Thursday, August 6, 2015
QURAN SIO MANENO YA ALLAH WALA MUNGU
Ndugu msomaji,
Huu ni MSIBA mkubwa sana kwa Waislam wote duniani. Waislam wamekuwa na tabia ya kusema kuwa, eti Quran yote ni maneno ya Allah. Unapo wauliza, huyo Allah aliwezaje ongea na Muhammad, wanabakia kimya na kuanza kukutukana. Zaidi ya hapo, leo nitawawekea ushahid tosha kuwa Quran sio maneno ya Allah.
Haya ungana nani kwa ushahidi:
SHETANI ANASEMA KWENYE QURAN
Surah Al Hijr 39. Shetani akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
Kwenye Surat Al Hijr, tumesoma kuwa Shetani ndie anazungumza katika hiyo aya ya 39. Kumbe basi, Shetani ni msemaji ndani ya Qurani.
HAPA TUNASOMA KUWA ZAKARIA NA YEYE NI MZUNGUMZAJI KATIKA QURAN
Surat Maryam: Zakaria Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
Waislam, hivi Quran ni maneno ya nani?
Endelea kupata darasa hapa:
MARYAM NA YEYE NI MSEMAJI KATIKA QURAN
Surat Maryam aya 18: Maryamu akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.
Waislam, mbona na Maryam anasema kwenye Quran? Au siku hizi Maryam amekuwa Allah? Huu ni Msiba mkubwa sana kwa Waislam.
MALAIKA NAO WANASEMA KWENYE QURAN
Surat Maryam aya 21: Malaika akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
Ndugu msomaji, kwanini Waislam wanapenda kusema uongo namna hii, eti Quran yote ni Maneno ya Allah? Mbona tunasoma viumbe wengine wakisema ndani ya Quran?
ISSA BIN MARYAM NA YEYE ANASEMA KWENYE QURAN
Surat Maryam aya 36: Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
Issa na yeye alisema kwenye Quran. Lakini Muhammad yeye hakuwai sema chochote kile kwenye Quruani wala kuzaliwa kwake hakukutajwa kwenye Quran. Huu ni Msiba mkubwa sana kwa WAISLAM.
SWALI LANGU KWA WAISLAM NI DOGO SANA:
1. NI NANI MSEMAJI KATIKA QURAN?
2. QURANI NI MANENO YA NANI?
Mkiweza nijibu kwa aya na bila shari, leo hii nitasilimu na kuwa Muislam.
Waislam huwa wanasema kama huamni kuwa Quran ni maneno ya Mungu, basi teremsha aya kama za Quran, huku tukifahamu kuwa kuna aya nyingi ambazo wasemaji wake ni wengine na sio Allah.
Sasa, huu utata tunawaachia waislam waje hapa kutujibu bila ya kuweweseka.
QURAN NI MANENO YA NANI?
Wednesday, August 5, 2015
MATOLEO 20 TOFAUTI YA QURAN ::::::::20 VERSIONS OF QURAN::::::::::
MATOLEO 20 TOFAUTI YA QURAN
20 VERSIONS OF QURAN
Je, Kati ya haya Matolea 20 (Ishirini) ya Quran, toleo lipi ni la kweli?
Ndugu msomaji,
Leo nitaweka ukweli kuhusu Quran ambayo ina Matoleo 20 na kati ya hayo Ishirini (20) Matoleo 7 (Saba) yametajwa katika Hadith Mwaminifu za Muhammad.
Hapa chini ni Wasomaji Saba (7) ambao wote wana Matoleo Mawili mawili. Hawa Wasomaji saba wanapatikana hapa:
Nafi (from Medina; d.169/785)
Ibn Kathir (from Mecca; d.119/737)
Abu `Amr al-'Ala' (from Damascus; d.53/770)
Ibn `Amir (from Basra; d.118/736)
Hamzah (from Kufah; d.156/772)
al-Qisa'i (from Kufah; d.189/804)
Abu Bakr `Asim (from Kufah; d.158/778)
WASOMAJI SABA NA MATOLEO YAO YA QURAN
1. Msomaji : Nafi`
MATOLEO YAKE
Warsh
Qalun
2. Msomaji: Ibn Kathir
MATOLEO YAKE
al-Bazzi
Qunbul
3. Msomaji: Abu `Amr al-'Ala'
MATOLEO YAKE
Al-Duri
al-Suri
4. Msomaji: Ibn `Amir
MATOLEO YAKE
Hisham
Ibn Dhakwan
5. Msomaji: Hamzah
MATOLEO YAKE
Khalaf
Khallad
6. Msomaji: al-Qisa'i
MATOLEO YAKE
al-Duri
Abu'l-Harith
7. Msomaji: Abu Bakr `Asim
MATOLEO YAKE
Hafs
Ibn `Ayyash
HAWA NI WASOMAJI WENGI WATATU NA MATOLEA YAO MAWILI KILA MMOJA
"The Three" readers
1. Msomaji: Abu Ja`far
MATOLEO YAKE
Ibn Wardan
Ibn Jamaz
2. Msomaji: Ya`qub al-Hashimi
MATOLEO YAKE
Ruways
Rawh
3. Msomaji: Khalaf al-Bazzar
MATOLEO YAKE
Ishaq
Idris al-Haddad
Wadhalimu wa dini ya Kiislamu wanakiri kuwa kuna WASOMAJI wengi zaidi, lakini wanasema kuwa hawa walio tajwa hapo juu ndio thabit na sahihi. Kumbe basi kuna VERSIONS ISHIRINI ZA QURAN !!!!!!
SASA MASWALI YAKUJIULIZA NI HAYA:
1. Kati ya hao wasomaji wakurani, ni yupi yupo sahihi?
2. Kama Allah ndie aliteremsha Quran kwa Muhammad, kivipi awe na wasomaji wengine na kumsahahu Muhammad mtume wake kipenzi?
Ndugu msomaji, leo tumejifunza kuwa katika Uislam kuna siri nyingi sana ambazo zimefichwa na wanaona aibu kusme aukweli kuwa QURAN INA VERSIONS 20. HUU NI MSIBA KWA ALLAH NA MTUME WAKE MUHAMMAD.
Mungu awabariki sana na kuendelea kuwafungua macho.
Katika huduma yake
Max Shimba Ministries Org.
Kutoka Kwenye Uislamu Hadi Kwenye Ukristo
Jina langu ni Tahir na hii ni safari yangu kutoka kwenye Uislamu hadi kwenye Ukristo.
Mara baada ya kufika Marekani nikitokea Palestina miaka 14 iliyopita, nilimwoa msichana mzuri wa Kikristo. Msichana huyu alijaribu kuwa Mwislamu ili kunifurahisha mimi, lakini kadiri alivyojitahidi kufanya hivyo, ndivyo nilivyozidi kuwa mbali naye. Tulizaa mtoto mmoja, lakini ndoa yetu haikudumu maana ni vigumu sana kupenda wakati moyo wako umejaa chuki. Chuki ndicho kitu ambacho nilifundishwa wakati wa kukua kwangu kule Palestina – chuki dhidi ya Wayahudi, Wakristo na hata dunia nzima. Ukiwa kama Mpalestina, unafundishwa tangu ziku ya kwanza kwamba dunia yote ndiyo inayohusika na mateso yetu, na hasa Wayahudi na Wakristo.
