Tuesday, April 30, 2013

Biblia inasema je ju ya chale/ kujitoboa mwili?


Agano la kale liliwaamuru waIsraeli, “Msiikate miili yenu kwa ajili ya wafu wala kuchanja chale juu ya ngozi za miili yenu.Mimi ni Bwana” (mambo ya walawi 19:28). Hata hivyo ijapokuwa waumini kwa sasa hawako chini ya sheria ya agano la kale (warumi 10:4; wagalatia 3:23 – 25; waefeso 2:15), hoja ya kuwa kulikuwa na sheria juu ya chale lazima lituletee maswaliagano jipya haisemi lolote juu ya muumini achanjwe chale au asichanjwe.

Kulengana na swala la chale na kujikata alama mwilini, mtazamo wetu ni uwe; je, twaweza kumuomba Mungu atumie alama hizo kwa utukufu wake? “kwa hivyo mnapokula, mnapokunywa, chochote mfanyacho, kifanyeni kwa utukufu wa Mungu” (wakorintho wa kwanza 10:31). Biblia haituamuru kinyume cha chale na alama za mwili lakini pia haituonyeshi ya kuwa ana haja na alama hizo miilini mwetu.

Jambo lengine ni nidhamu. Biblia inatushauri kuvaa mavazi yetu kwa nidhamu (Timotheo wa kwanza 2:9). Kuvaa ki nidhamu ni kuziba sehemu zote zilizotarajiwa kuzibwa na mavazi. Lengo la nidhamu hii ya ki mavazi si juu ya wewe mwenyewe bali kwa ajili ya wengine wasije wakanaswa na hali yakuvutiwa nawe kiasi cha kukutamani. Chale pia zinaushawishi Fulani kwa hivyo zinakeuka mipaka ya nidhamu hii.

Kanuni muhimu ya kibiblia ni kutazama jambo kwa mfumo wa imani. Kama hulionei shaka moyoni juu yakuwa linampendeza Mungu basi lifanye. “kwa kuwa lolote ambalo, si la imani ni dhambi” (warumi 14:23). Tunapaswa kufahamu kuwa miili yetu na nafsi zetu pia zimekombolewa na ni mali ya Mungu. Ijapokuwa haelekei moja kwa moja juu ya chale na alama za miili, wakorintho wa kwanza 6:19 -20 inatupatia kanuni moja, “Nini? Hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, ambaye mnaye kutoka kwa Mungu na ninyi si mali yenu wenyewe. Mmenunuliwa kwa thamani kwa hivyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambvyo ni vya Mungu.” Miili yetu sharti iandamane na ukweli kokote tuendako. Kama miili yetu ni mali ya Mungu basi lazima tuwe na ruhusa yake kabla hatujajichanja chale hizo au alama hizo za mwili.

Mkristo ni mtu gani?


Kwa tafsiri kutoka kamusi ya Webster Mkristo ni “mtu mwenye kukiri imani ndani ya Yesu kama Kristo au Imani yenye msingi wa mafundisho na ufunuo wa Yesu.” Ijapokuwa huu ni mwanzo mwema wa kufahamu Mkristo ni mtu gani, kama maelezo mengi ya kidunia yalivyo, inapungukiwa na uhalisi wa kibiblia juu ya Maana kamili ya Ukristo au Mkristo. 


Neno Mkristo limetumika mara tatu katika agano jipya (Matendo 11:26; Matendo 26:28; Petero Wa Kwanza 4:16). Wafuasi wa Yesu Kristo waliitwa kwa mara ya kwanza “Wakristo” antiokia (Matendo 11:26) kwa sababu tabia zao, matendo yao na hotuba zao zilikuwa kama za Kristo. Ilitumika kiasili na watu wasiookoka wa Antiokia kama jina la kimajazi kuwadhihaki wakristo hao. Ina maana sawa na “Kuwa mmoja wa kundi la kristo” au “mfuasi wa Kristo,” ambayo imefanana na tafsiri ya Neno hili katika kamusi ya Webster.

Kwa bahati mbaya, neno Mkristo limepoteza kwa kiwango kikubwa usawa wa matumizi yake na Linatumika mara kwa mara kumaanisha tu mtu mwenye dini au pengine muadilifu kinyume cha Mfuasi halisi wa Yesu Kristo aliyezaliwa mara ya pili. Watu wengi wasioamini na kuwa na tumaini ndani ya Yesu Kristo hujichukulia tu kuwa ni wakristo kwa sababu wanahudhuria ibada za Kanisa ama wanaishi katika taifa la kikristo. Lakini, kuenda kanisani, kuwahudumia wale wasiobahatika maishani au kuwa mtu mzuri haviwezi kukufanya kuwa mkristo. Kama Muinjilisti mmoja alivyosema, “kuenda Kanisani hakufanyi mtu kuwa Mkristo sawa na mtu kuenda gereji hakumfanyi kuwa gari.” Kuwa mshirika wa kanisa anayehudhuria ibada kila mara na kutoa kwa ajili ya kazi za kanisa hakuwezi kukufanya wewe kuwa Mkristo.

Je ni nini kitawapata watu wale hawajawai pata nafasi ya kusikia kuhusu Yesu?


Je ni nini kitawapata watu wale hawajawai pata nafasi ya kusikia kuhusu Yesu? Je Mungu atawahukumu wale ambao hajawai sikia kuhusu Yesu?"

Jibu: Watu wote wamewajibika kwa Mungu hata kama wamesikia au hawaja “sikia kumhusu” Bibilia yatwambia wazi wazi kuwa Mungu anajidhihirisha mwenyewe kwa uungu (Warumi 1:20) na katika Roho za watu (Mhubiri 3:11). Shida ni kwamba ni uzao wa dhambi wa mwanadamu. Zote twakataa hii hekima ya Mungu na kuasi (Warumi 1:21-23). Kama isingekuwa ni neema ya Mungu, tungejitolea kwa mioyo ya dhambi, kujiruhusu kujigundulia vile maisha ni bure, yakustaajabisha ni sehemu kando naye Mungu. Anafanya haya kwa wale wanaoendelea kumkataa (Warumi 1:24-32).

Ukweli ni, si eti watu wengine hawajasikia juu ya Mungu. Badala, shida ni wamaekataa chenye wamesikia na chenye kinaonekana katika uumbaji. Kumbukumbu La Torati 4:29 yasema, “Lakini huko, kama mkimtatufa BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.” Aya hii yatufunza nguzo muimu. Kila mmoja anayemtafuta Mungu atampta. Kama mtu amenuia kumjua Mungu, Mungu atajudhihirisha kwake.

Shida pekee, “Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu” (Warumi 3:11). Watu wanakataa hekima ya Mungu ambayo ipo katika uumbaji na katika mioyo yao, na badala wanaanza kuabudu “miungu” yao wenyewe wamejitengenezea. Ni ubumpavu kubishana juu ya haki/uungwana wa Mungu kumtuma mtu jahanamu mwenye hakuwa na nafasi ya kuisikia injili ya Kristo. Watu watawajibika kwa Mungu kwa yale yote Mungu ameyafunua kwao. Bibilia inasema watu wanakataa hekima na kwa hivyo Mungu ako haki anapowahukkumu kwenda jahanamu.

Mpango Wa Wokovu ni nini?


Una njaa? Si njaa ya chakula, lakini je, una njaa ya kitu Fulani zaidi maishani? Je, kuna hali Fulani ya kutotosheka ndani yako? Ikiwa iko basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mkate wa kweli. Kila ajaye kwangu hatahisi njaa na aniaminiye hataona kiu” (Yohana 6:35).

Je, umechanganyikiwa? Je, huoni mbele ya maishani mwako? Je, unajihisi kama umeachwa kwenye giza na huoni pa kutokea? Ikiwa hali yako ni kama hiyo basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu. Anifuataye hatatembea gizani, bali atakuwa na nuru ya uzima” (Yohana 8:12).

Je, unajisikia kama umefungiwa nje ya maisha yako? Je, umejaribu njia nyingi na kutambua ya kwamba kile ulichokitarajia hakipo ndani yake? Je, unatafuta njia ya kufikia maisha makamilifu? Ikiwa haya ndiyo uyatafutayo, Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mlango wa kondoo; aingiaye kupitia mimi ataokolewa. Ataingia na kutoka na kupata malisho” (Yohana 10:9).

Je, watu wengine husababisha kushindwa kwako? Je, uhusiano wako nao umekuwa si wa kina na bila muelekeo? Je, ni kama watu wanakutumia tu kwa manufaa yao? Ikiwa ndiyo hali unayopitia Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema hutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo……. Mimi ndimi mchungaji mwema; Ninajua kondoo wangu na kondoo wangu wananijua” (Yohana 10: 11,14).

Je, unashangazwa na kinachotendeka baada ya maisha haya? Je, umechoshwa na maisha ya kupigania tu vitu vinavyooza na kushika kutu? Je, wakati mwingine maana ya maisha yako huionea shaka? Je, unataka kuishi hata baadaya kufa? Ikiwa haya ndiyo uliyonayo basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Aniaminiye ataishi, hata ajapokufa; na aishiye na kuniamini hata kufa kamwe” (Yohana11:25-26).

