Saturday, January 16, 2016

ALLAH, MUHAMMAD NA UISLAM WASEMA NI MARUFUKU KWA MUISLAM KUWA RAFIKI NA MKRISTO

Ndugu msomaji,

Leo ningependa tujifunze kuhusu chuki iliyo ndani ya Allah na dini yake ya Uislam. Wengi wenu huwa mnadai na au fikiria kuwa Mungu wa Biblia aliye jaa upendo ni huyo huyo wa kwenye Quran ya Jibril. La hasha.

Allah ambaye ndie munguwa Waislam yeye amejaa chuki na anawataka na kuwaamrisha Waislam wote kufanye chuki iliyo ndani ya Quran.

Hebu anza moja kwa moja kusoma chuki za Allah:
ALLAH ANAWAAMBIA WAISLAM WOTE KUWA: NI MARUFUKU KUWA MARAFIKI NA WAKRISTO:

Surat Al Maida 51. Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. http://www.quranitukufu.net/005.html

SASA, kama Allah ni Yehovah wa Biblia, mbona hatusomi Mungu wa Biblia akisema muwachukie watu ambao sio wa imani yenu?

SOMA Luka 6:35 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

35 Bali, wapendeni adui zenu, watendeeni mema. Wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo mtapata zawadi kubwa nanyi mtakuwa wana wa Mungu Aliye Juu. Yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na watu waovu.

MUNGU WA BIBLIA ANSEMA Wapendini adui zenu, ni tofauti kabisa na Allah anaye sema WACHUKIENI WAKRISTO NA WAYAHUDI. Allah wa Quran sio Mungu wa Biblia.

ALLAH ANASEMA KUWA, WAISLAM HAWARUHUSIWI KUWAPENDA WAKRISTO HATA KAMA NI BABA ZAO AU MAMA ZAO AU NDUGU ZAO:

Suratul Al Mujaadalah 22. Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa. http://www.quranitukufu.net/058.html

HIVI, kweli bado unaamini kuwa Allah ni? Mbona sifa zake zote ni za SHETANI wa aliye semwa kwenye Biblia?

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA WAISLAM WASIWAFANYE WAKRISTO NA WAYAHUDI KUWA MARAFIKI ZAO.

Surat An Nisaai 144. Enyi mlio amini! Msiwafanye Wakristo na Mayahudi kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu? http://www.quranitukufu.net/004.html

Allah anaendelea kuonyesha sifa za Shetani. Leo anasema na kuwaamrisha Waislam kuwa, WASIWE NA URAFIKI NA WAKRISTO. Hivi Mungu gani huyu anaye penda kuchonganisha watu? Hii tabia ya chuki ni ya nani kama si SHETANI?

Hebu tumsome YESU WA KWENYE BIBLIA ANASEMA NINI?

‘Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. MWIVI HAJI ILA AIBE NA KUCHINJA NA KUHARIBU; MIMI NALIKUJA ILI WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. ‪#‎YOHANA‬ 10:7-15

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA WAISLAM NI MARUFUKU KUWA NA UMOJA NA WASIO WAISLAM

Surat Al Imran 118. Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.

Allah anaendelea kupanda chuki kubwa kubwa kwa Waislam, sasa anasema kuwa Waislam wasiwe na wasiri na watu ambao sio Waislam, hata kama huyo mtu ni Baba yao, mama yao nk. Hii chuki inapatika kwa SHETANI na sio Mungu wa kwenye Biblia.

ALLAH ATEREMSHA YA NA KUSEMA KUWA WAKRISTO NI MAADUI ZA WAISLAM.

Surat An Nisaai 101. Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.

ALLAH AWAAMRISHA WAISLAM KUWAKATAA WAKRISTO

Surat Al Mumtahinah 4 ...............Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake.

ALLAH AWAAMRISHA WAISLAM KUPIGANA NA KUWAUWA WAKRISTO.

Surat Tawba 123. Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mngu

Mwana wa Mungu siku zote Shetani kazi yake ni kuiba, kuua na kuharibu. Ndiyo kazi yake. Hajawahi kubadilika. Toka afukuzwe mbinguni hiyo ndo imekuwa kazi yake hapa duniani. Na Bwana Yesu amelisema hilo bila kumung’unya maneno. Bwana Yesu dhamira yake ni kutupa uzima tele.

Adui siku zote amekuwa ni muuaji tu. Kila sehemu anakopita yeye ni mharibifu. Huwa inafika mahala najiitisha kikao na kujiuliza sisi wanadamu tuna matatizo gani. Kwa nini kufanya urafiki na Shetani na kukubali kuwa mtumwa wake? Unapokubali kuwa mtenda dhambi maanake umekubali kufanya urafiki na Shetani maishani mwako.

Mwana wa Mungu Bwana Yesu anasema yeye amekuja ili wanadamu WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE.

Ikiwa adui amepora chochote ndani yako, ameua chochote ndani yako, amefanya uharibifu wowote ndani yako, ndani ya ndoa yako, au ndani ya familia yako, ndani ya kazi yako, ndani ya biashara yako, katika ukoo wako, kwa watoto wako, kwa wazazi wako, basi nakutangazia BWANA YESU ALIKUJA ILI UWE NA UZIMA, KISHA UWE NAO TELE. Ni ombi langu Bwana akupe uzima tele katika kila eneo adui alifanya uharibifu. Kama ilikuwa kwenye ndoa, kwenye biashara, kwenye kazi, kwenye kuutafuta uso wa Mungu. katika kupata watoto, kupata mume, kupata mke n.k Bwana akupe hitaji lako.

Shetani yuko chini ya miguu yako mpendwa, simama kurudisha chochote adui alikuwa amefanya uharibifu dhidi yako na usikubali kushindwa na Shetani. Yesu aliyemo ndani yako ni mkuu kuliko Shetani. Anataka akupe uzima tena uzima tele.
Barikiwa sana.

Yamkini unataka kuokoka? Basi wasiliana nasi tukusaidie
kuchukua uamuzi mwema wenye busara maishani mwako.

Yesu anakupenda.

Max Shimba Ministries

Thursday, January 14, 2016

MAJINI NI MAISLAM


MAJINI KATIKA DINI YA KIISLAM ( Q 72:1-14 )

1. QURAN INASEMA KUWA MAJINI YANAZALIANA NA KUFA KAMA BINADAMU 2. ALLAH AYARUHUSU MAJINI KUZAA NA BINADAMU 3. QURAN INAKIRI KUWA MAJINI NI MAISLAM NA YALISILIMU PALE QURAN ILIPO TEREMSHWA KWA MUHAMMAD. 4. MAJINI YANAMWABUDU ALLAH 5. KILA MUISLAM AMEPAGAWA NA MAJINI KATIKA MWILI WAKE


Leo ningependa tujifunze kidogo kuhusu Majini au Mashetani katika Uislam.

JINI NI NINI?

Katika lugha ya kiarabu, neno Jini linamaanisha kitu kilichofichwa au kisichoonekana QURAN 1:71 Neno hili hutumiwa na Waarabu kwa ajili ya kutaja jina fulani. Kwa Waarabu, Jini anayevaa sura ya kike humwita Jinivya, hivyo majini Ghul/Ghilan, nao hujifunua kwa sura ya kike.

Katika imani ya Kiislamu, wao huamni kwamba Majini hutofautiana na Mashetani. Majini waliosilimu wao huitwa majini mazuri na hawa wakiwa katika hali kujionyesha kwa wanadamu, hao huitwa AJINU na wale walioacha kusilimu mwaka 610 AD (Baada ya Kristo) katika safari ya mtume Muhamad alipotoka Taif , wao wanaitwa Mashetani . Hivyo, wao wanapokuwa katika hali ya kutoonekana huitwa ALBAHATWA lakini pia Majini wote wanapokuwa katika hali ya kutoonekana waweza kuitwa ALBAHATWA, yaani PEPO.

QURAN INASEMA KUWA MAJINI YANAZALIANA NA KUFA KAMA BINADAMU

Muislamu huamini kwamba kuna majini ya kike na kiume. Lakini pia , huamini kuwa Majini huoana na kuzaliana QURAN 55:56 na kuwa Majini huzaa sana kuliko binadamu na kwamba, Jini mmoja anaweza kuzaa watoto 300, na kuwa Jini huzaa watoto 3 hadi 4 kwa mkupuo. Somo QURAN 55:26-28 na kuwa Majini wanaweza kuishi miaka 400-1,000 kisha wanaweza kufa. Tofauti yao na binadamu ni kwamba wao wanaishi miaka mingi kuliko binadamu. Lakini pia, huamini kuwa wapo Majini wanaokula, wanaomeza, wanaokunywa, ila tofauti yao na wanadamu ni kwamba wao hula kwa kutumia mkono wa kushoto.

ALLAH AYARUHUSU MAJINI YANAZAA NA BINADAMU

Pia hiamini kuwa Majini wana uwezo wa kuzaa na Wanadamu. Soma QURAN 17:64. Waislamu huamini kwamba mtu anauwezo wa kuoa au kuolewa na Jini bila kujua, na mwanadamu anauwezo wa kumuua Jini. Soma QURAN 57:14-15

SURATULJINN
Ndani ya QURAN pia imo sura inayoitwa Suratuljinn (QURAN 72). Sura hiyo huitwa hivyo kwa sababu ni sura ya Majini (Mapepo).

Kwa nini wanatajwa Majini katika imani ya Kiislamu?

QURAN INAKIRI KUWA MAJINI NI MAISLAM NA YALISILIMU PALE QURAN ILIPO TEREMSHWA KWA MUHAMMAD.

Majini wanatajwa sana katika dini ya Kiislamu kwa kuwa ni waislam kwa kusilimu, kwa kuiamini Quran tukufu aliyopewa mtume Muhamad.

Majini walisilimu na kuwa Waislamu mwaka 610 AD(Baada ya Yesu) SOMA 72:1-14 QURAN. Hivyo basi, unapotumia neon jinni maana yake unatumia lugha ya Kiarabu ukimaanisha Pepo mchafu. Ni kama Spoon/kijiko, vyote ni kitu kimoja. Ndani ya Quran, neon “PEPO” limetumika kama Paradiso, mbinguni. Lakini pia, tunapata neon jingine liitwalo AKHERA ila neno hilo halimaanishi PARADISO, bali kwa lugha ya Kiarabu neno hili “AKHERA” lina maana ya KUZIMU.

Lakini pia ukiangalia ndani ya SURALJINN ( QURAN 72:1-2, 8-9, 12 ) Mapepo hawa wanajieleza waziwazi kabisa kuwa mwanzo waliishi Mbinguni, walipogeuka kwa kuasi, walitegwa na Mungu. Linganisha na maandiko haya katika Biblia ( UFUNUO WA YOHANA 12:7-9; YUDA 1:6-8; UFUNUO 20:10; UFUNUO 21:8 ). Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, hawa majini ( Mapepo ) waliotegwa na Mungu Mbinguni wakiwa Malaika huko na kutupwa Duniani baada ya kuasi huko, sasa, wakati wa mtume Muhamad katika safari yake ya kurudi Taif mwaka 620 AD (baada ya Yesu) wapo walioamini na kuona kuwa Quran ni ya ajabu ya kuwatangazia neema ya kuabudu. Katika vol 8-9, husema , wanapojaribu kwenda Mbinguni ( walikotoka zamani ), hukuta ile Mbingu imezungushiwa vimondo vya moto. Hivyo, hudai kuwa mbingu yao iko Akhera, yaani Kuzimu, maana Mbingu ya juu ina moto na hawana uwezo wa kwenda huko. SOMA (QURAN 72:9), Mbingu ina utisho wa moto ila Akhera ( kuzimu ) hakuna shida kwao.

MAJINI YANAMWABUDU ALLAH

Hivyo basi, kulingana na jinsi Allah asemavyo ndani ya Quran kuwa nimeumba binadamu na majini ili muniabudu ( QURAN 57:58 ; 51:56) na kuwa , mbinguni mwao Majini wanaabudu (Majini waliosilimu mwaka 620 AD) ,SOMA QURAN 72:14, ambao ni wema wanaosafiri na kurithi uzima wa milele upatikanao Akhera ( Kuzimu ). Lengo kubwa la Shetani na Majini ni kufanya urafiki na wanadamu wengi ili kwa wingi huo apate watu wengi wa kwenda nao JEHANAMU ( QURAN 6:128 ). Jambo la muhimu kujua hapa ni kwamba moto wa milele hakuwekewa Mwanadamu bali ni Shetani na malaika zake wote ( Majini au mapepo ). Hawa, hawana nafasi tena ya kuungama au kutubu.

Yesu Kristo anayetambuliwa na Waislam kama Mtume tu, hakuwa na urafiki wowote na Shetani wala Mapepo ( Majini ). Aliyaamuru Majini kutoka ndani ya watu waliokuwa wakiteswa nayo ( MATHAYO 8:29: MARKO 5 N,K )

Wakati Yesu anaondoka hapa duniani, alichukuliwa na wingu na kupaa kuelekea juu. Mbinguni ni juu kama Quran inavyothibitisha. Yesu aliweza kupaa na kuingia Mbinguni lakini Majini ( Mapepo ) walioslimu wakijaribu tu, wanakutana na moto mkali. Tumeona kuwa Majini ambao ni Waislamu kwa kusilimu, wanaishi AKHERA yaani Kuzimu. Je, Waislamu wengine unadhani wataishia wapi milele? Katika imani ya Kiislam huamini kuwa, Muislam akifa anakuwa na Majini wawili wa Kumlinda humo Kaburini.

KILA MUISLAM ANA JINI KATIKA MWILI WAKE

Majini wamepewa ruhusa ya kukaa katika mwili wa Muislam yeyote, hivyo kila Muislam ana Jini kuanzia moja na kuendelea. Vile vile Majini wameruhusiwa kukaa katika nyumba za Waislam. Katika nyumba yoyote ya Muumini wa dini hiyo, kuna Jini au Majini wanaokaa humo. Ni ukweli usiopingika kuwa bila Majini hakuna Uislamu kama vile pasipo Roho Mtakatifu hakuna Ukristo. Majini ndiyo yaliyomchukua mtume Muhamad kwa muda wa siku 40 akiwa Mabondeni walikompeleka na kuanza kumuagiza kuhusiana na kuanzisha imani hiyo ya Kiislamu.

USHAURI WANGU KWA WA WAKRISTO:

Ushauri wangu wa bure kwa Mkristo ni huu, USIMUACHE KAMWE KRISTO NA KUINGIA KATIKA IMANI ZA MASHETANI (1TIMOTHEO 4:1-2 ).

Majini au Mashetani ni kitui kimoja na wala hakuna tofauti yao. Wote hao Mashetani/Majini yalimpinga Mungu na kutupwa duniani. Biblia inasema kuwa Hakuna Msamaha kwa Majini maana wao walisha hukumiwa na wanacho subiri ni kutupwa Jehannam.