Baada ya kuachana, baadaye mke wangu huyo wa zamani alikuja kuniambia kuwa amembatiza mwanangu. Nilikasirika mno kiasi kwamba nilienda kuingia moja kwa moja kanisani, nikamtukana mchungaji aliyefanya ubatizo ule, na nikamwambia kuwa angeenda jehanamu kwa sababu ya kitendo kile. Sikutaka kabisa mwanangu akue akiwa Mkristo!. Matokeo yake nilipigwa marufuku na mahakama kumtembelea mwanangu maana mke wangu alihofia kuwa ningeweza kuja kumteka mwanangu na kumpeleka Palestina. Hivi sasa sipati nafasi ya kumuona mara kwa mara.
Uzoefu wangu wa pili kuhusiana makanisa ulikuwa ni chuoni wakati mimi na rafiki yangu wa kike wa Kiarabu tulianza kujadiliana juu ya uwezekano wa kuwa Wakristo kwa kuwa tu tuliona ni dini isiyo na masharti magumu. Tulijua kuwa kile tulichokuwa tunakifanya ni kibaya na adhabu ya kuuacha Uislamu ni kupigwa mawe, lakini tulikuwa tunahitaji itikadi itakayohalalisha maisha yetu ya dhambi. Kutokana na ukaribisho tuliopata kutoka kwa msichana mmoja Mkristo wa Kiarabu kutoka pale chuoni, tulienda kutembelea kanisa lake Jumapili moja. Ibada ilikuwa imejaa furaha, jambo ambalo sikuwahi kuliona kwenye Uislamu. Baada ya ibada, tulipatiwa Biblia na kitabu kinachohusu Uungu wa Yesu Kristo. Miezi michache baadaye wakati wa mkesha wa Krismasi, tulitafuta kanisa ambako baadhi ya marafiki zetu wa Kiarabu walio Wakristo kutoka chuoni kwetu walituambia habari zake. Lakini tulishangaa kukuta limefungwa.
Nilikuwa na rafiki yangu aitwaye Khalil, ambaye tulikuwa tunazungumza pamoja juu ya maisha na hali ya dunia. Wakati mwingine tulikuwa tukijiuliza maswali kuhusu Uislamu na kushangaa kwa nini mambo ni hovyo sana kwenye nchi za Kiislamu. Tulikuwa tukijiuliza iwapo dini hii, ambayo hata hatukuifuata kikamilifu, ilikuwa ni dini ya kweli. Lakini maswali yetu hayakutufanya tufanye uamuzi wa mara moja.
Nilioa tena. Safari hii ilikuwa ni ndoa ya kupangwa. Nilioana na msichana mmoja kutoka Palestina. Hii ilitokea baada ya familia yangu kunikatalia katakata kumuoa msichana wangu wa chuoni wakidai kuwa hakuwa safi kiasi cha kutosha kwa ajili yao. Nilimleta mke wangu mpya hadi Marekani, lakini nilikuta ni vigumu sana kumpenda maana hata sikuwa namfahamu vizuri. Kwa hiyo, nilikuwa nafurahi kwa sababu kazi yangu ilikuwa inanifanya niende mji hadi mji. Hiyo iliniwezesha kufanya mambo yangu ambayo hata hakuna haja ya kuyasema (ikiwa ni pamoja na kuwa na msichana kwenye kila mji.
Kisha Septemba 11, 2001, ilitokea. Majengo pacha ya ghorofa yalipoanguka [kule Marekani baada ya kulipuliwa na ndege zilizobamizwa humo], heshima kidogo iliyokuwa imesallia kwangu juu ya Uislamu nayo iliporomoka yote. Suala hili lilinisukuma kabisa kwenye kuanza kuitafuta Kweli.
Niliachishwa kazi kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyosababishwa na tukio la 9 -11. Wakati nikiwa kwenye mtandao wa intaneti kila siku kutafuta kazi, “kwa namna fulani”, kila mara nilijikuta nikiangukia kwenye mitandao ya majadiliano ya Kikristo. Na hata siku moja niliweza kupata Biblia ya Kiarabu kwenye mtandao.
Usiku mmoja wakati wa majira ya baridi nilijikuta nikisoma Injili ya Yohana. Sikuwa nikiiamini Biblia hata kidogo, maana nilikuwa nimefundishwa maisha yangu yote kuwa Biblia ni kitabu ambacho kimebadilishwa na wanadamu.
Lakini nilipoanza kusoma, nilishangaa. Nilianza kusoma juu ya Yesu na maisha yake mazuri, safi, yasiyo na dhambi, matakatifu, ya kushangaza, na ya kimiujiza, na sikuweza kuiweka Biblia ile chini. Nakumbuka nilisoma Injili ile yote mwanzo hadi mwisho. Nilipomaliza kusoma, ilikuwa tayari ni alfajiri! Nilikuwa nalia sana kiasi kwamba niliogopa kwamba ningemuamsha mke wangu. Sikutaka anione nikilia ili asije akaniuliza ni kwa nini ninalia.
Siku chache baadaye, nilifungua kompyuta yangu, na kwa sababu nisiyoijua, nikawa natafuta makanisa ya Kiarabu yaliyo kwenye eneo lile. Hatimaye nilipiga simu kwenye kanisa mojawapo. Upande wa pili, simu ilipokelewa na aliyepokea akaniambia kuwa baba yake alikuwa ndiye mchungaji, lakini alishakufa. Alinipatia namba nyingine ya kupiga – kwa mtu aliyeitwa Farooq. Huyu bwana ndiye mchungaji wangu hadi sasa na ni mtu ambaye Bwana amemchagua awe wa kunifikisha kwake. Tulijadiliana mambo mengi ya ndani kama vile tabia na haiba ya Muhammad, maisha yake, wake zake wengi aliooa na vita alivyopigana. Farooq alinipatia kitabu alichoandika ambacho kinalinganisha Uislamu na Ukristo, kikiwa na rejea kutoka kwenye Quran na Biblia.
Nilipoanza kusoma kitabu cha Farooq, nilipatwa na mshtuko pamoja na mshangao. Nilizitafuta rejea zote za Biblia na za Quran – zote zilikuwa sahihi – na sikuamini macho yangu! Nilitambua kuwa kumbe nilikuwa nimedanganyika maisha yangu yote! Jambo kubwa lililonivuta lilikuwa ni tofauti ya jinsi dini hizi mbili zinavyowatendea wanawake.
Sikumbuki siku hasa ambayo Farooq aliniongoza kuomba sala ya kumpokea Bwana na Mwokozi, lakini ilikuwa ni kwenye mapema mwaka 2002. Ninaikumbuka fika siku niliyobatizwa. Ilikuwa ni siku ya ajabu sana na pia iliniogopesha! Na hivi sasa nimeshakuwa mtu tofauti sana tangu nilipomkubali Kristo. Niko huru! Nimeshatambua kuwa hakuna kamwe ulinganifu kati ya Ukristo na Uislamu. Pale ambapo mwanzoni nilikuwa nina sheria na taratibu nyingi za kufuata kutoka kwenye Quran na Hadithi, hivi sasa nina uhusiano na Mungu. Ni tofauti kabisa. Uislamu unategemea kulazimisha, lakini Ukristo unaleta amani na upendo mwingi sana. Hivi sasa mimi ni mtu tofauti kabisa. Nimejitoa kikamilifu kwa mke wangu na ninaendelea kujifunza kumpenda. Hivi sasa, badala ya kwenda kwenye starehe, ninasoma Biblia. Ninahudhuria kanisani na kwenye masomo ya Biblia kila ninapoweza. Na sina chuki tena dhidi ya Wayahudi.
