BWANA YESU asifiwe!
Je, Mwanamke anaweza kuvaa suruali akiwa katika mazingira ya kikazi kama Jeshini au Kama ni Fundi Umeme au Hotelini n.k?
Je, Mwanamke anaweza kuvaa Suruali akiwa kwenye mazingira ya baridi kali la barafu? Au anaweza kuvaa kulingana na tamaduni yanchi zao?
Je, ipo wapi aya ndani ya Biblia isemayo Suruali ni vazi la wanaume?
Nimekutana na swali jana ya kuwa "Je ni halali kwa mwanamke kuvaa suruali?" Nikapewa na andiko katika Kumbukumbu laTorati 22:5 Haya Wapendwa tunasemaje juu ya hili!! Maoni yangu ni haya yafuatayo Kwani Imeandikwa wapi kwamba Suruali ni Vazi la Kiume?
Pia Biblia inataja kuwa kuna mavazi ya kikahaba, (Mwanzo 38:14 ) ukisoma Mithali 7:10 inasema “Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;…mtu yeyote aliyekuwa ameonekana ameyavaa hayo” Kulikuwa na mavazi ya kikuhani pia ambayo yakivaliwa, yanamjulisha Yule ni Kuhani nk. yote hayo mtu alipokuwa akivaa yalikuwa yaashiria kitu Fulani rohoni.
Shalom ndugu zangu mimi nimesoma swali hilo na nimebarikiwa sana na kufurahi sana na mimi pia naomba nichangie kidogo juu ya suala hili nionavyo mimi kuvaa suruali kwa mwanamke sio dhambi ila itakua dhambi tu kama itasababisha wengine kutenda dhambi katika Mathayo 18:7 Biblia inasema ''Ole kwa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha, maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; LAKINI OLE WAKE MTU YULE ALILETAYE JAMBO LA KUKOSESHA.''
Kwa hiyo ndugu zangu Suruali itakuwa dhambi kama itawashawishi wengine kuingia dhambini maana tukisema tu kuvaa nguo fulani ni dhambi basi mvaaji hatakiwi kuvaa hata kama yuko chumbani na mmewe maana kuvaa nguo hiyo ni dhambi na dhambi zingine ni dhambi hata kwa kusababisha mfano unakuta kijana anaenda kutongozea kijana mwingine kwa binti na ukimuuliza atakwambia kutongoza sio dhambi ila dhambi ni kuzini lakini ukweli hiyo ni dhambi kubwa wote mnajua na hili pia la kuwavalia wengine nusu uchi ni dhambi na kwa habari ya Suruali kuwa ndio vazi la kiume napata tafakari hii.
HOJA YA KUFIKICHA AKILI:
Je, ipo wapi aya ndani ya Biblia isemayo Suruali ni vazi la wanaume?
Biblia iliposema mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanaume haikutaja Suruali. Kwa upande wangu neno Suruali kwenye Biblia lipo katika Danieli 3:21 ikizungumzia habari ya wale vijana watatu, Anania, Azariya na Mishael "Shedrack, Meshach, and Abednego) waliotupwa katika tanuri la moto huku wakiwa wamevaa Suruali zao na joho zao. Hawa walikua wanaume wote hata hivyo hapa haionyeshi kwamba hayo ndio mavazi ya wanaume.
Muhimu na cha kuzingatia ni kwamba Biblia imeagiza wanawake wavae nguo za kujisitri na nguo hizi haijalishi ni sketi au Suruali maana wapo wadada wengine huvaa sketi za kuwachora maungo yao utasema hata heri ya anayevaa suruali. Pia hakuna haja ya kuiga kila mtindo maana kuna baadhi ya mitindo chanzo chake ni kuzimu. Kumbuka pia tunaitwa Wakristo yaani wanaomfuata Kristo. Matendo 11:26, pia tukumbuke kuwa kama tutaupenda sana ulimwengu na mambo yake basi kumpenda MUNGU hakumo ndani yetu hivyo hakuna haja ya kuwaweka majaribuni wenzako na ukiangalia wengi wa wanaovaa nguo ambazo zinalalamikiwa ni wale ambao hawajaolewa na akiolewa anaacha hapo ndio unajua kwamba alikua anavaa zamani kwa sababu fulani ambayo ni dhambi.
Warumi 14 : 2 - Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
๐� _Wewe ambaye unaitazama suruali kama dhambi kwako ukiivaa, usijaribu kuvaa kwako ni dhambi, umekwisha kujihukumu nafsi, na kila tendo lisilo tokana na imani ni dhambi_ Yule avaaye kwa nia ya vazi, la kujisitiri, kwa nia safi, nia yake haikuwaza uovu, amevaa yeye kama yeye, usimuhumukumu wewe usiye vaa, maana yeye anaimani na dhamiri yake yamshuhudia vema.
Mathayo 5 : 28 - lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Agano la kale dhambi ilikuwa ni matendo, na yalihumumiwa matendo, lakini agano jipya Yesu anahukumu kuanzia nia, yaani mpaka umezini, siku ulio zini, siyo siku ulioanguka, ulizini na kuanguka tangu ulipo anza mchakato wa nitalala na huyu binti, au ulipo kubali kwamba ntakupa๐�๐, sasa wewe unaye vaa Suruali ndani yako umekusudia nini, ndo hukumu inako anzia.
Warumi 8 : 27 - Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Mungu anatujua vizuri, kwa kuichunguza Nia ya moyo na kujua, huyu amevaa suruali lakini lengo, ka msukumo awatege watu, aonyeshe umbo lake, nk, nk... Huyu amevaa walaaa hana lolote ndani, kavaa kujisitiri na safari, na kazi hii, sheria ya ofisini nk, na Ameamua kuvaa ya heshima
Lakini wapendwa tusiwe na ufahamu mdogo, wewe waihukumu Suruali kama dhambi, hujui gauni, blause, sketi nayo ni dhambi, ila tu umevaaje, ikoje? Kwani vimini ni Suruali? Vitop ni suruali? Magauni na sketi za mpasuo hatari ni suruali? Je, ni vizuri kwa sababu ni nguo za kike? Kata K, Suruali siyo dhambi kwa sababu imevaliwa na mvulana ni vazi lake? Tusiwe na ufahamu finyu panua fikira.
Kama watoto wa MUNGU tuliozaliwa sio kwa mwili bali kwa ROHO WA MUNGU basi na tuenende kama watakatifu wa MUNGU pasipo lawama.
Natamani niendelee lakini mwisho kabisa Biblia katika Waefeso 5:10 inasema ''MKIHAKIKI NI NINI IMPENDEZAYO BWANA'' .
MUNGU awabariki sana na kila mtu awe ni mwanamke au mwanaume kwa kila tendo lolote afanyalo ahaakiki kama anampendeza MUNGU maana tukitenda kwa kumpendeza MUNGU hatutalalamikiwa .
MUNGU awabariki sana Na nahitaji michango ya watumishi wengine hapa au kwenye page yetu ya facebook itwayo Maisha ya Ushindi FUNGUA HAPA KUTOA MAONI YAKO.
Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
Shalom
No comments:
Post a Comment