuwa umetenda dhambi na ni halali wewe kufungwa kwakuwa wewe ni mkosaji, lakini akipatikana mwenye nguvu yeye anaweza kumfungua yule aliyetekwa kihalali. Mungu anasema yeye ‘atasema na wale waliowafunga watu kihalali ili awatoe, leo Yesu amekuja kutafuta na kuwaweka huru waliofungwa kihalali kwaajili ya dhambi zao pia.

Roho ya mtu inaweza kukamatwa, mwili kukamatwa, sehemu ya mtu inawezwa kukamatwa, kushikwa sana mahali. Umeshikwa usisome, usishike mimba, lakini Mungu amekuja ili akutoe kwenye vifungo (Ayubu 33:20-30). Mkozi wetu Yesu ni hodari anataka utoke upate starehe na furaha tena. Bwana nataka utoke kwenye mashimo na uyaelekee mafanikio yako na ndoa yako yenye furaha kwa jina la Yesu.

“Bwana wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda, wameonewa pamoja; na wote waliowachukua mateka wanawashika sana; wanakataa kuwaacha. Mkombozi wao ni hodari; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli” Yeremia 50:33 - 34

Ukisikia Tangazo hili si wakati wa kufanya moyo wako mgumu, ni wakati wa kukimbilia nyumbani mwa Bwana ili ukutane na Yesu. Ukimpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa miasha yako yeye anakueka huru pamoja na familia yako na mambo yako yote.

Yeremia 52: 31 Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, AKAMTOA GEREZANI.
32 Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake juu ya viti vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli.

Luka 4: 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

Shalom,

Max Shimba Ministries

Ingia kwenye www.maxshimbaministries.com na jifunze mengi. 

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW