BADO
HUJASTAHILI
KUTOKA:
KWENYE GIZA LA UDANGANYIFU WA KIISLAMU
HADI:
KWENYE NURU YA UTUKUFU WA YESU
-UKWELI-
Ushuhuda wa Lazaro
Nakala ya Bure
Ni furaha yangu kubwa katika Bwana kwamba nimeweza kukushirikisha ushuhuda wangu binafsi. Jinsi Bwana alivyonichagua mimi na jinsi nilivyokuja kwenye miguu ya Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi.
MAISHA YANGU YA ZAMANI
Mtu fulani aliniuliza, “Mchungaji waweza kunieleza upi ni muujiza mkuu unaoukumbuka katika umri wako huu?” Nikamjibu “katika ufahamu wangu muujiza mkuu katika umri huu ni kwamba katika mwaka 1988 nilikuwa Maulvi (Msomi wa Kiislamu) na leo mimi ni Mchungaji.” Nilisoma kozi ya juu kabisa ya kidini (Maulvi Fazil, Alam Fazil, Fazil-e-Ijaz). Baada ya kuhitimu shahada yangu ya Uzamili ya Sanaa katika Kiarabu kutoka Lahore nilikwenda Iraq kwa masomo ya juu zaidi.
MASOMO YA JUU KULE IRAK NA SAUDI ARABIA
Kutoka mwaka 1974 hadi 1978 nilisoma Chuo Kikuu cha Irak. Nilitunukiwa shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Sheria za Kiislamu katika Kiarabu na Uajemi (Mufti) kwa sababu nilikuwa naenda kuwa Maulana (mufii wa Kiislamu). Lugha yangu ya kwanza ni Punjabi. Nilisoma kwa Kiarabu hadi nikatokea kufanya mitihani ya falsafa ya udaktari (PhD) kwa lugha ya Kiarabu. Pamoja nami katika darasa walikuwepo wanafunzi ambao lugha yao kuu ilikuwa Kiarabu. Nilipata alama 995 kati ya alama 1000 ambapo nilivunja rekodi katika Chuo Kikuu cha Irak hadi siku ya leo(mwaka1995). Nilisoma sheria za kiislam kuanzia mwaka 1978 hadi 1980 katika mji Mtakatifu wa MAKA (Saudi Arabia). Niliteuliwa kuwa mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu nchini Saudi Arabia kuanzia mwaka 1980 hadi 1984.
NCHINI ISLAMABAD KAMA MWANASHERIA MKUU WA MAHAKAMA YA SHERIA
Nilirudi nchini mwangu mwaka 1985 na nikateuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu wa Islamabad (1984-1989). Nilirithi chuki ya kumchukia Kristo na Wakristo kutoka kwa mababu zangu. Niliwatesa Wakristo na nilikuwa kinyume na Yesu. Nilijaribu kwa nguvu zangu zote kukomesha mikutano yao ya dini, niliwaadhibu na kuwanenea mabaya kwa uwezo wangu wote. Kama mtuhumiwa wa Kikristo angeletwa mbele yangu mahakamani, angearifiwa na wanasheria kwamba huyu hakimu atakuhukumu kifo tu. Akijua kuwa wewe ni Mkristo inatosha, hata hitaji maelezo zaidi. Atakapo fungua faili lako na kusoma kwamba wewe ni Mkristo inamtosha kukuhukumu kifo.
