Tuesday, January 10, 2017

YESU KRISTO NI MUNGU ALIYEUMBA KILA KITU

Image may contain: text
Yesu Kristo ameumba mbingu, nchi, watu, na ulimwengu wote.
Biblia Takatifu inatuambia kwamba:
“...tuliumbwa katika Kristo Yesu...” (Waefeso 2:10)
Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa sisi wanadamu wote pamoja na viumbe vyote ni kazi ya mikono ya Yesu. Yesu ameumba vitu vyote; tendo la mtu kuukana Uungu wa Yesu ni jambo la kumkosea heshima Mungu aliyekuumba. Ndio maana Yesu aliwaambia Wayahudi kwamba: “...ninyi mwanivunjia heshima Yangu...” (Yohana 8:49).
Tusomapo Biblia Takatifu katika kitabu cha YOHANA sura ya kwanza, tunaona pameandikwa:
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” (Yohana 1:1,3,14)
Huyo “Neno” anayetajwa hapo ndiye Yesu Kristo. Mwandishi wa kitabu hicho cha YOHANA ametumia usemi wa: “...Neno alikuwako kwa Mungu...” akiwa anawafahamisha hususani Wayahudi waliokuwa wanajua kuwa YEHOVA ndiye Mungu wao. Kwa hiyo Yohana anasema “...Neno alikuako kwa Mungu...” kwa maana ya kwamba; huyu “...Yesu alikuwako kwa YEHOVA...” ambaye wao Wayahudi walimtambua kuwa ndiye Mungu wao.
Pia zaidi tunaona Yohana anafafanua kwa kusema kuwa; huyu “...Yesu alikuwa Mungu...” Ufafanuzi zaidi tunauona katika YOHANA 1:14 ambapo Yohana amefafanua kwa kusema; “...Yesu alifanyika mwili; akakaa kwetu...” Biblia Takatifu inamtaja kwa wazi kabisa kuwa Yesu ni Mungu na ameumba vitu vyote “...Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika...” (Yohana 1:3).
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

KATIKA TAURAT, ZABURI, INJILI HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM

1. KATIKA TAURAT YA MUSA, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM
2. KATIKA INJIL YA YESU, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM.
3. KATIKA ZABURI YA DAUDI, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM.
A. Kwanini Waislam wanadai eti Musa alikuwa Muislam, wakati Taurat iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?
B. Kwanini Waislam wanadai eti Yesu alikuwa Muislam, wakati Injili iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?
C. Kwanini Waislam wanadai eti Daudi alikuwa Muislam, wakati Zaburi iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?
Kama Waislam wanabisha, nionyesheni ipo wapi Taurat aliyo iteremsha Allah kwa Musa tuione? Na iwe na aya inayosema kuwa Musa alikuwa Muislam.
Quran inasema kuwa Allah ameitunza Taurat na Injil katika Surah 15 aya 9. Vile vile tunasoma kuwa Taurat na Injil vinasemwa kama kumbukumbu katika Surah 16:43, 21:7, 21:48, 21:105 na 40:53-54.
Kwahiyo, Surah 15:9 inakubali kuwa Taurat na Injil zimetunzwa na Allah. Kama ni kweli haya madai ya Quran:http://www.quranitukufu.net/005.html
1. Ipo wapi nakala ya Taurat ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
2. Ipo wapi nakala ya Injil ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
3. Ipo wapi nakala ya Zaburi ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyo teremshwa na Allah kabla ya Quran, na iwe na aya Adam anasema kuwa yeye ni Muislam.
Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyoteremshwa kabla ya Quran, na iwe na aya ambayo Ibrahim anasema kuwa yeye ni Muislam.
Waislam, ipo wapi Taurat ambayo mnadai kuwa Allah aliiteremsha kwa Musa? Mbona kila siku mnatuletea aya za Quran ambazo sio Taurat?
Kama kweli Allah aliteremsha Taurat kwa Musa, basi tuonyesheni wapi ilipo hiyo Taurat na sio aya dhaif za Quran. Hivi Quran sasa imekuwa Biblia - Mkusanyiko wa Vitabu?
Allah anadai kuwa aliteremsha Injil: Surat Al Maida 46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu. http://www.quranitukufu.net/005.html
Waislam, tuonyesheni wapi ilipo nakala ya Injil ambayo Allah anadai kuitunza katika Surat Al Hjr aya ya 9?
Hakika Allah hakuteremsha kitabu chochote kile zaidi ya maneno matupu yaliyo ndani ya Quran ya Jibril.
Allah sio Mungu. Musa hakuwa Muislam, Daudi Hakuwa Muislam, Ibrahim Hakuwa Muislam. Yesu hakuwa Muislam.
Kama kuna Muislam anao ushahid kuwa Musa, Daudi, Ibrahim, Yesu walikuwa Waislam, basi watuonyeshe wapi vilipo vitabu vyao ambavyo Allah anadai kuviteremsha. Waislam, sina muda na aya za Quran zilizo kuja miaka maelfu baadae.
Max Shimba Ministries.

