Wednesday, July 8, 2015

YESU KRISTO NI MUNGU: THIBITISHO SABA

UFUNUO WA YOHANA 1:1-7
Kitabu hiki kinaelezea jinsi itakavyokua baadaye kwa watendao maovu pamoja na wasiowaminifu, na pia watakatifu pamoja na waminifu. Lakini uzuri wa haya yote, ni jinsi kinavyotuelezea. Yesu ni nani hasa. Na kwa thibitisho sahihi na pasipo shaka kimeelezea kuwa Yesu ni Mungu.
Ni hoja ya uzima na mauti kumjua Yesu ni nani - Yohana 8:24,26 Yesu alisema, "Kwa hivyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu, kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu"
Mathayo 22:36-38, Mariko 12:26-29 ...Yesu aliulizwa katika amri zote ni ipi ilio ya kwanza, na kwa upezi akakalili kumbukumbu la torati 6:4 "sikia ee israeli Bwana Mungu wetu bwana ni mmoja..." Yesu akiwa Mungu alijua hakuna kabisa Mungu mwingine ila yeye mwenyewe. Kijitabu hiki kimeandikwa ili kiweze kuthibitisha umoja wa Mungu.

THIBITISHO SABA ZINAZO AMINIKA
Kitabu hiki cha ufunuo wa Yohana kimetupatia thibitisho saba ambazo haziwezi kukataliwa ya kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Mungu.
Yohana aliamini jambo hili kabla ya kuandika kitabu hiki cha Ufunuo. Yohana wa kwanza 5:20 "...nasi twajua kwamba mwana wa Mungu amekwisha kuja naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake, yeye aliye wa kweli yaani ndani ya mwanawe Yesu Kristo huyu ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele."

1. THIBITISHO LA KWANZA
Ufunuo wa Yohana 1:8 Yesu akasema, "Mimi ni Alpha na Omega, mwanzo na mwisho, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja Mwenyezi."
Ufunuo wa Yohana 1:17-18 "...mimi ni wa kwanza, na wa mwisho, na aliye hai nami nilikuwa nimekufa; ...na tazama, ni hai hata milele na milele."
Yesu alisema yeye ndiye wa kwanza na wa mwisho, hakika hili lamthibitisha yeye ni Mungu, kwa maana Mungu wa Israeli alisema katika kitabu cha Nabii Isaia 44:6 "...Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu."
Je ni thibitisho lingine lipi tunahitaji litufahamishe Yesu ni Mungu?
Kuelewa jambo hili vizuri utapaswa uelewe hali mbili za asili ya Mungu (dual nature). Mungu ambaye ni Roho alichukua mwili wa nyama kwa muda wa miaka thelathini na nusu "Emmanuel" .
Yohana 1:1 "Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu."
Yohana 1:14 "...Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu ---“ (Mungu) alifanya jambo hili aweze kutoa uhai wake na kumwaga damu kwa ondoleo la dhambi zetu.

2.THIBITISHO LA PILI
YOHANA 4:2 "...Na mara nalikuwa katika roho, na tazama kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na Mmoja ameketi juu ya kile kiti."
UFUNUO 4:6-8-- "Na kwa kile kiti kulikuwa na makundi yaliokuwa yakimwabudu aliyekalia kiti hicho."
Mstari wa 8, unatuelezea vizuri ni nani aliyekuwa amekikalia kiti hicho. "Wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu Bwana Mungu mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
UFUNUO 1:8 Yesu akasema ya kwamba yeye ndiye aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja, Mungu mwenyenzi. Kuna Mungu Mwenyenzi mmoja tu.
UFUNUO 4:11 "Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote,--"
YOHANA 1:3 na (10)...yazungumza juu ya Yesu ya kwamba vitu vyote viliumbwa naye, na ulimwengu haukumwelewa.
WAKOLOSAI 1:16-17 Mtume Paulo alisema,"kwa kuwa katika vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake," Na kwa thibitisho zaidi ya kuwa Yesu Kristo ndiye Bwana Mungu Mwenyezi, tunasoma kwenye kitabu cha Isaya 44:24...Mungu mwenyenzi kwa agano la kale akisema..."Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote, nizitandaye mbingu peke yangu; nienezaye nchi; ni nani aliyekuwa pamoja nami;
UFUNUO 5:9....Nao waimba wimbo mpya kwa Mwana kondoo wakisema, "Wewe ....ulitukomboa ukamnunulia Mungu kwa damu yako..." Damu ya nani?
MATENDO YA MITUME 20:28...Kanisa la Mungu lilinunuliwa kwa damu yake (Mungu) mwenyewe.
YOHANA WA KWANZA 3:16--"Katika hili tumelifahamu pendo la Mungu, kwa kuwa Yeye (Mungu) aliutoa uhai wake kwa ajili yetu."

3. THIBITISHO LA TATUUFUNUO 11:16-17
Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu .... wakaanguka kifudifudi wakamsujudia Mungu, wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu
(Mstari wa 17)... Mwenyezi uliyeko na uliyekuweko na utakayekuja. (Read English King James version).
(Mstari wa 15)...Kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki. Huu mstari unaelezea kuwa Yesu atamiliki milele na milele! Na kuthibitisha zaidi. Soma Ufunuo 1:8...Yesu akasema mimi ndimi (mmoja) aliyeko, aliyekuweko na atakayekuja, Mwenyezi.

Monday, July 6, 2015

YESU NI MWANA WA MUNGU


Je, ina maana gani Yesu kuwa Mwana wa Mungu 

Ndugu Msomaji,
Yesu si Mwana wa Mungu kulingana na ubaba wa kawaida wa binadamu. Mungu hakuoa na kupata mwana wa kiume. Mungu hakufanya tendo la ndoa na Mariamu, na pamoja naye kuzaa mtoto wa kiume. Yesu ni Mungu katika hali kwamba ni Mungu anajithirihisha kama mwili. (Yohana 1:1, 14) Yesu ni mwana wa Mungu kwa dhana kwamba Mariamu alipata mimba kupitia Roho Mtakatifu. Luka 1:35 yasema, “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.”

YESU NI MUNGU KATIKA MWILIYohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!

YESU AKUBALI KUITWA MUNGU NA WANAFUNZI WAKETomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”

MALAIKA WANAMWABUDU YESUKatika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

ROHO MTAKATIFU NI MUNGU

Ndugu msomaji,

Watu wengi hawafahamu kuhusu Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu Ni Nani?

Baadhi ya watu wanadhani Roho Mtakatifu ni aina fulani ya nishati, uweza au radi. Lakini wanakosea.

Roho Mtakatifu Ni Mtu, nikimmanisha kuwa sio Mtu kwa maantiki ya Binadamu. 

Na kwa kweli ni ‘mtu’ muhimu sana; ni Nafsi ya Tatu katika Utatu wa Mungu (Mt 28:19) (2Kor 13:13). Yeye ni mtu roho, kama vile wewe ulivyo ila Yeye hafungwi na mwili. Twaweza kumwomba kila siku tukisema, ‘Roho Mtakatifu,  nijaze kwa uweza wako, niongoze, nipe hekima na ujasiri’ kwa sababu ni mtu kweli tunayeweza kuzungumza naye na kujihusisha naye.

Wengine wanasema kuwa ni Nguvu Fulani ya Mungu. Wengine wanasema ni Malaika Jibril. Lakini, Biblia inatumabia nini kuhusu Roho Mtakatifu?

Hebu ungana nami moja kwa moja na tujifunze kwa pamoja kwa kutumia aya za Biblia kuhusu Roho Mtakatifu. Kwa kifupi, ROHO MTAKATIFU ni Mungu. 

Swala la kuwa Roho mtakatifu ni Mungu limo ndani ya aya nyingi za biblia kama vile Matendo 5:3-4. Katika ayah ii Petro anapambana na anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na nasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali Mungu.” Hili ni tangazo la wazi kwamba kumdanganya Roho mtakatifu ni kumdanganya Mungu. Tunaweza pia kujua Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana tajwa na hali sawa na za Mungu. Roho mtakatifu yuko kila mahali katika Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” tena katika wakorintho wa Kwanza 2:10 tunaona hali yakuwepo kila mahali kwa Roho mtakatifu “Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”

Tunaweza kujua kweli kwamba Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana akili, hisia na mapenzi yake. Roho mtakatifu hufikiri na hujua (Wakorintho wa kwanza 2:10). Roho mtakatifu anaweza kuugua (Waefeso 4:30). Roho hutuombea (Warumi 8:26-27). Roho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11). Roho mtakatifu ni Mungu, sehemu ya tatu ya utatu wa Mungu. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26).

Je, Roho Mtakatifu Ni Nafsi Halisi?

Madaktari husema kwamba nafsi halisi ni sharti iwe na akili, hiari, na hisia. Na Roho Mtakatifu tunampima kwa vigezo hivyohivyo vitatu.

Je, Roho Mtakatifu Ana Akili?
Akili ni uwezo wa kujifunza, kuelewa na kufikiri. Ndiyo, ana akili sana! (Rum 8:27) (1Kor 2:10-13).

Je, Roho Mtakatifu Ana Hiari?
Hiari inahusiana na kusudio, uchaguzi, takwa na azimio. Ndiyo, Roho Mtakatifu ana hiari yake mwenyewe na anakubaliana na Baba na Mwana (1Kor 12:11).

Je, Roho Mtakatifu Ana Hisia?
Je, ana hisia na hisia kali? Anapenda na hiyo ndiyo hisia yenye nguvu sana aliyonayo, na kuna hisia kali katika kuugua kwake awapo kwenye maombezi (Rum 15:30; 8:26,27).

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba Ministries Org.

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Friday, July 3, 2015

MTUME MUHAMMAD ALITUMIA NDUMBA

Max Shimba Ministries's photo.
1. Mtume Muhammad alitumia Ndumba
2. Mtume Muhammad adai eti Nywele zake zinatibu jicho ovu.
3. Wapi katika Biblia tunasoma kuwa Manabii na Mitume wa Biblia walitumia Ndumba?

Ndugu Msomaji,
Leo ningependa tusome kuhusu Muhammad na Utumiaji wa NDUMBA katika Uislam,

MTUME MUHAMMAD ANATUMIA NDUMBAMuhammad alitumia ndumba [nguvu za kimazingaombwe] dhidi ya jicho ovu na wanyama jamii ya mjusi wenye sumu Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3525 uk.48.
Hivi wapi tunasoma katika Taurat au Zaburi au Injir kuwa Mitume na Manabii wa kwenye Biblia walitumia NDUMBA?

Hivi Allah hana uwezo wa kutibu jicho ovu au Sumu mpaka atumie NDUMBA?

MUHAMMAD SASA AMPA MKE WAKE AISHA NDUMBAMuhammad alimpa ‘Aisha ndumba ili kutibu jicho ovu. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na. 5445,5447-5450 uk.1196.

Hivi Ndumba ina tofauti gani na UCHAWI? Sasa hapo juu tumesoma kuwa Muhammad ametoa NDUMBA kwa mke wake kipenzi.

Wapi tunasoma kuwa Manabii wa Biblia walitumia NDUMBA?
Muhammad aliamini katika jicho ovu, na kulikuwa na hirizi dhidi yake al-Tabari juzuu ya 39 uk.134.
Sura mbili za mwisho (113 and 114) ziliandika juu ya ubaya wa jicho ovu kufuatana na Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3517 uk.41.

Hata hivyo, sura za 113 na 114 hazimo katika toleo la Ibin Mas’ud katika Korani (The Fihrist uk.57). Kuondolewa huko hakukuwa kwa bahati mbaya. Ilitaarifiwa kuwa Ibn Mas’ud alisema, "Hirizi mbili-Sura za [113, 114] si Kitabu cha Mungu."

Ibn Mas’ud alikuwa katibu muhtasi wa Muhammad. Muhammad aliwaambia watu wengine wajifunze kutoka kwa Ibn Mas’ud na wengine watatu. (Bukhari juzuu ys 6 kitabu cha 60 sehemu ya 8 na.521 uk.486-487).

MUHAMMAD ASEMA NDUMBA NANGAE HUTIBU JICHO OVUNdumba hutibu jicho ovu. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3510, 3511 uk.41; juzuu ya 5 na.3512 uk.42.

ALBADIRI NI NDUMBA 

Wednesday, July 1, 2015

Zul-Qarnain na Kutua kwa Jua katika Sura 18:85-86

Je, ni kweli kuwa jua linazama katika chemichemi za maji zenye tope au giza, au Koran ina makosa, au kuna maelezo mengine? Kwanza tutaangalia maana ya wazi Sura ya 18:85-86, na kisha tutaangalia maelezo na majibu ya baadhi ya Waislam kuhusu jambo hili.
Unajimu Kidogo
Inawezekana kuwa haijulikani kwa mapana kwamba watawala wa kislam wa Abbasid, Waarabu na Waajemi waliendelea sana katika unajimu, wakizipa majina nyota nyingi, hata walinukuru na kusahihisha baadhi ya orodha za hesabu za watawala wa Misri (Ptolemy’s tables). Hata hivyo jua ni kubwa mara nyingi zaidi ya dunia nzima, na dunia husafiri ikilizunguka jua. Jua halizami katika chemichemi za maji zenye tope.
Zul-Qarnain ni Nani?
Hatuna ushahidi kama Muhammad alimwambia mtu yeyote kuwa Zul-Qarnain alikuwa nani hasa. Waislam wana mitazamo minne tofauti.
  
Alexander Mkuu
 (wa Makedoni) ni mtazamo wa Waislam wengi zaidi. Zul-Qarnain humaanisha kuwa ni "mtu mwenye pembe mbili." Kuna hadithi ya kubuniwa isemayo kuwa Alexander Mkuu alikuwa mungu na alikuwa na pembe mbili za kondoo dume zilizokuwa zinakua pembeni mwa kichwa chake. Licha ya ukweli kwamba hii haikuwa kweli (na ni tatizo kupata kofia ya vita—helimeti inayoweza kutosha), hadithi hii ilijulikana, na waislam wengi hudhani kuwa Allah katika sura ya 18 Alexander alitajwa kwa jina hili, mungu.
  
Koreshi I Muajemi 
ni mtizamo mwingine. Ufalme wake hasa ulikuwa ufalme uliohusisha makundi mawili: Wamedi na Waajemi, lakini zaidi ya hayo hakuna uthibitisho kuwa pembe mbili zinamhusu yeye.
  
Mfalme wa Yemeni
 ambaye alivaa kofia ya vita yenye pembe mbili za kondoo dume, ni mtazamo walionao baadhi ya Waislam.
  
Mtu asiyejulikana 
ni mtizamo wa nne. Hata hivyo inaonekana si vema sana kutoa maelezo juu ya watu ambao msemaji hajawahi kuyasikia.
  
Hitimisho:
 Haijalishi kuwa Zul-Qarnain alikuwa nani hasa. Kama aligundua kuwa jua hutua kwenye chemichemi za maji zenye tope, na huwa halizami kwenye chemichemi za maji zenye tope, kwa hiyo huu ni ubatili, bila kujali mtu ambaye Muhammad alimzungumzia.
Sura 18 Mawazo na Majibu

Je Uislam Umejiboresha na kuwa Mzuri Kuliko Ukristo?


Je Muhammad anatimiza na kukamilisha lengo na huduma ya Kristo? Muhammad anajibu ‘ndiyo’ kwa msistizo.

Thiolojia ya msingi ya kiislam inafundisha kwamba kwa vile Allah alimtuma Gabriel akiwa na Kurani kwa Muhammad Mjumbe wa Allah, Muhammad na Kurani vinatimiza na kukamilisha lengo na huduma ya Kristo na Agano Jipya. Muhammad anaelekea kutambua umuhimu wa Biblia (Sura 4:47; 4:136; 4:163; 5:44-48; 5:82-83; 6:92, 154), lakini, ukristo na Agano Jipya vinatakiwa kujinyenyekeza kwa uislam na Kurani, ufunuo mpya na ulio bora zaidi.

Sura 5:15-16 inaeleza mtazamo wa Muhammad kwa kutumia mfano. Kwa muktadha wa upotofu wa Muhammad wa mafundisho ya kikristo ya Yesu kuwa Mwana (v. 17), na katika muktadha wa madai yake kuwa Wayahudi wamelaaniwa (v. 13), kifungu hiki kwenye Kurani (kikiwa kinaviwakilisha vingine) kinasema kwamba Wakristo (na Wayahudi) wamekuwa wakitembea gizani hadi wakati Muhammad alipokuja:

5:15 Watu wa Kitabu [Wayahudi na Wakristo] . . . mwanga umekuja kwenu sasa kutoka kwa Mungu, na Maandiko [Kurani] ikifafanua mambo, 16 ambayo kwayo Mungu huwaongoza wale wafuatao mambo yanayompendeza kwenye njia za amani, akiwatoa kutoka gizani na kuwaleta kwenye mwanga, kwa matakwa yake, na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka. (Haleem) (linganiasha na 4:157).

