Wednesday, February 22, 2017

KWA JINA LA YESU MTATOA PEPO

Image may contain: one or more people and text
Marko 16:17-18 inasema, "ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina Langu watatoa pepo...."
Kila Mkristo anao uwezo wa kuwatoa pepo! Sio swala la kwamba "una nguvu" kiasi gani au jinsi gani upo "kiroho" ; cha muhimu ni kuwa Yesu Amekupa mamlaka Yake; unatembea katika jina Lake.
Shetani hana haki ya kuendesha mambo katika maisha yako, au nyumbani mwako au katika maisha ya wale uwapendao. Tumia mamlaka yako katika Kristo dhidi yake.
Matendo 16:16-18 Ikawa tulipo kuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye juu, wenye kuwahubiria Njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo Akakasirika, akageuka akamwambia yule pepo, nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
Unaweza kuwatoa pepo siku yoyote, muda wowote na mahala popote, kwa kutumia jina la Yesu tu.
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

KANISANI JUMAPILI YA FEBRUARY 19, 2017 NA RAIS OBAMA, WASHINGTON DC.

Image may contain: 7 people, people standing and wedding

Its great to see the OBAMA Family in church. You know its a good idea to serve GOD after serving in the highest office on Earth

Max Shimba Ministries 

HATIMAE SHETAN KWA KINYWA CHAKE AKIRI KUWA YESU NI MUNGU

Image may contain: text
AKIRI KUWA YESU NDIYE ATAKAE MHUKUMU SIKU YA MWISHO/KIYAMA:
Ndugu msomaji,
Unapoona mada hii inajirudia katika mandiko tofauti, tofauti, ikithibitisha mamlaka kuu na nguvu za Yesu kuanzia mbinguni, duniani na hadi chini ya aridhi;
Nikwamba INAKUJENGEA IMANI WEWE USIYE AMINI UUNGU, UKUU, NA MAMLAKA YA YESU.
Kwahiyo shetani yeye anaitumia fulsa hiyo ya kuivunja imani hiyo ya Yesu kwa kusema "Yesu ni mtu tu kama nyinyi sichohote silolote" NAKUIVUNJA IMANI YA WATU WAKIFIKILI YESU SILOLOTE,
Tuanze na Qur'an Al-Hijr 34 ( ALLAH ) akasema basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! 35 na hakika juu yako ipo laana mpaka siku ya malipo, 36 akasema (Iblisi) mola wangu mlezi! NIPE MHULA MPAKA WATAKAPO FUFULIWA. 37: (ALLAH) akasema HAKIKA WEWE NI KATIKA WALIO PEWA MHULA. 38 MPAKA SIKU YA WAKATI MAALUMU.
Katika mstari wa 36 shetani anaomba apewe MHULA MPAKA WATAKAPO FUFULIWA.
JE NINANI HUYO AMBAE SHETANI ANASEMA ATAFUFUA?
Yohana 11:25 YESU akamwambia, MIMI NDIMI HUO UFUFUO NA UZIMA, yeye aniaminiye Mimi HAJAPO KUFA ATAKUA ANAISHI:
Kumbe shetani anamfahamu fika Yesu na ndio maana anamuomba atakapo kujakufufua wafu siku ya mwisho ndipo nae ahukumiwe.
Katika mstari wa 37-38 tunaona Allah kwa kinywa chake anamwambia shetani kwamba AMEPEWA MHULA MPAKA WAKATI MAALUMU.
ALLAH #HAKUMWAMBIA SHETANI KWAMBA NIMEKUPA MHULA, LA HASHA,
BALI ALIMWAMBIA #UMEPEWA MHULA.
JE MUNGU ALIYE MPA MHULA SHETANI ANAITWA NANI?
KWASABABU ALIYE PEWA MHULA NI SHETANI, NA SHETANI ANAMJUA ALIYE MPA MHULA, SHETANI MWENYEWE ANATHIBITISHA KWA KINYWA CHAKE:
UTHIBITISHO WA AYA:

KUNYWA MAJI YA UZIMA

Image may contain: text
Njoo Kwake Kristo Yesu
“Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.” (Ufunuo Wa Yohana 22:17)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

HABARI NJEMA

Image may contain: text
Injili, ambayo inamaanisha, “Habari Njema,” ni kwamba Mungu ametuandalia njia ya kumrudia huku akiadhibu dhambi zetu. Njia hiyo ni kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (Yohana 14:6)
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Warumi 5:8)
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.” (Waefeso 2:8)
“Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” (Wakorintho Wa Pili 5:21)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

