Sunday, March 19, 2017

MAPEPO NI NINI? SEHEMU YA PILI

Image may contain: 6 people, crowd and text


Somo: Mapepo ni nini?
Lengo Kuu:Uhusiano Baina ya Mtu na mapepo
Lengo Mahsusi: Kujua namna ya kuzishinda roho za kipepo na kazi zake.
Uhusiano Baina ya Mtu na mapepo.
Bwana Yesu asifiwe sana,
Ndugu zangu wapendwa, karibu katika mwendelezo wa somo letu. Katika sehemu iliyotangulia, tulijifunza dhana ya pepo, asili na mkuu wa mapepo. Pia, tuligusia kwa ufupi juu ya utiifu wao juu ya Mungu na hatua ya kuchukua ili kukabiliana na uhalifu unaoendelezwa na mapepo kupitia maombi, toba na kulishika neno la Bwana.
Ndugu mpendwa, katika sehemu hii, tutachunguza Uhusiano uliopo baina ya mtu/binadamu na mapepo.
Tunaposema uhusiano katika muktadha huu, tunamaanaisha, vitu vinavyoweza kumkutanisha mwanadamu na pepo/ roho wabaya.
Yafuatayo ni baadhi ya maeneo yanayoweza kuwakutanisha binadamu na mapepo:-
(a) Sadaka- mwanadamu katika kukamilisha ibada zake, huweza kujikuta anatoa sadaka kwa mapepo. Tukio hili huweza kudumisha uhusiano baina yake na pepo. Zoezi hili, linafahamika sana kama tambiko, amabapo zawadi za wanyama, pombe, mazao mbali mbali na pesa pia hutolewa kwaajili ya masuala ya kiibada.
Sambamba na hili, wakuu wa ibada hizi, hujihusisha na shughuli za uaguzi, uganga, utabili na kubashiri,ramuli n.k.
Kwakufanya ibada hizi,mwanadamu hujifungamanisha na mapepo/ roho wachafu na kuongozwa nao.
Mara nyingine, watu hufanya ibada hizi wakidhani wanamwabudu Mungu na sadaka hizi wanamtolea Mungu, kumbe siyo kweli (Kumbukumbu la Torati 32:17).
Ndugu zangu, ibada hizi ni machukizo kwa Mungu na hapendezwi nazo. Mungu huchukia ibada hizi, yeye hafurahii ibada za namna hii kwakuwa ni ibada za mashetani.(1Wakorintho 10:20-30)
(b) Dhambi na Upagani- huu ni mlango mkuu wakuwanganisha watu na mapepo. Watu wengine hudhania kuwa wapagani hawatahukumiwa, ndugu yangu hukumu ipo tuu, ili mradi tu wewe ni binadamu, lazima hukumu ipo. Kujitenga na Mungu kwa kutenda dhambi adhabu yake ni hukumu, na hata mpagani atahukumiwa kwa dhamili yake. (1Timotheo4:1&2). Ndugu mpendwa, kubali leo umpokee Yesu, awe Bwana mwokozi wako, uwe huru.
(c) Kutii mafundisho ya uongo- mafundisho ya uongo ni yote yanayoenda kinyume na mwongozo wa Mungu. Kwa kuyatii, basi ni dhambi, na hukumu ya dhambi ni mauti. Kutolifata neno la Mungu kama lilivyo ni kufuata mafundisho ya uongo. Ndugu, tambua ya kuwa neno liko wazi na limefunuliwa kwa wote, hakuna atakayesema hakujua. Kila kona leo, kuna dini nyingi amabazo nyingine, hazifundishi kweli ya Mungu kama ilivyo, jiepushe na kujitenga na roho hizo, (1Timotheo 4:3-5).
(d) Kuyafuga- hii ni hali ya kukaa nayo. Njia hii, hutumiwa aidha kwa woga au kwa kuyapenda. Ndugu, hakuana urafiki kati ya pepo na mwanadamu. Daima lengo la pepo ni kuharibu na kuua. Kuna watu wanafuga mapepo, wengine wanayatumia kiganga, wanapagawa mapepo n.k. hili hufanaya roho hizi zifanye masikani ndani ya mtu, ndani ya uzao wake, mali, shamba na ahata mifugo (Mathayo 8:30-32).
Ndugu mpendwa, Kwa kuyapa nafasi mapepo kuwepo katika familia yako, hutoa mwanya wa kuitesa familia kizazi hata kizazi. La msingi hapa ni kuziamuru hizi roho ziondoke katika familia yako. Omba kwa vita na kukemea, ujitenge, uitenge familia yako, uzao wako, mali zako, shamba, biashara, mifugo na kila kitu, kiwe huru. Kikabidhi mikononi mwa Mungu awe Bwana na Mlinzi wako na kila kitu chako.
Je, mtu/ binadamu hupataje mapepo? Chanzo/asili yake ni nini? Endelea kufuatana nami toleo lijilo......Somo: MAPEPO NI NINI? [SEHEMU YA TATU]