Mkristo wa leo mwenye ufahamu wa Biblia atatambua mara moja tamathali ya mwanga. Yesu anasema kuwa alitumwa toka mbinguni kama nuru ya ulimwengu, na Wakristo wamevuka kutoka giza kwenda nuruni (John 1:4-5, 8:12, 9:5, 12:46; 1 Petro 2:9). Lakini, sasa, Muhammad anadai kuwa Wakristo wamekuwa wakiishi kwenye giza, na amekuja kufafanua mambo kwao, kana kwamba mambo yalikuwa yamevurugwa. Kurani inatoa maongozi kwenye "njia iliyonyooka", mada ambayo imerudiwa mara kadhaa kwenye Maandiko ya kiislam (k.m. Sura 1) na "inafafanua mambo." Mstari wa 16 ni moja ya mistari ambayo Muislam anaweza kuufikiria wakati anapoonyesha kuwa uislam ni dini ya amani. Lakini je ni kweli?

Mkristo aliyejitoa, na mwenye ufahamu wa Biblia hawezi akaamini kwa vyovyote vile kuwa Uislam ni bora, tunawezaje kuuunja mvutano huu uliokwama? Je tuupuuzie? Kwa kuzingatia matokea ya karibuni kama mashambulizi ya kigaidi ya Marekani (Septemba 11, 9/11), jambo hili haliwezekani tena. Je tunajifanya kuamini kuwa dini zote ni sawa? Lakini jambo hili linatulazimisha kuyakana baadhi ya mafundisho ya msingi yasiyoweza kujadiliwa ambayo dini zote zinakuwa nazo na yale ambayo hayawezi kupatanishwa. Kwa jinsi hiyo basi, je tunabishania mafundhisho haya ya kuwazika tu?

Kujadili mambo ya kuwazika kama vile Umoja wa Utatu wa Mungu, kuna sehemu yake katika mazungumzo ya Waislam na Wakristo, lakini hakuna upande unaoweza kudai kuwa unaweza kuthibitishwa kwa uelekevu rahisi wa kutambua (simple observation). Kurani kila sehemu inatamka kwa dhati Umoja wa Mungu, wakati Agano Jipya linatamka kwa udhati kuwa Yesu ni Mungu na Roho Mtakatifu ni nafsi. Kwa hiyo tumepambanisha kifungu kitakatifu kimoja dhidi ya kingine, na ili kuuvunja mvutano huu usiokwisha ni lazima tutumie njia zingine. (Kwa habari zaidi za kuaminika kwa Agano Jipya, tembelea tovuti hii, site; kwa matatizo asilia ya Kurani, nenda hapa here.)

Kwa kuwa Muhammad anampinga Kristo na ukristo kuwa ni kweli, sisi Wakristo tunapaswa kumjibu. Je Yesu angesemaje? Kama ilivyotokea kuwa, Yesu ametupa mafundisho wazi kabisa ya namna ya kumtathmini nabii anayekuja baada yake katika historia, hasa kama huyo nabii anadai kuwa mkubwa kuliko Yesu: tathmini matunda yake.

Kwenye muktadha wa Hotuba ya Mlimani, Kristo aliongea kwa makutano, ama hakuna mtu kati yao aliyekuwa mwana thiolojia ama ni wachache tu, bali walikuwa wakulima wa hali ya chini. Kwenye Mathayo 7:15-20, Kristo anatumia lugha isiyokuwa na utata kuhusu namna ya kuutambua ukweli wa manabii:

Uislam na Fani ya Tiba

Uislam na Fani ya Tiba
Mchango katika Historia
 

Toleo la Juni 2006
Kwa kiasi kikubwa, fani ya tiba ya kisasa imetokana na fani ya tiba ya kimagharibi (Ulaya), ambayo ina asili ya fani ya tiba ya Ugiriki na Urumi kale. Ingawa jambo hili ni sahihi, limerahisishwa kupita kiasi; watu wengi zaidi, Waislam kwa wasio Waislam, hawafahamu kuwa fani ya tiba ya kimagharibi isingekuwa hapa ilipo sasa bila ya mchango mkubwa na muhimu sana wa fani ya tiba ya Kiislam. Yafuatayo ni maelezo kwa muhtasari ya baadhi ya michango, yakifuatiwa na mafundisho ya Koran na Hadithi kuhusu fani ya tiba.
Mwanzo wa Fani ya Tiba katika Uislam
Ingawa Waarabu kabla ya Muhammad walikuwa na ufahamu wa fani ya tiba ya kale, Wamisri, Wabizanti (Byzantines) na Waajemi walikuwa wameendelea sana. Walifanya upasuaji, walikuwa na dawa nyingi zilizotokana na mitishamba na mimea mingine, waliunganisha mifupa, walifahamu kuondoa maji machafu na takataka, na waliwatenga wenye ukoma. Hata hivyo, palikuwa na ushirikina mwingi na dawa mbaya za tiba pia.
 
Waislam wanakubaliana kwa ujumla kuwa Waabbasidi (Abbasids) hawakuwa waangalifu sana katika imani yao kama Waislam (mtawala mmoja alizama kwenye dimbwi la mvinyo), lakini kupitia kwao kuvumiliana, sayansi na fani ya tiba vilishamiri.
 
Madaktari wa kwanza kwenye ulimwengu wa Kiislam kwa kiasi kikubwa walikuwa ni Wakristo wa Kinestoria kama hawa wafuatao. Jurji bin Bakhtishu’ kutoka Iran ya magharibi (aliyekufa mwaka 830 B.K., 215 A.H.) na wanawe walikuwa madaktari chini ya khalifa al Mansur. Yuhanna ibn Masawayh (aliyekufa mwaka 243, 857) Mnestori Hunayn ibn Ishaq (miaka kama 800- 873 B.K. (260 A.H.)) aliteuliwa na al Ma’mun kuwa kiongozi wa Dar al Hikmah (Nyumba ya Hekima), na ndiye aliyetafsiri kazi nyingi za tiba ya fani na za sayansi kuwa Kiarabu. (Tazama http://www.masnet.org/history.asp?id=1033) na http://www.nlm.nih.gov/hmd/arabic/bioI.html
Kwa habari zaidi).