YESU NDANI YA OFISI YANGU
Katika asubuhi mwanana ya Aprili 26 mwaka 1989, nilikuwa nimekaa ofisini mwangu nikiwa na katibu wangu (mwanamke) akiwa anafanya shughuli fulani za mambo ya dini. Mara majira ya saa 5.30 asubuhi ofisi yangu ilianza kujawa na mwanga wa ajabu na wa kushangaza ambao ulikuwa mwangavu na unaong’aa kuliko jua. Wakati huo nilikuwa nimefuga ndevu ndefu zilizonifikia tumboni na nywele ndefu zilizonifika mabegani. Katibu wangu alikuwa akihofia mpira huu wenye mwanga usio wa kawaida ambao nuru yake ilizidi kuwa angavu, na alianza kuniuliza mimi “Maulana (msomi wa Kiislamu) ni nini kinachotokea ofisini kwetu?” Mimi binafsi nilikuwa naogopa na ili kuficha woga wangu nilimwambia aende nje ya ofisi. Baada ya dakika chache ule mwanga ulitoweka, lakini katikati ya ofisi yangu nilimwona mtu aliyekuwa amesimama. Na ndevu za rangi ya dhahabu na nywele za rangi ya dhahabu ndefu hadi mabegani akiwa amevalia vazi ling’aalo sana. Nilikuwa nikimtazama ana kwa ana. Alianza kuongea na mimi na kuniambia “Angalia Maulana umenitesa mno lakini upo kwenye mipango yangu tangu milele” Niliwaza huyu alikuwa Malaika wa Mauti na leo ndio siku yangu ya mwisho ulimwenguni. Nilikuwa nikitetemeka ndani yangu na kuyaogopa sana haya mazingira kwa sababu nilikuwa na uhakika huyu alikuwa Malaika wa Mauti na kwamba leo ndio mwisho wangu duniani. Katika hofu yangu ya kutisha nilihisi shinikizo kubwa ndani ya nafsi yangu na nikaanza kumlalamikia. Nikamwuliza “wewe ni nani na umedirikije kuingia ofisini mwangu? Walinzi wa usalama wako wapi? Kwanini hawakukuzuia? Unataka nini toka kwangu?” Ndani ya sekunde moja nilimwuliza swali zaidi ya moja. Nikamwambia, “Jitambulishe” Akajibu “Nimekukomboa wewe (Fidiya) na kujitoa sadaka kwa ajili yako (Qurbani), wakati neno “kujitoa sadaka” (Qurbani) linapozungumzwa linaeleweka kirahisi zaidi na Muislam. Kwa mujibu wa sadaka Hazrat-I-Ibrahim (Abraham) ya kumtoa mwanae Ishmael kutokana na Imani ya kiislam. Nilitiwa moyo na jibu hili na kwa haraka nikamwuliza “Je, wewe ni Hazrat-I-Ibrahim aliyemtoa sadaka mwanae Ishmael?” Akajibu “Hapana nimeyatoa maisha yangu kwa ajili yako na kwa ulimwengu mzima msalabani (Saleeb) lakini wewe umenitesa mno. Hii ndio sababu Mimi mwenyewe nimekuja nikufanye uwe wangu.”
Nikiwa kama Msomi wa Kiislamu sikuwahi kusoma Biblia au maandiko mengine yeyote ya Kikristo na wala sikuwa na hamu na Kristo wala Ukristo. Lakini baada ya kusikia neno ‘msalaba’ (saleeb), niligundua kuwa huyu ni nabii ISSA (Yesu). Nikawaza moyoni mwangu, “Huyu ni mtu wa namna gani? Ninamtesa, ninamtukana na kumnenea maneno mabaya na yeye binafsi anakuja ofisini mwangu.” Kwa kila mtu kuna moyo wa ndani uitwao dhamiri. Sauti yangu ya ndani ilikuwa ikiniambia “Maulana acha usumbufu wako, yule unayemtesa anaongea na wewe. Achana na usumbufu wako na uadui na umpokee Yeye.”
Namshukuru Mungu kwamba sikumpokea Kristo baada ya kusoma Biblia au baada ya kuzidiwa nguvu na wasomi wa Kristo kwenye mdahalo. Mshahara wangu kwa mwezi ulikuwa rupia za Pakistani 120,000 (kadiri ya dola za Marekani 3,000). Mshahara wangu ulikuwa ukitumwa kwangu moja kwa moja kutoka Falme za Kiarabu za Saudia. Mimi nilikuwa ni mtu niliyezoea kulala peke yangu kwenye kitanda kikubwa (master bed). Haikuwa rahisi kwangu kukalia kochi la mtu mmoja. Nilikuwa mkubwa sana kiasi kwamba walizoea kunitengea kochi la watu wawili nikalie. Kwa kitambo niliwaza juu ya faraja na anasa zote ulimwenguni nilizokuwa nikizipata kama Mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu ndipo nilipomjibu “Sikuamini, sina chochote cha kufanya na wewe wala msalaba wako.”
DINI YANGU YA ZAMANI NA UDHURU
Nilimpa udhuru mwingi kulingana na imani yangu na nilimwambia nabii wangu ni mkuu kuliko manabii wote. Lakini Akaniambia “Njoo toka nje ya ofisi yako.” Sielewi jinsi nilivyokwenda kwenye ubaraza wa ghorofa nikipaa pamoja naye angani, kisha toka kwenye ubaraza wa ghorofa nikaona mbingu zimefunguka. Akanionyesha Nabii wangu na vitu vingi vinginevyo. Kisha tukarudi ofisini na akaniambia. “Inabidi unifuate, nataka nikufanye mtumishi wangu, nataka nikufanye shahidi wangu.” Dhamiri yangu ikaanza “Maulana mpokee, ni kweli yeye ni Mkuu na mtukufu. Kubali ukweli huu kwamba wewe upo kinyume nae na umemtesa lakini anakupenda.” Nikamjibu “Sawa Issa Masih, kuanzia leo na kuendelea wewe ni wangu na mimi ni wako.” Na huyu Issa Masih akaenda zake toka ofisini mwangu kwa njia ile ile aliyojia.
