Thursday, November 7, 2013

UTATA NDANI YA KORAN: NINI KITAKUWA CHAKULA CHA WATU JEHANNAM

Leo Allah ameamua kutueleza kuwa, watu watakuwa wanakula nini huko Jehannam. Soma aya hapa chini:

Quran 88:6. Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. 

Quran 69: 36. Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. 


Sasa angalia UTATA UNAPO INGIA: Quran 39: 62-69

62. Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? ***63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. ***64. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu. ***65. Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. ***66. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo. ***67. Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka. ***68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. ***

Ndugu zanguni, Koran ni kitabu cha ajabu sana, maana kinapingana kila sehemu.  Leo tumesoma nini watu watakula Jehannam. Hivyo, kuhusu mada hii moja peke yake, Qur'ani ina utata tatu:

"Kula matunda ya mti wa Zaqqum" (37:66) inapingana na "kula tu Dhari" (88:6).
"Kula matunda ya mti wa Zaqqum" (37:66) inapingana na "kula tu pus mchafu" (69:36).
"Kula tu Dhari" (88:6) inapingana na "kula tu pus mchafu" (69:36).

Koran imejaa UATATA na si kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Wednesday, November 6, 2013

KUTOKANA NA KORAN: YESU ANAUMBA, ANAPONYA, ANAFUFUA WATU, LAKINI MUHAMMAD HAKUWA NA UWEZO HUO

Koran leo imekiri kuwa Yesu ni zaidi ya Mtume. Ukisoma hii aya hapa chini utaona kuwa Yesu aliumba, hii sifa ya kuumba ni ya Mungu Pekee. Yesu alifufua watu, Yesu Aliponya watu. n.k. Lakini hatusomi kuwa Muhammad alifanya hayo.  Hebu soma Koran.

Quran 5: 110. Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu!

Ndugu zanguni, leo tumejifunza kuwa Yesu hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa anafanya mambo ambayo ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya hao. Ushaidi huu umewekwa kwenye Koran. Madai ya kuwa Yesu alikuwa Mtume/Nabii kama wengine, yanashindwa nguvu, baada ya kusoma hii aya ambayo imetuonyesha adhama ya Mungu ndani ya Yesu. Je, kuna Nabii au Mtume yeyote Yule aliye wai kuumba?

Hebu tusome hadith ifuatayo kutoka kwa Al Bukhar.

Ibn 'Abbas akasema, "Hiyo ilionyesha kifo cha Mtume wa Allah ambacho Allah alimtaarifu." 'Umar alisema, "Sielewi haya isipokuwa kile wewe unakielewa." 'Aisha: Mtume katika maradhi yake ambayo yalimuua, Alikuwa akisema, "O' Aisha bado nahisi maumivu yanayosababishwa na chakula nilicho kula nilipo kuwa Khaibar, na kwa wakati huu, Najisikia kama aorta   yangu inakatwa kutoka sumu niliyo kula. "(Sahih al-Bukhari, Volume 5, Kitabu 59, Namba 713)

Kwenye Hadith tuliyo soma tunaona kuwa Mtume wa Allah alikuwa anasumbuliwa na Sumu aliyo lishwa kwa Mtego na Yule Mama wa Kiyahudi. Hadithi hii inatupa ushaidi kuwa Mtume wa Allah alikuwa akiomba uponyaji kutoka kwa Allah. Swali la kujiuliza, Je, Muhammad alipo baada ya maombi haya  kwa Allah?

Endelea kupata somo:

Kwenye hadith ifuatayo hapa chini, tunasoma kuwa Jibril nayeye amekuja kumuombea uzima Mtume wa Allah, lakini maombi hayo hayakumponya Mtume wa Allah.

Kutoka kwa Ibn Sad ukurasa 265
Mtume wa Mwenyezi Mungu aliugua na yeye yaani Gabriel, alimuombea juu yake, akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu mimi nakuombea uzima na nazuia kutoka kwenu kila kitu kibaya na madhara yeyote (kuizuia kwako wewe) dhidi ya hasidi kila na kutoka kila uovu na Allah atakuponya.

Je, Baada ya haya Maombi, Mtume wa Allah alipona? Kutokana na Hadith yetu ya kwanza, Mtume wa Allah hakupona licha ya kupata Maombi kutoka Malaika Jibri. Lakini katika Koran tunasoma kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kuponya watu, kufufua watu, kuumba, jambo ambalo Jibril na Mtume wa Allah, Muhammad hawakuwa nalo.

