Na Mark Gabriel
Ilikuwa saa 9 kamili alfajiri wakati baba yangu aliposikia mlango wa nyumba yetu ukigongwa. Wakati alipofungua mlango, watu 15 hadi 20 waliingia kwa haraka ndani wakiwa wamebeba silaha za Urusi Kalashnikov za uvamizi. Walikimbilia ghorofani wakipitapita kila mahali katika nyumba wakiwaamsha watu na kunitafuta mimi. Walikuwa wametapakaa kila mahali mle ndani kabla mmoja wao hajanikuta nimelala kitandani mwangu. Wazazi wangu, kaka zangu na wenzi wao na watoto walikuwa wameamka, wakilia na kuhofia sana wakati hao watu waliponiburuza na kuondoka na mimi. Kila mtu wa eneo lile alisikia habari za vurumai hizo. Nilipelekwa mahali palipoonekana kama jela na nikawekwa rumande. Asubuhi yake wazazi wangu kwa hasira na majonzi walijaribu kutafuta kwamba nini kilichonitokea. Moja kwa moja walienda kituo cha polisi na kudai “mtoto wetu yuko wapi? Lakini hakuna yeyote aliyejua lolote juu yangu. Nilikuwa katika mikono ya polisi wa siri wa Misri.
Matukio Yaliyosababisha Kukamatwa Kwangu Miaka kumi na tano iliyopita nilikuwa Imamu wa msikiti katika jiji la Giza, Misri, mahali ambapo yale mapiramidi maarufu ya Misri yamepangwa. (Imam wa msikiti ni wadhifa unaofanana na mchungaji wa kanisa la Kikristo) Nilihubiri ujumbe wa wiki siku za ijumaa kuanzia saa 6 hadi 7 mchana, ikiwa ni pamoja na kufanya wajibu zinginezo zilizonihusu.
Ijumaa moja ujumbe wangu wa wiki ulikuwa Jihad. Niliwaambia watu 250 waliokuwa wamekaa uwanjani mbele yangu Jihad katika uislamu inatetea taifa la Kiislam na Uislam dhidi ya mashambulizi ya maadui. Uislam ni dini ya amani na itapigana na yule anayepigana nayo tu. Hawa makafiri, wamataifa, wapotoshaji, Wakristo na wanaomhuzunisha Allah, Wayahudi, mbali ya wivu wa Uislam wa amani na Mtume wake; walieneza uongo kwamba Uislam ulienezwa kwa upanga na kwa nguvu kali sana zenye vurugu. Makafiri na washitaki wa Uislam hawayakubali maneno ya Allah.
Katika hatua hii nilinukuu kutoka katika Koran “wala usimuue yeyote ambaye uuaji kwa Allah umekatazwa ila kwa sababu ya haki” (Surah 17:33 Koran Tukufu). Nilipozungumza maneno haya ndio kwanza nilikuwa nimetoka kuhitimu Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Kairo Misri. Chuo Kikuu cha zamani na chenye fahari zaidi cha Kiislam duniani. Kinafanya kazi kama mamlaka ya kiroho ulimwenguni mwote. Nilikuwa nafundisha katika Chuo Kikuu na nilikuwa Imam siku za mwisho wa juma katika msikiti huu. Nilikuwa nakihubiri kile walichonifundisha, lakini kwa ndani nilihitaji kuyaweka mawazo yangu kwenye nafsi yangu. Hata hivyo, nilijua kile kinachowapata watu waliohitilafiana na agenda za Al-Azhar. Watafukuzwa na wasingeruhusiwa kufundisha Chuo Kikuu kingine chochote katika Taifa hilo.
Nilifahamu kwamba nilichokuwa nakifundisha pale msikitini na katika Al-Azhar hakikuwa kile nilichokiona katika Koran, ambayo nilikuwa nimeikariri yote nikiwa na umri wa miaka 12. Kilichonichanganya zaidi ni kwamba niliambiwa nihubiri kuhusu Uislam wa upendo, wema na msamaha. Wakati huo huo wale waumini wakereketwa; wale ambao ndio waliotarajiwa kuishi kwa kutenda Uislam kamili; walikuwa wakiyapiga mabomu Makanisa na kuua Wakristo. Kwa wakati huohuo vuguvugu la jihad lilikuwa limepamba moto ndani ya Misri. Matukio ya mashambulizi na kupigwa mabomu, dhidi ya Wakristo yalikuwa ya kawaida sana. Ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.