Nimekuwa nikimweleza karibu kila mtu ninayekutana naye huu ushuhuda wangu na imani yangu. Nilishawaeleza familia yangu, wafanyakazi wenzangu, na hata watu tu wa mtaani. Familia yangu hawakufurahia sana, hususani mke wangu ambaye bado hataki kukubali kwamba nimeshabadili dini. Anadhani kuwa iko siku fahamu zangu zitanirudia hivyo nitarudi kwenye Uislamu. Familia yangu, kwa upande mwingine, walijaribu kunirudisha kwenye Uislamu kwa njia ya hoja na mijadala juu ya Uislamu na Ukristo, baadaye wakaamua kunipuuza. Lakini hatimaye wakafika mahali pa kukubaliana na hali yangu kutokana na uhusiano mzuri na wa upendo tulio nao. Kama tungekuwa bado tunaishi Palestina, nina uhakika kuwa wangeshanikataa au hata kutishia maisha yangu.
Tuesday, August 4, 2015
UISLAM NI DINI YA MAKAFIRI
Hakuna ubishi katika hili, kuwa Dini inayo thibitisha kuwa wao ni Makafiri ni ya Uislam.
Nini Maana ya Kafiri?
Neno Kafir limetoka katika neno "Kafara" likiwa lina maanisha kupinga Mungu, kuficha , kukataa au kufuru . Kwa hiyo, kaafir ni Mtu au Kiumbe au Roho au Malaika au miungu anaye kufuru, anakataa au anakanusha.
USHAHIDI WAKUPINGA MUNGU KATIKA UISLAM
Shahada: LA ILAHA ILLALLAH Muhammadur Rasulullah, Quran 3:18 na soma hapa pia (Sahih Al-Bukhari, Volume 4, Book 56, Number 725)
Hakuna Mungu ila Allah na Muhammad ni Mtume wa Allah. Hii ni Shahada wanayo sema Waislam au mtu anaye taka kuwa Muislam.
Hii Shahada katika Surat Ali Imran inasema kuwa Hakuna Mungu ila Allah. Huu ni mtego ambao Ibilisi anautumia kwa hwa Waislam na wanakanusha kuwepo na au uwepo wa Mungu. Zaidi ya hapo, Waislam wanakanusha na au ficha ukweli kuwa Yesu ni Mungu.
Hivyobasi, kufuatana na ushahid yakinifu hapo juu wa SHAHADA ya LA ILAHA ILLALLAH Muhammadur Rasulullah, leo tumejifunza kuwa Allah wa Waislam na Mtume wake na Waislam wote wanapinga uwepo wa Mungu na kufanikiwa kuwa MAKAFIRI kutokana na maana ya KAFIR katika Uislam.
Ngoja niweke maana ya hiyo SHAHADA neno kwa neno:
Maneno hayo manne "lâ ilâha illâ allâh" yana maanisha hivi:
:
lâ = HAKUNA, no, not, none, neither
ilâha = MUNGU, a god, deity, object of worship
illâ = ISIPOKUWA but, except (illâ is a contraction of in-lâ, literally if not)
allâh = ALLAH, allâh
Kama tulivyo soma hapo juu maana ya hayo maneno Manne. Utangundua kuwa Neno ILAHA maana yake ni MUNGU na Neno ALLAH halina Tafsir na kubakia ALLAH (Thibitisha kupitia Al Tafsir Kitengo cha Tafsir cha Serikali ya Saudi Arabia/ http://www.altafsir.com/).
Huo ndio mtego wenyewe. Kumbuka Allah hana wa kufananishwa na au linganishwa. Hivyo Kumfananisha Allah na Mungu wa Buddah, au Mungu wa Rasta Fari au na Mungu wa Wabantu ni KUKUFUR. Allah yeye kasema hana wa kufananishwa wala linganishwa. Kumbe basi Allah sio Mungu.
Allah Anasema:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
"Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona."
Ash-Shuuraa – 11
Hivyo basi, Allah ni Kafir. Muhammad ni Kafir na Waisla wote ni Makafir maana wote wanapinga Uwepo wa Mungu kwa kusema Shahada.Tusome Biblia na tuone inasemaje kuhusu mtu anaye sema hakuna Mungu:
Biblia inasema: Zaburi 14: 1; Mpumbavu asema moyoni mwake hakuna Mungu wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo hakuna atendaye mema.
Jibu mmesha pata kuhusu mtu yeyote yule (na/au kiumbe chechote kile) anayesema hakuna Mungu.
Leo tumejifunza kutoka Uislam kuwa, MAKAFIR ni WAISLAM na sio Wakristo wanakubali Mungu.
Mungu awabariki sana,
Karibu kwa Yesu aliye hai na Mungu Mkuu,
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
Monday, August 3, 2015
USHUHUDA: MWANASHERIA MKUU WA SHERIA ZA KIISLAM WA IRAKI AMPOKEA YESU
BADO
HUJASTAHILI
KUTOKA:
KWENYE GIZA LA UDANGANYIFU WA KIISLAMU
HADI:
KWENYE NURU YA UTUKUFU WA YESU
-UKWELI-
Ushuhuda wa Lazaro
Nakala ya Bure
Ni furaha yangu kubwa katika Bwana kwamba nimeweza kukushirikisha ushuhuda wangu binafsi. Jinsi Bwana alivyonichagua mimi na jinsi nilivyokuja kwenye miguu ya Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi.
MAISHA YANGU YA ZAMANI
Mtu fulani aliniuliza, “Mchungaji waweza kunieleza upi ni muujiza mkuu unaoukumbuka katika umri wako huu?” Nikamjibu “katika ufahamu wangu muujiza mkuu katika umri huu ni kwamba katika mwaka 1988 nilikuwa Maulvi (Msomi wa Kiislamu) na leo mimi ni Mchungaji.” Nilisoma kozi ya juu kabisa ya kidini (Maulvi Fazil, Alam Fazil, Fazil-e-Ijaz). Baada ya kuhitimu shahada yangu ya Uzamili ya Sanaa katika Kiarabu kutoka Lahore nilikwenda Iraq kwa masomo ya juu zaidi.
MASOMO YA JUU KULE IRAK NA SAUDI ARABIA
Kutoka mwaka 1974 hadi 1978 nilisoma Chuo Kikuu cha Irak. Nilitunukiwa shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Sheria za Kiislamu katika Kiarabu na Uajemi (Mufti) kwa sababu nilikuwa naenda kuwa Maulana (mufii wa Kiislamu). Lugha yangu ya kwanza ni Punjabi. Nilisoma kwa Kiarabu hadi nikatokea kufanya mitihani ya falsafa ya udaktari (PhD) kwa lugha ya Kiarabu. Pamoja nami katika darasa walikuwepo wanafunzi ambao lugha yao kuu ilikuwa Kiarabu. Nilipata alama 995 kati ya alama 1000 ambapo nilivunja rekodi katika Chuo Kikuu cha Irak hadi siku ya leo(mwaka1995). Nilisoma sheria za kiislam kuanzia mwaka 1978 hadi 1980 katika mji Mtakatifu wa MAKA (Saudi Arabia). Niliteuliwa kuwa mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu nchini Saudi Arabia kuanzia mwaka 1980 hadi 1984.
NCHINI ISLAMABAD KAMA MWANASHERIA MKUU WA MAHAKAMA YA SHERIA
Nilirudi nchini mwangu mwaka 1985 na nikateuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu wa Islamabad (1984-1989). Nilirithi chuki ya kumchukia Kristo na Wakristo kutoka kwa mababu zangu. Niliwatesa Wakristo na nilikuwa kinyume na Yesu. Nilijaribu kwa nguvu zangu zote kukomesha mikutano yao ya dini, niliwaadhibu na kuwanenea mabaya kwa uwezo wangu wote. Kama mtuhumiwa wa Kikristo angeletwa mbele yangu mahakamani, angearifiwa na wanasheria kwamba huyu hakimu atakuhukumu kifo tu. Akijua kuwa wewe ni Mkristo inatosha, hata hitaji maelezo zaidi. Atakapo fungua faili lako na kusoma kwamba wewe ni Mkristo inamtosha kukuhukumu kifo.
YESU NDANI YA OFISI YANGU
Katika asubuhi mwanana ya Aprili 26 mwaka 1989, nilikuwa nimekaa ofisini mwangu nikiwa na katibu wangu (mwanamke) akiwa anafanya shughuli fulani za mambo ya dini. Mara majira ya saa 5.30 asubuhi ofisi yangu ilianza kujawa na mwanga wa ajabu na wa kushangaza ambao ulikuwa mwangavu na unaong’aa kuliko jua. Wakati huo nilikuwa nimefuga ndevu ndefu zilizonifikia tumboni na nywele ndefu zilizonifika mabegani. Katibu wangu alikuwa akihofia mpira huu wenye mwanga usio wa kawaida ambao nuru yake ilizidi kuwa angavu, na alianza kuniuliza mimi “Maulana (msomi wa Kiislamu) ni nini kinachotokea ofisini kwetu?” Mimi binafsi nilikuwa naogopa na ili kuficha woga wangu nilimwambia aende nje ya ofisi. Baada ya dakika chache ule mwanga ulitoweka, lakini katikati ya ofisi yangu nilimwona mtu aliyekuwa amesimama. Na ndevu za rangi ya dhahabu na nywele za rangi ya dhahabu ndefu hadi mabegani akiwa amevalia vazi ling’aalo sana. Nilikuwa nikimtazama ana kwa ana. Alianza kuongea na mimi na kuniambia “Angalia Maulana umenitesa mno lakini upo kwenye mipango yangu tangu milele” Niliwaza huyu alikuwa Malaika wa Mauti na leo ndio siku yangu ya mwisho ulimwenguni. Nilikuwa nikitetemeka ndani yangu na kuyaogopa sana haya mazingira kwa sababu nilikuwa na uhakika huyu alikuwa Malaika wa Mauti na kwamba leo ndio mwisho wangu duniani. Katika hofu yangu ya kutisha nilihisi shinikizo kubwa ndani ya nafsi yangu na nikaanza kumlalamikia. Nikamwuliza “wewe ni nani na umedirikije kuingia ofisini mwangu? Walinzi wa usalama wako wapi? Kwanini hawakukuzuia? Unataka nini toka kwangu?” Ndani ya sekunde moja nilimwuliza swali zaidi ya moja. Nikamwambia, “Jitambulishe” Akajibu “Nimekukomboa wewe (Fidiya) na kujitoa sadaka kwa ajili yako (Qurbani), wakati neno “kujitoa sadaka” (Qurbani) linapozungumzwa linaeleweka kirahisi zaidi na Muislam. Kwa mujibu wa sadaka Hazrat-I-Ibrahim (Abraham) ya kumtoa mwanae Ishmael kutokana na Imani ya kiislam. Nilitiwa moyo na jibu hili na kwa haraka nikamwuliza “Je, wewe ni Hazrat-I-Ibrahim aliyemtoa sadaka mwanae Ishmael?” Akajibu “Hapana nimeyatoa maisha yangu kwa ajili yako na kwa ulimwengu mzima msalabani (Saleeb) lakini wewe umenitesa mno. Hii ndio sababu Mimi mwenyewe nimekuja nikufanye uwe wangu.”
Nikiwa kama Msomi wa Kiislamu sikuwahi kusoma Biblia au maandiko mengine yeyote ya Kikristo na wala sikuwa na hamu na Kristo wala Ukristo. Lakini baada ya kusikia neno ‘msalaba’ (saleeb), niligundua kuwa huyu ni nabii ISSA (Yesu). Nikawaza moyoni mwangu, “Huyu ni mtu wa namna gani? Ninamtesa, ninamtukana na kumnenea maneno mabaya na yeye binafsi anakuja ofisini mwangu.” Kwa kila mtu kuna moyo wa ndani uitwao dhamiri. Sauti yangu ya ndani ilikuwa ikiniambia “Maulana acha usumbufu wako, yule unayemtesa anaongea na wewe. Achana na usumbufu wako na uadui na umpokee Yeye.”
Namshukuru Mungu kwamba sikumpokea Kristo baada ya kusoma Biblia au baada ya kuzidiwa nguvu na wasomi wa Kristo kwenye mdahalo. Mshahara wangu kwa mwezi ulikuwa rupia za Pakistani 120,000 (kadiri ya dola za Marekani 3,000). Mshahara wangu ulikuwa ukitumwa kwangu moja kwa moja kutoka Falme za Kiarabu za Saudia. Mimi nilikuwa ni mtu niliyezoea kulala peke yangu kwenye kitanda kikubwa (master bed). Haikuwa rahisi kwangu kukalia kochi la mtu mmoja. Nilikuwa mkubwa sana kiasi kwamba walizoea kunitengea kochi la watu wawili nikalie. Kwa kitambo niliwaza juu ya faraja na anasa zote ulimwenguni nilizokuwa nikizipata kama Mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu ndipo nilipomjibu “Sikuamini, sina chochote cha kufanya na wewe wala msalaba wako.”
DINI YANGU YA ZAMANI NA UDHURU
Nilimpa udhuru mwingi kulingana na imani yangu na nilimwambia nabii wangu ni mkuu kuliko manabii wote. Lakini Akaniambia “Njoo toka nje ya ofisi yako.” Sielewi jinsi nilivyokwenda kwenye ubaraza wa ghorofa nikipaa pamoja naye angani, kisha toka kwenye ubaraza wa ghorofa nikaona mbingu zimefunguka. Akanionyesha Nabii wangu na vitu vingi vinginevyo. Kisha tukarudi ofisini na akaniambia. “Inabidi unifuate, nataka nikufanye mtumishi wangu, nataka nikufanye shahidi wangu.” Dhamiri yangu ikaanza “Maulana mpokee, ni kweli yeye ni Mkuu na mtukufu. Kubali ukweli huu kwamba wewe upo kinyume nae na umemtesa lakini anakupenda.” Nikamjibu “Sawa Issa Masih, kuanzia leo na kuendelea wewe ni wangu na mimi ni wako.” Na huyu Issa Masih akaenda zake toka ofisini mwangu kwa njia ile ile aliyojia.
KUJIUZULU KWANGU
Mara moja niliandika barua ya kujiuzulu na kuituma Saud Arabia kwa njia ya fax. Baada ya kupokea fax yangu Imam wa Khana-e-Kaba, Sheikh Abdala, alipanda ndege ya kwanza na kuja Islamabad na akaja moja kwa moja ofisini mwangu. Aliniuliza kwa mshangao mkubwa katika lugha ya kiarabu “Je, wewe si kichaa?” Nikamjibu, “Mimi sio kichaa lakini mimi ni Mkristo.” Alifahamu vyema kwamba natoka katika familia ya Kiislamu ambapo wote ni wasomi wa Kiislamu, na kwamba mimi ni wa 8 katika mlolongo wa wasomi wa Kiislamu baada ya baba yangu na mababu zangu waliotutangulia. Ndipo Sheikh akatoa amri kwa wenye mamlaka, “Anapaswa kuadhibiwa vilivyo kwa sababu ameukataa Uislamu na mtume wetu, kama akienda nje na kuwaeleza watu wengine imani yake mpya, itakuwa kufuru kwetu sisi. Mpeni wakati mgumu gerezani ili kwamba kwa wakati ujao asiwepo yeyote atakaye diriki kutumia jina hili ‘Ukristo’ tena.”