Njia ni nini? Ukweli ni nini? Uzima ni nini? Yesu akajibu, “Mimi ndimi njia kweli na uzima.Hakuna afikaye kwa baba bila kupitia kwangu” (Yohana 14:6). 

Monday, April 29, 2013

Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga? Je, Ushoga ni dhambi?


Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi 1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.

Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.

Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).

Biblia inasema nini juu ya kushirikiana katika ngono kabla kuoana?


Pamoja na matendo mengine ya uchafu, kufanya kitendo cha mapenzi kabla kuoana kumekatazwa katika maandiko (matendo 15:20; warumi 1:29; wakorintho wa kwanza 5:1; 6:13, 7:2; 10;8; wakorintho wa pili 12:21; wagalatia 5:19; waefeso 5:3; wakolosai 3:5; wathesalonike 4:3; yuda7). Biblia inasisitiza kuepuka kitendo hicho kabla ya ndoa.hii ina maana ya kuwa ni dhambi kama ya uzinifu kwa kuwa hujaunganishwa na unayefanya naye kitendo hicho. Mapenzi baina ya mume na mke waliooana ndiyo mapenzi yanayokubalika mbele za Mungu (waebrania 13:4).

Kushirikiana katika ngono kabla ndoa kumeenea sana kwa sababu nyingi. Mapenzi yanastarehesha. Mungu aliyaumba hivyo. Anawataka wanaume na wanawake wafurahie kitendo cha ngono (ndani ya ndoa). Hata hivyo, lengo la msingi la ngono si starehe bali kuzaana tukaongezeke. Hivyo tunazuiwa kufanya kitendo cha ngono kabla ndoa ili tusijipatie watoto tusiowatarajia. Kama jambo hili lingezingatiwa, magonjwa ya zinaa na wamama wasioolewa na kuavya mimba na kadhalika kungepungua. Kujizuia kunaokoa maisha, kunalinda watoto wachanga na kuleta ladha halisi ya ngono pamoja na heshima kwa Mungu.

Biblia inasema nini juu ya kunywa kileo? Je, ni dhambi kwa mkristo kunywa kileo?


Maandiko yana ilani nyingi juu ya kunywa kileo (mambo ya walawi 10:9; hesabu6:3; kumbukumbu la torati 29:6; waamuzi 13:4,7,14; samueli wa kwanza 1:15; methali 20:1; 31:4,6; isaya 5:11;22; 24:9; 28:7; 29:9; 56:12; mika 2:11; luka 1:15). Maandiko hayakatazi mkristo kunywa pombe, divai wala kinywaji chochote chenye kileo ndani. Maana maandiko mengine huzungumzia kileo kwa kuhalalisha matumizi yake. Mhubiri 9:7 inaamuru, “ kunywa kileo na moyo mkunjufu.” Zaburi 104:14-15 inaeleza Mungu hutoa divai “ inayofurahisha mioyo ya wanadamu.” Amosi 9:14 inazungumzia juu ya kunywa divai kutoka kwa shamba lako kama alama ya baraka za Mungu. Isaya 55;11 inapongeza “ naam, njoo ununue divai na maziwa…”

Kile Mungu anachowaamuru wakristo juu ya kileo ni wajizuie na ulevi (waefeso 5:18). Biblia inakataza ulevi na athari zake (methali 23:29-35). Wakristo wanakatazwa kuachilia miili yao itawalwe na vitu vinginevyo. (wakorintho wa kwanza 6:12; petro wa pili 2:19). Kunywa kileo kingi kunaathiri mtu. Maandiko yanakataza chochote kile ambacho kwa kukifanya unasababisha wengine kujikwaa( wakorintho wa kwanza 8:9-13). Kwa mujibu wa haya ni vigumu mkristo kukiri kuwa anakunywa kileo kwa utukufu wa Mungu ( wakorintho wa kwanza 10;31). 

Yesu aligeuza maji kuwa Divai. Huenda ikawa Yesu alikuwa akinywa divai katika karamu Fulani Fulani (Yohana 2:1-11; Mathayo 26: 29). Katika nyakati za agano jipya, maji yalikuwa yakijawa na vidudu na uchafu kama hali ilivyo sasa katika mataifamengine ya ulimwengu wa tatu. Hii ndiyo sababu watu walipendelea kunywa divai kutoka kwa zabibu ili kuepukana na taka taka hizi. Katika timotheo wa kwanza 5:23, Paulo alimkataza timotheo kunywa maji yaliyokuwa yakimtatiza tumbo lake na mahali pake anywe divai. Divai ilikuwa na asili ya kileo ndani lakini haikuwa na kiwango cha kilevi sawa na cha leo. Haikuwa maji ya mzabibu moja kwa moja wala kileo sawa na cha leo. Maandiko hayakatazi mkristo kunywa kileo cha aina yoyote bali yanakataza ulevi na utumwa wa kileo (waefeso 5:18; wakorintho wa kwanza 6:12).