Shetani bado ni “mfalme wa nguvu za anga” (Waefeso 2:2). Hii inamaanisha kwamba Shetani na Malaika wengine walioasi wanaweza kushawishi mia zetu na mawazo yetu kupitia miziki, runinga, mijadala, nk. Tumeambiwa kujihadhari katika mawazo na nia zetu (2Wakorintho 10:3-5). 2Wakorintho 4:4 inatuambia kuwa mungu wa dunia hii amepofusha mawazo ya watu ili wasiamini.

Shetani ndiye yuko nyuma ya dini zote za uongo na dini za dunia. Shetani atafanya na kila kitu katika uwezo wake ili ampinge Mungu na wale wote wanaomfuata. Ingawa hatima ya Shetani imewekwa muhuri kuwa tanuru la moto milele (Ufunuo Wa Yohana 20:10).

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba Ministries Org.

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Wednesday, January 13, 2016

WAISLAM WANAULIZA: JE, ALIYE TAJWA KWENYE KUMBUKUMBU YA TORATI NI MUHAMMAD AU YESU?



Swali: Katika Kumbukumbu 18:17-18; 33:1-2, na 34:10-11, ni Muhammad aliyetabiriwa hapa, kama baadhi ya Waislam wanavyodai?Jibu: Kumbukumbu 18:15-18 inasema Mungu atamwinua nabii, kuwa watamsikia, kama Musa kutoka miongoni mwao, miongoni mwa ndugu zao.

Je Yesu alikuwa nabii?
Je Wayahudi walio wengi walimsikia Yesu?
Je Yesu alikuwa mmoja wa Wayahudi?
Je Yesu alikuwa Myahudi?

Waislam wanapaswa kutokuwa na shida kuafiki kuwa mistari hii inamfaa Yesu kuliko Muhammad. Kama angalizo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) pia alizungumzia jinsi ambavyo Kumbukumbu 18:15 isivyoweza kuwa inamwongelea mtu mwingine yoyote yule isipokuwa Yesu Kristo kwenye Disputation with Manes sura ya 43 uk.219.Yafuatayo ni maoni zaidi.

a. Kumbukumbu 33:1-2 inasema "Bwana", na Waislam hawamwiti Muhammad Bwana wao. (Waislam wa ‘Alawite na makundi mengine ya Ghulat wanamchukulia Muhammad kuwa Mungu, lakini maoni hayo siyo kawaida kwa Waislam.)

b. Kumbukumbu 34:10 kwamba "Wala hakuinuka tena katika Israeli nabii kama Musa." Wasifu huu uliandikwa, huenda na Yoshua, muda mrefu kabla Yesu hajaja.

c. Kumbukumbu 34:10 inasema "uso kwa uso", na Muhammad hajawahi kusema kuwa alipata maneno yake moja mwa moja kutoka kwa Mungu, bali kupitia malaika (Sura 2:97). Yesu aliwasiliana moja kwa moja na Mungu Baba kwa mujibu wa Yohana 1:18 na vifungu vingine.

d. Mstari unaofuatia, 34:11, unasema kuwa hakuna nabii mwingine yoyote aliyefanya miujiza hiyo mikubwa kama Musa.

Muhammad, kama ilivyoandikwa kwenye Kurani (Sura 17:90-93) hakuwahi kufanya miujiza kama hii, isipokuwa kusema Kurani. (Kurani inapingana na jinsi mapokeo ya baadaye ya Hadithi yanavyosema.)

e. Kwenye Kurani yenyewe, Sura 29:27 inasema unabii umekuja kupitia Isaka na Yakobo. Kwenye tafsiri ya Yusuf Ali ya Kurani, anasema, "Na tumewapa (Abraham) Isaka na Yakobo, na tumeagiza miongoni mwa wazao wake unabii na ufunuo . . ."

Wakati ambapo mabano kwenye jina la Abraham yapo kwenye tafsiri ya Yusuf Ali, neno lote "Abraham" halimo kwenye Kurani ya Kiarabu, na Yusuf Ali aliona haja ya kuongeza neno "Abraham" kwenye maandiko ambayo Waislam wanayaona kuwa ni neno la Mungu.

f. Mwisho, Petro, mtume wa Yesu, alisema andiko hili lilitimia kwa Yesu kwenye Matendo 3:22-26. Mtume Petro alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kujua jambo hili.

1. Ama, Yesu alifanya makosa ya kumruhusu mtu mwongo kama Petro kuwapotosha watu, kwa kwa karibu miaka 2,000, ambao wamekuwa wakijaribu kumfuata Mungu, na Mungu hakuinua kidole kuwaambia watu ukweli.
2. Au, Yesu alijua alichokuwa anafanya wakati alipomchagua Petro, na Mungu hakusahihisha kitu ambacho hakikihitaji masahihisho yoyote yale.
3. Vinginevyo, Petro hakusema hivyo, na kitabu cha Matendo ya Mitume kilipotoshwa kabla ya maelezo ya maneno hayo ya kwanza tuliyo nayo toka nje ya Biblia yanayoturejesha kwa Yesu, karibu mwaka 138 B.K.