MSIKITI WA IJUMAA TABORA WAUZWA

MSIKITI WA IJUMAA TABORA WAUZWA
Baadhi ya viongozi wa msikiti wa Ijumaa ambao ndio msikiti mkuu wa mkoa wa Tabora wametuhumiwa kula njama na kuuza msikiti huo bila kuwahusisha waumini na viongozi wenzao.
Chanzo cha kuaminika kilichopo mjini Tabora kimeiambia 100.5 Times Fm kuwa waumini waliingiwa na shaka baada kuona msikiti huo umefungwa ghafla kwa siku mbili mfululizo na kwamba baada ya kufuatilia waligunduamkuwa viongozi hao wameuuza kwa matajiri ambao ni wenyeji wa Nairobi,Kenya.
Hali ya sintofahamu ilibuka katika eneo hilo na kutokea mzozo mkubwa baina ya watuhumiwa na waumini wanaodai msikiti huo.
Imeelezwa kuwa ilimlazimu mufti kusafri haraka mpaka mjini Tabora ili kuutatua mgogoro huo.
Hadi taarifa hii inaenda hewani Mufti alikuwa akiendelea na zoezi la kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo huku akihoji sababu za kufungwa kwa msikiti huo ikiwa ni kinyume cha taratibu.
Bado haijafahamika lengo la matajiri hao kuununua msikiti huo.
http://www.habari5.com/zilizopita/item/5391-msikiti-wa-ijumaa-tabora-wauzwa-kimyakimya-mufti-simba-aingilia-kati-kuunusuru

WAUMINI WACHARUKA! VIONGOZI WA MSIKITI WADAIWA KUTAFUNA MILIONI 20/-


Na Dotto Mwaibale
TAFRANI kubwa imezuka katika msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa msikiti huo kudaiwa kutafuna zaidi ya shilingi milioni 20.
Fedha hizo imeelezwa kuwa zilichangwa na waumini wa msikiti huo kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya baada ya unaotumika kuchakaa.
Imamu mkuu wa msikiti huo aliyetajwa kwa jina la Hamidu Mitanga alilazimika kutoweka ndani ya msikiti huo baada ya kuendesha swala ya Ijumaa iliyofanyika jana mchana kutokana na waumini kuwa na jaziba kufuatia imamu huyo kutamuka kuwa hakuhitaji kuulizwa maswali yoyote kuhusu upotevu wa fedha hizo na kuwa uongozi uliopo utaendelea kuwepo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msikitini hapo Dar es Salaam leo mchana wakati wa swala ya Ijumaa mmoja wa waumini wa msikiti huo Mbarouk Mohamed Makame alikiri kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za waumini zilizochangwa kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
"Suala la upotevu wa fedha hizo lipo na limeleta changamoto kubwa kwa waumini na kusababisha kuwepo kwa makundi mawili moja likiwa lile linalolalamikiwa kutafuna fedha hizo na lile linalotaka fedha hizo zitolewe maelezo zilipo," alisema Mzee Makame.
Mzee wa msikiti huo na Mwenyekiti wa Kamati ya watu 10 Saidi Ngubi alisema fedha zinazoshindwa kutolewa maelezo ya matumizi yake na viongozi wa msikiti huo zilitokana na mradi wa maji na michango ya waumini.
"Mimi ndiye niliyeanza kuuliza matumizi ya fedha hizo lakini viongozi hao wakawa hawana majibu na badala yake waliivunja kamati yetu na kuchagua nyingine jambo lililoleta sintofahamu," alisema Ngubi.
Imamu mkuu wa msikiti huo Hamidu Mitanda alisema fedha hizo zilitumika kwa ajili ya mchakato mzima wa kupata umiliki wa kiwanja ulipo msikiti huo na michoro ya ujenzi wa msikiti mpya na kuwa yeye ndiye aliyeanzisha mpango wa kupata msikiti ulio bora na si bora msikiti.
"Binafsi sina shida na cheo hiki cha Uimamu kwani nina shughuli zangu nyingi mkitaka kuniondoa fuateni taratibu kama zili zilizoniweka madarakani na sisi kama viongozi dhamira yetu ni kuwa na msikiti uliobora wa ghorofa na si bora msikiti" alisema Mitanga.
Mitanga alisema chokochoko hizo zilianza tangu mwaka 2007 ambapo tulikubaliana kila muumini kati ya waumini 205 achangie sh.5000 za ujenzi lakini waliochangia walikuwa ni waumini wachache ambapo zilipatikana sh.milioni moja tu.
Imamu huyo alisema uongozi unaoendesha msikiti huo hauko tayari kuachia madaraka kwa tuhuma hizo ambazo hazina ukweli alizodai zinachochewa na baadhi ya waumini.
http://www.wavuti.com/2016/02/waumini-wacharuka-viongozi-wa-msikiti.html

Saturday, February 18, 2017

YAANI NILIKUWA NAJIULIZA TU – SINA JIBU – NAOMBA KUELEWESHWA.