Kileo, kinapotumiwa kwa uchache hakina athari kwa mwenye kukitumia. Kutumia kiasi kichache cha kileo ni jambo linaloruhusiwa mkristo. Ulevi na utumwa wa kunywa kileo ni dhambi. Kwa sababu ya kushindwa kujizuia katika viwango vya matumizi ya kileo, kukwaza wengine na hata kupatikana na hatia mbali mbali, ni vizuri mkristo aepukane kabisa na matumizi ya kileo cha aina yoyote.

Je! Mkristo anaweza pagagwa na Mapepo?


Bibilia kwa ukamilifu haitaji kama Mkristo anaweza shikwa na pepo. Ingagwa, kwa vile Mkristo amejazwa na Roho Mtakatifu (Warumi 8:9-11; 1 Wakorintho 3:16; 6:19), inaweza ooneka kinyume kwamba Roho Mtakatifu anaweza kumuruhus pepo kushika mtu ambaye Roho Mtakatifu anakaa ndani yake. Hii mara nyingine ni jambo la kutatanisha; ingawa, tunaamini sana kuwa Mkristo hawezi shikwa na pepo. Tunaamini kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kushikwa na pepo na kukandamizwa na pepo au kushawishika na pepo. Kupagagwa na pepo yahuzisha,pepo kuwa na uhusika wa Karibu au kuongoza mawazo yako/mafikirio yako/matendo ya mtu (Luka 4:33-35; 8:27-33; Mathayo 17:14-18). Kukandamizwa na pepo au kushawishiwa na pepo inahuzisha pepo kumkabili mtu kiroho na kumtia moyo kwa matendo ya dhambi (1 Petero 5:8-0; Yakobo 4:7). Tambua kwamba kurasa zote za Agano Jipya zashugulikia vita vya kiroho, kamwe hatwambiwi kutoa pepo kutoka kwa mkristo (Waefeso 6:10-18). Wakristo wameambiwa kumtoroka shetani (1 Petero 5:8-9; Yakobo 4:7), si kutoa mapepo.


Ni jambo lisilofikirika kuwa Mungu anaweza kumruhus mwanawe, ambaye alimununua kwa dhamani, kwa damu ya Yesu Kristo (1 Petero 1:18-19), na kufanywa viumbe vipya (2 Wakorintho 5:17), kupagagwa na kutawaliwa na mapepo. Naam, mkristo twafanya vita na shetani na mapepo yake, lakini si kutoka ndani yetu. Mtume Yohana anasema, “Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mtungu; ninyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko aliye katika dunia” (1 Yohana 4:4). Ni nani aliye ndani yetu? Roho Mtakatifu. Ni nani aliye katika dunia? Ni shetani na mapepo yake. Kwa hivyo, mkristo ameushinda ulimwengu wa mapepo, na hali ya kupagagwa na pepo halitafanywa kuwa la kibilia.

Ubatizo wa Rohoho Mtakatifu ni nini?





Ubatizo wa Roho mtakatifu unaweza kufafanuliwa/kuelezwa kuwa ile kazi ambayo Roho Mtakatifu wa Mungu unamweka muumini kuwa na ushirika na Kristo na kwa ushirika na waumini wengine katika mwili wa Kristo wakati wa kuokolewa. Wakorintho wa kwanza 12:12-13 ni ukurasa wa katikati katika Bibilia kuhusu ubatizo wa Roho Mtakatifu, “Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.” (1Wakorintho 12:13). Bali Warumi 6:1-4 haitaji roho wa Mungu, bali yaelezea sehemu ya wakristo mbele za Mungu kwa lugha sawa na ile ya ujumbe wa kwanza Wakorintho: “Tusema nini basi? Tudumu kaitka dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”

Hoja zifuatazo zatosha kudumisha uelefu wetu juu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kwanza, 1Wakorintho 12:13 yataja wazi kwamba wale wote waliobatizwa wananyweshwa Roho mmoja (kuwepo kwa Roho mtakatifu). Pili, hamna mahali katika Bibilia Wakristo wameelezwa wabatizwe, ndani ya, au kwa Roho au kwa vyovyote vile watafute ubatizo wa Roho Mtakatifu. Hii yaonyesha kuwa Wakrisot walikuwa na uzoevu. Tatu, Waefeso 4:5 yaonekana kuashiria ubatizo wa Roho. Kama hii ndio hali, ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kitu cha kweli kwa kila Mkristo, kama vile “Imani mija” na “Baba mmoja” viko.