Viongozi wa awali wa kanisa walisema kuwa mstari huu ulimwongelea Yesu. Baadhi yao ni
Justin Martyr 138-165 B.K.
Irenaeus 182-188 B.K.
Tertullian 220-220 B.K.
Origen 225-254 B.K.
Chrysostom 407 B.K.

Justin Martyr alizaliwa karibu mwaka 114 B.K., ingawa watu wengine hudhani mwaka 110 B.K. Apology yake ya kwanza iliandikwa kati ya mwaka 138 B.K. na mwaka 165 B.K. wakati wa kifo chake. Ni dhahiri kuwa alitakiwa kusoma unabii huu unaomwongelea Yesu kabla ya kuandika.

Muislam anaweza kusema kuwa Justin hakukosea tu bali pia manuscripts zote za Agano Jipya ziliunukuu usemi wa Petro kimakosa.

Pia, tafsiri kwenye lugha nyingine zilifanywa mapema sana; tarehe za hapo juu si za tafsiri za kwanza, bali ni tarehe za manuscripts za zamani zaidi ambazo zipo leo hii.
Hizi zinaaminika kwa sababu zimepita kwenye mtiririko huru ambao watu wanaweza kuutumia kuthibitisha manuscripts za Kiyunani.

Mtiririko wote wa manuscripts hizi, kutoka Afrika kwenda Asia, unaafiki kuwa Petro alisema hivi akimwongelea Yesu.

Tazama When Cultists Ask uk.43-44,45-46 na When Critics Ask uk.125-126, uk.131-132, na uk.133 kwa habari zaidi.Mungu awabariki sana

Max Shimba Ministries Org

KATIKA TAURAT, ZABURI, INJILI HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM

KATIKA TAURAT YA MUSA, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM
KATIKA INJIL YA YESU, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM
KATIKA ZABURI YA DAUDI, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM.

A. Kwanini Waislam wanadai eti Musa alikuwa Muislam, wakati Taurat iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?

B. Kwanini Waislam wanadai eti Yesu alikuwa Muislam, wakati Injili iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?

C. Kwanini Waislam wanadai eti Daudi alikuwa Muislam, wakati Zaburi iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?

Kama Waislam wanabisha, nionyesheni ipo wapi Taurat aliyo iteremsha Allah kwa Musa tuione? Na iwe na aya inayosema kuwa Musa alikuwa Muislam.

Quran inasema kuwa Allah ameitunza Taurat na Injil katika Surah 15 aya 9. Vile vile tunasoma kuwa Taurat na Injil vinasemwa kama kumbukumbu katika Surah 16:43, 21:7, 21:48, 21:105 na 40:53-54.
Kwahiyo, Surah 15:9 inakubali kuwa Taurat na Injil zimetunzwa na Allah. Kama ni kweli haya madai ya Quran:http://www.quranitukufu.net/005.html

1. Ipo wapi nakala ya Taurat ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
2. Ipo wapi nakala ya Injil ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
3. Ipo wapi nakala ya Zaburi ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?

Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyo teremshwa na Allah kabla ya Quran, na iwe na aya Adam anasema kuwa yeye ni Muislam.

Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyoteremshwa kabla ya Quran, na iwe na aya ambayo Ibrahim anasema kuwa yeye ni Muislam.

Waislam, ipo wapi Taurat ambayo mnadai kuwa Allah aliiteremsha kwa Musa? Mbona kila siku mnatuletea aya za Quran ambazo sio Taurat?

Kama kweli Allah aliteremsha Taurat kwa Musa, basi tuonyesheni wapi ilipo hiyo Taurat na sio aya dhaif za Quran. Hivi Quran sasa imekuwa Biblia - Mkusanyiko wa Vitabu?

Allah anadai kuwa aliteremsha Injil: Surat Al Maida 46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu. http://www.quranitukufu.net/005.html

Waislam, tuonyesheni wapi ilipo nakala ya Injil ambayo Allah anadai kuitunza katika Surat Al Hjr aya ya 9?

Hakika Allah hakuteremsha kitabu chochote kile zaidi ya maneno matupu yaliyo ndani ya Quran ya Jibril.

Allah sio Mungu. Musa hakuwa Muislam, Daudi Hakuwa Muislam, Ibrahim Hakuwa Muislam. Yesu hakuwa Muislam.

Kama kuna Muislam anao ushahid kuwa Musa, Daudi, Ibrahim, Yesu walikuwa Waislam, basi watuonyeshe wapi vilipo vitabu vyao ambavyo Allah anadai kuviteremsha. Waislam, sina muda na aya za Quran zilizo kuja miaka maelfu baadae.

Max Shimba Ministries.

Tuesday, January 12, 2016

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA KUWA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM



1. ALLAH ASEMA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM
2. MUHAMMAD AKIRI KUWA NA YEYE ATAINGIA JEHANNAM
3. ALLAH NA YEYE ANAINGIA JEHANNAM

Jamani huu ni Msiba katika taifa la Islam kwa kushindwa kusoma aya hii ambayo ipo wazi (Quran 40:60) http://www.quranitukufu.net/040.html .