Hata hivyo, kufikia mwaka 931 B.K., madaktari 869 walikuwa katika mtihani wa hati ya Khalifa al Muqtadir mwaka 931 B.K.

Waganga na Wafamasia Muhimu Zaidi wa Kiislam

Uislam na Sayansi: Mitazamo Iliyosahauliwa Imekumbukwa

Uislam na Sayansi:
Mitazamo Iliyosahauliwa Imekumbukwa 

Toleo la Juni 2006
Je, maneno kama aljebra, alkali, pombe, astrolabe, naphtha, na zircon kitu gani kinachoyapatanisha hasa? Maneno haya yote ni ya Kiingereza yaliyotoholewa kutoka katika Kiarabu na maneno ya Kiajemi yanayoturudisha nyuma kwenye miaka ya 700-1150 BK, wakati kituo cha kujifunza Sayansi bila shaka kilikuwa Mashariki ya Kati.

Watu wengi yawezekana wasijue mchango muhimu uliotolewa kwa sayansi na hesabu kutoka Mashariki ya Kati. Ifuatayo ni orodha fupi ya mafanikio ya mambo haya, na kisha hutafiti kauli za kisayansi zilizomo katika Korani. Lakini kuna maendeleo mengi makubwa ya kitabibu ambayo hayajatajwa hapa; huleta sifa kwa mjadala wake wenyewe.
 
Sayansi ya Mashariki ya Kati ya Zamani
Hata Wasumeria wa kwanza (3500-2000 KK) walikuwa na mchanganuo wa wanyama wote waliowajua. (Wadudu wakubwa kama vile nzige walijumuishwa pamoja na ndege, kama viumbe warukao.) Wamisri wa zamani na Wababeli walitumia nyota ili kuwasaidia kujua ni wakati gani wangeanza kupanda. Watu hao wa zamani walikuwa na maendeleo kadhaa katika kutengeneza meli, ufugaji wa wanyama, na upasuaji, hata upasuaji wa kichwa. Wamisri walitumia dawa ya meno tangu mwaka 2500 KK. Mitatu kati ya michango muhimu sana ya kisayansi ni kuandika, kulima pamoja na sayansi na teknolojia ya vitu yabisi kama vyuma.
 
Pengine mafanikio ya juu zaidi kielimu ya ulimwengu wa zamani yalikuwa maktaba ya mji wa Alexandria. Hapa kulitunzwa mamia ya maelfu ya juzuu za nakala asilia au nakala za fasihi nyingi za ulimwengu wa watu wa wakati ule.
Uhandisi na Uhandisi Majengo wa Zama za Kale
Wamisri walikuwa na gubeti tangu 2500 KK. Katika uhandisi majengo, kila mtu anajua mapiramidi ya kuvutia nchini Misri na mahekalu (Ziggurats) ya Sumeria na Babeli.
 
Kitu kisichojulikana sana ni kuwa Kaskazini-mashariki mwa Iran kulikuwa na bwawa kubwa, lililoibuka hasa katika mwaka 1800 KK, kushinikiza wahamiaji wengi katika nchi za India na Iran. Bwawa nchini Yemen liliufanya ufalme wa Sheba kuwa kituo maalum cha kilimo na biashara hadi hapo lilipovunjwa pia zaidi ya karne moja kabla ya Muhammad. Ujenzi wa mifereji, bustani zinazoning’inia, na miji yenye kuta nene ni mambo ya kuvutia hata leo. Na kwa hakika, kama ungeliweka Mji wa Ashuru, Ninawi kati ya Ufaransa na Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, pasingekuwa na upande wowote ambao ungeweza kuuteka. Hatimaye ulitekwa, lakini ni kwa sababu tu mto wa Khosr ulipofurika na mafuriko yake yalivunja sehemu ya ukuta wa mji huo..
Mashariki ya Kati ya Kale na Hesabu
Haya majengo ya kiuhandisi yasingeweza kujengwa kama pasingekuwa na msaada wa hesabu. Wababeli wa zamani walikuwa na mfumo wa kuhesabu hadi 60. Walipendelea namba zinazoshabihiana; kwa mfano, wangegawa a/b kama *l/b. Wababeli wa zamani walikuwa wa kwanza kutumia aljebra kwa hesabu za mistari na hesabu za mchanganyiko wa namba na herufi (quadradic problems). Chati iitwayo Plimpton 322 ni chati ya namba za Pythagorean (a^2 + b^ + c^2). Wababeli walibuni vipimo vya namba za mraba kama uchoravyo mstatili na kisha kuhesabu ukubwa wa eneo. Kimahesabu, watu hawa hawakutumia kitu chochote zaidi ya vipimo vya mraba (squares). Wakati huo huo Wababeli walikuwa na thamani tofauti ya pai (pi), na iliyokuwa sahihi zaidi ilikuwa 3.125. Mwanamahesabu wa Kiarabu wa karne ya 10 Abu’l-Wafa’ alisema watu waliotoa elimu ya kimahesabu walikuwa mafundi sanaa (wanasanaa) na wasanii.
 
