Tuesday, January 10, 2017

NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU, WAKUJUE WEWE ULIYE MUNGU WA PEKEE, WA KWELI NA YESU KRISTO ULIYE MTUMA

No automatic alt text available.
Ndugu wasomaji,
Leo nitaielezea aya ya Yohana 17: 3 ambayo Waislam wamekuwa wakiitumia mara nyingi sana kudai kuwa eti, Yesu amekana kuwa yeye ni Mungu. Waislam kwa kupitia mihadhara ya kidini na kwa kutumia vijarida mbali mbali wanatishia Umma wa Wakristo kuwa, Yesu ameukana Uungu. Je, hayo madai ya Waislam ni kweli? Je, hiyo aya ina la zaidi la kujifunza?
Ili uielewe Biblia vizuri, nilazima usome aya kadhaa ili upate kuelewa nini hasa Mungu anasema kupitia Neno lake. Hivyo basi, nimeweka aya ya 4 na ya 5 ili kufafanua nini hasa Yesu alikuwa anasema katika Yohana 17.
Ngoja niziweke aya zote hapa:
Yohana 17: 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. 4 Nimekutukuza Wewe duniani kwa kuitimizaile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
Yesu katika aya ya 5 [Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako] ==> YESU anasema kuwa
1. Yeye aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo! Hapo panaanza kukupa mwanga halisi, wa nini Yesu alikuwa anasema na Yesu ni nani. Imani zote zinakiri kuwa aliye kuwepo kabla ya vitu vyote ni Mungu. Lakini katika aya ya 5, Yesu nae anadai kuwepo kabla ya uumbaji.
2. Yesu anaendelea kusema katika aya hiyo hiyo kuwa, yeye alikuwa na adhama ya Mungu -"UTUKUFU". Yesu anamwambia Mungu Baba kuwa, AMTUKUZE YESU KWA UTUKUFU ALIOKUWA NAO KABLA YA ULIMWENGU HAUJAKUWAKO. Sasa, kama Yesu, sio Mungu na alikuwa Binadamu wa kawaida, kwanini basi amwambie BABA YAKE AMTUKUZE? Yesu anatumia mamlaka gani hayo kudai Utukufu ambao sio wake bali ni wa Mungu pekee?
3. Kama Yesu sio Mungu. Je, alipo dai atukuzwe na Mungu Baba, huoni kuwa alikuwa anakufuru? Lakini Hatusomi kuwa YESU aliwai tenda dhambi yeyote ile. Hata dini ya Waislam, inakiri kuwa, Katika Binadamu wote ambao waliishi Duniani, ni Yesu pekee aliweza kuishi bila ya kuetnda dhambi na kuwa na dhambi.
Ndugu wasomaji, madai ya Waislam kuwa Yohana 17:3 INAPINGA UUNGU WA YESU ni Batili kabisa, maana, leo tumejifunza katika Yohana hiyo hiyo kuwa Yesu aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo na Yesu anautukufu wa Mungu.

WAISLAM 667 WANAMPOKEA YESU KILA SAA.

Image may contain: 1 person, text and outdoor
Haya yalisemwa na SHEIKH AHMAD AL KATANI.
Akitoa ushuda kupitika Televisheni ya Al Jazeerah, Sheik Ahmad Al Katan ambaye ni Rais wa Kitengo cha Sayansi na Sharia za Kiislam huko Libya amekiri kuwa, kila saa likipita, Waislam 667 wanampokea Yesu na kuukacha Uislam.
Akionyesha kupagawa na kuto jua nini afanye, Sheikh Ahmad Al Katani alisema, Mfano kule Misri, nchi ambayo Biblia zilikuwa hazinunuliwi, lakini kwa mwa mmoja tu, teyari Biblia LAKI SITA zimeuzwa nchini humo, na maelfu kwa maelfu wanaendelea kuingia Ukristo.
Alisema tena, kule Sudan zaidi ya watu MILIONI MOJA wameingia Ukristo kwa kipingi cha miaka miwili tu.
Kwa habari kamili ingia kwenye live https://muslimstatistics.wordpress.com/2012/12/14/al-jazeerah-6-million-muslims-convert-to-christianity-in-africa-each-year/