Katika mada hii, nitawawekea aya kutoka Koran na simulizi za Muhammad ambazo zinatushuhudia kuwa, Waislam wote wataingia Jehanamu.

Hebu tumsome kwanza Allah katika aya aliyo iteremsha kwa Mtume wake Muhammad (Pbuh).
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike. http://www.quranitukufu.net/040.html
Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni ili wadhalilike”

Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana katika dini na taifa la Kiislam. Allah amesha toa hukumu kwa wamfuatao na inafahamika fika kuwa, Wale wote waingiao Jehannam, hao walikuwa hawafanyi Mapenzi ya Mungu wa Biblia. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Huu ushaidi ndio tulio usoma katika Quran 40:60. http://www.quranitukufu.net/040.html

Sasa tuwasikilize na maswahiba wa Mtume Muhammad.

Simulizi:Pia imesimuliwa na Ibn Jarir, iliyosimuliwa na Abu Kurayb, imesimuliwa na Ibn Yaman, imesimuliwa na Ibn Malik Maghul, imesimuliwa na Ibn Ishaq ambaye alisema, "Kila mara Abu Maysarah anapo kwenda kulala na akiwa kitandani kwake yeye husema, 'Mimi nasikia Uchungu kuzaliwa na Mama yangu. 'na kisha anaanza kulia kwa Machozi. Alipoulizwa kwa nini alikuwa akilia, alijibu yafuatayo,' Tuliambiwa na Mtume wa Allah kwamba SISI WAISLAMU tutaingia Jehannamu, LAKINI HATUKUAMBIWA kwamba TUTATOLEWAJE HUKO JEHANNAMU NA HATUKUAMBIWA NI KIVIPI TUTATOKA HUKO'"

Mfuasi huyu wa Muhammad anaoneka kupatwa na mshtuko mkubwa, pale alipo ambiwa kuwa, Waislam wote wataingia Jehannam. Mshtuko huu umemfanya ailaani siku ambayo alizaliwa. Kitu cha kujiuliza, kwanini Allah ambaye ni mungu wa Waislam anatoa ahadi ya Jehannam na si Akhera kama wafundishavyo Waislam?

MUHAMMAD NA YEYE AKIRI KUINGIA JEHANNAM"Wamegawanyika Mayahudi katika mapote 71, wakagawanyika Wakristo
katika mapote 72 na Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu)) [Ahmad, Abu Daawuud, atTirmidhiy na ad-Daarimiy]

Kama ushahid unavyo sema hapo juu kuwa Madhehebu yote ya Waislam yataingia Motoni, sasa, ni dhehebu lipi hilo ambalo halita ingia motoni?

JE, ALLAH NA YEYE ATAINGIA JEHANNA? AMINI USIAMINI, ALLAH NA YEYE ANAINGIA JEHANNAM KAMA VIUMBE
Sasa tusome Sahih Hadith: Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 371 Amehadithia Anas: Mtume wa Allah alisema, "watu watatupwa (Kuzimu) Jehannam na matokeo yake Jehannam itasema:" Je, kuna zaidi watu zaidi? (50.30) mpaka Allah atakapo weka mguu wake juu ya Kuzimu na Jehannam itasema, 'Qati! Qati! (Imetosha imetosha!) " Ushaidi zaidi: Bukhari :: Kitabu 9 :: Juzuu 93 :: Hadith 481, Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 373

Sasa tumefahamu siri kubwa hapa. Kumbe na Allah ataingia motoni. Jamani, hivi huu si ndio Msiba mkubwa sana kwa dini ya Muhammad? Allah nayeye anaingia motoni.

Katika Biblia tunasoma kuwa Shetani na yeye ataingi mtoni, tena atakuwa wa Mwisho kama Allah alivyo kuwa wa Mwsiho pale Jehannam ilipo itisha watu zaidi. Sasa rejea kwenye Biblia: Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. HAPO TUNASOMA KUWA IBILISI anaingia Motoni na kuwakuta wenzake humo, kama ambavyo Sahih Bukhari imesema kuwa Allah anaingia Jehannam na kuwakuta Waislam huko.

ALLAH ANAINGIA JEHANNAMAbu Huraira anasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):
“Pepo na Jahannam zilikuwa na mzozo, kila kimoja kikijaribu kuonyesha ule ubora wake juu ya kingine.” Basi Jahannam ikazungumza: “Mimi nimependelewa kwa kuwepo kwa wale watu wenye kiburi na nguvu ndani yangu.” Pepo ikajibu: “Mimi sijui ni kwa nini hakuna mtu isipokuwa wale dhaifu na wanyenyekevu ndio walioingizwa ndani yangu!”

Hivyo Mwenyezi Mungu akaiambia Pepo:
“Wewe ndiye Msamaha Wangu, na kupitia kwako ninatoa msamaha kwa yeyote kati ya waja Wangu.”
Halafu Yeye akazungumza na Jahannam:
“Wewe ndio ghadhabu Yangu, na kupitia kwako wewe ninamuadhibu yeyote nitakaye kumuadhibu. Kila mmoja wenu atajaa.”
“Bali Jahannam haitajaa, hivyo Mwenyezi Mungu ataingiza mguu Wake ndani yake.”
Kisha Jahannam itagutia:
“Tosha! Inatosha!”

