Thursday, October 24, 2013

Yesu Kristo ameumba mbingu, nchi, watu, na ulimwengu wote.


Biblia Takatifu inatuambia kwamba:
...tuliumbwa katika Kristo Yesu...” (Waefeso 2:10)
Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa sisi wanadamu wote pamoja na viumbe vyote ni kazi ya mikono ya Yesu. Yesu ameumba vitu vyote; tendo la mtu kuukana Uungu wa Yesu ni jambo la kumkosea heshima Mungu aliyekuumba. Ndio maana Yesu aliwaambia Wayahudi kwamba: “...ninyi mwanivunjia heshima Yangu...” (Yohana 8:49).
Tusomapo Biblia Takatifu katika kitabu cha YOHANA sura ya kwanza, tunaona pameandikwa:

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu Wakeutukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” (Yohana 1:1,3,14)  

Huyo “Neno” anayetajwa hapo ndiye Yesu Kristo. Mwandishi wa kitabu hicho cha YOHANA ametumia usemi wa: “...Neno alikuwako kwa Mungu...” akiwa anawafahamisha hususani Wayahudi waliokuwa wanajua kuwa YEHOVA ndiye Mungu wao. Kwa hiyo Yohana anasema “...Neno alikuako kwa Mungu...” kwa maana ya kwamba; huyu “...Yesu alikuwako kwa YEHOVA...” ambaye wao Wayahudi walimtambua kuwa ndiye Mungu wao.

Pia zaidi tunaona Yohana anafafanua kwa kusema kuwa; huyu “...Yesu alikuwa Mungu...” Ufafanuzi zaidi tunauona katika YOHANA 1:14 ambapo Yohana amefafanua kwa kusema; “...Yesu alifanyika mwili; akakaa kwetu...” Biblia Takatifu inamtaja kwa wazi kabisa kuwa Yesu ni Mungu na ameumba vitu vyote “...Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika...” (Yohana 1:3).

Yesu Kristo Ndiye anayekuja kuuhukumu ulimwengu wote siku ya kiyama

Jambo hili si mzaha wala uzushi bali ni kweli; Yesu Kristo anakuja kuhukumu ulimwengu wote. Yesu Kristo ametutamkia kwa kiywa Chake kwa kusema kwamba;
Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.” (Yohana 5:22,23)
Katika hukumu siku ya kiyama hatutegemei kumwona YEHOVA akija kuhukumu ulimwengu, bali, Yesu Kristo ndiye ajaye kuhukumu ulimwengu. Hii itakuwa hivyo ili WATU WOTE WAMHESHIMU Yesu sawa sawa na jinsi ambavyo wanamheshimu YEHOVA. Hapo ndipo viumbe vyote watathibitisha kuwa Yesu ni Mungu. Biblia Takatifu inasema kwamba:
...kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA...” (Wafilipi 2:10,11)
Hakika Yesu ni Mungu. Najua hapa huwachanganya baadhi ya watu hata wanaweza kuhoji;

Je! Wapo Miungu wangapi? Kwa maana tunasikia habari za Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu? Inawezekanaje tuseme Yupo Mungu mmoja wakati hapo tunaona wapo watatu?

Ni kweli Utatu Mtakatifu wa Mungu umekuwa mgumu sana kueleweka kwa watu wengi kutokana na mafundisho dhaifu waliyoyapokea kutoka kwa viongozi wao wa madhehebu yao na imani zao. Je! Utatu Mtakatifu wa Mungu ni uzushi uliotungwa na wanadamu kwa lengo la kupotosha watu au Biblia Takatifu inatuthibitishia wazi wazi kuhusu Utatu Mtakatifu wa Mungu? Hebu twende katika neno la Mungu tuone jinsi lisemavyo.

Biblia Takatifu inatuambia kwamba:

Yesu Kristo anayo amri na mamlaka ya kusamehe dhambi


Kuna jambo lililowahi kutokea hadi likawashangaza watu; hebu fatilia kisa hiki. Biblia Takatifu inasema kwamba:

Wakaja watu wakimleta mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia (Yesukwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi waliokuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,
Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?

Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambiaMbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?

Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi – Akamwambia yule mwenye kupooza,
Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.” (Marko 2:3-12)

Yesu Kristo hajaumbwa bali alikuwepo tangu milele yote

Ni kweli kabisa kwamba Yesu alikuwepo tangu milele yote kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile. Bwana Yesu kwa kauli ya kinywa chake mwenyewe anasema kwamba:
Na sasa, Baba, unitukuze Mimi pamoja Nawe, kwa utukufu ule Mimi niliokuwa nao pamoja Nawe kabla ya ulimwengu kuwako.” (Yohana 17:5)
Neno “UTUKUFU” maana yake ni heshima, uweza, uzuri, umaarufu, nguvu, sifa na mamlaka. Mambo hayo yote Yesu alikuwa nayo kabla hata ulimwengu haujaumbwa. Yesu Kristo alikuwapo hata kabla ya kuzaliwa na Mariamu; jambo hili pia Yesu Kristo kwa kinywa Chake Yeye mwenyewe ametuthibitishia alipokuwa akiwaambia Wayahudi kwamba:

Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?

Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini Mimi namheshimu Baba yanguna ninyi mwanivunjia heshima Yangu. Wala mimi siutafuti utukufu Wangu; Yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti mileleBasi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akuilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si situ; anitukuzaye ni Baba Yanguambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe haujapata bado miaka hamsini, nawe umemona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi niko.” (Yohana 8:47-58)

Katika kisa tulichokisoma katika maandiko hayo (Yohana 8:47-57) tunajifunza mambo kadhaa hapo. Tumeona dhahiri jinsi ambavyo hata baadhi ya Wayahudi ilivyo wawia vigumu sana kumwelewa huyu Yesu ni nani; hata wakadiriki kusema kuwa Yesu anayo mapepo (mashetani). Hawakumwelewa kwa sababu walimtazama Yesu kibinadamu kama jinsi wao walivyo, lakini hawakujua kuwa Yesu ni alikuwepo hata kabla ya Yeye kuzaliwa na Mariamu. Huyo Ibrahimu anayeongelewa hapo ni yule ambaye habari zake tunazisoma katika kitabu cha MWANZO cha Biblia (Ibrahimu baba yake Isaka na Ishmaili). Wayahudi walishangaa; Inawezekanaje huyu Yesu aseme alimwona Ibrahimu aliyeishi na kufa miaka mingi tena zaidi ya elfu moja iliyopita, wakati huyu Yesu tumemwona utotoni mwake na hata sasa bado hajatimiza umri wa miaka hamsini? Hayo yalikuwa ni mawazo ya kibinadamu; tena inaezekana hata wewe ukawa ni miongoni mwa waliokuwa wanawaza hivyo; lakini, Yesu mwenyewe anatuthibitishia kwa kinywa Chake kwa kusema:

Sunday, October 20, 2013

The Name of God in the Bible and the Quran

Part Two: The Name of Allah


We have already presented proof that God’s name in the Bible is YHWH. We must now look at what the Quran calls the name of its god. After doing this, we shall see the implication of this on the relationship between the picture of God found in the Bible and the picture of God in the Quran.
What is the name of God in the Quran? Some passages give us an indication (quotations will be from Pickthall’s version):
Surah 1.1 (and before every Surah except #9)
In the name of Allah, the Beneficent, the Merciful.
Surah 11.41
And he said: Embark therein! In the name of Allah be its course and its mooring. Lo! my Lord is Forgiving, Merciful.
Surah 12.66
He said: I will not send him with you till ye give me an undertaking in the name of Allah that ye will bring him back to me, unless ye are surrounded. And when they gave him their undertaking he said: Allah is the Warden over what we say.
Surah 12.80
So, When they despaired of (moving) him, they conferred together apart. The eldest of them said: Know ye not how your father took an undertaking from you in Allah's name and how ye failed in the case of Joseph aforetime? Therefore I shall not go forth from the land until my father giveth leave or Allah judgeth for me. He is the Best of Judges.
Surah 16.115
He hath forbidden for you only carrion and blood and swineflesh and that which hath been immolated in the name of any other than Allah; but he who is driven thereto, neither craving nor transgressing, lo! then Allah is Forgiving, Merciful.
Surah 27.30
Lo! it is from Solomon, and lo! it is: In the name of Allah, the Beneficent, the Merciful;
By analogy with the use of the name Jehovah (YHWH) in the following passages in the Bible, one could conclude that the name of God is Allah in the Quran (New American Standard Bible):
Deuteronomy 18:7
then he shall serve in the name of the LORD [YHWH] his God, like all his fellow Levites who stand there before the LORD.
1 Samuel 20:42
Jonathan said to David, "Go in safety, inasmuch as we have sworn to each other in the name of the LORD [YHWH], saying, ‘The LORD will be between me and you, and between my descendants and your descendants forever.’" Then he rose and departed, while Jonathan went into the city.
2 Kings 2:24
When he looked behind him and saw them, he cursed them in the name of the LORD [YHWH]. Then two female bears came out of the woods and tore up forty-two lads of their number.
2 Chronicles 33:18
Now the rest of the acts of Manasseh even his prayer to his God, and the words of the seers who spoke to him in the name of the LORD [YHWH] God of Israel, behold, they are among the records of the kings of Israel.
Psalms 124:8
Our help is in the name of the LORD [YHWH], Who made heaven and earth.
Jeremiah 26:9
"Why have you prophesied in the name of the LORD [YHWH] saying, ‘This house will be like Shiloh and this city will be desolate, without inhabitant’?" And all the people gathered about Jeremiah in the house of the LORD.
Micah 4:5
Though all the peoples walk Each in the name of his god, As for us, we will walk In the name of the LORD [YHWH] our God forever and ever.
Similar passages are Deuteronomy 18:22; 21:5; 1 Samuel 17:45; 2 Samuel 6:18; 1 Kings 18:32; 22:16; 1 Chronicles 16:2; 21:19; 2 Chronicles 18:15; Psalm 118:10-12, 26; 129:8; Isaiah 50:10; Jeremiah 11:21; 26:16, 20; 44:16; Zephaniah 3:12; Zechariah 13:3. As YHWH is most frequently used of the Supreme Being in the Old Testament, as Allah is used in the Quran, it would appear that Allah is the name of God in the Quran, like YHWH is the name of God in the Bible.