MAHAKAMA YA KADHI NI HATUA YA AWALI KATIKA KUIFANYA TANZANIA KUWA TAIFA LA KIISLAM

Image may contain: 4 people, people standing and text
na Max Shimba Ministries
Mahakama ya Kadhi ni nini?
Mahakama ya kadhi ni chombo cha kiislam kwa ajili ya kufanya mashauri ya ndoa , mirathi na mambo ya kidini kwa kutumia Sharia.
Sharia ni nini?
Sharia ni mkusanyiko wa sheria za dini ya kiislam ambazo zinatokana na kitabu cha quran na tamaduni za kiislam kwa kufuata mafundisho na hadithi za Mtume Muhammad.
Mambo ya kidini yanayo hukumiwa na mahakama ya kadhi ni yapi?
Ni mambo yote yanayokwenda kinyume na tamaduni za kiislamu. Mfano Kula hadharani wakati wa mwezi, wa Ramadhani, kuchinja kwa mtu ambaye siyo muislamu, kufanya biashara ya vileo, biashara ya nyumba za kulala wageni, biashara ya Nguruwe, mavazi yasiyoendana na tamaduni za kiislam kwa maana hiyo ili uwe salama kwa swala la mavazi sharti uvae hijabu kwa wanawake, kanzu na kibaragashia kwa wanaume, msuri na visuruari vizivyogusa viatu.
Kwa nini waislam wanataka Mahakama ya kadhi iingizwe kwenye katiba ya nchi?
Waislam wanataka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye katiba ya nchi ili itambulike kisheria na iwe na nguvu kama mahakama za kawaida za makosa ya jinai na hiyo iwe na mamlaka ya kuhukumu watu wote waislam, wakristu na hata wapagani limradi tu hawaishi kwa kufuata tamaduni za kiislam. Mfano mtu atakaye kutwa anakula hadharani wakati wa mwezi wa ramadhani sharia itachukuwa mkondo wake na hukumu iliyotawala kwenye sharia kwa mtu anayeishi kinyume na tamaduni za kiislam ni kuuwawa kwa kuchinywa na jukumu hilo liko kwa Makadhi.
Hivyo basi mahakama ya kadhi ikiingizwa kwenye katiba itakuwa na nguvu za kuhukumu mambo ya siasa, kijamii na makosa ya jinai kwa ujumla kwa raia wote na si kwa waislam peke.
Muundo wa mahakama ya kadhi
Mahakama ya kazi inafuata muundo wa mahakama za kawaida hivyo zinaanzia ngazi ya chini kabisa kwenye wilaya na hadi ngazi ya kitaifa na mahakimu wa mahakama za kadhi ni makadhi amboa wote ni waislam
Kazi za Makadhi
1. Kusikiliza mashauri na kuhukumu kwa kufuata sharia.
2. Kuhakikisha anatokomeza ukristu katika eneo lake na uislam unatawala.
3. Kuhakikisha hakuna kanisa linajengwa katika eneo lake na wala kanisa linapo bomoka halitaruhusiwa kukarabatiwa wala kujengwa tena. Kujenga kanisa ni kinyume na tamaduni za kiislam ndiyo maana utaona wameanza kuchoma makanisa huko Zanzibar na sehemu zingine za Afrika kama Nigeria.
Madhara ya Mahakama ya Kadhi
1. Kuvunjika kwa umoja wa kitaifa uliopo kati ya waislam, wakristu na wapagani
2. Ugomvi wa kimasrahi kati ya Wakristo, wapagani na waislam. Endapo Mahakama ya kadhi itaingizwa kwenye katiba ya nchi ni wazi itagharamikiwa na serikali na hivyo viongozi wa dini ya kiislam ambao ndiyo watakuwa makadhi watatumia fedha za walipa kodi wa Tanzania ambao ni waislam, wakristu na wapangani kujinufaisha wenyewe kwa kujitengenezea ajira. Vipi kuhusu viongozi wa dini za wakristu Maaskofu, Mapadri, Wachungaji na Viongozi wa dini za Jadi nao watakuwa wanalipwa na Serikali?
3. Kutoweka kwa Wakristo kutokana na utawala wa sharia, sababu hukumu iliyo tawala kwenye sharia ni kifo hivyo wakristu watauwawa kwa kuwa hawatakubali kuishi tamaduni za kiislam
4. Kuporomoka kwa uchumi wa nchi na kuongezeka kwa tatizo la ajira kwa mfano mashule ya wakristu au taasisi za Kikristu zitachomwa kama ambavyo unaona yanatokea nchini Nigeria.
Viwanda vyote vya vileo vitafungwa, makumbi ya starehe yote yatafungwa. Ukiangalia uchumi wa Tanzania unategemea sana viwanda vya bia, Sigara nk. Sector hiyo ndiyo imeajiri watu wengi sana, anzia kwenye viwanda vyenyewe njoo kwenye mabaa, grosary na makumbi ya starehe ambayo yanatoza ushuru kwa ajili ya Serikali.
MAHAKAMA YA KADHI NI HARAM=TANZANIA
======== USIKOSE MADA YA "MAHAKAMA YA KADHI HAIPO KWENYE QURAN" ===============
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries

HATUUTAKI UISLAMU KWA KUWA MUHAMMAD HAJUI KAMA ATAINGIA PEPONI AU MOTONI

No automatic alt text available.
Qur’an 46;9 (Surat Al-Ahqaf) Sema; mimi si kiroja (mpya) katika mitume wala sijui nitakavyofanywa, wala mtakavyofanywa ninyi, sifuati yaliyofunuliwa kwangu, sikuwa mie lolote, ila ni muonyaji tu ninayedhihirisha.
Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema, Mtume wa Allah (s.a.w) amesema, “Hakuna yeyote miongoni mwenu atayeokolewa na amali yake” Wakasema hata wewe mtume wa Allah? Mtume (S.A.W) akasema, “Wala mimi isipokuwa anifunike Allah kwa rehema zake; hivyo fanyeni amali njema kwa uadilifu” (Bukhari Hadithi Na. 470, Juzuu ya
Hadithi ya Aisha kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Fanyeni yaliyo sahihi na yatekelezeni, na furahini kwa kuwa hakuna yeyote atakayeingiziwa peponi kwa amali (matendo) yake” Wakauliza ‘hata wewe mtume wa Allah?’ Mtume (s.a.w) akasema, ‘Hata mimi isipokuwa kama Allah atanifunika kwa rehema zake” (Bukhari Hadihthi Na. 474, Juzuu ya
Sasa kama mtume mwenyewe hajui hatima yake siku ya mwisho kuna haja gani Wakristo tunaojitamua kuufuata UISLAMU? Yaani tumwache Yesu mwenye uhakika na watu wake na kile atakachowapa wanaomfuata
Yohana 10;27-28
27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
28 Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Eti tuufuate Uislamu chini ya kiongozi Muhammad ambaye hajui hatima yake kama ataenda peponi, au ataenda motoni, bila shaka kwa Mkristo anayejitambua hawezi kuwa Muislamu.
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

YESU KRISTO NI MUNGU ALIYEUMBA KILA KITU

Image may contain: text
Yesu Kristo ameumba mbingu, nchi, watu, na ulimwengu wote.
Biblia Takatifu inatuambia kwamba:
“...tuliumbwa katika Kristo Yesu...” (Waefeso 2:10)
Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa sisi wanadamu wote pamoja na viumbe vyote ni kazi ya mikono ya Yesu. Yesu ameumba vitu vyote; tendo la mtu kuukana Uungu wa Yesu ni jambo la kumkosea heshima Mungu aliyekuumba. Ndio maana Yesu aliwaambia Wayahudi kwamba: “...ninyi mwanivunjia heshima Yangu...” (Yohana 8:49).
Tusomapo Biblia Takatifu katika kitabu cha YOHANA sura ya kwanza, tunaona pameandikwa:
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” (Yohana 1:1,3,14)
Huyo “Neno” anayetajwa hapo ndiye Yesu Kristo. Mwandishi wa kitabu hicho cha YOHANA ametumia usemi wa: “...Neno alikuwako kwa Mungu...” akiwa anawafahamisha hususani Wayahudi waliokuwa wanajua kuwa YEHOVA ndiye Mungu wao. Kwa hiyo Yohana anasema “...Neno alikuako kwa Mungu...” kwa maana ya kwamba; huyu “...Yesu alikuwako kwa YEHOVA...” ambaye wao Wayahudi walimtambua kuwa ndiye Mungu wao.
Pia zaidi tunaona Yohana anafafanua kwa kusema kuwa; huyu “...Yesu alikuwa Mungu...” Ufafanuzi zaidi tunauona katika YOHANA 1:14 ambapo Yohana amefafanua kwa kusema; “...Yesu alifanyika mwili; akakaa kwetu...” Biblia Takatifu inamtaja kwa wazi kabisa kuwa Yesu ni Mungu na ameumba vitu vyote “...Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika...” (Yohana 1:3).
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

