Tuesday, September 27, 2016

MSIKITI WALIPULIWA NA BOMU UJERUMANI




Ulinzi umeongezwa katika Mji wa Dresden Ujerumani baada ya Mabomu maliwili kulipuka Msikitini na kwenye ukumbi wa mikutano.
Habari zinasema kuwa hakuna aliye umia kutokana na milipuko hiyo ambayo inasadikika kuwa ni Mabomu ya kutengeneza nyumbani.
Mabomu haya yanakuja baada ya Mwisho wa wiki ujao ni sikukuu ya umoja nchini Ujerumani ambayo Chancellor Angela Merkel anategemea kuhudhuria. Maadhimisho hayo ni ya miaka 26 ya umoja wa Ujerumani Mashariki na Magharibi.

MUHAMMAD ANAMPENDA SHETANI MPAKA AKAAMUA KUMSILIMISHA


Ndugu zanguni,
Leo nawaletea ushahidi mwingine wa mapenzi ya Muhammad na Shetani ambaye alisilimu na kuwa Muislam. Hebu ungana nami moja kwa moja.
Ni bahati mbaya kwamba Adamu Hawa hawakufanikiwa kufanya jitihada za kumwezesha shetani na wanae kuuomba msamaha kwa mwenyezi Mungu na kuwa Waislamu, ni mtume Muhammad tu ndiye aliyemsilimisha shetani akawa muislamu… (KITABU CHA ASILI YA MAJINI UK 20)
Sasa Ikiwa shetani ni muislamu, na sisi tunajua kuwa shetani yeye ndiye adui yetu namba moja ambaye sisi hatupaswi kushirikiana nae,
Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, nae atawakimbia.
Sasa iweje tena tumfuate shetani katika uislamu? Kwa kuwa shetani ambaye aliwadanganya Adamu na Hawa.
Kwanini tuifuate dini ambayo ina mapenzi na Shetani?
KUMBE NDIO MAANA SHETANI AKAWEKA AYA ZA SHETANI KWENYE QURAN.
KUMBE SHETANI NI RAFIKI YA MUHAMMAD NA NI MUISLAMU. HUU NI MSIBA KWA WAISLAM

Monday, September 26, 2016

YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WAISLAMU WOTE PAMOJA NA MUHAMMAD, MAJINI, NA ALLAH



Nani atakuhukumu walimwengu wote?
Biblia inakujibu kuwa Yesu ndie atakaye hukumu walimwengu wote, ikimaanisha Muhammad, Allah, Waislam wote, Majini yote yatahukumiwa na Yesu.
(Zaburi 58:11 ), ‘Hakika yuko Mungu anayetawala katika dunia“. (Ufunuo 18;8 ) “Kwasababu hiyo, mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti na huzuni na njaa naye atateketeza kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“. Tene ndiye atakaye ihukumu Dunia yote “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote,bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.
(Mathayo 25:31-32 ) “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake,naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi”.
(Matendo 10:42 ) “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( WARUMI 2:16 ) “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na injili yangu,kwa Kristo Yesu“. (2 Timotheo 4:1 ) “Nakuagiza mmbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu waliohai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.
Sasa kwanini suimpokee Yesu ambaye atakuhumu maisha yako/ Kumbuka, HAKIMU NI YESU NA SIO ALLAH, AU MUHAMMAD.
Karibu kwa Yesu
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo

YESU ALIUMBA KILA KITU



Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake (Yohana 1:3,14 ) “vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika. Naye Neno alifanyika mwili; nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli”. 

Yesu aitwa Neno la Mungu (Ufunuo 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(Yohana 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.

Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..

Katika yeye vtu vyote viliumbwa (Wakolosai 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani. Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.