MAHAKAMA YA KADHI HAIPO KWENYE QURAN

Image may contain: 5 people
KUMBE ALLAH HAITAMBUI MAHAKAMA YA KADHI
Ndugu wasomaji.
Leo ningependa kusema kuwa, dai la Waislam wa Tanzania la Mahakama ya Kadhi halina msingi wala usaidizi wa Quran.
Kwa wanao ifahamu Quran, watakubaliana na mimi kuwa HAKUNA AYA HATA MOJA ambayo Allah alisema na au Waamrisha Waislam waende kwenye Mahakama ya Kadhi. Narudia tena hakuna aya.
SASA NDUGU WAISLAM:
1. Who appoints Chief Kadhi and Kadhis?
--Nani na au mnamteuaje Kadhi Mkuu na Kadhi? Leteni aya.
2. What are the qualification for appointment to the office of a Kadhi (including a Chief Kadhi)?
-- Je, mnatumia qualification/elimu zipi kuchagua/kufanya utezi wa Ofisi ya Kadhi na Kadhi mkuu/ Leteni aya.
3. Since the Kadhis are not trained lawyers who understand the Evidence Act and the Civil Procedure Act, how and/or what will they use to administer their Courts?
-- Inafahamika kuwa Kadhi sio Mawakili walio somea ambao wanaelewa ushahid wa keshi ambazo si za jinai na jinai, SASA hawa Kadhi watatumia nini katika kusimamia Mahakama ya Kadhi?
4. Muslims are mainly of two sects in Tanzania - the Sunni and Shia. Majority of the Muslims in Tanzania are Sunni Muslims but there is a significant population of Shia Muslims too and consideration ought to be given to the appointment of Kadhis of the Shia Sect to cater the interest of the Shia Muslims. Will they have two different Courts? For Sunni and Shia?
--- Waislam wapo katika makundi mawili makubwa, Sunni na Shia. Wengi wa Waislam wa Tanzania ni Sunni, ingawa kuna Shia wengi vile vile. JE, Hii Mahakama ya Kadhi itatumia Kadhi wa dhehebu lipi katia ya hayo mawili? Je, watakuwa na Mahakama mbili tofauti za Sunni na Shia?
5. How will Muslim Women be protected since: Muslim law regards women as less than men in matters of both marriage and divorce, as well as devolution of property: Holy Quran Surah 2:228-232, and Surah 65:1-7 (only a man may divorce his wife even if he is required to provide for her); a man may beat his wife, even if lightly, the evidence of two women, is equal to evidence of one man (Surah 2:282). The application of such beliefs of faith are contrary to the Constitution.
---Kivipi Wanawake wa Kiislamu watatetewa kwenye hizi mahakama? Inafahamika kuwa Sheria za Kiislam zinakiri kuwa Mwanamke ni nusu ya Mwanaume, au yupo chini sana ya Mwanaume. Je, katika kesi ya kutoa talaka na mirathi, hii mahakama itawezaje kumtetea Mwanamke ambaye yupo nusu ya Mwaume? Sura 2: 228-232 na Sura 65:1-7 ( zinasema mwenye haki ya kutoa talaka ni Mwaume tu) Mume anahaki ya kumpiga mkewe, Ushahidi wa wanawake wawili ni sawa na ushahid wa mwanaume mmoja, (Sura 2:282). Huu utamaduni wa Kiislam, ni kinyume na sheria za nchi.
Je, Mwanamke atatetewa vipi kwenye hizi Mahakama?
Islamic "Kadhi" courtsis illegal and discriminatory.
Kwanini mnamsaidia Allah kwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi?
Waislam, nileteeni aya ambayo Allah anasema kuwa muende kwenye Mahakama ya Kadhi.
Mkiniletea aya kutoka Quran inayo waamrisha kwenda kwenye Mahakama za Kadhi, leo hii nitasilimu na kuwa Muislam.
SWALI LA MWISHO:
KWANINI ALLAH HAKUTEREMSHA AYA INAYO WARUHUSU WAISLAM KUWA NA MAHAKAMA YA KADHI?
Haya nasubiri ajibu ya aya na sio matusi.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries Org.

KATIKA QURAN WAKRISTO HAWAITWI MAKAFIRI

Image may contain: text
Je, Makafiri ni akina nani?
Je, unawafahamu makafiri wa kwanza ni akina nani?
Neno kafiri ni neno ambalo lipondani ya Biblia takatifu, kabla hata ya Muhammad mtume wa waislamu kuzaliwa na wala uislamu haujakuwepo nawala Muhammad wala Quran haijaandikwa nawale Waarabu wa 4. Neno hilo kafiri lipo kwenye biblia kwa maana nyepesi neno hilo waislamu wamekuta likitumiwa na waliokuwa wanatumia biblia takatifu.
Katika Quran sijaona Wakristo wakiitwa MAKAFIRI, bali Quran nzima inawaita WAKRISTO wamchao mungu tena wasomi, SURATUL AL-MAIDAH 5:82.
Kwa kuthibitisha kuwa neno KAFIRI limo ndani ya BIBLIA hebu tuziangalie aya chache ndani ya Biblia.
EZEKIEL 34: 28-31
Mistari hiyo ni mungu mwenyewe anawahakikishia wana wa Israel kuwa hawatakuwa mateka wa MAKAFIRI, hivyo neno hilo hapo limetumika kabla hata uislamu haujakuwepo.
NEHEMIA 5: 8-9
NEHEMIA 5:17
NEHEMIA 6:16
MAOMBOLEZO 1:3
MAOMBOLEZO 1:10
MAOMBOLEZO 5:2
1TIMOTHEO 1:8-11
YUDA 1:4
1YOHANA 4:1-6
Maneno hayo yalisemwa kabla ya Muhammad hajazaliwa wa Quran haijaandikwa nawale waarabu wa4 yaani Saydina Abubakar, Omar, Athumani na Ali na uislamu ulikuwa haupo.
TUANGALIE NENO KAFIRI LINAVYOTUMIKA
_________________________
Neno KAFIRI ni neno la Kiarabu lenye maana ya Mpingaji kwa kiswahili.
Yaani anaepinga maneno ya Mwenyezi Mungu neno hili lilikuwepo kwenye Biblia kama tulivyoona kwenye baadhi ya mistari ya biblia hapo juu.
Ilikuwepo neno mpingaji KAFIRI nilazma kuwepo na kauli tangulizi iliyotangulia kusema kwahiyo kauli itakayofuata ya kupinga inaitwa kauli ya mpingaji kwa kiarabu KAFIRI.
Waislamu mara zote hukosi kuwasikia wakisema hawa MAKAFIRI wanatupa tabu au tuwakomeshe au wapigwe hawa MAKAFIRI kauli zao hizo zikitulenga sisi WAKRISTO.
SWALI LA UFAHAMU
Ni kati ya WAKRISTO au WAISLAMU nani MAKAFIRI?
2) Ni kati ya Imani ya KIKRISTO na dini ya KIISLAMU ni nani ilitangulia kuwepo duniani?
3) Ni kati ya YESU na Muhammad ni nani aliyepinga kauli ya mwenzake iliyotangulia?
HISTORIA FUPI KATI YA YESU NA MUHAMMAD.
Bwana Yesu ndiye mwanzilishi wa Imani ya Kikristo.
Waebrania 12:2
Huu ni mwaka 2015 tangu bwana Yesu alipopaa kurudi mbinguni na ni mwaka wa 1436 kwa mwaka wa kiislamu niandiko somo hili la KAFIRI kwani Muhammad alizaliwa mwaka wa 570 nandiye mwanzilishi wa dini ya kiislamu baada ya Yesu.
Hii inathibitisha kuwa Yesu alitangulia kuwepo duniani kabla ya Muhammad hakuna anaepinga hilo.
Kwamaana hiyo kauli za Yesu zitakuwa tangulizi na kauli za IMANI ya Kikristo zitakuwa kauli tangulizi.
Na kauli za Muhammad na Waislamu zitakuwa kauli za kupinga tangulizi.
Yohana 9:35-38
Kauli ya kusema yeye ni mwana wa mungu alijisema yeye mwenyewe Yesu aliitumia mwenyewe katika mistari ya sura ya hapo juu.
Hiyo ni kauli tangulizi ikipatikana kauli inasema Yesu sio mwana wa mungu hiyo ni kauli inayopinga maanayake ni KAFIRI?
JE NI NANI ALIEANZA KUSEMA YESU NI MWANA WA MUNGU?

KWANINI TUNAKULA NGURUWE? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: 4 people, people standing, shorts and outdoor
Kwa taarifa yako Allah ameruhusu kula Nguruwe.
* Mafundisho ya Quran Kuhusu Nyama ya nguruwe;
Pamoja na kuwa waislamu wanatushutumu sana wakristo kuwa tunakula Nguruwe Quran inajikanganya sana katika swala zima la kuliwa ama kutokuliwa kwa mnyama huyu ni muhimu kuangalia, kwa ufupi hakuna aya maalumu katika Quran inayoharimisha na kukataza kula nguruwe
Quran inasemaje kuhusu nyama ya nguruwe;-
Quran inaeleza wazi kuwa Mungu aliharimisha Vitu vizuri (akiwemo Nguruwe) kwa Wayahudi kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, yaani Mwenyezi Mungu aliwakataza kula nyama hii kama sehemu ya kuwahukumu wayahudi na si vinginevyo soma (Surat an-nisaa 4;160).
Quran inasema hivi katika aya hiyo “Basi kwa dhulma yao hao Mayahudi tuliwaharimisha vitu vizuri walivyohalalishiwa na vilevile kwa sababu ya kuzuiliwa kwao watu wengi na njia ya mwenyezi Mungu”
ni aya iliyo wazi kuwa wayahudi walizuiliwa vitu vizuri kwaajili ya dhuluma Mungu alitaka kuwahukumu kwa kuwanyima baadhi ya vitu vizuri Quran inakiri wazi kuwa Nguruwe ni kitu kizuri Umeona?
Quran inafundisha kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyo harimishwa (Surat al-Imran 3;50).
Quran inasema haya katika aya hii “ Na nitakuwa Msadikishaji way ale yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati na nimekuja ili NIKUHALALISHIENI yale MLIYOHARIMISHWA na nimekujieni na hoja Kutoka kwa Mola wenu kwa hiyo mcheni mwenyezi Mungu na NITIINI”
Hayo ni meneno ya Yesu Ndani ya Quran ikionyesha wazi kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyoharimishwa katika Tourati na anatuamuru kumtii, ni wazi kuwa Yesu ameruhusu kula Nguruwe na Quran pia
Quran imehalalisha kula vilivyo vizuri walavyo waliopewa kitabu (Al-maida 5;3-5).
Sura hii almaida maana yake maswala ya meza inasema hivi “……..Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni Halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao…”
Hii ni aya iliyo wazi inayoruhusu kila muislamu kula vyakula vya wakristo na wayahudi na sisi kula vyao umeona!
Quran ina kigugumizi kwa vile hakuna katazo la moja kwa moja kuhusu kutokula Nguruwe yaani inakataza kula Nguruwe na wakati huohuo inaruhusu endapo utashurutishwa na njaa (Al-baqara 2;173) au kama una dharula waweza kula hapa ndipo quran inapojikanganya ni muhimu kujiuliza imekataza au imeruhusu? Na dharula hii ni ipi? Quran inajibu kuwa dharula hii ni njaa (Al-an nam 6;145)Quran inasema kula bila kupita kiasi hili ni jema kwani Biblia inafundisha kuwa hata kama una njaa kiasi gani kula kupita kiasi hata kama si nguruwe chakula chochote ni ulafi ni dhambi (Galatia5;21)
Quran inafundisha kuwa Mungu hakuharimisha chochote ila wazee wa kiyahudi waliharimisha kwa mapokeo yao tu (Al-an nam 146)
Quran inatahadharisha kuwa makini kumzulia Mungu uongo kuwa ameharimisha kitu kumbe hakuharimisha chochote (An Nahl 16;116)
Quran inaamuru uletwe Ushahidi kuwa ni wapi Mungu ameharimisha wanyama? Soma (Al an- am 6;150).
Hivyo ukisoma kwa makini Quran utaona hakuna kilicho haramu ndugu zangu waislamu kula nguruwe ni ruksa ila kiasi tu usizidishe ndivyo Quran inavyofundisha kama husadiki pale uwanja wa sabsaba Tanga kwa Minchi waislamu wenzenu hujumuika kula kiti moto kila iitwapo leo kwani wameelimika na wamegundua siri hii. Mimi sikushawishi ila nina kuweka huru kama mwalimu wa kweli ya Mungu “….. Mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru
Mafundisho ya Agano jipya kuhusu vyakula (Nguruwe).
Biblia inasema mafundisho yoyote yanayokataza mtu kula vitu Fulani ni mafundisho ya Mashetani (1Timoth 4;1-5). Ndio maana waganga wa kienyeji mtu anapokwenda kuaguliwa hukatazwa kula baadhi ya vitu Mungu sio Mganga wa kienyeji. Na wanaomwamini hawana sheria ya kuwazuia nini cha kula au kutokula
Biblia inasema hakuna kitu najisi kwa mtu asiye najisi lakini kitu Fulani ni najisi kwake yeye aliye najisi (Rumi14;14)Biblia inafundisha kuwa kula au kutokula hakuongezi utakatifu wala hakuzuii tamaa za mwili (Kolosai 2;16-23) hivyo hatupaswi kujitia katika mambo ya kutunga tu ya mtu,au akilizake na maono ya wanao abudu malaika kumuabudu Mungu hakuji kwa kula au kutokula aina fulani ya vyakula bali katika moyo safi (Math 5;8)
Biblia inafundisha kuwa unajisi wa mtu hautoki nje bali ndani ya mtu pia Yesu alitakasa vyakula vyoote (Marko 7;14-16,17-19)
Paulo mtume alifundisha kuwa chakula ni kwa tumbo tu na si mambo ya rohoni
(1Koritho 6;13). Hoja ya Pepo waliotolewa na Yesu kuwaingia nguruwe je ina maana gani?
USIKOSE SEHEMU YA PILI........
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom.