KATIKA TAURAT, ZABURI, INJILI HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM

1. KATIKA TAURAT YA MUSA, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM
2. KATIKA INJIL YA YESU, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM.
3. KATIKA ZABURI YA DAUDI, HAKUNA NENO ISLAM AU WAISLAM.
A. Kwanini Waislam wanadai eti Musa alikuwa Muislam, wakati Taurat iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?
B. Kwanini Waislam wanadai eti Yesu alikuwa Muislam, wakati Injili iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?
C. Kwanini Waislam wanadai eti Daudi alikuwa Muislam, wakati Zaburi iliyo kuwepo Kabla ya Quran haisemi na wala haina neno "ISLAM" au WAISLAM"?
Kama Waislam wanabisha, nionyesheni ipo wapi Taurat aliyo iteremsha Allah kwa Musa tuione? Na iwe na aya inayosema kuwa Musa alikuwa Muislam.
Quran inasema kuwa Allah ameitunza Taurat na Injil katika Surah 15 aya 9. Vile vile tunasoma kuwa Taurat na Injil vinasemwa kama kumbukumbu katika Surah 16:43, 21:7, 21:48, 21:105 na 40:53-54.
Kwahiyo, Surah 15:9 inakubali kuwa Taurat na Injil zimetunzwa na Allah. Kama ni kweli haya madai ya Quran:http://www.quranitukufu.net/005.html
1. Ipo wapi nakala ya Taurat ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
2. Ipo wapi nakala ya Injil ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
3. Ipo wapi nakala ya Zaburi ambayo Allah ameitunza na aliiteremsha kabla ya Quran?
Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyo teremshwa na Allah kabla ya Quran, na iwe na aya Adam anasema kuwa yeye ni Muislam.
Kama Waislam wanabisha, tuleteeni nakala ya Taurat iliyoteremshwa kabla ya Quran, na iwe na aya ambayo Ibrahim anasema kuwa yeye ni Muislam.
Waislam, ipo wapi Taurat ambayo mnadai kuwa Allah aliiteremsha kwa Musa? Mbona kila siku mnatuletea aya za Quran ambazo sio Taurat?
Kama kweli Allah aliteremsha Taurat kwa Musa, basi tuonyesheni wapi ilipo hiyo Taurat na sio aya dhaif za Quran. Hivi Quran sasa imekuwa Biblia - Mkusanyiko wa Vitabu?
Allah anadai kuwa aliteremsha Injil: Surat Al Maida 46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu. http://www.quranitukufu.net/005.html
Waislam, tuonyesheni wapi ilipo nakala ya Injil ambayo Allah anadai kuitunza katika Surat Al Hjr aya ya 9?
Hakika Allah hakuteremsha kitabu chochote kile zaidi ya maneno matupu yaliyo ndani ya Quran ya Jibril.
Allah sio Mungu. Musa hakuwa Muislam, Daudi Hakuwa Muislam, Ibrahim Hakuwa Muislam. Yesu hakuwa Muislam.
Kama kuna Muislam anao ushahid kuwa Musa, Daudi, Ibrahim, Yesu walikuwa Waislam, basi watuonyeshe wapi vilipo vitabu vyao ambavyo Allah anadai kuviteremsha. Waislam, sina muda na aya za Quran zilizo kuja miaka maelfu baadae.
Max Shimba Ministries.