Ndugu zanguni,

Kwanini mfuate Mtume ambaye hakuwa na uwezo wa kuponya?

Kwanini mumsikilize, Malaika ambaye hakuwa na Nguvu za kuponya, licha ya kuwa alitumwa na Allah?

Kwanini Allah amtume Jibril kwenda kumwombea Mtume Muhammad, huku akifahamu fika kuwa Muhammad hato pona?

Hayo ni maswali machache tu ambayo unaweza jiuliza. Je, Allah ni Mungu? Kama ni Mungu, kwanini alishindwa kuponya Mtume wake Muhammad (Pbuh)?

Biblia inasema yafuato kupitia Injili kutokana na Marko.

Marko 16: 17“Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina Langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, 18watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu cho chote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,
nao watapona.”
Wakristo wamepewa uwezo wa kuombea wagonjwa katika Jina la Yesu, jamba ambalo halipo kwenye Uislam. Biblia inasema kwa Jina la Yesu, tutatoa Pepo Wachafu, n.k. Haya mamlaka tumepewa na Yesu. Yesu ametupa Jina lake ambalo lipo juu ya majina yote. Ndio jina pekee linaloweza kutoa pepo, kuponya, kufufua na kufanya mengi. Yesu hakuwa Nabii au Mtu wa Kawaida. Matendo yake yanajidhihiriza kila siku kupitia wafuasi wake.

Nawasihi mumpokee Yesu ambaye alikuwa na uwezo wa kufufua watu, kuponya watu na kuumba. Haya maneno yamesemwa na Allah kwenye Koran na Biblia inakiri hayo.


Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini alimtuma Jibril kumwombea Muhammad wakati akifahamu kuwa Muhammad atakufa?

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Tuesday, November 5, 2013

UTATA NDANI YA KORAN: NANI ALIKUWA MTEREMSHAJI WA KWANZA WA QURAN KWA MTUME MUHAMMAD?

Adui wa Jibril au Roho Takatifu?

Somo letu la leo tutazungumzia utata ulio jaa ndani ya Koran. Leo hii tutajinfunza kuhusu nani alikuwa wa kwanza kuteremsha Koran kwa Mtume wa Allah. 

Katika Qura 2:97 tunasoma kuwa, Jibril ndie aliye kuwa wa kwanza kushusha aya za Quran kwa Mtume wa Allah. Soma kifungu hiki hapa:

Quran 2:97. Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Hiyo aya hapo juu ipo wazi kabisa kuwa, aliye kuwa adui wa Jibril ndie aliye kuwa mshushaji wa Quran kwa Mtume wa Allah ajulikanaye kwa jina la Muham'mad. Hebu tuendelee kusoma Quran hiyo hiyo na tuone kama ni kweli adui wa Jibril alikuwa wa kwanza kufanya hiyo kazi au kulikuwa na mtu mwingine aliye kuwa anafanya kazi hiyo hiyo ya kushusha Quran kwa Mtume wa Allah.

Rejea hapa:

Quran 16:102. Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu.

103. Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu mbayana.

Katika aya tulizo zisoma hapo juu, tunagundua kuwa Allah alimtumia Roho Takatifu kushusha Aya kwa Mtume wake na si Jibril kama wanavyo dai Waislam na tulivyo soma kwenye Surah 2 aya 97 ni Adui wa Jibril ndie aliye shusha Quran.

Katika Surah 2:97 tunasoma kuwa Mteremshaji wa Quran ni adui wa Jibril.

Katika Surah 16:102-103 tunasoma kuwa Roho Takatifi ndie anateremsha Quran.

Ndugu zanguni. Hivi kwanini Koran inamakosa namna hii? Nani alikuwa mteremshaji wa Koran? Ni Adui wa Jibril au Roho Takatifu?

Nimategemeo yangu kuwa, hili soma litawafungua macho na kufahamu ukweli kuhusu Quran. Kama kweli Allah ni Mungu na yeye ndie aliye kuwa anaishusha Quran kupita Jibril, basi asinge fanya kosa la kumsingizia Roho Takatifu kuwa na yeye alikuwa anashusha Quran au Adui wa Jibril.

Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini afanye makosa makubwa namna hii?

Je, Roho Takatifu ni adui wa Jibril?

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

UTATA NDANI YA KORAN: JE, INJIL ILIKUWEPO WAKATI WA MUSA



Ndugu zanguni, 

Leo nitazungumzia makosa na utata ndani ya Koran. Katika somo letu la leo, mtaona utata na makosa kutoka kwa Allah, alipo kuwa anamjibu Musa maombi yake. Allah anamjibu Musa na kumweleza kuwa eti Nabii asiye fahamu kusoma na kuandika yupo ndani ya Injili, huku ikifaamika kuwa Injili ilikuwa bado haikushushwa.

Aya nyingi katika Qur'ani zipo wazi kwamba Injil ilitolewa kwa Yesu ambaye alizaliwa miaka mia kadhaa [1400 BC] baada ya Musa.

Lakini cha kushangza, eti Musa aliye ishi miaka 1400 kabla ya YESU kuzaliwa na yeye anajibiwa na Allah kuhusu Injili ya Yesu kama vile yeye Musa alizaliwa baada ya Yesu. Soma majibu ya Allah kwa Musa hapa chini. 

Quran 7: 155. Na Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Na ulipo fika mtetemeko mkubwa alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ungeli taka ungeli wahiliki wao na mimi zamani! Unatuhiliki kwa waliyo yafanya wajinga katika sisi? Haya si chochote ila ni mtihani wako, umpoteze umtakaye na umhidi umtakaye. Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria. ***

156. Na utuandikie mema katika dunia hii na katika Akhera. Sisi tumerejea kwako. (Mwenyezi Mungu) akasema: Adhabu yangu nitamsibu nayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia khasa wanao mchamngu, na wanao toa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu, ***

157. Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa. ***

Koran imejaa mashaka kila sehemu. Leo tunaona Allah anamjimu Musa kuhusu Injili ambayo ilishushwa mika 1400BC. Hivi huyu Allah alipitiwa na kuanza kuzumguzia Isa Bin Maryama kwa Musa au ni kufichuka kwa siri kwamba Quran si kitabu cha Mungu? 

Kama kweli Allah ni Mungu, kwanini afanye makosa makubwa namna hii?

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Monday, November 4, 2013

UISLAM NDIO DINI PEKEE YENYE MTUME MWENYE WAZIMU


Ndugu zanguni.

Biblia inasema kuwa, mtawafahamu kwa matunda yao, hayo yalikuwa maneno kutoka Injili ya [Mathayo 7:16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya].

Mtume Muhammad alishindwa kuonyesha uadilifu katika kazi yake. Kazi aliyo dai katumwa na Mungu, ilijaa maswali mengi ambayo yaliwafanya watu wamuite yeye, Muhammad, “Mwendawazimu”. Kitendo cha Mtume kuoa Mtoto wa miaka 6, kulileta kizungumkuti, kwasabau kitendo hicho si cha kibinadamu na hakikufanywa na Mitume walio kuja kabla yake. Hapa chini ni aya kutoka Koran iliyo teremshwa na mungu wa Islam kupitia msaada wa Gibril.

Quran 15: 6. Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.

Muhammad anaitwa mwendawazimu mbele ya kadamnasi. Hayo madai ya uwendawazimu hayakukataliwa na mtume wa Allah. Alicho fanya Muhammad ni kukaa kimya, jambo ambalo ni jibu tosha kuwa alikubali kuwa yeye ni Mwendawazimu. Uhakikisho wa uwendawazimu wake upo kimaandishi.

Hebu tusome Simulizi zake kidogo: "Kitab al-Tabaqat al-Kabir", (Kitabu cha Madarasa Meja), na Ibn Sad, kutafsiriwa na S. Moinal Haq, [4], ukurasa wa 225; Muhammad akisema:

O Khadija, Ninaona Mwanga, na nasikia Masautisauti, nina hofu kuwa mimi nina Wazimu. 

Kwenye hiyo simulizi yake, hapo juu, Mtume wa Allah anakiri kuwa yeye ni mwendawazimu. Kukiri huko, kunatuletea maswali mengi, ambayo nategemea mengi ya maswali hayo, yatakosa majibu. Lakini ni vyema tujiulize maswali. Kwanini Allah aliteremsha aya inayo muita Mtume wake Mwendawazimu? Kwanini Muhammad hakukataa kuitwa Mwendawazimu? Utume wa huyu Muhammad umejaa shaka, pale alipo kubali kuwa yeye ni mwendawazimu. Rejea kwenye simulizi yake hapo juu. Nita nukuu sehemu fupi ya kukubali kwake “O Khadija, …….nina hofu kuwa mimi nina Wazimu”.

Hatujawai soma kwenye vitabu vingine vitakatifu kuwa Mitume wa Mungu wa Biblia walikubali kuwa wao ni Wendawazimu, lakini leo hii tumejifunza kuwa Muhammad mtume Allah, anakubali kuwa yeye ni Mwendawazimu.

Hivi, kwanini tufuate mtume aliye kubali kuwa yeye ni Mwendawazimu? Hilo ni swali la msingi. Allah anasema kuwa watu wa Kitabu ambao ni Wayahudi na Wakristo ndio wenye elimu na muwaulize wao, mtakapo kuwa na maswali.

Allah amesha jibu. Wakristo ndio wenye majibu katika hii duni.

MUHAM-MAD ANASEMA: "Nina hofu kuwa mimi nina Wazimu"

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Hell pictures_ A Trip To Hell (Full version) / 지옥그림_지옥을 견학하다 (Full version)

http://www.youtube.com/watch?v=dWXkBBIaiVc

http://www.youtube.com/v/dWXkBBIaiVc?version=3&autohide=1&feature=share&showinfo=1&autohide=1&attribution_tag=hY2elLNSMwttZSEiiRSDCA&autoplay=1

ALLAH ANASEMA KATIKA KORAN KUWA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM

Jamani huu ni Msiba katika taifa la Islam kwa kushindwa kusoma aya hii ambayo ipo wazi (Quran 40:60).

Katika mada hii, nitawawekea aya kutoka Koran na simulizi za Muhammad ambazo zinatushuhudia kuwa, Waislam wote wataingia Jehanamu.

Hebu tumsome kwanza Allah katika aya aliyo iteremsha kwa Mtume wake Muhammad (Pbuh).

Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.

Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni”


Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana katika dini na taifa la Kiislam. Allah amesha toa hukumu kwa wamfuatao na inafahamika fika kuwa, Wale wote waingiao Jehannam, hao walikuwa hawafanyi Mapenzi ya Mungu wa Biblia.  Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Huu ushaidi ndio tulio usoma katika Quran 40:60.


Sasa tuwasikilize na maswahiba wa Mtume Muhammad.

Simulizi:
Pia imesimuliwa na Ibn Jarir, iliyosimuliwa na Abu Kurayb, imesimuliwa na Ibn Yaman, imesimuliwa na Ibn Malik Maghul, imesimuliwa na Ibn Ishaq ambaye alisema, "Kila mara Abu Maysarah anapo kwenda kulala na akiwa kitandani kwake yeye husema, 'Mimi nasikia Uchungu kuzaliwa na Mama yangu. 'na kisha anaanza kulia kwa Machozi. Alipoulizwa kwa nini alikuwa akilia, alijibu ayafuatayo,' Tuliambiwa kwamba SISI WAISLAMU tutaingia Jehannamu, LAKINI HATUKUAMBIWA kwamba TUTATOLEWA HUKO JEHANNAMU NA HATUKUAMBIWA NI KIVIPI TUTATOKA HUKO'"

Mfuasi huyu wa Muhammad anaoneka kupatwa na mshtuko mkubwa, pale alipo ambiwa kuwa, Waislam wote wataingia Jehannam. Mshtuko huu umemfanya ailaani siku ambayo alizaliwa. Kitu cha kujiuliza, kwanini Allah ambaye ni mungu wa Waislam anatoa ahadi ya Jehannam na si Akhera kama wafundishavyo Waislam?

Ndugu zanguni, ningependa mfahamu kuwa, utakapo ingia Jehannam, kutakuwa hakuna tena njia nyingine ya kutoka huko. Pale Jehannam ndio mwisho wa maisha ya walio tenda dhanb. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Je, kufanya mapenzi ya Allah ni sawa na kutenda dhanb? Je, Uislam ni dini ya haki, kama wanavyo sema wafundishaji wa dini hiyo? Jiulize tena, kwanini Allah anatoa ahadi ya Jehannam kwa wafuatayo mafundisho yake?