Kuutafuta UkweliWakati mwingi nilijaribu kutazama kimantiki aina ya Uislam niliokuwa naufanya kwa kujiambia nafsi yangu “Sawa, hauko mbali sana na ukweli. Kwanza kuna mstari katika Koran kuhusu upendo, amani, msamaha na huruma. Unachotakiwa tu ni kutojali kipengele kinachohusu jihad na cha kuua wasiokuwa Waislam.” Nilipitia kila tafsiri ya koran nikijaribu kukwepa Jihad na kuua wasio Waislamu, bado niliendelea kugundua utekelezaji wa hayo ukiungwa mkono. Wanazuoni walikubali kwamba Waislam lazima wakazie Jihad kwa makafiri (wale wanaoukataa Uislam na waasi wale wanaoucha Uislam). Bado Jihad haikuwa na maelewano na mistari iliyozungumzia kuishi kwa amani na wengine. Mikanganyo yote katika Koran ilikuwa kweli inasababisha matatizo kwa imani yangu. Nilitumia miaka 4 kusomea Digrii yangu ya kwanza, nilihitimu nikiwa wa pili kati ya wanafunzi elfu sita. Halafu kulikuwa na miaka mingine 4 kwa ajili ya Digrii yangu ya pili na mitatu zaidi kwa ajili ya Ph.D (udaktari wa falsafa) yote nikisomea Uislam.
Ninafahamu mafundisho vizuri katika sehemu moja pombe imekatazwa; katika sehemu nyingine imeruhusiwa (linganisha Surah 5:90-91 na Surah 47:15). Katika sehemu moja Koran inasema Wakristo ni watu wema ambao wanampenda na kumwabudu Mungu mmoja, kwahiyo mnaweza kuwa marafiki nao (Surah 2:62,3:113-114). Halafu unakuta mstari mwingine unaosema Wakristo lazima waslim, walipe kodi la sivyo wauwawe kwa upanga (Surah 9:29) Wanazuoni wanasuluhisho la kitheolojia kwa matatizo haya, lakini nashangaa ni jinsi gani Allah, mwenye enzi na mwenye nguvu sana, awe aidha amejichanganya mwenyewe namna hii kubwa au anabadili nia yake kwa kiasi kikubwa namna hii, hata nabii wa Kiislam Mohammed, aliitekeleza imani yake katika njia ambazo zinapingana na Koran. Koran inasema Mohammed alitumwa ili kuonyesha rehema za Mungu kwa ulimwengu. Lakini alikuja kuwa dikteta wa kivita, akishambulia, kuua na kuchukua mali na kupora ili kufadhili himaya yake. Iweje hivyo iwe ni kuonyesha rehema?
Allah, Mungu aliyefunuliwa katika Koran, sio Baba wa Upendo. Inasema kwamba anatamani kuwaongoza watu upotevuni (Surah 6:39,126). Hawasaidii wale walioongozwa nae upotevuni (Surah 30:29) na anatamani kuwatumia kujaza watu kuzimu (Surah 32:13). Uislamu umejaa ubaguzi dhidi ya wanawake, dhidi ya wasio Waislam, dhidi ya Wakristo na zaidi hasahasa dhidi ya Wayahudi.
Chuki imejengwa katika dini. Historia ya Uislam ambayo ilikuwa ndio eneo langu nililobobea hasa, ingeweza ikaainishwa kama mto wa damu. Mwishoni nilifikia mahali ambapo nilikuwa nahoji imani na Koran pamoja na wanafunzi wangu katika Chuo Kikuu. Baadhi yao walikuwa wanachama wa vuguvugu la ugaidi na walighadhibika. “Huwezi kuushutumu Uislam. Ninini kimetokea? Unatakiwa utufundishe. Unatakiwa kukubaliana na Uislam”. Chuo Kikuu kikasikia kuhusu hilo, na niliitwa kwa ajili ya mkutano Desemba 1991. Kufupisha mkutano, nikawaambia kilichokuwepo moyoni mwangu. Siwezi tena kusema kwamba Koran imekuja moja kwa moja toka mbinguni au toka kwa Allah. Huu hauwezi kuwa ufunuo wa Mungu wa kweli. Haya yalikuwa maneno ya kufuru kubwa katika mtazamo wao. Wakanitemea mate usoni, mtu mmoja akanitukana “wewe mkufuru! mbegu haramu!” Chuo Kikuu kikanifukuza na kuita kikosi cha polisi wa siri wa Misri.
Gereza la Misri