Hesabu za maumbo ya pembetatu za Wamisri zilikuwa bora kuliko za Wababeli, kwa sababu Wamisri walikuwa na ufahamu juu ya kona, na walikuwa na ile thamani ya pai ya 31/7 au 3.16. Hii si mbali na 3.14159. Na hii imo katika nyaraka za Rhind Paparas—paparas (mwaka wa 1650 KK) na Paparas ya Moscow iliyokuwapo wakati ule ule. Majengo mengi ya Kimisri yalikuwa na pande za 3 kwa 4, lakini hawakujua juu ya nadharia ya Pythagoras (Pythagorean theorem). Sayansi na hesabu nyakati za zamani zilikuwa za "kivitendo". Pengine hii ndiyo sababu, kwa shauku tu, hapakuwa na yeyote aliyekuwa na wazo la "sifuri" hadi ilipogunduliwa nchini India.
Aljebra Zilitoka Wapi?
Hesabu ya aljebra ya kwanza tunayoifahamu ilikuwa imehifadhiwa katika Paparas ya Rhind iliyotolewa nakala na mwandishi wa Kimisri aliyeitwa Ahmes (mwaka wa 1650 KK.). Huu ni muda mrefu sana kabla Musa hajazaliwa. Wakati huo huo Wayunani walikuwa wakipendelea zaidi hesabu za maumbo, Wachina walikuwa wakikokotoa hesabu za mchanganyiko wa namba na herufi kabla Kristo hajazaliwa, na Wahindu (kwenye miaka ya 628-1150 BK) walikokotoa na kupata majibu ya maswali tata zaidi ya hesabu. Huko Baghdadi Muhammad ibn Musa al-Khowarizmi/Khawarizmi (mwaka wa 825 BK), Abu Kamil (mwaka wa 900 BK) na al-Karkhi (mwaka wa1100 BK) waliziendeleza hesabu za aljebra zaidi. Kwa kiasi kikubwa sana ziliziambukiza hesabu za Ulaya wakati Robert wa Chester alipotafsiri kitabu cha al-Khowarizmi kwenye mwaka wa 1140 BK kiliitwa kwa Kilatini Liber Algorism, maana yake kwa ujumla ni "Kitabu cha al-Kowarizmi." Na neno algorism baadaye lilikuwa algorithm and aljebra [kwa lugha ya kimahesabu].
 
Hapa chini jedwali laorodhesha baadhi ya wanasayansi wa Mashariki ya kati na wale wa Kiarabu pamoja na wanamahesabu.
 
Avicenna (Ibn-Sina) 979/980-1037 BKLicha ya kuwa tabibu muhimu sana kati ya enzi za Warumi na enzi ya leo, alikuwa mwanasayansi pia, mwanafalsafa, na mjenga hoja aliyeandika takriban kazi sanifu zipatazo 200. Albert Magnus wa England alijifunza mengi kutoka kwake
Averroes (Abu al-Walid Muhammad bin Ahmad ibn Muhammad ibn Roshd) 1126-1198 BKAlimsujudu [mwanafalsafa] Aristotle. Alisema mengi juu ya umaskini na masumbuko kutokana na jinsi Waislam walivyowachukulia
Avempace (Ibn Gabirol) 1021-1058 BKMwanafalsafa wa Kiyahudi na Kihispania aliyemwuunga mkono Aristotle
al-Karkhi miaka ya 1100 BKMichango mbalimbali katika kwa hesabu za Aljebra
Kemia/Alkemia na Fizikia
Makhalia wa Abbasid wa Baghdadi walikuwa na shulu ya Alkemia kwenye ya karne ya 9 au ya 10. Kazi za kwanza kabisa za Alkemia ya Kiarabu nusu ni za Kiarabu na nusu ni Kisiria. Khalid mwana wa Yezid (alikufa mwaka 708 BK) mwanafunzi wa mtawa wa Kisiria Marianus, alikuwa mwandishi wa kwanza wa Kiislam juu ya Alkemia, kufuatana na kitabu Kitab-al-Fihrist. Vipaji vya Wanaalkemia viliharibiwa kwa kujaribu kubadili madini ya "risasi" na vitu vingine kuwa dhahabu, lakini katika mchakato huo waligundua mambo mengi hii ni pamoja na Kemia pia. Wafuatao ni baadhi ya wanakemia maarufu wa Kiajemi na Kiarabu.
 
Geber (Jabir ibn-Hayyan) Kwenye miaka ya 760-815Mwanaalkemia wa Kiarabu aliyechuja chachu kitaalam na kutengeneza tindikali itokanayo na maji na naitrojeni. Alianza utafiti juu ya kubadili maumbo ya vitu yabisi (metals) na alivutiwa sana na kimiminika kiitwacho Zebadi (Mercury). Alikuwa mwenye sifa na maarufu kiasi kwamba kemia ikapewa jina la utani "Usanifu wa Jabir"
Ibn al Haytham Alikufa mwaka 1039 BH [Baada ya Hija]Alisomea mambo ya shinikizo, sumaku na sayansi ya mambo ya mwanga. Alisema kuwa huwa tunaona kwa kutumia mwanga unapoyaingia macho yetu, si miale ambayo jicho hutupa nje.
Quth al-Din 1236 BKAlielezea umbo la upinde wa mvua
Rhazes (Al-Razi) kwenye miaka ya 850-925Mkemia wa kiajemi (na mwana anga) aliyetengeneza chokaa ya kuta za nyumba ya Paris na alijifunza madini ya shaba na kristole (crystalline) yaani antimony
Abdul Salam of Pakistan. 1926-1996 BKAlishiriki tuzo ya Nobel ya mwaka 1979 katika Fizikia. Alikuwa Qadiani ambaye Waislamu wengi humchukulia kama wenye mafundisho potofu wasio waislamu
Geber (Jabir ibn-Hayyan) (alikufa mwaka 808 BK 193 BH [Baada ya Hija]) alikuwa Msufi mwenye imani ya kujikana mwenyewe kwa ajili ya mambo ya kiroho. Alikuwa na maabara huko Dameski. Vitabu vyake 200, vinane kati ya hivyo vilikuwa vya kemia, kujumlisha vitabu juu ya usindikaji, kutengeneza rangi, na uzito pamoja vipimo mbalimbali. Ama kwa hakika, wengine waiita kemia jina la utani "usanifu wa Jabir." Alitengeneza mezani iliyoweza kupima hadi uzito wa 1/6 ya gramu. Wakati watu wa Ulaya wa baadaye walidhani kuwa Phlogiston iliongezwa kwenye vitu vilipounguzwa, lakini Jabir alielewa kwa usahihi kwamba nguvu ya vitu vilivyoungua ilikuwa ikitoka, na kuacha mabaki ya majivu yasiyounguzika. Aligundua karatasi isiyounguzwa na moto, kizuia kutu, na kilichozuia maji kwenye nguo. Kwa uhalisia, alikuwa na wito wa karibu toka kwa watu japo alishauri kuwa maabara ya kikemia yalipaswa kuwa mbali na miji. 