KUJIUZULU KWANGU
Mara moja niliandika barua ya kujiuzulu na kuituma Saud Arabia kwa njia ya fax. Baada ya kupokea fax yangu Imam wa Khana-e-Kaba, Sheikh Abdala, alipanda ndege ya kwanza na kuja Islamabad na akaja moja kwa moja ofisini mwangu. Aliniuliza kwa mshangao mkubwa katika lugha ya kiarabu “Je, wewe si kichaa?” Nikamjibu, “Mimi sio kichaa lakini mimi ni Mkristo.” Alifahamu vyema kwamba natoka katika familia ya Kiislamu ambapo wote ni wasomi wa Kiislamu, na kwamba mimi ni wa 8 katika mlolongo wa wasomi wa Kiislamu baada ya baba yangu na mababu zangu waliotutangulia. Ndipo Sheikh akatoa amri kwa wenye mamlaka, “Anapaswa kuadhibiwa vilivyo kwa sababu ameukataa Uislamu na mtume wetu, kama akienda nje na kuwaeleza watu wengine imani yake mpya, itakuwa kufuru kwetu sisi. Mpeni wakati mgumu gerezani ili kwamba kwa wakati ujao asiwepo yeyote atakaye diriki kutumia jina hili ‘Ukristo’ tena.”
MATESO KWA KUMPOKEA YESU
Mara moja nilikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. Usiku walinipeleka mahabusu. Nilipigwa kikatili sana kule jela na asubuhi nikaambiwa “Oh maulana, kujiuzulu kwako hakujakubaliwa. Tafadhali rudi kwenye kiti chako na uendelee na kazi yako” Nikajibu, “Hapana mimi ni Mkristo”
JINSI FAMILIA YANGU ILIVYOLICHUKULIA
JAMBO HILO
Baba yangu alifariki mwaka 1978 lakini wakati hayo yaliponitokea mama na kaka yangu walikuwa bado hai. Kwa sasa wote wawili wameshafariki. Walikuja gerezani na walisema, “Tumekupatia elimu nzuri namna hii na kutumia hela zetu nyingi kwa ajili yako. Tulikupeleka Irak kwa ajili ya masomo ya juu, kwanini sasa unaenda kuwa kafiri? (neno linalotumika kwa wale wanaoukataa uislam). Tafadhali rudi ofisini kwako uchukue nafasi yako.” Nikajibu, “Amme (mama) Hapana. Tangu jana nimekuwa Mkristo.” Shangazi yangu aliyekuwa amesimama pamoja nao alianza kunitukana. Alidhani labda nikishasikia maneno hayo mabaya ningerudi nyuma kwenye Uislamu. Alisema “Mpeni ndoo ya takataka na ufagio mrefu mikononi mwake halafu mwacheni akaishi na wafagizi (Wakristo).” Kwasababu Waislamu wengi wa Pakistani hudhani Wakristo ndio wafagizi, lakini wanasahau kwamba hata kule Saudia Waislamu hufanya kazi ya ufagizi na kazi nyingine nyingi za ajira ndogo. Nikamjibu, “Kama ni kwa ajili ya Masihi (Kristo) natakiwa kuifanya kazi hii nitaifanya. Kwa sababu yeye alikuja kwangu moja kwa moja na kuongea nami, alinionyesha utukufu wake na nguvu iliyopo Mbinguni ambayo sasa inakaa katika chembechembe zote za damu yangu. Sasa Anaishi ndani yangu siwezi kumwacha.” Wakasema “sawa” na wakaondoka.