Lakini Yesu anasema haya:
Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 

Ndugu zanguni, mwamini Yesu ili uwe na uzima wa milele. Yesu anakupenda. Yesu Ndie Njia Pekee. Yesu Ndie Uzima. Dini haita kupeleka kwa Baba aliye Mbingu, lakini Yesu anasema Yeye NDIE NJIA.

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries


Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Sunday, November 3, 2013

When was the Bible written and who wrote it?

The following dates are not always exact, but are very good estimates.

Old Testament

BookAuthorDate Written
GenesisMoses? - 1445 B.C.
ExodusMoses1445 - 1405 B.C.
LeviticusMoses1405 B.C.
NumbersMoses1444 - 1405 B.C.
DeuteronomyMoses1405 B.C.
JoshuaJoshua1404-1390 B.C.
JudgesSamuel1374-1129 B.C.
RuthSamuel1150? B.C.
First SamuelSamuel1043-1011 B.C.
Second SamuelEzra?1011-1004 B.C.
First KingsJeremiah?971-852 B.C.
Second KingsJeremiah?852-587 B.C.
First ChroniclesEzra?450 - 425 B.C.
Second ChroniclesEzra?450 - 425 B.C.
EzraEzra538-520 B.C.
NehemiahNehemiah445 - 425 B.C.
EstherMordecai?465 B.C.
JobJob???
PsalmsDavid1000? B.C.
Sons of Korah wrote Psalms 42, 44-49, 84-85, 87; Asaph wrote Psalms 50, 73-83; Heman wrote Psalm 88; Ethan wrote Psalm 89; Hezekiah wrote Psalms 120-123, 128-130, 132, 134-136; Solomon wrote Psalms 72, 127.
ProverbsSolomon wrote 1-29
Agur wrote 30
Lemuel wrote 31
950 - 700 B.C.
EcclesiastesSolomon935 B.C.
Song of SolomonSolomon965 B.C.
IsaiahIsaiah740 - 680 B.C.
JeremiahJeremiah627 - 585 B.C.
LamentationsJeremiah586 B.C.
EzekielEzekiel593-560 B.C.
DanielDaniel605-536 B.C.
HoseaHosea710 B.C.
JoelJoel835 B.C.
AmosAmos755 B.C.
ObadiahObadiah840 or 586 B.C.
JonahJonah760 B.C.
MicahMicah700 B.C.
NahumNahum663 - 612 B.C.
HabakkukHabakkuk607 B.C.
ZephaniahZephaniah625 B.C.
HaggaiHaggai520 B.C.
ZechariahZechariah520 - 518 B.C.
MalachiMalachi450 - 600 B.C.

New Testament

BookAuthorDate Written (A.D)
MatthewMatthew60's
MarkJohn Marklate 50's
early 60's
LukeLuke60
JohnJohnlate 80's
early 90's
ActsLuke61
RomansPaul55
1 CorinthiansPaul54
2 CorinthiansPaul55
GalatiansPaul49
EphesiansPaul60
PhilippiansPaul61
ColossiansPaul60
1 ThessaloniansPaul50 - 51
2 ThessaloniansPaul50 - 51
1 TimothyPaul62
2 TimothyPaul63
TitusPaul62
PhilemonPaul60
Hebrews(Paul, Apollos, Barnabas...?)60's
JamesJames, half brother of Jesus40's or 50's
1 PeterPeter63
2 PeterPeter63 - 64
1 JohnJohnlate 80's
early 90's
2 JohnJohnlate 80's
early 90's
3 JohnJohnlate 80's
early 90's
JudeJude, half brother of Jesus60's or 70's
RevelationJohnlate 80's
early 90's

Saturday, November 2, 2013

KORAN INAKIRI KUWA UISLAMU NI DINI YA WAARABU PEKEE

Katika hii mada ninawaletea ushaidi kuwa Uislam ni dini ya Waarabu peke yao.

Waislamu bila kuchoka wamekuwa wakidai kuwa Uislamu utatawala dunia nzima. Katika kufanya hivyo, wao watakuwa wamekwenda kinyume na maneno ya Allaha kama yarivyo teremshwa kwenye Qur'an. Kwa hiyo, ni haki kwa kusema wao ni Makafiri.

Quran 10: 47. Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.