Waislam Wauliza Wakristo

Swali la 1: Kwa nini mnaliamini Agano la Kale?
Jibu: Maandiko na elimukale (archaeology) vinaonyesha kuwa hakuna mabadiliko makubwa kwenye nakala za sasa kwa sababu angalau tano:
1. Mungu aliahidi kulinda neno lake katika Isaya 55:10-11; 59:21; 1 Petro 1:24-25, Mathayo 24:35. Hatima ya yote tunapaswa kuamini kuwa ama Mungu anaaminika au haaminiki. Lakini kama Muislam anaamini kuwa Mungu hakulinda neno lake katika Agano la Kale, na kwamba hakulinda neno lake katika Agano Jipya, ni kwa nini abadilishe na kulinda neno lake kwenye Kurani?
2. Yesu na Agano Jipya limethibitisha maandiko ya Agano la Kale katika Mathayo 19:4; 22:32,37; 39; 23:35; Marko 10:3-6; Luka 2:23-24; 4:4; 11:51; 20:37; 24:27,44
3. Ushahidi wa Elimukale: Kwenye Septuagint, Torati ilitafsiriwa kwenye Kiyunani/Kigiriki karibu mwaka 400 K.K. Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls) yaliandikwa kuanzia karibu mwaka 100 K.K hadi baada ya Kristo, na tunaweza kuyalinganisha na Biblia zetu za leo. Tafsiri za Kiaremi (Aramaic Targums) zilitolewa karibu na muda Yesu alipokuwepo duniani. Maandiko toka Bahari ya Chumvi yana vipande karibu 95,000 kutoka kwenye nyaraka 867 zilizoandikwa kwa mkono za Agano la Kale na maandiko mengine. Karibu 1/3 ya nyaraka zilizoandikwa kwa mkono za Hati toka Bahari ya Chumvi ni nyaraka za Agano la Kale kwa mujibu wa NIV Study Bible uk.1432. Elimukale inaonyesha kuwa Biblia ambayo Yesu aliijua ilikuwa imehifadhiwa. Nahal Hever ni pango karibu na Engedi, ambalo lina kipande kilichoandikwa kati ya mwaka 50 K.K. na 50 B.K. cha Manabii Wadogo katika lugha ya Kiyunani. Huko Masada, kulikuwa na nakala ya kitabu cha Yoshua iliyoandikwa mwaka 169-93 K.K. Mafunjo ya Nash (Nash Papyrus), yaliyoandikwa mwaka 150 K.K., yana amri kumi. Hati ya wadi Muraba’at ya Manabii Wadogo iliandikwa karibu mwaka 132 B.K.
4. Waandishi wa kanisa la awali, kuanzia kama mwaka 97/98 B.K, walilitumia Agano la Kale mara nyingi sana. 

Angalia kwa orodha ya angalau waandishi 15 wakristo hadi mwaka 258 B.K waliotumia Agano la Kale.

5. Waandishi wa Kiyahudi, ingawa walikuwa maadui wa ukristo, walilihifadhi Agano la Kale lile lile lililomo kwenye Biblia za kiprotestant za leo. Kipekee, waandishi wa kiyahudi Philo na Josephus walitumia Agano la Kale mara nyingi sana.
Kwa muhtasari, Mungu ni Mwenye enzi, ajuaye yote, na asiye na uzembe wa aina yoyote ile. Tunaweza kuamini kuwa ameweka muelekeo sahihi kwa wote wanaotafuta kumfuata kokote anakowaongoza.

Swali la 2: Je tunaweza kuliamini Agano Jipya?
Jibu: Ndiyo, kuna sababu tano zinazofanana na zile zilizotangulia, kuanzia na tumaini kuwa Mungu hataruhusu watoto wake wadanganywe kabisa, hadi kwenye ushahidi mkubwa wa nyaraka zilizoandikwa kwa mkono.
1. Mungu ameahidi kulinda neno lake katika Isaya 55:10-11; 59:21; 1 Petro 1:24-25, Mathayo 24:35. Tunaweza kumwamini Mungu.
2. Nyaraka za zamani zaidi zilizoandikwa kwa mkono zilizolindwa ni pamoja na:
100 B.K. uk.6 (kipande cha Luka)
117-138 B.K. John Rylands (Yohana 18:31-33,37-38)
100-150 B.K. Chester Beatty II (uk.45)
125-175 B.K. - Bodmer II (uk.66)
125-175 B.K. uk.104 (kipande cha Mathayo)
Zaidi ya nyaraka 30 zilizoandikwa kwa mkono zilizoandikwa kabla ya mwaka 300 B.K.

A’isha: Mke wa Muhammad Mwenye Miaka Tisa

Watu wengi wamesema kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na mke wake mwenye umri mdogo zaidi, A’isha, binti wa Abu Bakr, alipokuwa na miaka karibu 53 na [A’isha] alikuwa na miaka tisa. Baadhi ya Waislam wanakataa maneno haya. Kama mtu atadai kuwa Muhammad na A’isha walijamiiana wakati A’isha alipokuwa na umri wa miaka tisa, na walifanya makosa, jambo hili litakuwa ni kashfa kubwa sana kwa Muhammad. Kwa upande mwingine, kama ilikuwa kweli, jambo hili litaonyesha sura tofauti kabisa ya Muhammad itakayo washtua watu wengi. Kwa hiyo basi, madai haya dhidi ya Muhammad ni ya kweli au uongo? 
 