LEO TUTAMTAZAMA BWANA YESU NA MUHAMMAD NI NANI MWENYE MATUMAINI YENYE UHAKIKA KATI YOA

Image may contain: 2 people, text
Tutapitia kauli zao walizozisema wakiwa Duniani, na kila mmoja atahukumu ni yupi mbora wa kufwata kati ya Bwana Yesu na Muhamad.
BWANA YESU ANASEMA
Yohana 8:12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Yohana 10:9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
Yohana 10:11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Yohana 10:14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yohana 6:40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 8:14 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako.
Yohana 14: 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia.
Ufunuo 1:17… Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
MUHAMMAD ANASEMA
Q 46:9. Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.
Q19:71. Wala hakuna yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia (hiyo Jehanam). Ni wajibu wa Mola wako uliokwisha hukumiwa.
Na ktk Sahihi Al-Bukhari IV, Hadith Na. 728, na VI, Hadith Na. 294. Muhamad anasema Eeh ndugu zangu Abdul Manaf, Abbas bin Abdul bin Mutalib, Safiyyah(shangazi) na binti yangu Fatima mimi sina uwezo wa kuwaokoa dhidi ya ghazabu ya Mungu.
Q 10:102. Basi, je! Wanangojea jingine ila (kuwajia) mfano wa siku za (adhabu zilizowafika) watu walio pita kabla yao? Basi Ngojeni! Mimi pia ni pamoja nanyi katika wanao ngojea.
Fafanuzi yake: Ukimwone mwenzio amenyolewa kwa jambo hilo hilo unalolifanya, basi kitie maji upesi kichwa chako kwani na wewe utanyolewa km alivyonyolewa.
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.
"Mwenye kubadili dini yake (ya kiislamu, muueni" (A) Bhukari 6922, Abu Dawuwd 4329, At - Tirmidhiy 1483
O Khadija, Ninaona Mwanga, na nasikia Masautisauti, nina hofu kuwa mimi nina Wazimu. "Kitab al-Tabaqat al-Kabir", by Ibn Sad, , ukurasa wa 225
Ndugu msomaji (Mkristo na Mwislam) tukiacha yote ni nani hapo anamatumaini ya uhakika ya kumfuata kati ya Bwana Yesu na Muhamad?
Bwana Yesu apewe sifa.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UTATU NI UPENDO

Image may contain: text


Yehova anaonyesha upendo wake kwa kutumia Utatu. Hebu ungana nani na uone jinsi upendo wa Mungu ulivyo kwa Mwanadamu.
(a) Baba – Yohana 3:16
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”
(b) Mwana- Efeso 5:25
“Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili yake.”
(C) Roho Mtakatifu – Rumi 15:30
“Ndugu zangu nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu”
Hoja inayohusu Utatu Mtakatifu iko wazi sana unaposoma Maandiko Matakatifu na ukiyafanya ndiyo dira yako .
Yesu mwenyewe alipokuwa hapa duniani alisema
Yohana 15: 24 “ kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine wasingalikuwa na dhambi ,lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu na kutuchukia “
Swali la ufahamu : Hao watu pale walikuwa wanamuona nani? Baba au Yesu au walikuwa wana muona Yesu ambaye ni Baba? Tafakari.
Katika Yohana 16:13-16
“Lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari zake .Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari .Na yote aliyonayo Baba ni yangu kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu kuwapasheni habari .Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona”.
Swali la ufahamu: Yesu yuko mbinguni na bado tena yuko duniani pote akiwa nani?
Matendo 20:28
“ Jitunzeni nafsi zenu na lile kundi lote nalo ambalo Roho Mtakatifu amewaweka nyinyi kuwa waangalizi ndani yake mpate kulilisha Kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe”
Swali la ufahamu:
“Aliyesulubiwa msalabani ni Mungu,Yesu au Roho Mtakatifu? Bila shaka ni Yesu Kristo”
- Kwanini Kanisa lisiwe mikononi mwa Yesu aliyesulubiwa? Ni kwa sababu Mungu ,Baba,Mwana,na Roho Mtakatifu ni umoja (1 Yohana 5:6-7)
- Mwana amemtukuza Baba duniani (Yoh 17: 4)Baba amewaketisha mwana katika mkutano wake wa kuume wa kiti chake cha enzi mbinguni.
- (Ufunuo 22:1, Marko 16:19)
- Mwana amempa Roho Mtakatifu kazi ya kulitunza kanisa ambalo Mungu alilinunua kwa damu yake.
Ayubu 11:7-10
“ Je wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikiria upeo wa huyo mwenyenzi? Ni juu mno kama mbingu waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni kufanya nini wewe cheo chake ni kirefu kuliko dunia ni kipana zaidi ya bahari”.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UTATU NI MUNGU