"MUISLAMU ZINDUKA KUTOKA USINGIZINI ILI UJUE KUWA MKRISTO SIYO KAFIRI"


Najua unaweza kustaajabu ni vipi muislamu wewe uzinduke ili hali unajiona kuwa u macho haupo kwenye Usingizi? ninaposema kuwa unajiona u macho ni katika imani uliyo nayo juu ya Mkristo kuwa ni kafiri, hivi ndivyo unavyoamini kwa sababu uliminishwa hivyo, ukaamini hivyo, kwa sababu tu Quran inasema! 👇
وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
التوبة (30) At-Tawba
Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!
Muislamu ukisoma aya hii moja kwa moja unaamini kuwa Wakristo ni Makafiri kwa kusema kuwa Masihi Yesu ni Mwana wa Mungu! unaamini kabisa kuwa hayo maneno ya kusema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, tunayosema sisi kwa vinywa vyetu yaani sisi ndo tumebuni, hivyo unatuona sisi ni Makafiri! tena unafurahia ujio wa Quran kuwa umekuja kwa ajili ya 👇
وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا
الكهف (4) Al-Kahf
Na kiwaonye wanao nena: Mwenyewe Mungu ana mwana.
مَّا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا
الكهف (5) Al-Kahf
Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu.
Nawe unaamini fika kuwa Quran imekuja kwa ajili ya kuwaonya Wakristo kwa sababu wanasema kwa vinywa vyao kuwa Mwenyezi Mungu ana mwana, nawe bila kuzinduka uangalie kama kuna usahihi wa jambo hilo unakurupuka na kuanza kusema kuwa, Wakristo ni Makafiri, LEO naomba nikuzindue ili kama unapenda kwenda kwenye UFALME WA MUNGU, basi uungane nami leo.
JE! NI KWELI KWAMBA WAKRISTO WANASEMA KWA VINYWA VYAO KUWA YESU NI MWANA WA MUNGU?
Hili 👆ni Swali la msingi sana mtu kujiuliza, kabla ya kuamini kuwa Wakristo wanasema kwa vinywa vyao na kuwaona ni makafiri (wenye kwenda kinyume na Mungu) kabla Wakristo hawajapatikana, na Yesu ambaye ndiye chimbuko la Wakristo hajazaliwa, Malaika alisema. 👇
Luka 1:30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

UPO WAPI UTHIBITISHO WA AYA KUWA MUHAMMAD ALITAIRIWA?

Image may contain: food
KUMBE MTUME MUHAMMAD HAKUTAIRIWA.
Ndugu msomaji,
KATIKA sehemu nyingi za ulimwengu, watoto wa kiume wanatahiriwa kwa sababu za kiafya. Watu fulani katika nyakati za zamani, kama vile Wamisri, walitahiriwa, yaani, walikatwa magovi ya kiungo chao cha kiume.
Yesu mwenye asili mbili ya Binadamu na Mungu, yeye alitairiwa kama BINADAMU. Kwa mujibu wa Agano la Kale, mapokeo haya yalianzia na Ibrahimu, Katika Mwanzo 17:10-13, imeandikwa, “Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na nyinyi. Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako. Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa na fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.
Katika Injili kwa mujibu wa Luka 2:21: “Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.” Kwa hiyo, kutahiriwa ilikuwa ni sehemu ya njia ya Yesu.
LAKINI NILIPO ISOMA QURAN NA KUSOMA VITABU VINGINE VYA KIISLAM KAMA SAHIH AL BUKHARI, NIKAGUNDUA KUWA, NABII WA ALLAH AITWAYE MUHAMMAD YEYE HAKUTAIRIWA NA HAKUNA UTHIBITISHO WA KIMAANDIKO AU HISTORIA KUWA MUHAMMAD ALITAIRIWA.
Waislam bila ya jazba wala kutokwa mapovu. Naomba mnijibu swali langu:
Kwanini mnafuata Muhammad nabii wa Allah ambaye hakutairiwa?
Kumbuka kutuna hakufai na ni ishara kuwa wewe umejambiwa mdomoni na Shetani:
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa: Mtume (s.a.w) amesema, "Ye yote mwenye kutukana, basi huyo amejambiwa na Shetani katika Mdomo wake." (Fat'hul Baary J. 10, Uk. 176)
NATANGULIZA POLE KWA WAISLAM KWA KUMFUATA MUHAMMAD AMBAYE HAKUTAIRIWA.
Shalom.

JE, BWANA YESU ANAPATAJE KUWA MUNGU?