Ndugu zanguni, ningependa mfahamu kuwa, utakapo ingia Jehannam, kutakuwa hakuna tena njia nyingine ya kutoka huko. Pale Jehannam ndio mwisho wa maisha ya walio tenda dhanb. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Je, kufanya mapenzi ya Allah ni sawa na kutenda dhanb? Je, Uislam ni dini ya haki, kama wanavyo sema wafundishaji wa dini hiyo? Jiulize tena, kwanini Allah anatoa ahadi ya Jehannam kwa wafuatayo mafundisho yake?

Lakini Yesu anasema haya:Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Ndugu zanguni, mwamini Yesu ili uwe na uzima wa milele. Yesu anakupenda. Yesu Ndie Njia Pekee. Yesu Ndie Uzima. Dini haita kupeleka kwa Baba aliye Mbingu, lakini Yesu anasema Yeye NDIE NJIA.

Mungu awabariki sana,

Katika Huduma Yake,

Max Shimba
For Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Monday, January 11, 2016

SIFA-ADHAMA SABA ZA ROHO MTAKATIFU

Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 17Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.

Yesu Kristo ametupa zawadi ya ajabu sana: Zawadi ya Roho Mtakatifu. Katika baadhi ya maeneo, zawadi hiyo inajulikana kama Roho Mtakatifu, na sehemu nyingine ametajwa kama Msaidizi (Msaidizi na Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu ni sehemu ya tatu ya Uungu, sehemu ya tatu ya Utatu wa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Yeye ni Msaidizi katumwa na Yesu, baada ya Msaidizi wetu kuja ambaye ni Roho Mtakatifu, Yesu alipaa tena mbinguni. Roho Mtakatifu hutolewa kwa wote ambao wamempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao

Kuna mambo saba ambayo tunahitaji kuelewa kuhusu Roho Mtakatifu. Tunajua kwamba, katika Biblia, saba ni namba ya kukamilika/ kukamilisha, au ukamilifu, na sifa saba zote tofauti za Roho Mtakatifu ni kweli kamili na kamilifu. Tunaweza kuzitegemea sifa hizi za ajabu za Roho Mtakatifu, wakati wote, katika kila hali na katika maisha yetu yote.

1. Roho Mtakatifu ni Msaidizi Mwenye Upendo. Tunapokabiliana na mateso katika maisha, mwongozo wa Roho Mtakatifu ni muhimu zaidi na ni faraja katika mioyo yetu: Roho Mtakatifu ni mtu ambaye ana upendo kwetu na anajua kila kitu kuhusu maisha yetu. Roho Mtakatifu alitupenda tangu kabla ya kuumbwa ulimwengu. Yeye alivyotupenda vizuri. Yeye anatupenda milele na anaendelea kutupenda milele yote. Roho Mtakatifu tu ndie mwenye uwezo wa kweli wa kutufariji mioyo yetu, kwa sababu hakuna mtu anaye tupenda sisi kama anavyotupenda Yeye Roho Mtakatifu.

Warumi 5: 5 wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo Lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

2. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwaminifu. Watu, hata wale ambao wana upendo kwetu, wakati mwingine wanaweza kushindwa kutusaidia. Wao (Ndugu na Marafiki) wakati mwingine si waaminifu. Na inaweza kuumiza sana nafsi yetu - rafiki anaweza kuwa mbaya kuliko jino la nyoka, na mchungu kupita nyongo. Huwa tunakata tamaa wakati mtu ambaye anatupenda anapobadirika wakati tunapokuwa na taabu, lakini, Mungu Roho Mtakatifu kamwe hawezi kufanya hivyo na kamwe hawezi kukuacha wakati wa taabu. Yeye anatupenda hata mwisho, kwani, Yeye peke yake ni Mwaminifu. Dhambi haiwezi kututenganisha na upendo wake, hakuna, kwa kweli, yeye alitupenda wakati sisi bado tulikuwa wafu katika dhambi zetu. Alitupenda huku qkijua jumla ya uovu wetu na dhambi zetu. Wema wetu wote kamwe haukumfanya yeye atupende zaidi, na zambi zetu zote hazimfanyi yeye Roho Mtakatifu asitupende au punguza upendo wake kwetu. Tunaweza kumwamini kikamilifu katika Yesu, kwa maana Yeye ni milele mwaminifu. Yeye kamwe hata tuacha, lakini atakuwa pamoja nasi mpaka mwisho wa maisha yetu hapa duniani.

