Wednesday, November 16, 2016

SHETANI LA ULAFI KATIKA UISLAMU


Ndugu msomaji,
Leo ningependa tujifunze kidogo kuhusu roho ya ulafi ambayo inawasumbuwa ndugu ztu katika Adam. Hebu tusome Biblia kama ushahidi.
Wafilipi 3: 19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
Walafi wao wamesha amua kuabudu chakula na mungu wao ni matumbo yao. Mtu mlafi akiona chakula, basi yeye hula kwa haraka haraka na kujaza tumbo lake mpaka anavimbiwa. Ulafi ni dhambi kama ilivyo sema kwevye Wafilipi hapo juu. Ulafi ni kuabudu tumbo.
Mithali 23: 20 Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. 21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Watu wanao kula nyama kwa Pupa mpaka wanavimbiwa na kushindwa kutembea, hao wana roho chafu ya ulafi, na ni dhambi kuabudu chakula au kuwa mtumwa wa chakula au mtumwa wa tumbo lako.
Kuna dini fulani wao wanapo dai kuwa wanafunga siku thelasini, huwa wanabadilisha masaa ya kula na kula usiku kucha mpaka wanavimbiwa matumbo yao. Hiyo dini ni dini ya walafi na wanatenda dhambi, huku wao wakifikiria kuwa wanafunga kwa Allah wao.
Wagalatia 5: 16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
26 Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.

UTATA MKUBWA KATIKA KORAN: ADAM ALIUMBWAJE?


Binadamu aliumbwa kutoka nini? Tone la Damu? Maji? Udongo? Vumbi?
Jamani huu nao ni Msiba Mkubwa katika taifa la Allah. Hivi, Allah alikuwa msanii au alikuwa nani/ Maana anapenda sana kuchanganya madawa. Leo ALLAH AMELETA UTATA Katika uumbaji wa Binadamu. Sasa tuanze kwa kusoma kitabu chake kilicho shushwa na Jibril msaidizi wake.
Je, Adam aliumbwa kwa tone la Damu?
Quran 96 1-2
1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, ***2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, ***
Allah anasema kuwa, Binadamu aliumbwa kwa tone la damu. Endela kupa ilmu ya Koran.
Je, Adam aliumbwa kutokana na Maji?
Quran 25:54. Naye ndiye aliye muumba mwanaadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji. Na Mola wako Mlezi ni Muweza. ***
Allah anachanganya madawa. Sasa anaumba Mwanadamu kupitia MAJI. Tuendelee kusoma usanii wa Allah.
Je, Binadamu aliumbwa kutoka kwa Udongo?
Quran 15:26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. ***
Allah amebadilika tena, sasa anaumba Mwanadamu kupitia Udongo. Jamani huu si Msiba?
Endelea kupata Elimu.
Je, Binadamu aliumbwa kutoka VUMBI?
Quran 30:20. Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kutoka Vumbi. Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote. ***
Ndugu zanguni, hivi kweli Koran ilishushwa kutoka kwa Mungu? Mbona kuna UTATA kila sehemu?
Binadamu aliumbwa kutoka nini? Tone la Damu? Maji? Udongo? Vumbi?
Kweli Allah anafahamu yote, ingawa hajui alimuumbaje Adam.
Katika Huduma yake
Max Shimba Ministries Org.

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA KWANZA)


Ndugu msomaji,
Mwezi huu nitaweka mada kadhaa zitakazo fundisha kuwa, Isa wa Quran na Yesu wa Biblia ni wawili na tofauti:
MAANA YA JINA LA ISA
Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maana. Mfano majina haya ya kiarabu yana maana hizi: Muhammad, linamaanisha mwenye kushukuriwa, Abdalla ni Mtumwa wa Allah; Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira; Abu Huraira ni baba wa Mapaka. Aidha majina ya Kiebrania nayo pie yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova; Ezekiel inamaanisha Mungu hutia nguvu, Daniel – Mungu ni hakimu wangu.
JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?
Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa/tafsiriwa na Imam Baidawi Vol 1 Ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe "ZERUZERU". Hii ndio maana ya Jina la Isa wa Quran. Je, Yesu wa Biblia maana yake nini?
JINA LA YESU MAANA YAKE NINI?
JINA Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11.
Katika Biblia ambayo ina jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; Neno Mwokozi kwa Kiingereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa Kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226.
Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
Leo tumejifunza kwa kifupi tu kuwa, Jina la ISA lenye maana ya Wekundu unao zidiana na weupe ni TOFAUTI KABISA NA Jina la Yesu lenye maana ya MWOKOZI katika Biblia. Zaidi ya hapo, tafsir ya Jina la Yesu kwa Kiarabu ni Yasu na sio Isa kama ambavyo Waislam wanadai katika vitabu vyao.
Mungu awabariki sana na tuendele kujifunza Neno lake bila ya kuchoka.
Katika huduma Yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Max Shimba Ministries Org.

YESU ALIMAANISHA NINI ALIPO SEMA MSIDHANI NALIKUJA KUTANGUA TORATI?


Baadhi ya watu wameshindwa kuelewa kuwa torati imeondolewa kwa sababu ya maneno ya Yesu aliposema “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Mathayo 5:17-18). Watu hawa hutumia andiko hili kujenga hoja kuwa Torati haikuondolewa.
Maana ya neno tangua:
Kulingana na kamusi ya Kiswahili Sanifu, neno “tangua” maana yake ni vunja kanuni au maafikiano; batilisha.
Maana ya neno “hata”:
Neno “hata” maana yake ni “mpaka”
Kwanza kabisa naomba nitoe mifano kadhaa ya mambo yaliyokuwa ni lazima muumini wa Agano la Kale afuate ili ahesabiwe haki ambayo leo hii ukiyafuata hauwezi kuhesabiwa haki mbele za Mungu:
1. Kutahiriwa; Katika Agano la Kale muumini asiyetahiriwa hangeweza kuhesabiwa haki hata kidogo. Katika Agano Jipya kutahiriwa siyo lazima ili uhesabiwe haki na Mungu (Mwanzo 17:9-10, Galatia 6:15).
2. Katika Agano Jipya tunaweza kula vyakula vyote isipokuwa vilivyotolewa sadaka kwa sanamu au vilivyonyongwa bila kuchinjwa, lakini wakati wa Agano la Kale kulikuwa na kuzuiliwa kula baadhi ya vyakula hasa baadhi ya wanyama kama vile sungura, nguruwe, samaki wasio na magamba, nk. (Matendo 26:12-18).
3. Katika Agano la Kale kulikuwa na utaratibu wa kutoa sadaka za wanyama ili mtu aweze kuhesabiwa haki. Hii ilikuwa sheria. Katika Agano Jipya Yesu amelitangua kabisa hilo halipo tena. Damu yake iliyomwagika inatosha kuondoa dhambi ya kila amwaminiye Yesu.
4. Katika Agano Jipya Kuhani alipaswa kuwa mtu mmoja tu amabaye alipaswa kuendesha ibada yote na kutoa sadaka za kuteketezwa. Hilo nalo Yesu alilitangua baada ya Kifo chake Msalabani kila amwaminiye anakuwa kuhani wa Mungu na anaweza kufanya ibada ya kuongea na Mungu moja kwa moja bila kupitia kwa mtu mwingine.

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA PILI)


Je, kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?
Taarfa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.
Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa == Gabrieli alivyomtokea mama wa Yesu:
WAISLAM-JIBRIL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Msikitini Qurani 19:16-17
WAKRISTO-GABRIEL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa nyumbani kwake - Lk 1:26-28
WAISLAM-Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji kipi wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Quran inasema kuwa Jibril ndiye aliyemletea utume Muhammad asiwapelekee Mayahudi (hana kosa) Sura 2:97
WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na Malaika Gabriel akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israeli (Lk 1:26) Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.
WAISLAM-Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili - Sura 19-17
WAKRISTO-Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu – Luka 1:28
WAISLAM-Jibril alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu - Sura 19-19
WAKRISTO-Lakini malaika Gabrieli alimwambia mama wa Yesu kuwa utachukua mimba – Luka1: 31
WAISLAM-Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu – Sura 19: 21. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe mwana mtakatifu.
WAKRISTO-Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu mama ya Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu (Luka 1:31; 2:21) Gabrieli hakusema kuwa atampa mwana Mariamu. Bali alisema, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani motto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.
TOFAUTI YA KUZALIWA KWA ISA NA YESU

QURAN NI SAWA NA GAZETI LA UDAKU


WAPAGANI WANASEMA QURAN NI SAWA NA HADITHI ZA KALE.
Hapa ni ushahidi wa baadhi ya mistari ya kuchaguliwa kutoka Quran kutuambia kwamba wapagani walikuwa na ufahamu kwamba Muhammad alikuwa anawaambia hadithi ya kale walizokuwa wamesikia kabla ya-Muhammad:
Wasioamini walisema kuwa Quran ni kama hadithi za watu wa kale wa Kipagani ... 08:31
Wasioamini walisema kwamba Aya za Muhammad zilinakiliwa kutoka hadithi za kale ... 16:24
Wapagani wengi walishasiikia hadithi za ufufuo kutoka katika hadithi zamani za Kipagani... 23:83
Makafiri walisema kuwa 'Qur'ani ni hadithi za kale ambazo walisikia kabla ya Muhammad' ... 25:5
Wasioamini walisisitiza kwamba Qur'ani ni hadithi kutoka vitabu vya kale ... 27:68
Wakasema makafiri Quran imejaa visa vya watu wa kale ... 46:17
Wasioamini wanaliziita na kuzifananisha aya za Muhammad na hadithi za kale ... 68:15
Quran ni sawa na gazeti la udaku tu.
Max Shimba Ministries

MUHAMMAD NI ADUI WA WAKRISTO


Quran 4:51 na 57 (Surat Al Maida)
Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika hao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
Ndio maana huwa nasema Uislam ni dini ya mashetani.

UISLAM NI DINI YA JEHANNAM


Quran 50 au Surat Qaf 30 (kuapa)
Siku tutakayoiambia Jahanamu, ‘Je! Umejaa?’ Nayo itasema ‘Je kuna ziada (zaidi? Naije tu!
Imesimuliwa na Anas kuwa: mtume alisema watu watatupwa jahanamu, Naye Allah ataiuliza jahanamu akisema je umejaa nayo jahanamu itasema kwani kuna nyingine zaidi na ije tu? Mpaka Allah atakapo ingiza mguu wake nayo jahanamu itasema inatosha! Inatosha

SABABU TANO KWANINI WAKRISTO WANAABUDU JUMAPILI


Ndugu msomaji,
Katika kijarida hiki kifupi, nitakuwekea sababu tano (5) kwanini Wakristo wanaabudu siku ya Jumapili.
Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-
1) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].
2) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].
3) Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO 2:1]
4) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].
5) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.
Hakuna andiko lolote linalosema mtu yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi. Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].
KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA
Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13].
Wokovu wetu siku hizi uko ndani ya Kristo, siyo kwa kushika Torati ya Musa. Kuna watu wasiijua Biblia tena hawaelewi hata Agano Jipya. Hawaelewi KWA NINI Yesu alikufa. Kwa mfano wanaposema, ‘Imeandikwa katika Kutoka 20:8-11 lazima tushiike sabato!’ Je! ina maana mtume Paulo alifundisha uongo? Au alitaka kutudanganya? Au Unafikiri Biblia inajipinga yenyewe? Je! Unaamini Biblia siyo neno la Mungu? Au kwa nini watu wanapenda kujizika katika Agano la Kale?
Najua kuwa narejea kwenye mambo yale yale ambayo tayari nimekwisha yaandika hapo juu. Lakini mambo hayo ni ya kimsingi. Ni lazima tuyaelewe mambo hayo pale tunapoyaangalia maisha ya watu wa Agano la Kale! Kwa kupitia Biblia nzima tunajifunza sasa juu ya Yesu Kristo na wokovu wake. Lakini kama Biblia ni neno la Mungu (na ndivyo lilivyo) kwa nini basi waopo watu wanaopinga mpango wa Mungu kupitia mwanae Yesu Kristo ili waweze kubakia katika mpango wa kale ambaop Mungu mwenyewe ameuondoa?
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo… Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.”
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 16, 2016

NENO "MUNGU" KWA KIARABU NI "ILAHA"


USHAHIDI UPO NDANI YA QURAN NA AYA ALIITEREMSHA ALLAH MWEYEWE.
Shahada: LA ILAHA ILLALLAH Muhammadur Rasulullah, Quran 3:18 na soma hapa pia (Sahih Al-Bukhari, Volume 4, Book 56, Number 725)
Hakuna Mungu ila Allah na Muhammad ni Mtume wa Allah. Hii ni Shahada wanayo sema Waislam au mtu anaye taka kuwa Muislam.
Kwasababu Waislam ni wabishi, basi leo nawawekea maana ya hiyo SHAHADA neno kwa neno:
Maneno hayo manne "lâ ilâha illâ allâh" yana maanisha hivi:
:
lâ = HAKUNA, no, not, none, neither
ilâha = MUNGU, a god, deity, object of worship
illâ = ISIPOKUWA but, except (illâ is a contraction of in-lâ, literally if not)
allâh = ALLAH, allâh
Kama tulivyo soma hapo juu maana ya hayo maneno Manne. Utangundua kuwa Neno ILAHA maana yake ni MUNGU na Neno ALLAH halina Tafsir na kubakia ALLAH (Thibitisha kupitia Al Tafsir Kitengo cha Tafsir cha Serikali ya Saudi Arabia/ http://www.altafsir.com/).
Kumbuka Allah hana wa kufananishwa na au linganishwa. Hivyo Kumfananisha Allah na Mwenyezi Mungu wa Wakristo ambaye ni Yesu au mungu Buddah, au mungu wa Rasta Fari au na mungu wa Wabantu ni KUKUFUR. Allah yeye kasema hana wa kufananishwa wala linganishwa. Kumbe basi Allah sio Mwenyezi Mungu.
NARUDIA TENA, TAFSIR YA NENO:
ILAHA ==> MUNGU
ALLAH ==> ALLAH
Hakuma wa kubisah sasa kuwa Allah sio Mungu.
LEO KWA MARA NYINGINE TENA TUMEJIFUNZA KUWA ALLAH SIO MUNGU.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

Jesus is good because He is God

 

TRENDING NOW