YESU NI MUNGU

YESU ALIUMBA KILA KITU

Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo

www.maxshimbaministries.org

SINAGOGI SIO MSIKITI

TUNAZIDI KUCHAMBUA HOJA ZA MIHADHARA ya Kiislamu

LEO TUANGALIE SINAGOGI!! Sehemu ya pili
Kama tulivyosema Neno SInagogi linatokana na Kigiriki συναγωγή sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania בית כנסת beit knesset yaani "nyumba ya mkutano".
Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia sinagogi.
Katika lugha ya kiebrania neno “ beit ” linamaana “ nyumba” ndio maana hata ukisoma bethsaida “ Nyumba ya mvuvi” au bethsania-Nyumba ya masikini. Bethlehemu, nyumba ya mkate. (Soma injili imetajwa sana majina haya )
Katika Israeli ya Kale (kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK) inaonekana hakukuwa na sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.
Inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.
Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.
Neno hilo limetumiwa katika maana hiyo ya mukutano kwenye Septuajinti, yaani, tafsiri ya Kigiriki ya Maandiko ya Kiebrania. Lakini, baada ya muda neno hilo lilitumiwa kurejelea jengo ambapo watu walikutana kuabudu. Kufikia karne ya kwanza W.K., karibu kila mji ambao Yesu alitembelea ulikuwa na sinagogi; majiji yalikuwa na masinagogi kadhaa; jiji la Yerusalemu lilikuwa na masinagogi mengi.
Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:
• sanduku la Torati ni kabati au sanduku ambako hati za kuviringisha zenye mwandiko wa Biblia ya Kiebrania hutunzwa;
• taa inayoendelea kuwaka muda wote;
• meza ya msomaji ambako hati za torati hufunguliwa na kusomwa;
• mimbari ya mafundisho;
• kinara cha menorah chenye mishumaa 7 au 9.
Karibu na sanduku hilo, kulikuwa na viti vya mbele vilivyopangwa kuelekea kutaniko, navyo vilikaliwa na maofisa-wasimamizi wa sinagogi pamoja na wageni wowote waheshimiwa. (Mathayo 23:5, 6)
Hii ni tofauti ni Misikiti ya kiislamu isiyokuwa na Viti
Karibu na eneo la katikati la sinagogi palikuwa na jukwaa lililokuwa na kinara na kiti cha msemaji . Kwenye upande wa mbele, wa kushoto, na wa kulia wa jukwaa hilo, kulikuwa na viti vya washiriki wa kutaniko .

KAMA YESU NI MUNGU, KWANINI ALIKUFA?

Image result for je yesu ni mungu

JE, MUNGU ANAKUFA?
Hayo ni maswali ya Waislam kila siku, na kwenye hii mada nitayajibu.
SOMA: 1 Petro 3: 18 - 19 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
Neno la Mungu linasema kuwa MWILI WAKE NDIO ULIUWAWA BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA. Sasa hakuna kushangaa tena maana tufahamu ulio uwawa ni Mwili wake tu bali Roho yake haikuuwawa.
Maandiko yanasema kuwa MUNGU NI ROHO, sasa aliye UWAWA NI MWILI TU BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA
1 Timotheo 6:15-16 15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina
Hii asilia ya Mungu haikubadirika pale ambapo “NENO” lilipo kuwa Mwili (Yohana 1:1, 14). Badala yake, Neno liliunga ubinadamu (Wakolosai 2:9). Hivyo basi, Umungu wa Yesu Kristo haukuharibika na au badirika. Zaidi ya hapo, Yesu hakuwa mtu tu ambaye alikuwa na Mungu ndani yake au Mtu aliye fanya kazi ya Mungu pekee, la hasha, Yesu ni Mungu katika Mwili na ni sehemu ya Pili katika Utatu Mtakatifu. Biblia inatuambia katika Waebrania 1 aya ya 3 kuwa: Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno Lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni. Hivyo basi, asilia hizi mbili za Yesu Kristo haziwezi kuchanganywa (Eutychianism), vile vile haziwezi kuwa pamoja na kuwa Mungu-Mtu (Monophysitism). Hizi asili mbili ni tofauti na zinajitemea na wakati huohuo ni moja katika Yesu (person of Jesus). Huu muungano unaitwa Hypostatic Union.
USHAHIDI ZAIDI WA ASILIA MBILI YA YESU
Mafundisho ya muungano wa Hypostatic ni ya “communication idiomatum” (Ni maneno ya Kilatini “Communication of properties”). Haya ni mafundisho ya adhama mbili za Yesu Kristo za Mungu na Binadamu zote zipo ndani ya Yesu Mtu “person of Jesus”. Hii inamaanisha kuwa, binadamu Yesu alikuwa na haki ya kusema kuwa “Alikuwa na utukufu na Baba Mungu kabla ya dunia kuumbwa soma Yohana 17:5), vile ile kudai kuwa alitoka Mbinguni (Yohana 3:13), na kudai kuwa alikuwa kila mahalai “omnipresence (Matayo 28:20). Haya madai yote ya Yesu ni adhama za Mungu na kuwa yeye Yesu alikuwanayo.

Saturday, September 24, 2016

ALLAH KATEREMSHA AYA NA KUSEMA SINAGOGI SIO MISIKITI

Image result for SINAGOGU

HUU NI MSIBA MKUBWA SANA KWA WAISLAM WOTE DUNIANI.

Hii mada ni fupi na ni MSUMARI WA MWISHO KWENYE JENEZA LA WAISLAMU.

Katika Surat Hajj, nukuu naiweka hapa chini andiko linataja majina ya majengo mbalimbali ya ibada ikiwemo na Sinagogi, Makanisa na Misikiti. Sasa kama SINAGOGI NI MSIKITI, kwanini Allah ameyatenganisha kwenye Quran yake?

KWANINI TUANDIKE MATE WAKATI WINO UPO. HAYA SOMA AYA HAPO CHINI NA UINGIE MWENYE KWENYE LINK YA QURAN NILIYO ITOA.

Suratul Hajj 40. Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na MAKANISA, NA MASINAGOGI, NA MISIKITI, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.http://www.quranitukufu.net/022.html

INGIA KWENYE LINK YA QURAN (SURATUL HAJJ AYA YA 40http://www.quranitukufu.net/022.html ) USOME MWENYE NA KUACHANA NA NGOJERA ZA WAFIA DINI WA MAREHEMU MUHAMMADhttp://www.quranitukufu.net/022.html

AYA HAPO JUU INATAJA MAJENGO TOFAUTI TOFAUTI YA IBADA IKIWEMO, SINAGOGI, KANISA, MISIKITI. KAMA SINAGOGI NI MISIKITI, KWANINI ALLAH AMEYANGANISHA NA AU TENGANISHA MAJENGO KATI YA SINAGOGO NA MISIKITI?

NDIO MAANA HUWA NASEMA UISLAM NI DINI YAKUTENGEZA TU NA WALA HAIKUWEPO KABLA YA MUHAMMAD.

Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.



Thursday, September 22, 2016

UMUHIMU WA KUWEKA IMANI YAKO KATIKA JINA LA YESU KRISTO

Image result for katika jina la yesu

“Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa Na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango WA hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, tutazame sisi. Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao. Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.”  (matendo ya mitume 3:1-8)
Ukifuatilia historia ya kilema huyu aliyeponywa utaona ya kuwa alikuwa hivyo tangu kuzaliwa, na alipopona alikuwa na umri uliopita miaka arobaini (matendo ya mitume 4:22)
Siri ya muujiza huu ilikuwa ni nini?  Je! Kilema huyo alipona kwa uwezo wa petro na yohana au kwa uweza wa Jina la Yesu Kristo! Nauliza maswali haya kwa kuwa watu wengi wakiona mtu anatumiwa na Mungu katika uponyaji wanaweka imani zao kwa huyo mtumishi badala ya kuweka imani zao katika Jina la Yesu Kristo!
Na ndivyo ilivyokuwa wakati kilema huyu alipopona, watu waliokuwa hekaluni waliwashangaa akina petro na yohana kama vile kilema alipona kwa uwezo wao. Petro alipoona hali hiyo aliamua kuwaeleza watu haoukweli ulivyo, akasema;  “Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana. Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi?”  (Matendo ya mitume 3:11-12).
Petro alikuwa anafanya jambo muhimu hapakwa kusaidia kubadilisha mawazo ya watu ya kufikiria kuwa uwezo uliomponya yule kilema ulikuwa ni wa petro na yohana ambayo haikuwa kweli. Kama uwezo huu haukuwa wao, muujiza huu siri yake ni nini? Petro aliendelea kusema hivi, “Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe. Bali ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe mwuaji; mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake. Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.” (Matendo 3:13-16)