MAHAKAMA YA KADHI HAIPO KWENYE QURAN

Image may contain: 5 people
KUMBE ALLAH HAITAMBUI MAHAKAMA YA KADHI
Ndugu wasomaji.
Leo ningependa kusema kuwa, dai la Waislam wa Tanzania la Mahakama ya Kadhi halina msingi wala usaidizi wa Quran.
Kwa wanao ifahamu Quran, watakubaliana na mimi kuwa HAKUNA AYA HATA MOJA ambayo Allah alisema na au Waamrisha Waislam waende kwenye Mahakama ya Kadhi. Narudia tena hakuna aya.
SASA NDUGU WAISLAM:
1. Who appoints Chief Kadhi and Kadhis?
--Nani na au mnamteuaje Kadhi Mkuu na Kadhi? Leteni aya.
2. What are the qualification for appointment to the office of a Kadhi (including a Chief Kadhi)?
-- Je, mnatumia qualification/elimu zipi kuchagua/kufanya utezi wa Ofisi ya Kadhi na Kadhi mkuu/ Leteni aya.
3. Since the Kadhis are not trained lawyers who understand the Evidence Act and the Civil Procedure Act, how and/or what will they use to administer their Courts?
-- Inafahamika kuwa Kadhi sio Mawakili walio somea ambao wanaelewa ushahid wa keshi ambazo si za jinai na jinai, SASA hawa Kadhi watatumia nini katika kusimamia Mahakama ya Kadhi?
4. Muslims are mainly of two sects in Tanzania - the Sunni and Shia. Majority of the Muslims in Tanzania are Sunni Muslims but there is a significant population of Shia Muslims too and consideration ought to be given to the appointment of Kadhis of the Shia Sect to cater the interest of the Shia Muslims. Will they have two different Courts? For Sunni and Shia?
--- Waislam wapo katika makundi mawili makubwa, Sunni na Shia. Wengi wa Waislam wa Tanzania ni Sunni, ingawa kuna Shia wengi vile vile. JE, Hii Mahakama ya Kadhi itatumia Kadhi wa dhehebu lipi katia ya hayo mawili? Je, watakuwa na Mahakama mbili tofauti za Sunni na Shia?
5. How will Muslim Women be protected since: Muslim law regards women as less than men in matters of both marriage and divorce, as well as devolution of property: Holy Quran Surah 2:228-232, and Surah 65:1-7 (only a man may divorce his wife even if he is required to provide for her); a man may beat his wife, even if lightly, the evidence of two women, is equal to evidence of one man (Surah 2:282). The application of such beliefs of faith are contrary to the Constitution.
---Kivipi Wanawake wa Kiislamu watatetewa kwenye hizi mahakama? Inafahamika kuwa Sheria za Kiislam zinakiri kuwa Mwanamke ni nusu ya Mwanaume, au yupo chini sana ya Mwanaume. Je, katika kesi ya kutoa talaka na mirathi, hii mahakama itawezaje kumtetea Mwanamke ambaye yupo nusu ya Mwaume? Sura 2: 228-232 na Sura 65:1-7 ( zinasema mwenye haki ya kutoa talaka ni Mwaume tu) Mume anahaki ya kumpiga mkewe, Ushahidi wa wanawake wawili ni sawa na ushahid wa mwanaume mmoja, (Sura 2:282). Huu utamaduni wa Kiislam, ni kinyume na sheria za nchi.
Je, Mwanamke atatetewa vipi kwenye hizi Mahakama?
Islamic "Kadhi" courtsis illegal and discriminatory.
Kwanini mnamsaidia Allah kwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi?
Waislam, nileteeni aya ambayo Allah anasema kuwa muende kwenye Mahakama ya Kadhi.
Mkiniletea aya kutoka Quran inayo waamrisha kwenda kwenye Mahakama za Kadhi, leo hii nitasilimu na kuwa Muislam.
SWALI LA MWISHO:
KWANINI ALLAH HAKUTEREMSHA AYA INAYO WARUHUSU WAISLAM KUWA NA MAHAKAMA YA KADHI?
Haya nasubiri ajibu ya aya na sio matusi.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries Org.