Image may contain: one or more people
………..
Seba anakaa na Rama. Zena akaja akasema, “Seba, huyo kibaka wako unayekaa naye aliyeiba simu yako yupo?”
Rama akitokeza na kusema, “Nipo sijaondoka,” je, hata ungekuwa wewe, ukisikia jibu la Rama si utajua kuwa anakubali kuwa yeye ni kibaka? – maana hakanushi kuitwa kibaka.
………….
Katika Sahih Bukhari, Volume 6, Book 60, Number 475 tunasimuliwa na Jundub bin Sufyan kuwa siku moja mtume aliugua sana. Mama mmoja, mke wa Abu Lahab akaenda akamwambia, “O Muhammad! I think that YOUR SATAN HAS FORSAKEN YOU, for I have not seen him with you for two or three nights!”
……….
Yaani, “Muhammad, nadhani SHETANI WAKO AMEKUACHA”
…………
Kisha tunaambiwa kuwa: ON THAT, ALLAH REVEALED:“By the fore-noon, and by the night when it darkens, YOUR LORD (O MUHAMMAD) HAS NEITHER FORSAKEN YOU, NOR HATED YOU.” i.e. (Surah 93:1-3).
…………
Yaani Allah alishusha Sura 93:1-3 kumjibu mke wa Abu Lahab.
Lakini badala ya kusema, “We mwanamke, mimi sio shetani,” yeye akasema tu kuwa, “Naapa kwa mchana! Na kwa usiku unapo tanda! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.”
…………..
Sasa, mimi nakuwa najiuliza tu – sina jibu:
1. Huyu mama alikuwa anamwongelea SHETANI, iweje atokeze ‘Mola’ kujibu swali hilo?
2. Kama mtu akija akasema, “Kaka yako yuko wapi?” je, anaweza kutoka DADA na kujibu, “Niko hapa?”
Shalom:
Imeletwa kwenu na Jimmy John:

NENO LAKO NI TAA YA MIGUU YANGU


Image may contain: text

UWEZA ULIO KATIKA NENO LA MUNGU

Neno ni nini?
Neno ni matamshi yenye maana yanayotoka kwenye kinywa cha mtu, au kitu !


Kibiblia Neno ni yale mambo yaliyojaza moyo wa mtu , Biblia inasema “Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake , hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoka yaliyo maovu; kwa kuwa mtu hunena yale yaujazayo moyo wake” Luka 6:45 Amplified Bible moyo umeandikwa kama (storehouse)

Neno la Mungu ni nini?
Neno la Mungu ni yale maneno yanayotoka kwa Mungu, na ni makusudio ya somo hili kujifunza uweza ulio katika neno la Mungu ili yamkini tupate kujua msaada tutakao upata kwenye neno hilo! Mungu anaongea sana kupita unavyofikilia lakkini unawezaje kulipokea neno na kulitumia hapo ndo wengi wanaposhindwa.

Uwezo wa NENO kukuongoza katika njia sahihi.

“Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu” Zaburi 119:105,

Neno linatuonyesha tunapoelekea, linatuongoza kutenda kwa usahihi kama vile nchi bila katiba inapotea, ndivyo mtu anayemwamini Yesu kutokuwa na neno la Mungu moyoni mwake! lazima atapotea! Mungu akamwambia Joshua “kitabu hiki cha torati kisitoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku…ndipo utakapoifanikisha njia yako…” Joshua 1:8. Ni kwa kufuata Neno la Mungu ndipo mtu anaweza ifanikisha njia yake!

Shalom,

Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

ALLAH KAMESA WAHUKUMU WAISLAM KUTUMIA INJILI NA SIO QURAN

Image may contain: one or more people, text and outdoor
Ndugu msomaji,
Surat AL Maida 47. Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.
http://www.quranitukufu.net/005.html
Allah kateremsha aya na kukiri mbele ya umma wake kuwa, INJILI NDIO IMEKAMILIKA NA HAINA SHAKA NDANI YAKE NA NDIO ITAKAYO TUMIKA KWENYE HUKUMU.
Jambo la kujiuliza, kwanini Allah hakusema tutahukumu kwa kutumia Quran?
Ushahidi zaidi wa Kiislam:
1. Sahih Al-Bukhari Hadith 4.657 Narrated by Abu Huraira
2. Sahih Al-Bukhari Hadith 4.658 Narrated by Abu Huraira
Je, Biblia nayo inasema nini kuhusu sisi Wakristo kutoa hukumu?
1 WAKORINTHO 6: 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu Malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
Biblia ndio imemaliza kabisaa na kusema kuwa, Wakristo wanahaki na uwezo na mamlaka ya kuhukumu mpaka Malaika.
Shauri ni lako, kuwa Muislam ambaye atahukumiwa kwa Injili, au kumfuata Yesu ambaye amekupa Mamlaka ya kutoa hukumu mpaka kwa Malaika.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction Muslims ...

TRENDING NOW