MATESO KWA KUMPOKEA YESU
Mara moja nilikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. Usiku walinipeleka mahabusu. Nilipigwa kikatili sana kule jela na asubuhi nikaambiwa “Oh maulana, kujiuzulu kwako hakujakubaliwa. Tafadhali rudi kwenye kiti chako na uendelee na kazi yako” Nikajibu, “Hapana mimi ni Mkristo”
JINSI FAMILIA YANGU ILIVYOLICHUKULIA
JAMBO HILO
Baba yangu alifariki mwaka 1978 lakini wakati hayo yaliponitokea mama na kaka yangu walikuwa bado hai. Kwa sasa wote wawili wameshafariki. Walikuja gerezani na walisema, “Tumekupatia elimu nzuri namna hii na kutumia hela zetu nyingi kwa ajili yako. Tulikupeleka Irak kwa ajili ya masomo ya juu, kwanini sasa unaenda kuwa kafiri? (neno linalotumika kwa wale wanaoukataa uislam). Tafadhali rudi ofisini kwako uchukue nafasi yako.” Nikajibu, “Amme (mama) Hapana. Tangu jana nimekuwa Mkristo.” Shangazi yangu aliyekuwa amesimama pamoja nao alianza kunitukana. Alidhani labda nikishasikia maneno hayo mabaya ningerudi nyuma kwenye Uislamu. Alisema “Mpeni ndoo ya takataka na ufagio mrefu mikononi mwake halafu mwacheni akaishi na wafagizi (Wakristo).” Kwasababu Waislamu wengi wa Pakistani hudhani Wakristo ndio wafagizi, lakini wanasahau kwamba hata kule Saudia Waislamu hufanya kazi ya ufagizi na kazi nyingine nyingi za ajira ndogo. Nikamjibu, “Kama ni kwa ajili ya Masihi (Kristo) natakiwa kuifanya kazi hii nitaifanya. Kwa sababu yeye alikuja kwangu moja kwa moja na kuongea nami, alinionyesha utukufu wake na nguvu iliyopo Mbinguni ambayo sasa inakaa katika chembechembe zote za damu yangu. Sasa Anaishi ndani yangu siwezi kumwacha.” Wakasema “sawa” na wakaondoka.
KULE GEREZANI
Adhabu yangu ya kwanza ilianza kwa kucha za vidole vyangu kunyofolewa kwa kuvutwa. Baada ya kupigwa kwa mara ya pili nilipelekwa hospitali. Pale hospitalini nilipewa maumivu mengine makali ya akili. Nilisikia kwamba mke wangu na mtoto wote wawili walikufa kwenye chumba cha uzazi wakati wa kujifungua. Kwanza madaktari walikuwa wakijaribu kuokoa maisha ya mtoto na ndipo wakati huo mke wangu alipofariki. Kisha baada ya masaa 4 mtoto wangu naye akafariki. Ndugu zangu wote, majirani na marafiki walikuja wakaniambia, “Unaona, Allah amekuadhibu. Mkeo na mtoto wamekufa. Kucha zako zimenyofolewa. Lakini bado muda wa kurudi nyuma upo.” Jibu langu pekee lilikuwa, “Hapana sasa anaishi ndani yangu.” Kwa wakati ule sikuwa najua kwamba huu ulikuwa mstari wa Biblia kwa sababu hakukuwepo mtu katika familia yetu nzima aliyekuwa anaifahamu Biblia. Hata mimi kama msomi wa kiislamu sikuwahi kujifunza ama kusoma Biblia. Kwa sasa nalijua andiko linalosema,“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Mungu hukaa ndani yenu” (1Kor 3:16).
Pili nilikuwa nimening’inizwa miguu yangu ikielekea chini lakini si kwa kamba wala minyororo. Safari hii walizitumia nywele zangu ndefu, na nilikuwa nikibembea mle chumbani kama mpira. Uzito wangu wote ulikuwa katika nywele zangu. Nilining’inizwa namna hii hadi damu kutoka kichwani ikaanza kudondoka sakafuni. Unaweza kufikiria wazi kwamba damu ili idondoke sakafuni nguo zangu zote zilikuwa zimeloa damu. Walidhani ningekufa kwa sababu kutokana na mateso uso, macho yangu yalivimba hadi macho yalifunikwa kabisa. Nilikuwa mnene na aliyezidiwa uzito, nilikuwa siwezi kufumbua macho yangu au hata kumwona mtu. Tena waliniuliza, “Sasa Maulana unawaza nini kuhusu dini yako mpya?” Nikawajibu, “Kristo ni wangu na mimi ni wake.” Leo sisi ni watumwa wa mapokeo ya wahenga wetu. Pale ambapo wahenga wetu walitufikisha, hatutaki kupaacha, wala dini zao. Hata hivyo wahenga wangu wote walikuwa Maulvi na wasomi wa Kiislamu na kwa sababu ya hilo ilikuwa ngumu kwao kumpokea Yesu.
KUVUNJWA MBAVU
Nilikaa miaka miwili katika gereza la Hari Pur Hazara. Mshtuko mkubwa wa tatu ambao niliupata gerezani ni kwamba mbavu zangu zote za pande mbili zilivunjwa kwa mateke ya askari polisi na maofisa. Naweza kukuonyesha mbavu zangu na mtu yeyote aliye na taaluma ya udaktari anaweza kuzikagua mbavu zangu wakati wowote. Baada ya kuzivunja mbavu zangu na kunipiga mateke bila huruma wakasema tena, “Tutakugharamia matibabu yako yote na tutakupeleka hospitali kama utarudi kwenye Uislamu.” Nikajibu, “Wala kamwe msiniambie jambo hili tena. Lolote mnalotaka kunifanyia mnaweza kufanya lakini siwezi kusikiliza maneno yanayonitaka nirudi nyuma kwenye dini yenu ya kizamani. Hata kama ningetaka kurudi nyuma siwezi kurudi nyuma kwa maana Yesu anaishi ndani yangu siwezi kumwacha.” Nilipelekwa hospitali madaktari waliamua kunifanyia upasuaji na walikuwa wakipanga kuniwekea vitu fulani kama chuma ambavyo vingekaza mbavu zangu tena. Wangenipeleka kwenye chumba cha upasuaji asubuhi ambayo ingefuata. Jinsi nilivyokuwa na maumivu makali ya kufa, ilipofika saa 10:30 alfajiri nilimwona Yesu Kristo tena ana kwa ana akiwa amesimama upande wangu. Nikamwambia, “Masihi (Yesu) wamenipiga na kunitesa bila huruma.” Yesu akajibu, “Bado hujastahili kunitumikia.” Nilifadhaika sana kwamba niliacha nafasi kubwa ya heshima kubwa namna ile, mke wangu na mtoto wamekufa, nimeiacha familia yangu, mali zangu zote zimechukuliwa, kucha zangu nazo zimeng’olewa, nilitundikwa kutumia nywele zangu, sasa hata mbavu zangu zimevunjwa na kile Yesu anachoniambia ni kitu kisicho cha kawaida kabisa.
YESU NI MPONYAJI
TOFAUTI KUBWA KATI YA MUHAMMAD NA YESU KRISTO
Tofauti Kati ya
Muhammad na Kristo
YESU DHIDI YA MUHAMMADI
UKRISTO DHIDI YA UISLAM
Muhhamad alikuwa nabii wa vita, Kristo ni Mfalme wa Amani. (Issa 9:6-7).
Wafuasi wa Muhammad waliua kwa ajili ya imani, wafuasi wa Kristo waliuawa kwa ajili ya imani (Mdo 12:2, 2TIM.4:7).
Muhammad alieneza mateso dhidi ya “makafiri” Kristo aliwasamehe na kumgeuza mtesaji mkuu (1TIM.1:13-15).