Angalia hii aya pia

Quran 14: 4. Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 

Kama aya hizi ni kweli, basi Uislamu si kwa mashirika/mataifa/ummah yasiyo ya Waarabu. Quran inasema kwamba kila watu wamepokea ujumbe wao kutoka kwa Mungu katika lugha yao wenyewe ili waweze kuelewa na Qur'ani akaishuka  kwa Waarabu ili Waarabu waweze kulewa nini Allah anasema.

Dhana hii ya Allah kushusha Kitabu kwa kila lugha ni muhimu sana kwasababu imejirudia mara nyingi na ndio msingi wa hili somo.

Quran 16: 36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha. 

Quran 5: 48. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana. 

Quran 36: 5. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.  6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.

Hizi aya zimekamilka na kueleza kiuwazi kuhusu kuja kwake kwa Waarabu pekee. Allah katika Koran anasema kwamba kila watu wamekuwa na Mtume wao wenyewe ambao aliwaonya katika lugha zao wenyewe, na kwamba amemtuma Muhammad kwa wale ambao bado hawajaanza mwongozo wowote, na ambao baba zao hawakuonywa, yaani Waarabu. Kwa njia hii watakuwa hawana udhuru wowote na hawezi kusema, lakini hatukuwai kupokea ujumbe wowote.

Endelea kusoma Koran hapa chini:
Quran 6: 156. Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma. 

157. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.

Quran ni wazi ilitumwa kwa Waarabu. Wale ambao si Waarabu hawawezi kuielewa Koran, hayo ni maneno ya Allah. Waislamu wanasisitiza kuwa hakuna tafsiri ya Qur'ani inaweza kuwa sahihi. Hivyo, haiwezi kamwe kuwa wazi kwa mashirika yasiyo ya Waarabu na haikutumwa kwa mashirika/ummah yasiyo ya Waarabu.

Uthibitisho mwingine kuwa Qur'ani ilitumwa tu kwa ajili ya Waarabu ni katika mistari ifuatayo hapo chini:

Quran 26: 198. Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, 199. Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.

Kama ambavyo Waarabu wana haki ya kuto amini kitabu chechote kile kilichotumwa kwa lugha ambayo si yakwao, ikimaanisha Kiarabu, vivyo hivyo, mashirika yasiyo ya Waarabu nao wana haki ya kuto iamini Koran, kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Ndio kwasababu Koran inasema Allah atatuma mjumbe kwa kila lugha ili wao wenyewe kwa wenyewe waweze kuelewa.

Kuhakikisha hakuta kuwa na kutokuelewana, Allah anashusha hii aya 05:19 Quran: Enyi Watu wa Kitabu! Bila ya shaka amekujilieni Mtume wetu akikubainishieni katika wakati usio kuwa na Mitume, msije mkasema: Hakufika kwetu mbashiri wala mwonyaji. Basi amekujieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu anao uweza wa kila kitu. 

Kwa mujibu wa Qur'an watu wote wamepokea ufunuo. Aya ya hapo juu inasema Qur'ani ni kwa wale ambao kamwe hawakupokea ufunuo, iliwasije kusema, `kuwa sisi hatuja wai kutumiwa mbashiri na hakuna mjuonyaji aliye tumwa kwetu'.

Jambo hili ni wazi, lakini Allah anataka liwe wazi hata na kwa asiye na ufahamu wowote ule aelewe kuwa Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee kwa kuzitaja sehemu halisi za kijiografia ambazo Muhammad alitumwa kama Mtume wa Allah.

Quran 6:92. Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao. 

Leo, tumejifunza kuwa, Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee na si kwa Mataifa yote. Sasa, nina uhakika baadhi ya Waislamu wanaweza kuleta aya nyingine zinazosema kwamba Uislamu ni kwa wanadamu wote. Kama Waislam watafanya hivyo, basi waelekuwa kwa kufanya hivyo ni kuthibitisha kwamba aya hapo juu ni za uongo.

Ama Quran ni pakiti ya uongo na utata au ni tu kwa Waarabu wa Makkah na jirani yake kama alivyo sema Allah ambaye ni mungu wa Waislamu.

Katika huduma yake,

Max Shimba



Copyright © Max Shimba Ministries 2013


Yesu ni Mungu Kutokana na Koran (Sehemu ya Kwanza)

Waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidini kupitia wahadhiri wao wa Dini wamekuwa wakipinga kuwa Yesu Kristo si Mungu kwa madai kuwa, Mungu hawezi kuzaliwa.