KATIKA QURAN WAKRISTO HAWAITWI MAKAFIRI

Image may contain: text
Je, Makafiri ni akina nani?
Je, unawafahamu makafiri wa kwanza ni akina nani?
Neno kafiri ni neno ambalo lipondani ya Biblia takatifu, kabla hata ya Muhammad mtume wa waislamu kuzaliwa na wala uislamu haujakuwepo nawala Muhammad wala Quran haijaandikwa nawale Waarabu wa 4. Neno hilo kafiri lipo kwenye biblia kwa maana nyepesi neno hilo waislamu wamekuta likitumiwa na waliokuwa wanatumia biblia takatifu.
Katika Quran sijaona Wakristo wakiitwa MAKAFIRI, bali Quran nzima inawaita WAKRISTO wamchao mungu tena wasomi, SURATUL AL-MAIDAH 5:82.
Kwa kuthibitisha kuwa neno KAFIRI limo ndani ya BIBLIA hebu tuziangalie aya chache ndani ya Biblia.
EZEKIEL 34: 28-31
Mistari hiyo ni mungu mwenyewe anawahakikishia wana wa Israel kuwa hawatakuwa mateka wa MAKAFIRI, hivyo neno hilo hapo limetumika kabla hata uislamu haujakuwepo.
NEHEMIA 5: 8-9
NEHEMIA 5:17
NEHEMIA 6:16
MAOMBOLEZO 1:3
MAOMBOLEZO 1:10
MAOMBOLEZO 5:2
1TIMOTHEO 1:8-11
YUDA 1:4
1YOHANA 4:1-6
Maneno hayo yalisemwa kabla ya Muhammad hajazaliwa wa Quran haijaandikwa nawale waarabu wa4 yaani Saydina Abubakar, Omar, Athumani na Ali na uislamu ulikuwa haupo.
TUANGALIE NENO KAFIRI LINAVYOTUMIKA
_________________________
Neno KAFIRI ni neno la Kiarabu lenye maana ya Mpingaji kwa kiswahili.
Yaani anaepinga maneno ya Mwenyezi Mungu neno hili lilikuwepo kwenye Biblia kama tulivyoona kwenye baadhi ya mistari ya biblia hapo juu.
Ilikuwepo neno mpingaji KAFIRI nilazma kuwepo na kauli tangulizi iliyotangulia kusema kwahiyo kauli itakayofuata ya kupinga inaitwa kauli ya mpingaji kwa kiarabu KAFIRI.
Waislamu mara zote hukosi kuwasikia wakisema hawa MAKAFIRI wanatupa tabu au tuwakomeshe au wapigwe hawa MAKAFIRI kauli zao hizo zikitulenga sisi WAKRISTO.
SWALI LA UFAHAMU
Ni kati ya WAKRISTO au WAISLAMU nani MAKAFIRI?
2) Ni kati ya Imani ya KIKRISTO na dini ya KIISLAMU ni nani ilitangulia kuwepo duniani?
3) Ni kati ya YESU na Muhammad ni nani aliyepinga kauli ya mwenzake iliyotangulia?
HISTORIA FUPI KATI YA YESU NA MUHAMMAD.
Bwana Yesu ndiye mwanzilishi wa Imani ya Kikristo.
Waebrania 12:2
Huu ni mwaka 2015 tangu bwana Yesu alipopaa kurudi mbinguni na ni mwaka wa 1436 kwa mwaka wa kiislamu niandiko somo hili la KAFIRI kwani Muhammad alizaliwa mwaka wa 570 nandiye mwanzilishi wa dini ya kiislamu baada ya Yesu.
Hii inathibitisha kuwa Yesu alitangulia kuwepo duniani kabla ya Muhammad hakuna anaepinga hilo.
Kwamaana hiyo kauli za Yesu zitakuwa tangulizi na kauli za IMANI ya Kikristo zitakuwa kauli tangulizi.
Na kauli za Muhammad na Waislamu zitakuwa kauli za kupinga tangulizi.
Yohana 9:35-38
Kauli ya kusema yeye ni mwana wa mungu alijisema yeye mwenyewe Yesu aliitumia mwenyewe katika mistari ya sura ya hapo juu.
Hiyo ni kauli tangulizi ikipatikana kauli inasema Yesu sio mwana wa mungu hiyo ni kauli inayopinga maanayake ni KAFIRI?
JE NI NANI ALIEANZA KUSEMA YESU NI MWANA WA MUNGU?