Saturday, October 19, 2013

THOUSANDS OF ARABS SHOUT JESUS **MUST WATCH**

THE BIBLE AND THE QURAN

Proof Quran copied the Jewish Talmud - Allah swears by lesser things in ...

MUNGU NDIYE MWEMA. JE, YESU NI MWEMA?

Leo nitajibu HOJA ya Waislam ya Mungu Ndiye Mwema.

Waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidni wamekuwa na tabia ya kutumia aya 18-19 iliyopo katika Luka Sura ya 18, inayo sema Mungu Ndiye Mwema. Waislam wanadai kuwa, katika aya hii, Yesu amekana kuwa yeye si "MWEMA" na kuwa Mungu Pekee ni Mwema, hivyobasi, kukana kwa Yesu kuwa yeye si Mwema kunapinga Madai ya Wakristo kuwa Yesu ni Mungu.

Kwa hivyo utaona kuwa wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia na kusema kuwa eti Yesu amekana kuwa yeye si MWEMA. Fundisho hili  la "MUNGU PEKEE NDIYE MWEMA" wanalieneza kwa kupitia Mitandao mbalimbali kama ya  Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingawa hawajabadili dini wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila Mkristo, je, ni kweli Yesu alikana kuwa yeye si MWEMA? Nakusihi fuatilia somo hili kwa makini ili kujua Ukweli wa aya hii:

Luka 18.18-19 "Tena mtu mkubwa mmoja alimuuliza Yesu, akisema, Mwalimu Mwema, nifanye nini ili kuuruthi uzima wa milele? Yesu akamwambia mbona unaniita Mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, Naye ndiye Mungu".

Ukitazama kwa haraka haraka namna wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu wanavyoifunda hii aya ya Biblia unaweza ukashawishika kuamini hicho wanachokifundisha, lakini ni vyema tukajifundisha kwa undani kadiri majibu ya Yesu kuwa "Mungu Pekee Ndiye Mwema" kisha tuone kama kuna ukweli juu ya hayo mafundisho yao, ya kusema kuwa Yesu kakataa kuwa yeye si Mwema na hivyo kunamfanya kuwa yeye si Mungu. 

Haya tuanze utafiti wetu.
Katika hii aya hapo juu, je, Yesu katoa jibu au kauliza swali? Hapa tunaona aya zinatufundisha waziwazi kuwa Yesu aliuliza swali na si kukana kuwa yeye si Mwema.

NUKUU: Yesu akamwambia Mbona waniita Mwema? Hapa Yesu kamuuliza swali, Yule mtu aliye muita “MWALIMU MWEMA” na si kukana kuwa yeye si “MWEMA" kama wanavyo fundisha Wahadhiri wa dini ya Kiislam katika Mihadhara yao ya kidini.

Baada ya Yule mtu kushindwa kujibu kwanini alimwita Yesu "Mwalimu Mwema". Yesu akasema yafuatayo:

Hakuna aliye Mwema ila mmoja, Naye ni Mungu. Je, Yesu alipo sema haya maneno alikana kuwa yeye si Mungu?

WAISLAM WANAKUBALI KUWA ALIYE MWEMA NI MUNGU TU.

Je, kuna sehemu yeyote ile katika Biblia ambayo Yesu anajiita yeye Mwema. Sasa tumsome Yesu katika Injili ya Yohana 10:14

Yesu anasema yafuatayo:

"14 Mimi ni Mchungaji MWEMA: ninawafahamu Kondoo wangu nao wananifahamu"

KATIKA YOHANA YESU ANAJIITA MWEMA.