Kwa kumalizia, ubatizo wa Roho Mtakatifu wafanya mambo mawili, 1) Watuunganisha na mwili wa Kristo, na 2) Waambatanisha kusulubiwa kwetu na Yesu. Kuwa na mwili wake, yamaanisha, tumefufuliwa naye kwa upya wa uzima (Warumi 6:4). Kwa hivyo lazima tuviweka katika matendo vipawa vyetu vya Roho ili tuuweke mwili wa Kristo kuendelea kufanya kazi kulingana na 1Wakorintho 12:13. Kushuhudia ubatizo wa roho mmoja huwa mzingi wa kuwa na umoja wa Kanisa, kulingana na mkudhatha wa Waefeso 4:5. Kuwa na ushirika wa karibu na Kristo katika mauti yake, kuzikwa kwake na ufufuo wake kupitia kwa ubatizo wa Roho waweka mzingi wa kutenganishwa na nguvu za dhambi na kutembea katika maisha mapya. (Warumi 6:1-10; Wakolosai 2:12).

Nawezaje kujazwa na Roho Mtakatifu?


Kifungu cha maana katika kuelewa juu ya kujazwa na Roho Mtakatifu in Yohana 14:16, mahali ampapo Yesu anaahidi kukaa kwa Roho Mtakatifu kwa wakristo, na huyo atadumu si kwa muda. Ni kitu cha maana kutofautisha kati ya kukaa kwa Roho Mtakatifu na kujazwa na Roho Mtakatifu. Kudumu kwa Roho Mtakatifu aupo kwa baadhi ya wakristo, bali ni kwa Wakristo wote. Kuna sehemu nyingi katika Bibilia zinazo pongeza huu msimamo wetu. Kwanza, Roho Mtakatifu ni zawadi iliyopewa Wakristo wote katika Kristo Yesu bila kupagua, na hakuna sheria za kutimiza ila tu ni kuwa na imani katika Kristo Yesu (Yohona 7:37-39). Pili, Roho Mtakatifu unapokewa wakati wa kuokoka (Waefeso 1:13). Wagalatia 3:2 inasisitiza ukweli huu pia, kwa kusema kwamba kutiwa muhuri na kujazwa na Roho Mtakatifu ulitokea wakati wa kuokoka. Tatu, Roho Mtakatifu unakaa kwa Wakristo milele. Wakristo wamepewa Roho Mtakatifu kama mtaji ama tibitisho la utukufu wao katika siku zijazo katika Kristo (2 Wakorintho 1:22; Waefeso 4:30).

Hili ni linganisho la kujazwa kwa Roho Mtakatifu ambao Waefeso 5:18 yazungumzia. Kikamilifu ni lazima tuzame katika Roho Mtakatifu ili atumiliki na katika hali hiyo atujaze. Warumi 8:9 na Waefeso 1:13-14 za sema kwamba anakaa kwa kila Mkristo, lakini anaweza kuhusunishwa (4:30), na kazi yake ndani yetu unaweza poa (1Wathesalonike 5:19). Wakati tunaruhusu haya kutokea hatuwezi kuhisi kikamilifu Roho Mtakatifu ukifanya kazi na nguvu zake ndani yetu. Kujazwa na Roho Mtakatifu haimaanishi tendo la nche pekee; pia yamaanisha tendo la kimawazo ambalo latutia moyo kwa kila tendo tutendalo. Zaburi 19:14 yasema, “Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wnagu.”

Dhambi ndiyo huzuia kujazwa kwa Roho Mtakatifu, na kumtii Mungu ndio njia pekee Roho anaweza kutunzwa. Waefeso 5:18 yatwaamuru kwamba tujazwe na Roho Mtakatifu; bali si kwa kuomba ili tujazwe na Roho Mtakatifu ambayo itawezesha kukamilisha kujazwa kwa Roho. Ni utiifu wetu wa sheria za Mungu wawezesha Roho kufanya kazi kwa huru ndani yetu. Kwa sababu tumeadhirika kwa dhambi, ni vigumu kujazwa na Roho wakati wote. Wakati twatenda dhambi ni lazima tutubu papo hapo kwa Mungu na tufanye upya mkataba wa kujazwa na Roho and kuongozwa na Roho Mtakatifu.

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration By Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological Institute A...

TRENDING NOW