KULE GEREZANI
Adhabu yangu ya kwanza ilianza kwa kucha za vidole vyangu kunyofolewa kwa kuvutwa. Baada ya kupigwa kwa mara ya pili nilipelekwa hospitali. Pale hospitalini nilipewa maumivu mengine makali ya akili. Nilisikia kwamba mke wangu na mtoto wote wawili walikufa kwenye chumba cha uzazi wakati wa kujifungua. Kwanza madaktari walikuwa wakijaribu kuokoa maisha ya mtoto na ndipo wakati huo mke wangu alipofariki. Kisha baada ya masaa 4 mtoto wangu naye akafariki. Ndugu zangu wote, majirani na marafiki walikuja wakaniambia, “Unaona, Allah amekuadhibu. Mkeo na mtoto wamekufa. Kucha zako zimenyofolewa. Lakini bado muda wa kurudi nyuma upo.” Jibu langu pekee lilikuwa, “Hapana sasa anaishi ndani yangu.” Kwa wakati ule sikuwa najua kwamba huu ulikuwa mstari wa Biblia kwa sababu hakukuwepo mtu katika familia yetu nzima aliyekuwa anaifahamu Biblia. Hata mimi kama msomi wa kiislamu sikuwahi kujifunza ama kusoma Biblia. Kwa sasa nalijua andiko linalosema,“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Mungu hukaa ndani yenu” (1Kor 3:16).
Pili nilikuwa nimening’inizwa miguu yangu ikielekea chini lakini si kwa kamba wala minyororo. Safari hii walizitumia nywele zangu ndefu, na nilikuwa nikibembea mle chumbani kama mpira. Uzito wangu wote ulikuwa katika nywele zangu. Nilining’inizwa namna hii hadi damu kutoka kichwani ikaanza kudondoka sakafuni. Unaweza kufikiria wazi kwamba damu ili idondoke sakafuni nguo zangu zote zilikuwa zimeloa damu. Walidhani ningekufa kwa sababu kutokana na mateso uso, macho yangu yalivimba hadi macho yalifunikwa kabisa. Nilikuwa mnene na aliyezidiwa uzito, nilikuwa siwezi kufumbua macho yangu au hata kumwona mtu. Tena waliniuliza, “Sasa Maulana unawaza nini kuhusu dini yako mpya?” Nikawajibu, “Kristo ni wangu na mimi ni wake.” Leo sisi ni watumwa wa mapokeo ya wahenga wetu. Pale ambapo wahenga wetu walitufikisha, hatutaki kupaacha, wala dini zao. Hata hivyo wahenga wangu wote walikuwa Maulvi na wasomi wa Kiislamu na kwa sababu ya hilo ilikuwa ngumu kwao kumpokea Yesu.
KUVUNJWA MBAVU
Nilikaa miaka miwili katika gereza la Hari Pur Hazara. Mshtuko mkubwa wa tatu ambao niliupata gerezani ni kwamba mbavu zangu zote za pande mbili zilivunjwa kwa mateke ya askari polisi na maofisa. Naweza kukuonyesha mbavu zangu na mtu yeyote aliye na taaluma ya udaktari anaweza kuzikagua mbavu zangu wakati wowote. Baada ya kuzivunja mbavu zangu na kunipiga mateke bila huruma wakasema tena, “Tutakugharamia matibabu yako yote na tutakupeleka hospitali kama utarudi kwenye Uislamu.” Nikajibu, “Wala kamwe msiniambie jambo hili tena. Lolote mnalotaka kunifanyia mnaweza kufanya lakini siwezi kusikiliza maneno yanayonitaka nirudi nyuma kwenye dini yenu ya kizamani. Hata kama ningetaka kurudi nyuma siwezi kurudi nyuma kwa maana Yesu anaishi ndani yangu siwezi kumwacha.” Nilipelekwa hospitali madaktari waliamua kunifanyia upasuaji na walikuwa wakipanga kuniwekea vitu fulani kama chuma ambavyo vingekaza mbavu zangu tena. Wangenipeleka kwenye chumba cha upasuaji asubuhi ambayo ingefuata. Jinsi nilivyokuwa na maumivu makali ya kufa, ilipofika saa 10:30 alfajiri nilimwona Yesu Kristo tena ana kwa ana akiwa amesimama upande wangu. Nikamwambia, “Masihi (Yesu) wamenipiga na kunitesa bila huruma.” Yesu akajibu, “Bado hujastahili kunitumikia.” Nilifadhaika sana kwamba niliacha nafasi kubwa ya heshima kubwa namna ile, mke wangu na mtoto wamekufa, nimeiacha familia yangu, mali zangu zote zimechukuliwa, kucha zangu nazo zimeng’olewa, nilitundikwa kutumia nywele zangu, sasa hata mbavu zangu zimevunjwa na kile Yesu anachoniambia ni kitu kisicho cha kawaida kabisa.
YESU NI MPONYAJI