Image may contain: text
Ni vyema sasa tukapiga hatua nyingine ya ufahamu kwa kuangalia swali hili makini ambalo kwa kiasi kikubwa pia huchanganya hisia za watu wengi katika ulimwengu wa imani, ambapo kile kinachoonekana kuwachanganya watu wengi hapa ni uelewa juu ya ukweli kuhusu chimbuko la Uungu wa Bwana Yesu na hivyo watu wengi kuhoji kuwa Yesu anapataje sasa kuwa Mungu?
Ni wazi kuwa swali hili hasa hulenga kutafuta kujua asili au chimbuko la mamlaka ya Kiuungu ya Yesu anayotajwa kuwa nayo hasa kutokana na kile kinachoonekana kuwa Bwana Yesu alikuwa na mwonekano unaoonyesha kuwa huenda naye alikuwa na asili au chimbuko la dunia hii.
Hivyo ili kupata majibu ya msingi ya hili ni vyema kwanza tuanze na hoja juu ya asili ya Yesu na ndipo tunaweza kufunguka zaidi kiufahamu na kuelewa mengi zaidi juu ukweli kuhusu Uungu wa Yesu.
Ufahamu juu ya asili ya Yesu:
Kile kilichoongeza upinzani mkubwa wa Mafarisayo na baadhi ya Wayahudi juu ya Uungu wa Yesu ni uelewa usiyo sahihi juu ya asili ya Yesu.
Ufahamu wa wengi kati ya Wayahudi uligotea katika dhana ya mwonekano wa ubinadamu wa Yesu na historia yake ya uzazi wa kidunia toka katika tumbo la Mariam, ambapo kama matokeo ya hili Wayahudi walisikika wakati fulani wakitamka:-
Yahana 6:42
Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?
Unaweza sasa kupata pichani juu ya mzizi wa hoja hii, na ni kama tunavyoona katika nukuu hiyo ya kitabu cha Yohana kuwa hoja kuu ya Wayahudi ilikuwa ni kile walichoona kuwa haikuwa sahihi kwa Yesu kusema ameshuka toka mbinguni maana kile wao wanachojua ni kuwa alizaliwa na bi’Mariam na baba yake ni Yusufu kwahivyo asili yake ni duniani tu.
Hivyo kwa hali hiyo iliwapa ugumu kukubali pale Yesu alipojitaja kuwa na asili ya mbinguni na kimsingi ndicho kilichokuwa chanzo kikubwa cha upinzani wao dhidi ya matamko ya Yesu.
Habu ona tena hoja ya Wayahudi pale Yesu alipoeleza uwepo wake wa milele’
Yohana 8: 56-58
Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. 57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? 58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

KAMA YESU NI MUNGU, KWANINI AZALIWE NA KUVAA MWILI WA KIBIDANAMU?

Image may contain: text
Ndugu msomaji,
Baada ya hoja na maswali mengi tuliyokwisha yapitia juu ya uhalali wa Uungu wa Yesu ndipo swali hili hufuatia ambapo hoja ya msingi hapa ni juu ya kile kinachoonekana kama kitu kisichowezekana kwa Yesu kuwa na asili ya Uungu na huku akiwa na umbile la kibinadamu umbile ambalo alilipata kwa njia ya kuzaliwa na Mariam, na kimsingi hapa ndipo mahali maswali mengi zaidi hujitokeza.
Kwanini kama ni Mungu avae ubinadamu?
Tendo la dhambi ya Adamu na Hawa lilimuingiza mwanadamu katika deni kubwa lisiloweza kulipwa na mwanadamu mwenyewe hebu tusome:-
Mwanzo 3:17
Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Kwa kadri ya Andiko hilo tunasoma kuwa Mungu alipomuweka Adamu na Hawa katika bustani ya edeni aliwapa masharti yahusuyo ulaji ambapo wanadamu hao walikatazwa kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, lakini mbali na kukatazwa huko pia walionyeshwa hasara ambayo wangeipata kama matokeo ya kukaidi agizo hilo la kula matunda hayo ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Kwa uwazi kabisa Mungu aliwaambia juu ya hatari hiyo ambayo wangejiingiza kwayo kuwa ilikuwa ni kifo’ (siku utakapokula utakufa hakika) kwahivyo kimsingi tendo la wazazi hao kujiingiza katika tendo hilo la dhambi ilikuwa ni sawa na kujiingiza katika deni la dhambi ambalo malipo yake ni mauti (kifo).
Na kwa hali hiyo basi mwanadamu huyu alihitaji msaada wa kunasuliwa toka katika deni hilo la dhambi, hivyo ilipasa upande wa pili unaoweza kukabili deni hilo kujitokeza ili kumsaidia mwanadamu kwakuwa kimsingi hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kukabili deni la kifo maana liko nje ya uwezo wa mwanadamu kama Daudi anavyoeleza:-