Bwana Uliyewaita Anastazia Hanson

OMBA KWA JINA LA YESU KRISTO

KILA mkristo anapenda awe na maisha ya maombi yaliyo na mafanikio – anapenda akiomba kitu kwa Mungu ajibiwe. Lakini mara nyingi nimewasikia wakristo kadhaa wakisema wameomba jambo Fulani kwa Mungu lakini hawajajibiwa. Wengine wanapofikia hali ya namna hii, hukata tama – hata wokovu unaanza kupoa utamu wake.
Image result for jina la yesu kristo
Kuna sababu nyingi ambazo zimeandikwa ndani ya Biblia zinazoeleza chanzo cha kutijibiwa maombi ya watu. Sababu mojawapo ni kutokuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu – au kwa tafsiri nyingine kuomba kinyume na maagizo ya Mungu (Yohana 5:14-15)
Yesu Kristo alituachia maagizo mbalimbali juu ya maombi katika kulitumia Jina lake – mojawapo ni hili;

                        Tumuombe Baba kwa jina la Yesu Kristo.
Katika kitabu cha Yohana 16:23-24; Yesu Kristo alisema;  “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.”
Wazo la kwanza tunalopata katika agizo hili ni kuelekeza mawazo na maombi yetu kwa baba Yetu aliye mbinguni wala si kwa malaika wala kwa wanadamu. Ndiyo maana imeandikwa; “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (Waebrania 11:6)
Yesu Kristo alipokuwa anawafundisha kuomba alisema; “basi ninyi saline hivi; Baba yetu uliye mbinguni….” Jambo kubwa alilotaka wanafunzi waone ni umuhimu wa kujua na kuelekeza mawazo na maombi yao kwa BABA MUNGU. Watu wengi wamekwama kwenye maombi kwa kuwa katika mawazo yao wamewategemea sana watu katika kupata majibu ya maombi yao badala ya kumtegemea Baba Mungu.
Sisemi ni vibaya kushirikiana na watu wengine katika maombi – hapana. Bali nataka ujue kuwa hata ukiwashirikisha watu wakusaidie kuomba – wewe elekeza mawazo yako kwa Baba Mungu na kumtegemea Yeye kukujibu.
Wazo la pili tunalolipata katika maagizo ya Yesu Kristo juu ya maombi yaliyoandikwa katika (yohana 16:23-24) ni tuombe kwa Jina lake. Hakusema tuombe kwa ajili yake au kwa niaba yake, bali alisema tuombe kwa jina lake.
Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.” (yohana 16:23-24)
Mara kwa mara utawasikia watu wakimaliza maombi yao kwa kusema “kwa ajili ya Yesu Kristo, amina”. Lakini sioni mahali ambapo Yesu Kristo alisema tuombe kwa ajili yake. Hebu fikiri mtu anaomba uponyaji wa tumbo halafu aombe akisema “Naomba tumbo langu lipone kwa ajili ya Yesu Kristo”. Je! Ni Yesu Kristo anayehitaji uponyaji au ni wewe?
Yesu Kristo alisema tuombe kwa Jina lake na siyo tuombe kwa ajili yake wala kwa niaba yake – kumbuka hilo kila wakati unapolitumia jina la Yesu Kristo katika maombi. Lakini kama unataka mtu apone kwa ajili ya Yesu Kristo, basi omba kwa jina la Yesu Kristo – ili Jina hili litukuzwe.

TRENDING NOW