Kuna imani nyingi sana hapa duniani, zingine zinadai kuwa "Hakuna Mungu" eti, kwasababu wameshindwa kuongea nae na au kumwona; Imani zingine zinadai kuwa "Hakuna Mungu" eti kwasababu Sayansi inashindwa kuhakikisha uwepo wake scientifically; Imani zingine zinadai kuwa, kivipi Yesu awe Mungu na biandamu kwa wakati mmoja, zinadai eti, Mungu halali, wala hali chakula, lakini wakati huo huo wanakiri kuwa Mungu anaweza kufanya jambo lolote lile atakalo; Haya yote ni madai ambayo hawawezi kuyathibitisha.
Hebu tusome Biblia:
2 Samweli 2:31-34 na Zaburi 14:1 ‘Mpumbavu amesema moyoni, mwake hakuna Mungu…..’ Mpenzi msomaji naamini unaendelea vema kwa ujumla kimwili na kiroho. Katika mwezi huu nataka niseme nawe juu ya kifo cha kipumbavu.
Mpumbavu ni nani? Kibiblia ni mtu yoyote aliyekataa kuwa na ufahamu au elimu ya Mungu ndani yake. Mtu aliyekataa uwepo wa Mungu au kuwa na Mungu maishani mwake.
Hivyo basi mpumbavu ni mtu ambaye moyoni mwake amesema hakuna Mungu. Mauti inayomkuta mtu ambaye amekana elimu au ufahamu au uwepo wa Mungu katika maisha yake ni mbaya sana, maana mwisho wake ni Jehannam. Mauti inayommkuta mtu kabla hajakubali uwepo wa Mugu katika maisha yake. Kifo kinachomkuta mtu ambaye hajampa Mungu nafasi ya utawala moyoni mwake mwisho wake ni ziwa la moto. Je wewe unataka kuishi milele yote kwenye ziwa la moto?
YESU ANAKIRI KUWA YEYE NI MUNGU KATIKA KITABU CHA UFUNUO:
Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.
Ukikataa kuwa Yesu sio Mungu, basi wewe ni mmoja wa lile kundi la Wapumbavu. Katika Zaburi, tumeambiwa kuwa Mpumbavu kasema kuwa Hakuna Mungu.
Tujifunze kwa Abneri. 2 Samweli 2:22-39 ukisoma vema hapa utaona habari za shujaa mmoja aliyeitwa Abneri. Kwa kifupi Abneri alikuwa;
Kiongozi wa majeshi ya Sauli, mpinzani mkubwa wa Daudi, baadaye alipelekea Daudi kuitawala Israeli yote, Alimwua Asaheli shujaa wa Daudi ndugu yake Yoabu, kiongozi wa majeshi wa Daudi. Na mwishowe Yoabu ndiye aliyemwua Abneri ili kulipiza kisasi cha kifo cha nduguye.
Sasa baada ya kifo cha Abneri, ndipo Daudi akamlilia Abneri akasema, ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu?, mikono yako haikufungwa wala miguu yako haikutiwa pingu; aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.
Ukiendelea kusoma habari hii utaona kwamba siku ile Daudi alikataa kula akimliilia Abneri, akisema hamjui ya kuwa mkuu mmoja, naye ni mtu mkubwa ameanguka leo katika Israeli?
Je kwa mazingira ya leo, mtu anawezaje kufa kifo cha kipumbavu?Unaposhindwa kutumia fursa zilizopo kuiponya nafsi yako matokeo yake ni kifo cha kipumbavu. Abneri hakufungwa mikono wala miguu lakini aliuawa. Daudi alikuwa akimuuliza Abneri kwa nini usitumie mikono na miguu yako kuiponya roho yako? .
Katika Zaburi 14;1 TUMEONA MPUMBAVU NI MTU YULE AMBAYE MOYONI MWAKE AMESEMA HAKUNA MUNGU, kwa lugha nyepesi amekataa kuwa na Mungu moyoni mwake na kwa sababu hiyo amekataa uongozi wa Mugu katika maisha yake.