Muhammad alikuwa mwondoaji uzima, Kristo alikuwa mpaji uzima (Yn.10:27-28). Muhammad na wapiganaji wenzake waliua maelfu, Kristo hakuua mtu yeyote bali aliokoa wengi (linganisha Yn.12:48).
Kanuni za Muhammadi zilikuwa KULAZIMISHA. Kristo alilenga KUGEUZA kwa hiari.(Mdo3:19).
Muhammad alitumia nguvu; Kristo alitumia IMANI (Yn.6:29,35)
Muhammad alikuwa MTU WA MAPAMBANO. Kristo alikuwa MKOMBOZI. (Kol. 1:13, 1The.1:10)
Muhammad aliwashinda maadui zake kwa upanga, Kristo aliwashinda maadui zake kwa upanga wa namna nyingine upanga wa Roho ambao ni Neno la Mungu (Ebr.4:12 Mdo 2:37)
Muhammad aliuambia umati “Silimuni ama mfe” Kristo alisema “Aminini na muishi (Yn.6:47, 11:25-26)
Muhammad alikuwa mwepesi kumwaga damu za watu (Rum 3:15-17). Kristo alimwaga damu yake mwenyewe kwa ajili ya wokovu wa wengi. (Efe.1:7)
Muhammad alihubiri “kifo kwa makafiri”, Kristo aliomba “Baba,uwasamehe kwa maana hawajui watendalo” (Lk.23:34)
Muhammad alitangaza vita takatifu (jihad) dhidi ya makafiri, Kristo alipata ushindi mtakatifu juu ya msalaba pale Kalvari. (Kol.2:14-15) na wafuasi wake walishiriki ushindi huo (Yn 16:33)
Muhammad aliwaamrisha watu wake kwa kuwalazimisha, Kristo aliwaamrisha watu wake kwa upendo (2Kor 5:14)
Magaidi wa siku hizi walipata msukumo huo kutoka kwa Muhammad na kutekeleza uovu wao kwa jina la mungu wao Allah, Wakristo walipata msukumo huo kutoka kwa Mmoja aliyesema “Heri wapatanishi…” (Mt.5:9)
Baadhi ya wafuasi wa siku hizi wa Muhammad waliitikia shambulizi la kigaidi kwa shangwe mitaani; wafuasi wa siku hizi wa Kristo walihuzunishwa sana kwa tukio lililopita la kikatili lililofanywa na wale ambao walikuwa “Wakristo” kwa jina tu (vita vya kidini na kihispania kukomesha uasi)
Waislam wengi wana amani na wanapenda amani kwasababu hawafuati kikamilifu mafundisho ya mwanzilishi wao; Wakristo wengi wana amani na wanapenda amani kwasababu wanafuata kikamilifu mafundisho ya mwanzilishi wao (Rum.12:17-21)
Muhammad aliwaita watumishi wake kupigana Yesu alisema, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu; kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu; watumishi wangu wangenipigania… lakini ufalme wangu sio wa hapa (Yn.18:36)
VIPEPERUSHI JIHAD AU VITA TAKATIFU, UVAMIZI WA KIISLAMU
Hadithi inafichua kwamba Muhammad alipenda dini yake ienezwe kwa Upanga.
UISLAM MPYA, NYUMA YA PAZIA
Uislam ambao Waislam wanaosilimisha hutambulisha katika nchi za Magharibi ni tofauti kabisa na Uislam uliopo Mashariki ya kati.
Kurani inasema “Pigana kwa ajili ya Allah” (Koran 2:244). Biblia inasema “Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama” na silaha za vita vyetu si za mwili” (Efe.6:12, 2kor.10:4)
Korani inasema “Piga na chinja wapagani popote unapowaona” (Koran 9.5). Kristo alisema “Hubiri injili kwa kila kiumbe” (Mk 16:15)
Koran inasema “Nitatia woga ndani ya mioyo ya wasio amini” (Korani 8:12). Mungu hutia hofu yake (uchaji, heshima, utisho na unyenyekevu) ndani ya moyo wa waaminio (Isa.8:13)
Korani ni kitabu cha mwongozo wa kigaidi ambacho kinaafiki mapigano, migogoro,ugaidi,unyonyaji na mauaji ya halaiki dhidi ya wale wasiokubali Uislam; Biblia ni kitabu cha mwongozo wa wito wa kueneza injili ya amani duniani kote(Rum.10:15)
Kazi ya Muhammad ilikuwa kushinda ulimwengu kwa ajili ya Allah; kazi ya Kristo ilikuwa kushinda nguvu ya dhambi na adhabu kwa kulipia kosa badala yetu (2kor.5:21; 1Pet.3:18)
Muhammad alimtambua Kristo kama nabii mzuri; Kristo alitamka Muhammad kama nabii wa uongo (Yn,10:10;Mt.24:11)
Muhammad alidai kulikuwa lakini Mungu mmoja, Allah; Kristo alidai kuwa alikuwa Mungu (Yn.10:30-31,Yn.8:58-59,Yn:5:18,Yn.14:9)
Kaburi la Muhammad: BADO ANALIMILIKI
Kaburi la Kristo:TUPU.
KATIKA VITA DHIDI YA DINI YA
UWONGO YA KIISLAMU
KAMA UNGEPENDA KUFAHAMU ZAIDI.TAFADHALI OMBA MATOLEO YETU MBALIMBALI JUU YA UISLAM. ZANA ZA NGUVU AMBAZO ZITAKUONGEZEA UFAHAMU WAKO WA UISLAMU NA VILEVILE KUKUSAIDIA KUSHUHUDIA WAISLAMU KIKAMILIFU ZAIDI. SAIDIA KUWAWEKA MATEKA HURU.
NI BURE KAMA UKIOMBA.
VIJITABU
UISLAMU UMWAGAJI DAMU.
Utumwa katika Uislamu
Utumwa katika Uislamu
Watu wote wa kale ikiwa ni pamoja na wanazuoni wa siku hiziwanakubali ukweli wa utumwa katika Uislamu na kubainisha hadhi waliyonayo watumwa hao. Wanazuoni wote wa zamani na hata wa siku hizi wanakubaliana na ukweli wa Utumwa katika Uislamu, na kufafanua hali halisi ya hadhi ya watumwa. Nimechagua maoni ya wanazuoni maarufu kuliko wote ili kuonyesha nuru na misimamo yao.
Wakati tunaposema kwamba Uislamu hauamini katika haki za binadamu na wala hautambui uhuru wa wa watu binafsi, watu wengi hubisha.
Tena vita ambavyo Mohammed na wafuasi wake walipigana vilikuwa ni vita vya uvamizi ili kueneza Uislam kwa nguvu, kupora utajiri wa nchi, kutwaa mali za nchi, na kuwateka kinamama na watoto.
Tunakutana na umati wa watu ambao wanaelezea mshtuko wao na kutokubaliana. Kwa sababu ya kuto kuamini huko, vyanzo vyetu vya taarifa vitakuwa wasomi wa Kiislamu.
Msomi wa Al-Azhar wa Misri
Katika kitabu chake “You Ask and Islam Answers”, (Wewe Uliza na Uislamu Ukujibu), Abdul-Latif Mushtahari ambaye ni Mwangalizi Mkuu na Mkurugenzi wa Kuhutubia na Kuongoza katikaChuo Kikuu cha Azhar anasema (uk 51, 52),
“Uislamu haukatazi utumwa ila unashikilia kwa sababu mbili;
Sababu ya kwanza ni vita (Iwe vita ya wenyewe kwa wenyewe au vita na watu wa nje ambapo mateka wanauwawa au kufanywa watumwa) ilimradi tu vita si ya Waislamu wakipambana wenyewe kwa wenyewe- hairuhusiwi kuwafanya watumwa wavunja sheria au wakosaji kama wao ni Waislamu. Ni wale mateka wasio Waislamu tu wanaoweza kuuwawa au kufanywa watumwa.