Warumi 15: 13Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

3. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Asiechoka. Wakati mwingine sisi tukijaribu kumfariji rafiki yetu/ndugu yetu katika shida zao au dhiki, huwa tunachoka, pale tunapo ona kuwa shida ya tunaye mfariji inapo kuwa haiishi huwa mara nyingi tunaacha kufanya hivyo na au kata tamaa. Kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kufarijika na au kufarijiwa, infact, tunapo endelea kuwafariji, ndio wanazidi kuharibika na ua hali inazidi kuwa mbaya. Mara nyingi basi, sisi hufa moyo, na kuwaacha peke yao na matatizo yao. Roho Mtakatifu kamwe huwa hakati moyo/au choka kukusaidia, zaidi ya hapo, Yeye huwasaidia hata wale ambao wanafikiria kuwa hawawezi kusaidika. Yeye Roho Mtakatifu, huwa hachoki na au choshwa, si kwa dhambi zetu, si kwa manung'uniko yetu, hata kwa kukataa kwetu, Yeye bado anatupenda na anahuruma.

Yohana 14: 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

4. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwenye Busara. Sisi mara nyingi huzungukwa na watu ambao wanadhani wao wana busara, na bado hao watu hawana uwezo wa kuangalia ndani ya moyo wako na kusema nini ni chanzo cha magonjwa yetu/matatizo yetu ya kiroho. Kama marafiki wa Ayubu (Katika Biblia) walivyo toa mawazo yao potofu, ndivyo hivyo ambavyo hata marafiki zetu wanaweza kutupa mawazo ambayo si sahihi, zaidi ya hapo, hata Madaktari wanaweza kutupa dawa ambazo si sahihi au kwa makosa na zikashindwa kutibu magonjwa yetu na hata kusababisha madhara makubwa, au hata mauti. Ili kutabumbua ugonjwa wa Kiroho kwa usahihi, basi inahitaji hekima kamili. Hivyo basi, Roho Mtakatifu kwa kutumia hekima yake, anaweza kuingalia Roho/moyo wako na kutambua nini hasa kinakusumbua na au wapi lipo tatizo lako la Kiroho. Yeye anaona mzizi wa watatizo upo wapi, na ni nini kinasababisha ugonjwa wako wa kiroho. Yeye si anafahamu wapi lipo tatizo lako, lakini vile vile yeye anaweza kukutibu hilo tatizo lako. Hivyo basi, Roho Mtakatifu Mwenye Busara, ana uwezo wa kuponya magonjwa yetu yote na kutufanya tukubalike mbele za macho ya Mungu. 

1 Wakorintho 2: 10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

5. Yeye ni Msaidizi Alie Salama. Mara nyingi sana marafiki na familia hutoa ushauri salama wakati sisi tupo katikati ya majaribu na mateso. Ushauri wowote unao fuata maarifa ya ulimwengu huu ni ushauri salama. Kumbuka kwamba Shetani mwenyewe wakati mwingine huja kama mfariji wa uongo, anatuhakikishia kwamba mambo yote ni salama huku akifahamu kuwa si kweli, na huku akiweka shaka katika Neno la Mungu. Lakini faraja ya Roho Mtakatifu ni salama, na unaweza kutulia katika faraja na Imani Yake (Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu anajua moyo wa Mungu na mapenzi ya Mungu kwako, na faraja yake kamwe haiwezi kwenda kinyume na Matakwa ya Mungu.

1 Wakorintho 2: 13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

6. Yeye ni Msaidizi alie hai. Yeye (Roho Mtakatifu) huwa awafariji tu kwa maneno, lakini kwa matendo. Yeye anatuombea, kutukumbusha ahadi kubwa ya Mungu na neema yake. Yeye kamwe hatuachi au kutuacha, lakini badala yake anatuongoza katika mapenzi kamili ya Mungu Baba.
Warumi 8: 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 27. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

7. Yeye ni Msaidizi wetu wa sasa na hata milele. Hatuitaji kumtafuta, bali yeye yupo nasi daima. Yeye kamwe hatotuacha, wala kutuacha. Tunaweza kumwambia na au kumwita wakati wowote ule tunahitaji msaada wake, na tuna uhakika kuwa yeye yupo nasi na anaweza kutusaidia.

Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

Hivyo basi, ndugu msomaji, leo tumekumbushana sifa Saba za Roho Mtakatifu.
1. Roho Mtakatifu ni Msaidizi Mwenye Upendo.
2. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi mwaminifu.
3. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Asiechoka.
4. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwenye Busara.
5. Yeye ni Msaidizi Alie Salama.
6. Yeye ni Msaidizi alie hai.
7. Yeye ni Msaidizi wetu wa sasa na hata milele.

Nimategemeo yangu kuwa, baada ya kuzisoma hizo sifa Saba za Roho Mtakatifu, utaanza kumtegemea na kuongea naye kila siku. Kumbuka, Roho Mtakatifu ni Msaidizi wetu na yupo nasi kila siku kama ambavyo Biblia Takatifu inavyo sema.

Mtegemee Roho Mtakatifu katika Maisha yako yote. Mtegemee katika kazi zako. Mtegemee katika Masomo yako. Mtegemee katika Biashara zako. Mtegemee katika Ndoa yako. Mtegemee katika kila jambo. Hakika Yeye anakupenda na alikufahamu wewe hata kabla ya kualiwa kwao. Yeremia 1: 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Katika Huduma Yake,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries 

April 13, 2015 ©2015

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction Muslims ...

TRENDING NOW