Andiko hili litaanza kwa kutoa ushahidi wa A’isha kuwa na miaka tisa wakati ndoa yake ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba, kisha litatoa vipingamizi 11 dhidi ya jambo hili, na mwishoni, litauliza itakuwa vipi endapo kila wazo lilikuwa sahihi.
 
Jambo hili ni la muhimu kwa desturi iliyotumika sehemu nyingi sana lakini ambayo imepuuzwa sana siku za leo: mabibi arusi watoto kwenye nchi za Kiislam waliotokana na mfano wa Muhammad.
Huko Iran, hadi kufikia Juni 2002 iliruhusiwa kisheria kwa msichana wa miaka 9 kuolewa kwa ruhusa ya wazazi. Voices Behind the Veil (Sauti Ttokea Nyuma ya Mtando) uk.136-137.
Huko Ivory Coast kitabu hiki pia kinatuambia kuhusu msichana wa miaka 12 ambaye alikuwa anaondoka nyumbani asubuhi kwa masaa mengi kabla ya kurudi nyumbani. Baada ya baba yake kumfunga, alimuunguza kwa kipande cha chuma, alimfungia kwa muda wa siku tatu bila chakula, hatimaye almwoza kwa mwanaume wa miaka 40. Hakuwahi kumpeleka shule kwa sababu alisema kuwa jambo hilo litawaondoa kwenye desturi zao, (mabinti) wataanza kuuliza maswali, na kutokupenda kuolewa mpaka wafikishe umri wa maka 19 au 20. 
Wataliban
 walizishawishi familia zao kuoza mabinti wao wakiwa na umri mdogo hata miaka nane. Voices Behind the Veil uk.110.
Gazeti la Dallas Morning News 9/28/03 uk.1,10S lilikuwa na habari ya kusikitisha kuhusu tabu ya wasichana wa Kiislam wa Nigeria ambao waliolewa wakiwa na umri mdogo sana, walipata ujauzito na walipopata uchungu wa uzazi miili yao midogo ilikuwa bado haijawa tayari. Kwa kiasi kikubwa habari hii ilikuwa mbaya, kimsingi wengi wa wasichana hao walihitaji kuzaa kwa upasuaji (C-section) lakini hawakuweza kupata huduma hiyo. Wengi wao walinusurika, lakini hawakuweza kupata watoto tena kwa sababu ya kuharibiwa kwa miji ya mimba.
 
Ili kuelewa asili ya mamlaka ya mfano wa Muhammad, ni muhimu tufahamu jambo moja kuhusu Hadithi za Kiislam. Hadithi zina nafasi ya juu sana katika madhehebu ya Suni kuliko mapokeo yalivyo na nafasi kwenye makanisa ya Katoliki na Orthodox. Waislam wa madhehebu ya Suni wanaamini kuwa mikusanyiko sita ya Hadithi ndiyo yenye mamlaka kubwa zaidi kwenye Uislam baada ya Kurani. Sehemu iliyobaki ya andiko hili inaonyesha kuwa dai hili ni la kweli kabisa, kwa mujibu wa vyanzo vingi vya awali vya Kiislam vyenye kuunga mkono. Pamoja na nukuu hizi toka kwenye Hadithi sita zinazoaminika ni nukuu toka kwa wana historia wa zamani wa Kiislam wanaoheshimika sana ibn Ishaq na al-Tabari.
 
1. Sahih al-Bukhari 810-870 BK, 256 BH
1a. "Alisimulia baba wa Hisham: Khadija alkufa miaka mitatu kabla ya Nabii kuondoka Madina. Alikaa huko miaka miwili au zaidi kisha akamuoa ‘Aisha alipokuwa msichana mwenye umri wa miaka sita, na Muhammad aliikamilisha ndoa yao kwa tendo la unyumba wakati ‘Aisha alipokuwa na umri wa miaka tisa." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 43 na.236, uk.153.
  

1b. Habari hizo zipo pia kwenye Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 43 na.234, uk.152.
  

1c. "Alisimulia ‘Urwa: Nabii aliandika (mkataba wa ndoa) na ‘Aisha wakati msichana alipokuwa na umri wa miaka sita na aliikamilisha ndoa yake nay eye kwa tendo la unyumba wakati akiwa na miaka tisa na ‘Aisha aliendelea kuwa naye kwa miaka tisa (yaani mpaka kifo cha Nabii). Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 62 sura ya 60 na.88, uk.65.
  

1d. Alisimulia ‘Aisha: Nabii alikuwa akinisitiri kwa Rida (vazi lenye kukinga sehemu ya juu ya mwili) yake nilipokuwa nawaangalia Waethiopia waliokuwa wanacheza kwenye ua wa nyuma wa msikiti. (Niliendelea kuangalia) hadi nilipotosheka. Hivyo unaweza kuelewa ni jinsi gani binti mdogo (ambaye hajafikia umri wa kuvunja ungo) ambaye ana hamu ya kufurahia burudani alivyofanyiwa mambo ya namna hii. Bukhari juzuu ya7 kitabu cha 62 sura ya 115 na.163, uk.119.
  

1e. "Alisimulia ‘Aisha: (mke wa Nabii) sikumbuki kama wazazi wangu waliamini dini yoyote ile isipokuwa dini ya kweli (yaani Uislam), na (sikumbuki) siku yoyote iliyopita bila sisi kutembelewa na Mtume wa Allah asubuhi na jioni." Bukharijuzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 4 na.245, uk.158. Kwa hiyo, ‘Aisha ama hakuwa mkubwa ama hakuwa amezaliwa kabisa wakati wazazi wake walipo badili dini na kuwa Waislam. Jambo hili linaendana na yeye kuwa mtoto wakati ndoa yake na Muhammad ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba.
 
2. Sahih Muslim 817-875 BK, 261 BH
Mkusanyiko huu unachukuliwa kuwa wa pili wenye kuaminika zaidi miongoni mwa Hadithi.
  

TRENDING NOW