KWANINI TUNAKULA NGURUWE? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: 4 people, people standing, shorts and outdoor
Kwa taarifa yako Allah ameruhusu kula Nguruwe.
* Mafundisho ya Quran Kuhusu Nyama ya nguruwe;
Pamoja na kuwa waislamu wanatushutumu sana wakristo kuwa tunakula Nguruwe Quran inajikanganya sana katika swala zima la kuliwa ama kutokuliwa kwa mnyama huyu ni muhimu kuangalia, kwa ufupi hakuna aya maalumu katika Quran inayoharimisha na kukataza kula nguruwe
Quran inasemaje kuhusu nyama ya nguruwe;-
Quran inaeleza wazi kuwa Mungu aliharimisha Vitu vizuri (akiwemo Nguruwe) kwa Wayahudi kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, yaani Mwenyezi Mungu aliwakataza kula nyama hii kama sehemu ya kuwahukumu wayahudi na si vinginevyo soma (Surat an-nisaa 4;160).
Quran inasema hivi katika aya hiyo “Basi kwa dhulma yao hao Mayahudi tuliwaharimisha vitu vizuri walivyohalalishiwa na vilevile kwa sababu ya kuzuiliwa kwao watu wengi na njia ya mwenyezi Mungu”
ni aya iliyo wazi kuwa wayahudi walizuiliwa vitu vizuri kwaajili ya dhuluma Mungu alitaka kuwahukumu kwa kuwanyima baadhi ya vitu vizuri Quran inakiri wazi kuwa Nguruwe ni kitu kizuri Umeona?
Quran inafundisha kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyo harimishwa (Surat al-Imran 3;50).
Quran inasema haya katika aya hii “ Na nitakuwa Msadikishaji way ale yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati na nimekuja ili NIKUHALALISHIENI yale MLIYOHARIMISHWA na nimekujieni na hoja Kutoka kwa Mola wenu kwa hiyo mcheni mwenyezi Mungu na NITIINI”
Hayo ni meneno ya Yesu Ndani ya Quran ikionyesha wazi kuwa Yesu alikuja kuhalalisha yale yaliyoharimishwa katika Tourati na anatuamuru kumtii, ni wazi kuwa Yesu ameruhusu kula Nguruwe na Quran pia
Quran imehalalisha kula vilivyo vizuri walavyo waliopewa kitabu (Al-maida 5;3-5).
Sura hii almaida maana yake maswala ya meza inasema hivi “……..Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni Halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao…”
Hii ni aya iliyo wazi inayoruhusu kila muislamu kula vyakula vya wakristo na wayahudi na sisi kula vyao umeona!
Quran ina kigugumizi kwa vile hakuna katazo la moja kwa moja kuhusu kutokula Nguruwe yaani inakataza kula Nguruwe na wakati huohuo inaruhusu endapo utashurutishwa na njaa (Al-baqara 2;173) au kama una dharula waweza kula hapa ndipo quran inapojikanganya ni muhimu kujiuliza imekataza au imeruhusu? Na dharula hii ni ipi? Quran inajibu kuwa dharula hii ni njaa (Al-an nam 6;145)Quran inasema kula bila kupita kiasi hili ni jema kwani Biblia inafundisha kuwa hata kama una njaa kiasi gani kula kupita kiasi hata kama si nguruwe chakula chochote ni ulafi ni dhambi (Galatia5;21)
Quran inafundisha kuwa Mungu hakuharimisha chochote ila wazee wa kiyahudi waliharimisha kwa mapokeo yao tu (Al-an nam 146)
Quran inatahadharisha kuwa makini kumzulia Mungu uongo kuwa ameharimisha kitu kumbe hakuharimisha chochote (An Nahl 16;116)
Quran inaamuru uletwe Ushahidi kuwa ni wapi Mungu ameharimisha wanyama? Soma (Al an- am 6;150).
Hivyo ukisoma kwa makini Quran utaona hakuna kilicho haramu ndugu zangu waislamu kula nguruwe ni ruksa ila kiasi tu usizidishe ndivyo Quran inavyofundisha kama husadiki pale uwanja wa sabsaba Tanga kwa Minchi waislamu wenzenu hujumuika kula kiti moto kila iitwapo leo kwani wameelimika na wamegundua siri hii. Mimi sikushawishi ila nina kuweka huru kama mwalimu wa kweli ya Mungu “….. Mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru
Mafundisho ya Agano jipya kuhusu vyakula (Nguruwe).
Biblia inasema mafundisho yoyote yanayokataza mtu kula vitu Fulani ni mafundisho ya Mashetani (1Timoth 4;1-5). Ndio maana waganga wa kienyeji mtu anapokwenda kuaguliwa hukatazwa kula baadhi ya vitu Mungu sio Mganga wa kienyeji. Na wanaomwamini hawana sheria ya kuwazuia nini cha kula au kutokula
Biblia inasema hakuna kitu najisi kwa mtu asiye najisi lakini kitu Fulani ni najisi kwake yeye aliye najisi (Rumi14;14)Biblia inafundisha kuwa kula au kutokula hakuongezi utakatifu wala hakuzuii tamaa za mwili (Kolosai 2;16-23) hivyo hatupaswi kujitia katika mambo ya kutunga tu ya mtu,au akilizake na maono ya wanao abudu malaika kumuabudu Mungu hakuji kwa kula au kutokula aina fulani ya vyakula bali katika moyo safi (Math 5;8)
Biblia inafundisha kuwa unajisi wa mtu hautoki nje bali ndani ya mtu pia Yesu alitakasa vyakula vyoote (Marko 7;14-16,17-19)
Paulo mtume alifundisha kuwa chakula ni kwa tumbo tu na si mambo ya rohoni
(1Koritho 6;13). Hoja ya Pepo waliotolewa na Yesu kuwaingia nguruwe je ina maana gani?
USIKOSE SEHEMU YA PILI........
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Shalom.