Sababu ya pili ni watumwa watokanao na udhalilishaji utokanao na kuwaingilia watumwa hao kingono njia ambayo huweza kumpatia mwenye watumwa watumwa wengi zaidi.’’
Habari hii iko wazi kabisa kwamba wafungwa wote wa kivita lazima wauwawe au wafanywe watumwa.
Wanazuoni wa zamani wanakubaliana kabisa na swala hili kama Ibn Timiyya, Ibn Hisham, Malik, nk.Ibn Timiyya anasema,
(Toleo 32, uk 89)
“Mzizi wa mwanzo wa utumwa ni wafungwa wa kivita. Bonasi (zawadi) imekuwa halali katika taifa la Mohammed.”
Kisha (Toleo 31, uk 380) anaonyesha wazi na bila aibu,
“Utumwa ulihalalishwa kwa sababu ya vita yenyewe; hata hivyo si ruhusa kumfanya Mwislam aliye huru kuwa mtumwa. Inaruhusiwa kuwaua makafiri au kuwafanya mateka na ni halali kuwachukua wazaliwa wake kama mateka”
Katika sehemu ya 4 uk 177 , maelezo ya maisha ya Mtume. (Al Road Al-Anf), Ibn Hishamanasema,
“Kutokana na sheria za Kiislamu zinazohusu wafungwa wa kivita, uamuzi umebakia kwa Maimamu wa Kiislamu. Wanao uchaguzi wa kuwaua au kubadilishana mateka wa Kiislamu au kuwafanya watumwa.
Hii inahusiana na wanaume, lakini wanawake na watoto hawaruhusiwi kuuwawa, lakini ni lazima wabadilishwe (kuwakomboa waislamu mateka) au kuwafanya watumwa kuwachukua kama watumwa na wajakazi”
Hii ni kauli ya Ibn Hisham ambaye kwake wasifu wa Waislamu wote na wanafunzi wa Mohammed unapatikana. Kusema kweli maswala haya ambayo Ibn Hisham aliyaweka kwenye kumbukumbu yalizoeleka na kufanyika mfululizo katika vitavyote vya Mohammed vya uvamizi.
Watu wote wa Muhammed (wake zake na Muhammad mwenyewe) waliwamiliki watumwa wengi wa kike na wakiume katika kampeni zake dhidi ya watoto wa Qurayza (kabila la Wayahudi), Muhammad aliwauwa wanaume wote (700-800) katika siku moja. Kisha akawagawanya wanawake na watoto miongoni mwa watu wake.
Akina Khalifa kwa vizazi vingi wamekuwa wakizifuata nyayo za Mohammed na kuwafanya watumwa (kwa mamia na maelfu) wanaume na wanawake waliotekwa vitani. Wengi wao wakiwa Waajemi na watu wa himaya ya Byzantines.
Waislamu wote ambao wamekuwa wakipanga matukio kutoka nyakati hadi nyakati bila kukosa wameziweka katika kumbukumbu kweli hizi zote. Jinsi Waarabu Waislamu walivyovamia Afrika na kuwaua na kuwafanya Waafrika watumwa inafahamika vizuri ni ukweli ulioko katika historia.
Kwenye toleo la 2, sehemu ya 3 uk 13, Malik Ibn Anas alirudia maandishi kama aliyoandika Ibn Hisham ambaye pia alinukuliwa na Ibn Timiyya na Ibn Qayyim Al-Jawziyya katika kitabu chake“Zad al Ma’ad” (sehemu ya 3, uk 486).
Wote hao walifundisha kanuni zilizo sawasawa na kusema maneno ambayo yote ni yale yale.
Swali hili lilitolewa kwa Ibn Timiyya ambaye alikuwa Mufti wa Kiislamu (Toleo 31, uk 376, 377)
“Mwanaume aliyemwoa mjakazi mtumwa akamzalia mtoto , yule mtoto atakuwa huru au atakuwa mtumwa aliyemilikiwa?”
Ibn Timiyya akasema kwa msisitizo,
|
JIHAD (VITA TAKATIFU)
KUUFAHAMU UANAJESHI WA KIISLAMU ULIOINUKA TENA
Mahojiano na Mama yake Kijana aliyejilipua kwa
MABOMU YA KUJITOA MHANGA
GAZETI MOJA la kila siku litolewalo kwa lugha ya Kiarabu huko Uingereza liitwalo Al-sharq Al-Awsat lilichapisha mahojiano na Umm Nidal, mama yake shahidi (mfia dini) Muhammad Farhat. Wakati wa Intifada ya kwanza Umm Nidal alimficha ‘Imad ‘Aql, kamanda wa kikosi cha jeshi la Hamas “Izz Al-Din Al-Qassan Brigedia” kwenye nyumba ya familia kwa zaidi ya mwaka. Ifuatayo ni dondoo kutoka katika mahojiano:
Swali: Ni kwa vipi wazo la kujihusisha na operesheni ya Fidaai (kujitoa mhanga) lilivyo jengeka ndani ya nafsi ya mwanao, Muhammad?”
Umm Nidal: “Jihad ni amri ya kidini iliyoamriwa kwetu. Ni lazima tuliingize wazo hili katika nafsi za watoto wetu, muda wote... Kile tukionacho kila siku - mauaji ya kinyama (ya watu wengi wasiokuwa na hatia); ulipuaji (wa) nyumba kwa mabomu, - hayo yaliimarika katika mioyo ya watoto wangu wa Kiume, hasa Muhammad, kupenda Jihad na kujitolea mhanga”
Swali: “Je, ulikuwa na wajibu wowote katika kupandikizia roho hii kwa Muhamad?”
Umm Nidal: “Allah asifiwe, mimi ni Mwislamu na naamini katika Jihad. Jihad ni msingi mmojawapo wa imani yetu na hili ndilo lililonitia moyo mimi kumtoa dhabihu Muhammad katika Jihad kwa ajili ya Allah. Mwanangu hakuharibiwa, hajafa, anaishi maisha ya furaha zaidi yangu. Kama mawazo yangu yangekuwa yamefungwa na mpaka wa dunia hii, nisingemtoa dhabihu Muhammad.”
“Mimi ni mama mwenye huruma kwa watoto wangu, nao wananihurumia na kunitunza. Kwa vile nampenda mwanangu, nilimtia moyo afe kifo cha mashujaa wafia dini kwa ajili ya Allah….Jihad ni wajibu uliowekwa juu yetu, na ni lazima tuuchukue. Nilimtoa dhabihu Muhammad kama sehemu ya wajibu wangu.”
“Hili ni jambo rahisi. Hakuna kutokukubaliana (mioyoni mwa wanazuoni) katika mambo haya. Furaha iliyoko katika dunia hii ni furaha ambayo haijakamilika; furaha ya milele ni uzima katika ulimwengu ujao, kupitia kujitoa mhanga. Allah asifiwe, mwanangu ameipata furaha hiyo.”
Swali: “ ‘Imad ‘Aql aliishi pamoja na wewe, na aliuwawa nyumbani mwako. Je,haiba yake ilimshawishi Muhammad?”
Umm Nidal: “Muhammad alikuwa na miaka saba wakati mfia dini ‘Imad ‘Aql alipoishi pamoja nasi nyumbani. Muhammad alijiunga na kikosi cha (Izz Al -Din) Brigedia ya Al-Qassan akiwa na miaka saba. Kuachilia mbali umri wake mdogo alikuwa (ni) msaidizi wa ‘Imad ‘Aql, kamanda wa Al-Qassan katika Ukanda wa Gaza. Wakati ambapo kaka zake hawakuwepo, angechungulia barabarani na kupeleka ujumbe kutoka kwa Aql kwenda kwa Majahidina. Mfia dini Muhammad alikuwa mwanafunzi wa Imad. Muhammad angemsikiliza ‘Imad na kumwangalia akipanga mikakati yake ya mashambulizi.”
|
WAISLAM WANAULIZA: JE, ALIYE TAJWA KWENYE KUMBUKUMBU YA TORATI NI MUHAMMAD AU YESU?
Swali: Katika Kumbukumbu 18:17-18; 33:1-2, na 34:10-11, ni Muhammad aliyetabiriwa hapa, kama baadhi ya Waislam wanavyodai?
Jibu: Kumbukumbu 18:15-18 inasema Mungu atamwinua nabii, kuwa watamsikia, kama Musa kutoka miongoni mwao, miongoni mwa ndugu zao.
Je Yesu alikuwa nabii?
Je Wayahudi walio wengi walimsikia Yesu?
Je Yesu alikuwa mmoja wa Wayahudi?
Je Yesu alikuwa Myahudi?
Je Yesu alikuwa nabii?
Je Wayahudi walio wengi walimsikia Yesu?
Je Yesu alikuwa mmoja wa Wayahudi?
Je Yesu alikuwa Myahudi?
Waislam wanapaswa kutokuwa na shida kuafiki kuwa mistari hii inamfaa Yesu kuliko Muhammad. Kama angalizo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) pia alizungumzia jinsi ambavyo Kumbukumbu 18:15 isivyoweza kuwa inamwongelea mtu mwingine yoyote yule isipokuwa Yesu Kristo kwenye Disputation with Manes sura ya 43 uk.219.
Yafuatayo ni maoni zaidi.
a. Kumbukumbu 33:1-2 inasema "Bwana", na Waislam hawamwiti Muhammad Bwana wao. (Waislam wa ‘Alawite na makundi mengine ya Ghulat wanamchukulia Muhammad kuwa Mungu, lakini maoni hayo siyo kawaida kwa Waislam.)
a. Kumbukumbu 33:1-2 inasema "Bwana", na Waislam hawamwiti Muhammad Bwana wao. (Waislam wa ‘Alawite na makundi mengine ya Ghulat wanamchukulia Muhammad kuwa Mungu, lakini maoni hayo siyo kawaida kwa Waislam.)
b. Kumbukumbu 34:10 kwamba "Wala hakuinuka tena katika Israeli nabii kama Musa." Wasifu huu uliandikwa, huenda na Yoshua, muda mrefu kabla Yesu hajaja.
c. Kumbukumbu 34:10 inasema "uso kwa uso", na Muhammad hajawahi kusema kuwa alipata maneno yake moja mwa moja kutoka kwa Mungu, bali kupitia malaika (Sura 2:97). Yesu aliwasiliana moja kwa moja na Mungu Baba kwa mujibu wa Yohana 1:18 na vifungu vingine.
d. Mstari unaofuatia, 34:11, unasema kuwa hakuna nabii mwingine yoyote aliyefanya miujiza hiyo mikubwa kama Musa. Muhammad, kama ilivyoandikwa kwenye Kurani (Sura 17:90-93) hakuwahi kufanya miujiza kama hii, isipokuwa kusema Kurani. (Kurani inapingana na jinsi mapokeo ya baadaye ya Hadithi yanavyosema.)
e. Kwenye Kurani yenyewe, Sura 29:27 inasema unabii umekuja kupitia Isaka na Yakobo. Kwenye tafsiri ya Yusuf Ali ya Kurani, anasema, "Na tumewapa (Abraham) Isaka na Yakobo, na tumeagiza miongoni mwa wazao wake unabii na ufunuo . . ." Wakati ambapo mabano kwenye jina la Abraham yapo kwenye tafsiri ya Yusuf Ali, neno lote "Abraham" halimo kwenye Kurani ya Kiarabu, na Yusuf Ali aliona haja ya kuongeza neno "Abraham" kwenye maandiko ambayo Waislam wanayaona kuwa ni neno la Mungu.
f. Mwisho, Petro, mtume wa Yesu, alisema andiko hili lilitimia kwa Yesu kwenye Matendo 3:22-26. Mtume Petro alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kujua jambo hili.
1. Ama, Yesu alifanya makosa ya kumruhusu mtu mwongo kama Petro kuwapotosha watu, kwa kwa karibu miaka 2,000, ambao wamekuwa wakijaribu kumfuata Mungu, na Mungu hakuinua kidole kuwaambia watu ukweli.
2. Au, Yesu alijua alichokuwa anafanya wakati alipomchagua Petro, na Mungu hakusahihisha kitu ambacho hakikihitaji masahihisho yoyote yale.
3. Vinginevyo, Petro hakusema hivyo, na kitabu cha Matendo ya Mitume kilipotoshwa kabla ya maelezo ya maneno hayo ya kwanza tuliyo nayo toka nje ya Biblia yanayoturejesha kwa Yesu, karibu mwaka 138 B.K.
Viongozi wa awali wa kanisa walisema kuwa mstari huu ulimwongelea Yesu. Baadhi yao ni
Justin Martyr 138-165 B.K.
Irenaeus 182-188 B.K.
Tertullian 220-220 B.K.
Origen 225-254 B.K.
Chrysostom 407 B.K.
Justin Martyr alizaliwa karibu mwaka 114 B.K., ingawa watu wengine hudhani mwaka 110 B.K. Apology yake ya kwanza iliandikwa kati ya mwaka 138 B.K. na mwaka 165 B.K. wakati wa kifo chake. Ni dhahiri kuwa alitakiwa kusoma unabii huu unaomwongelea Yesu kabla ya kuandika.
Muislam anaweza kusema kuwa Justin hakukosea tu bali pia manuscripts zote za Agano Jipya ziliunukuu usemi wa Petro kimakosa.
Justin Martyr 138-165 B.K.
Irenaeus 182-188 B.K.
Tertullian 220-220 B.K.
Origen 225-254 B.K.
Chrysostom 407 B.K.
Justin Martyr alizaliwa karibu mwaka 114 B.K., ingawa watu wengine hudhani mwaka 110 B.K. Apology yake ya kwanza iliandikwa kati ya mwaka 138 B.K. na mwaka 165 B.K. wakati wa kifo chake. Ni dhahiri kuwa alitakiwa kusoma unabii huu unaomwongelea Yesu kabla ya kuandika.
Muislam anaweza kusema kuwa Justin hakukosea tu bali pia manuscripts zote za Agano Jipya ziliunukuu usemi wa Petro kimakosa.
Pia, tafsiri kwenye lugha nyingine zilifanywa mapema sana; tarehe za hapo juu si za tafsiri za kwanza, bali ni tarehe za manuscripts za zamani zaidi ambazo zipo leo hii. Hizi zinaaminika kwa sababu zimepita kwenye mtiririko huru ambao watu wanaweza kuutumia kuthibitisha manuscripts za Kiyunani. Mtiririko wote wa manuscripts hizi, kutoka Afrika kwenda Asia, unaafiki kuwa Petro alisema hivi akimwongelea Yesu.
Tazama When Cultists Ask uk.43-44,45-46 na When Critics Ask uk.125-126, uk.131-132, na uk.133 kwa habari zaidi.
Mungu awabariki sana
Max Shimba Ministries Org
Subscribe to:
Comments (Atom)
The Intrinsic Nature of God’s Love
The Intrinsic Nature of God’s Love By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction The declaration of Scripture, “God is lo...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...