Sasa basi, kufuatana na Waislam kukubali kwao kuwa  "MUNGU PEKEE NDIE MWEMA" na Yesu kujiita Mwema katika Injili ya Yohana 10:14. Leo hii Yesu amewajibu Wahadhiri wa dini ya Kiislamu kuwa yeye ni Mwema na hivyo hii adhama ya Mwema inamfaya kuwa yeye ni Mungu, kutokana na Luka 18: 18-19. "Mungu Pekee ni Mwema".

Ni matumaini yangu kuwa leo hii umeweza kujua kwa undani maana ya "Mungu Pekee Ndiye Mwema" na Yesu alipo sema hayo alikuwa anamfahamisha yule kijana kuwa yeye ni Mungu na yule kijana hakukosea alipo muita MWALIMU MWEMA. 

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Saturday, October 5, 2013

JE MUNGU WA WAISLAMU (ALLAH S.W) NA MUNGU WA WAKRISTO (YEHOVA) NI MMOJA?

UTANGULIZI

Imekuwa ni kawaida sasa kwa miaka zaidi ya ishirini hivi, kusikia katika mihadhara inayoendeshwa na wahadhiri wa dini ya Uislamu, ambayo imeenea sehemu mbalimbali Duniani na haswa katika nchi za Africa Mashariki na Kati,(East and Central Africa). Wahadhiri hao hufundisha jamii kupitia Qurani na Biblia kwa kusema kuwa Mungu ni Mmoja tu. Wasema Mungu kwa Kiebrania anaitwa Yehova , kwa Kiarabu Allah, kwa Kiingereza God na kwa Kiswahili ni Mungu. Kwa hivyo wasema Mungu Allah kama Qurani inavyofundisha, ndiye Yehova kama Biblia inavyofundisha. Mihadhara hiyo inayoendeshwa na Waislamu imeenea sana, mfano Nchini Tanzania kuna vikundi vingi na kimoja wapo kinaitwa Al-Marid International Propagation Center. Hawa wameandika katika bango lao kwa kunukuu katika Biblia maneno aliyoandika Mtume Paulo katika Waefeso 4:4-6. Maneno waliyoyanukuu yanasema hivi “Bwana mmoja , Imani moja ….., Mungu mmoja , naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote. Nilipotembelea mkoa wa Morogoro pale mjini, eneo la kiwanja cha ndege nikaona Msikiti mmoja umeandikwa maneno haya ya Waefeso 4:4-6. Na nilipotembelea mji wa Nairobi Nchini Kenya pia nikaona kuna vikundi vingi vinavyoendesha mihadhara na kikundi kimoja wapo kinaitwa Kibera Islamic Propagation Centre. Hawa nao katika bango lao wameandika ujumbe unaosema hivi “Acha Biblia Ijisemee na kunukuu injili aya hii” Yohana 8:32 Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Kwa hivyo utaona kuwa wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia na kusema Allah Sub-Hana Wataala ndiye YEHOVA. Fundisho hili wanalieneza kwa kupitia Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingawa hawajabadili dini wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila mkristo, je, ni kweli Mungu Allah kama inavyotuhadithia Qurani ndiye Yehova kama Biblia inavyotufundisha? Nakusihi fuatilia somo hili kwa makini ili kujua Ukweli……

SEHEMU KUU ZA SOMO HILI NI HIZI……

1. Hoja za waislamu kusema Allah ndiye Yehova.

2. Je, jina la Mungu kadiri ya Qurani na Biblia ni moja?

3. Je, Malaika mkuu wa Allah ndiye wa Yehova?

4. Je, ni nani muumba,Allah au Yehova?

5. Mji aliochagua Allah je, ni sawa na wa Yehova?

6. Allah anavyofundisha kuhusu kujitakasa nafsi je, ni sawa na Yehova?

7. Je, mbingu ya Yehova ni sawa na ya Allah?

8. Mwisho wa wanaomwabudu Allah ni wapi?



1. Hoja za waislamu kusema Allah ndiye Yehova

Wahadhiri wa Dini ya Uislamu wanasema Mungu Allah ndiye Yehova kwa sababu Manabii wa Mungu kadiri ya Biblia na Qurani walifundisha kwa kusema Mungu ni mmoja tu. Na wanasoma aya hizi…


Nabii Musa alivyosema

Kumbukumbu la Torati 6:4

Sikiza ee Israeli; BWANA Mungu wetu BWANA ndiye mmoja.

Nabii Isaya alisema hivi

Isaya 45:18,21

Maana BWANA , aliyeumba mbingu, asema hivi, yeye ni Mungu ,ndiye aliyeumba Dunia na kuifanya ….. si mimi BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi. Mungu mwenye haki , mwokozi hapana mwingine zaidi ya mimi.

Nabii Daudi Alisema

Zaburi 86:10

Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, wewe ndiwe mfanya miujiza , ndiwe Mungu peke yako.



An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance

  Title: An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance Au...

TRENDING NOW