"MUISLAMU ZINDUKA KUTOKA USINGIZINI ILI UJUE KUWA MKRISTO SIYO KAFIRI"


Najua unaweza kustaajabu ni vipi muislamu wewe uzinduke ili hali unajiona kuwa u macho haupo kwenye Usingizi? ninaposema kuwa unajiona u macho ni katika imani uliyo nayo juu ya Mkristo kuwa ni kafiri, hivi ndivyo unavyoamini kwa sababu uliminishwa hivyo, ukaamini hivyo, kwa sababu tu Quran inasema! 👇
وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
التوبة (30) At-Tawba
Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!
Muislamu ukisoma aya hii moja kwa moja unaamini kuwa Wakristo ni Makafiri kwa kusema kuwa Masihi Yesu ni Mwana wa Mungu! unaamini kabisa kuwa hayo maneno ya kusema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, tunayosema sisi kwa vinywa vyetu yaani sisi ndo tumebuni, hivyo unatuona sisi ni Makafiri! tena unafurahia ujio wa Quran kuwa umekuja kwa ajili ya 👇
وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا
الكهف (4) Al-Kahf
Na kiwaonye wanao nena: Mwenyewe Mungu ana mwana.
مَّا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا
الكهف (5) Al-Kahf
Wao hawana ujuzi wa jambo hili, wala baba zao. Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu.
Nawe unaamini fika kuwa Quran imekuja kwa ajili ya kuwaonya Wakristo kwa sababu wanasema kwa vinywa vyao kuwa Mwenyezi Mungu ana mwana, nawe bila kuzinduka uangalie kama kuna usahihi wa jambo hilo unakurupuka na kuanza kusema kuwa, Wakristo ni Makafiri, LEO naomba nikuzindue ili kama unapenda kwenda kwenye UFALME WA MUNGU, basi uungane nami leo.
JE! NI KWELI KWAMBA WAKRISTO WANASEMA KWA VINYWA VYAO KUWA YESU NI MWANA WA MUNGU?
Hili 👆ni Swali la msingi sana mtu kujiuliza, kabla ya kuamini kuwa Wakristo wanasema kwa vinywa vyao na kuwaona ni makafiri (wenye kwenda kinyume na Mungu) kabla Wakristo hawajapatikana, na Yesu ambaye ndiye chimbuko la Wakristo hajazaliwa, Malaika alisema. 👇
Luka 1:30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

TRENDING NOW