Ndugu msomaji, nakusihi ufuatilie somo hili kwa makini ili ujue ukweli kuhusu Umungu wa Yesu Kristo katika Koran:

Je Yesu anazo sifa za kipekee za Mungu kutokana na Quran? Hebu tuanze utafiti wetu kwa kusoma Quran na tujionee wenyewe kama kweli Yesu ni Mungu au la.

Adhama ya Kwanza kutokana na Quran: Mungu ni Mfalme:

Koran inasema kuwa, sifa Moja ya Mungu ni “Mfalme”. Je, Yesu anayo hii sifa ya “Mfalme”? Haya tusome Quran kwanza.

Quran 59: 23
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Sasa tuangalie kama kweli Yesu anayo hii sifa ya Mfalme ambayo ni adhama ya Mungu pekee kutokana na Koran.

Biblia takatifi inasema yafuatayo kuhusu Yesu Kristo:
Ufunuo 17:14
Hawa watafanya vita na Mwana Kondoo na Mwana Kondoo atawashinda, kwamaana yeye ni Bwana wa Bwana na Mfalme wa Wafalme.

Katika aya hii tunasoma kuwa Yesu anaitwa “Mfalme wa Wafalme” ambayo ni adhama ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo shaidiwa na Koran Surah ya 59 na aya 23. Hivyo basi , Allah na Koran wamekiri kuwa Yesu ni Mungu kwasababu Biblia imetuthibitishia kuwa Yesu ni Mfalme wa Wafalme katika Ufunuo 17 na aya 14.

Tuendelee na ushaidi mwingine kutoka Koran ambao unatuhakikishia kuwa Yesu ni Mungu.

Adhama ya Pili kutokana na Quran: Mungu ni Mtakatifu:

Je, Yesu anayo hii sifa ya “Mtakatifu”? Tusome Quran kwanza:

Quran 59: 23 Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.

Katika Quran tumesoma kuwa, moja ya sifa za Mungu ni “Mtakatifu”, Je sifa hii ya utakatifu Yesu anayo?

Nenda kwenye hihiyo Kuran 19:19 Malaika akasema hakika mimi ni mjumbe ili nikupe Mwana Mtakatifu -Isa Bin Maryam.

Koran hiyo hiyo inatuhakikishia na kutujibu kuwa Yesu ambaye anajulikana kwa jina la Isa Bin Maryam katika Quran ni Mwana Mtakatifu. Hivyobasi, hii adhama ya Utakatifu ambayo ni ya Mungu pekee, tunasoma katika Quran iliyoteremshwa an Allah kuwa Yesu ameinyakua. Yesu anaitwa Mwana Mtakatifu.

Adhama ya Tatu kutokana na Quran: Bwana ni Mwenyezi Mungu

Hebu tufungue Quran na tusome kuhusu Bwana:

Quran 3:39 Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni Bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema naye ni Nabii Isa. 

Quran 39: 29
Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanao gombana, na wa mtu mwengine aliye khusika na Bwana Mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao? Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui. 

Quran 39:29 inasema kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana na hiyo ni sifa njema kwa Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hapo, Koran hiyo hiyo (Quran 3:39) inasema kuwa Isa Bin Maryam ni Neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu na ni Bwana. Koran imejibu kuwa, sifa ya Bwana ambayo ni ya Mungu pekee ni ya Yesu. Sasa tusome na Biblia kwa ushaidi zaidi kuhusu Yesu ni Bwana.  

Ufunuo 17:14
Hawa watafanya vita na Mwana Kondoo na Mwana Kondoo atawashinda, kwamaana yeye ni Bwana wa MaBwana na Mfalme wa Wafalme.

Katika Ufunuo tunasoma kuwa Mwana Kondoo ambaye ni Yesu Kristo anaitwa Bwana wa Mabwana. Hivyobasi, hii adhama ya “Bwana” ambayo ni ya Mungu pekee tunasoma katika Quran iliyoteremshwa an Allah kuwa Yesu ni Bwana na ameinyakua, vilevile, katika Biblia Takatifu tumesoma kuwa Yesu anaitwa Bwana, ambayo ni Sifa ya Mungu Pekee kutokana na Quran.

Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni Mungu kwa kuwa Yesu anazo adhama zote na/au sifa zote za Mungu.

Katika huduma yake,

Max Shimba


Copyright © Max Shimba Ministries 2013

TRENDING NOW