MUHAMMAD ALIKUWA AMEROGWA MPAKA AKAPOTEZA FAHAMU

No automatic alt text available.
Muhammad Aliwahi Kulogwa (Kwa Apizo, ‘Under a Spell’)
" ‘Aisha anasimulia: Nabii alifanyiwa uchawi hata akaanza kudhani kuwa anafanya kitu fulani wakati hakuwa anafanya. Siku moja alimwomba (Allah) kwa muda mrefu sana kisha akasema, ‘Naona kuwa Allah amenipa mwongozo wa namna ya kujitibu mwenyewe.’..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 10 na.490 uk.317.
Tazama pia juzuu ya 4 kitabu cha 53 (Wajibu wa Khumus) sura ya 34 na.400 uk.267, juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 56 na.89 uk.56-57, juzuu ya 8 kitabu cha 75 (Kitabu cha Maombi ‘Book of Invocations’) sura ya 59 na.400 uk.266-267. Juzuu ya 7 na.658-660 uk.441-443.
Pia tazama Muislam Sahihi juzuu ya 2 kitabu cha 4 (Kitabu cha Sala) sura ya 309 na.1888 uk.411
Muhammad alilogwa. Alisimulia ‘Aisha: Nabii aliendelea kwa kipindi fulani akidhania kuwa anafanya tendo la ndoa na mke wake, lakini haikuwa hivyo. Siku moja alisema kwangu, "O ‘Aisha! Mungu ameniagiza kuhusiana na suala nililomuuliza. Watu wawili walikuja, mmoja alikaa karibu na miguu yangu na mwingine karibu na kichwa changu. Yule aliyekuwa karibu na miguu yangu alimuuliza yule wa karibu na kichwa changu (akininyooshea kidole), ‘Mtu huyu ana shida gani? Yule mwingine akamjibu, ‘Ameathirika na uchawi. Yule wa kwanza akauliza, ‘Ni nani aliyemfanyia uchawi?’ Yule mwingine akajibu, ‘Lubaid bin A’sam." Yule wa kwanza akauliza, ‘(Alitumia) nyenzo gani?.’ Yule mwingine alijibu ‘Ngozi ya chavua ya mtende wa kiume na chanio lililowekwa nywele, na kuwekwa chini ya jiwe kwenye bwawa la Dharwan.’" Kisha Nabii alikwenda kwenye bwawa lile na kusema, "Hili ndilo bwawa lilelile nililoonyeshwa kwenye ndoto. Ncha za mitende yake inaonekana kama vichwa vya mashetani, na maji yake yanaonekana kama mchanganyiko wa hina."… ‘Aisha aliongeza, "(Mchawi) Lubaid bin A’sam alikuwa anatokea Bani Zuraiq, mshirika wa Wayahudi." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 56 na.89 uk.57. Tazama pia Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 75 (Kitabu cha Maombi ‘Book of Invocations’) sura ya 59 na.400 uk.266
1. Kwanini tumfuate Mtume aliyerogwa na kupoteza fahamu?
2. Hivi kuna Mtume au Nabii yeyote yule kwenye Biblia na yeye alirogwa?
3. Kwanini Allah alishindwa kumlinda Mtume wake kutoka nguvu za kurogwa?
4. Hivi wapi tunasoma kuwa Muhammad alifanyiwa maombi na urogi ukamtoka?
Hakuna ushahid wowote ule ambao unasema kuwa Muhammad aliombewa na kutokwa huo uchawi. Huu ni msiba kwa Nabii wa Allah kufa huku akiwa amefanyiwa urogi.
Ndugu msomaji,
Mtu yeyote yule akifa kwa kurogwa na huku akiwa amejaa Mashetani, basi huyo mtu yeye ataishia kwenye Jehannam ya moto.
Karibuni kwa Yesu aliye hai.
Max Shimba Ministries Org.

Jesus demonstrated He is God

 

TRENDING NOW