Je,
ungependa kuwafahamu waandishi wa Koran?
Katika
somo letu la leo, tutajifunza kuhusu waandishi wa Koran. Je, ni kweli Koran
ilishushwa? Je, kuna ushaidi wa kutosha wa kusaidia madai ya kuteremshwa kwa
Koran?
Unaposema
kuwa Allah ndie mwandishi wa Qur'ani, ni uongo mkubwa sana na wengi wameukubali huu uongo na udanganyifu
kwamba eti Koran ilishushwa wakatia inafahamika kuwa iliandikwa miaka 1400AD.
Mtu mwenye
fikra anaweza kusema bila ya wasiwasi kuwa Qur'ani iliandikwa na watu kadhaa
ambao wanajulikana kimajina. Waandishi Mashuhuri zaidi miongoni mwao ni hawa
hapa:
Imrul
Qays-mshairi: wa kale wa Arabia ambaye alifariki miaka michache kabla ya
kuzaliwa Muhammad
Zayd
b. Amr b. Naufal:-'lililopotoka' wa wakati wake ambaye alihubiri na kupandwa
Hanifism
Labid:-mshairi
mwingine
Hasan
b. Thabit:-mshairi rasmi wa Muhammad
Salman:
– Mshauri wa Kiajemi wa Muhammad
Bahira:-Nestoraian
Mkristo mtawa wa Kanisa huko Syria
Jabr:-Jirani
wa Kikristo wa Muhammad
Ibn
Qumta:-Mtumwa wa Kikristo
Khadija:-Mke
wa kwanza wa Muhammad
Binamu
Waraqa:- Ndugu ya Khadija
Ubay
b. Katibu Ka'ab;-Muhammad na Mwandishi wake
Muhammad:
– Mwenyewe
Hapa
chini, nitaandika historia fupi ya baadhi ya waandishi wa Koran. Nitaanza na
Bahira ambaye alikuwa ni Mtawa wa Kikrito.
Bahira
Bahira alikuwa Mtawa wa Kikristo wa Nestorian aliyeishi katika Sham (Syria).
Jina lake la Kikristo lilikuwa Sergio Georgius. Inaaminika kwamba alifukuzwa
kutoka utawa baada ya makosa.
Katika
mji wa Makkah, alikutana na Muhammad, akawa karibu sana na yeye na kukaa pamoja
naye. Yeye alikuwa na mazungumzo ya siri na Muhammad, ambayo yeye hakika alimwambia
Muhammad mambo mengi ya Ukristo. Aya kadhaa
katika Qur'an zinazozungumzia Ukristo zilitoka kwa huyu Mtawa Bahira.
Mfano,
aya zote za ndani ya Kuran zinazozungumzia kitabu cha Zaburi zilihaririwa na
huyu Mtawa Bahira:
4.163
Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na
Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na
Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na
Suleiman, na Daud tukampa Zaburi.
17: 55. Na
Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika
tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi.
21:105. Na
hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi
watairithi waja wangu walio wema.
2:113. Na
Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. Na Wakristo husema: Mayahudi hawana
lao jambo. Na ilhali wote wanasoma Kitabu hicho hicho (Biblia). Na kadhaalika
walisema wale wasio jua kitu mfano wa kauli yao hii. Basi Mwenyezi Mungu
atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitilafiana.