FUNDISHO LA UTATU MTAKATIFU:
JE NI UPAGANI KAMA WAISLAMU NA MASHAHIDI WA JEHOVA WANAVYODAI?
IS TRINITY PAGANISM?
Utangulizi : Siku zote Mkristo Mwana wa Mungu ,anapomuelezea Mungu katika ukuu na uwezo wake,kwa wale wasioamini hususani Waislam na Mashahidi wa Jehova (Jehova’s Witness), na akamtaja Mungu huyo kuwa ni Mungu katika Utatu Mktakatifu, huzuka malumbano au mabishano kuhusu jambo hilo. Mashahidi wa Yehova husema wale wanaomini katika Utatu Mtakatifu wamefuata imani za kipagani kwa sababu katika Biblia nzima hakuna mahali popote palipoandikwa Utatu Mtakatifu upinzani huo huandikwa mara kwa mara katika vijarida mbali mbali .
Hoja kuu kuwahusu ni kuwa siku zote hawapendi kukupa nafasi uwaelekeze kwa nini unasema hivyo , bali wakati wote hukutaka uoneshe neno “Utatu Mtakatifu “ ndani ya Biblia. Na kwa hakika hupati neno hilo “ Utatu Mtakatifu” ndani ya Biblia .
Swali la ufahamu : Je kukosekana neno UTATU MTAKATIFU ndani ya Biblia kama wanavyodai mashahidi wa Yehova kuna mfanya Mungu asiwe wa Utatu ? Jibu la swali hili ni rahisi sana SI KWELI. Hii ni kwa sababu, kuna maneno ambayo hayapo ndani ya Bblia yakimhusu Mungu, lakini yatumikapo huleta maana nzuri na yenye uhakika kuhusu yeye Mungu .Maneno hayo yanapotamkwa kwa lugha ya kigeni ni Omnipotence yaani Mungu ni mwenye nguvu zisizo shindikana na chochote , Omnipresence yaani Mungu yupo mahali pote kwa wakati wote na Omniscience yaani Mungu anajua yote maneno haya yaani Omnipotence , Omnipresence na Omniscience hayajaandikwa katika Biblia ya lugha ya Kiingereza, lakini yatamkwapo hueleza jambo la maana na lenye umuhimu kumhusu Mungu. Ndivyo ilivyopia kwa neno “Utatu Mtakatifu” yaani Trinity”
Waislam wao hupinga utatu mtakatifu kwa kujaribu kusoma baadhi ya aya zilizomo ndani ya Quran, kitabu kinachoongoza imani yao hasa pale wanaposema katika Suratul Al- Maidah,(meza), 5:73 “Kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo”.
Unaposoma ufafanuzi wa aya hiyo ya 73 iliyomo ndani ya Qurani hiyo hiyo unasema “unatajwa ukafiri wa kinasara (Ukristo) kwa itikadi zao zote tatu kuwa Nabii Issa (a) Mungu au (b) Mtoto wa Mungu au (c) Mmoja katika waungu hao watatu “yeyote katika itikadi hizi ni ukafiri usiokuwa na shaka na jaza yake ni moto tu”
Pengine jambo linalowasumbua waislam ni ukosefu wa ufahamu kuwa siku zote wanapomfikiria Issa kuwa ndiye Yesu wanapotoka sana .Hii ni kwa sababu Issa siye Yesu na tunatambua hayo hasa tunaposoma vitabu vya kiislam vilivyoandikwa na wanazuoni (wasomi ) wakubwa wa kiislam. Kwa mfano katika Qurani ya Tafsiri ya Imam Baidhwaw, juzuu 1 uk 160 ,anasema Issa maana yake ni wekundu unaozidiana na weupe, na wengine husema Issa maana yake ni dume la ngamia .Hoja hizi zinaungwa mkono na hadithi mbalimbali za kiislamu, zinazomzungumzia Issa, hasa ile inayopatikana katika Sahihi Bukhari Juzuu 4 Hadithi 653, na katika Al-lulu wal- Marjan,kitabu cha 3 Hadithi na 1528 uk.883 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema “Issa Ibn Mariam (a,s) alimwona mtu anaiba akamuuliza !umeiba? akasema hapana ,Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye .Issa (a.s) akasema nimemuamini Allah na limeniongopea jicho langu”.
Huyu Issa hawezi kuwa ndiye Yesu kwa sababu Yesu anayajua yote hahitaji kuelezwa na mtu .Katika Injili ya Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona”
Huyu Issa hawezi kuwa ndiye Yesu kwa sababu Yesu anayajua yote hahitaji kuelezwa na mtu .Katika Injili ya Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona”
Hivyo maelezo yaliyomo katika Quran pamoja na vitabu vya hadithi za kiislam yana thibitisha kuwa Issa siyo Yesu kwa sababu jina Yesu ni sawa na jina la kiebrania Yehshua ambalo maana yake Mwokozi Math 1: 21, Lk 2: 10- 11. Pia Yesu aliyajua yote hata yaliyomo katika mioyo ya watu hata bila ya wao kusema Marko 2: 8 , Yoh 1: 48-50 tofauti na Issa ambaye hajui jambo lolote na kwa mujibu wa Quran na hadithi zake Issa atahukumiwa kwenda Jehanamu ya moto (Suratul Anbiyaa, (manabii) 21:98, na 5:116-117). Kwa msaada zaidi wa kujua tofauti ya Issa na Yesu agiza kwetu somo hili tunalo.
Hoja wanazotumia mashahidi wa Yehova kupinga fundisho la utatu.
Math 4: 1 “ Yesu alijaribiwa na Ibilisi”
Yakobo 1: 13 “ Mungu hajaribiwi “
Yoh 8: 40 “ Yesu alisema mimi mtu”
Yoh 17: 3 “ Yesu alisema wakujue wewe mungu wa pekee.
I Tim 2: 5 “ Yesu ni mwanadamu tu ( siyo Mungu)
Math 4: 1 “ Yesu alijaribiwa na Ibilisi”
Yakobo 1: 13 “ Mungu hajaribiwi “
Yoh 8: 40 “ Yesu alisema mimi mtu”
Yoh 17: 3 “ Yesu alisema wakujue wewe mungu wa pekee.
I Tim 2: 5 “ Yesu ni mwanadamu tu ( siyo Mungu)