Image may contain: text


Katika Utatu tunafunuliwa kuwa Yesu ni Mungu kama alivyo Baba yake na Roho Mtakatifu.
Ungana nami na tusome Biblia takatifu kwa pamoja.
1. Baba ni Mungu:
Filipo 1:2 “ Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo”.
2. Mwana ni Mungu:
Yohana 1:1:14 Kolosai 2:9
• Hapo mwanzo kulikuwako Neno , naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu ------------, Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na kweli”.
• Kolosai 2: 9 “ Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya kimwili”.
3. Roho Mtakatifu ni Mungu
Matendo 5:3-4 “ Petro akasema Anania kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uwongo Roho Mtakatifu na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwishauzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako?.Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu”.
Roho Mtakatifu ni, nafsi ya tatu ya Mungu yenye hisia “emotion”, huhuzunika (Efeso 4:30), hunena, (Ufunuo 2:7), anaweza kuzimishwa ((1Thesalonike 5:19), Hufurahi (Rumi 14:17) .Hivyo Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe na wala siyo kitu tu (impersonal) (Yohana 4:24) .
Pia katika kitabu cha Isaya 63:7-10 “ Nitautaja wema wa BWANA, Sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israel, aliyowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Maana alisema, hakika ndiyo watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi (Yehoshua) wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia , akawa adui , akapigana nao”
Nategemea sasa umesha elewa kuwa, SOMO LA UTATU ni muhimu sana, maana linatufungua macho na kufahamu Uungu wa Yesu, Uungu wa Roho Mtakatifu na Uungu wa Yehova.
Shalom,
Max Shimna Mtumwa wa Yesu Kristo.

YESU NI NURU YA ULIMWENGU

Image may contain: cloud, night and text
Yohana 8:12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Mpokee Yesu na upate Nuru maishani mwako. 

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

YESU NI MLANGO

Image may contain: cloud, sky and text


Yohana 10:9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
Hakuna Njia nyingine zaidi ya Yesu. Ukitaka uhakikisho wa maisha baada ya kifo, basi ni lazima upitie MLANGO WA YESU.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: text
Katika somo hili, tutajifunza kuhusu Malaika na kwanini Mungu aliwaumba. Ni somo gumu kwa wengi, lakini litakufungua macho na utafahamu kazi ya Malaika na kwanini waliumbwa.
Maana ya Malaika:
Malaika ni viumbe vya kiroho ambao wako na hekima, hisia, na nia. Hii ni kweli kwa Malaika wazuri na wabaya (mapepo-Malaika walio asi). Malaika wako na hekima (Mathayo 8:29; 2 Wakorintho 11:3; 1 Petero 1:12), inaonyesha hisia (Luka 2:13; Yakobo 2:19; Ufunuo 12:17), na kujaribu kufanya penzi lao (Luka 8:28-31; 2 Timotheo 2:26; Yuda 6). Malaika ni viumbe vya kiroho (Waebrania 1:14) bila na kuwa na mwili. Ingawa hawana mwili, bado wako na hali ya mwili.
Neno "Malaika Mkuu" hutokea katika mistari miwili ya Biblia. Wathesalonike wa kwanza 4:16 inashangaa, "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya Malaika Mkuu na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza." Yuda mstari wa 9 inasema, " Lakini Mikaeli malaika mkuu aliposhindana na Ibilisi, na kuhojian naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee." Neno "malaika mkuu" linatokana na neno la Kigiriki lenye maana ya "malaika mkuu." Linahusu malaika ambao anayeonekana kuwa kiongozi wa malaika wengine.
Tutaanza kujifunza kuhusu Malaika wakuu Saba wa Mungu. Je umesha wai sikia majina yao?
Wengi wetu tumesikia baadhi tu. Lakini kwa kuanza, nitaweka majina yao yote kwa pamoja.
MALAIKA WAKUU:
1. Archangel Jegudiel au Yehudiel.
2. Archangel Gabriel.
3. Archangel Selaphiel.
4. Archangel Michael.
5. Archangel Uriel.
6. Archangel Raphael.
7. Archangel Barachiel.
Hawa Malaika wametajwa kwenye Biblia na kitabu cha Enoch. Kitabu cha Yuda/Jude kilinukuu aya kadhaa za Kitabu cha Enoch, aya ya 14 na 15.
Yuda mstari wa 9 inatumia kihuzishi dhahiri "malaika mkuu Mikaeli," ambayo inaweza kuonyesha kwamba Mikaeli ni malaika mkuu tu. Hata hivyo, Danieli 10:13 inaeleza Mikaeli kama "mmoja wa hao wakuu." Hii huenda inaonyesha kwamba kuna malaika mkuu zaidi ya moja, kwa sababu inamweka Mikaeli kuwa juu ya kiwango sawa kama wengine "wakuu." Hiku kuwa na uwezekano kwamba kuna Malaika wengi, ni bora tusipuuze neno la la Mungu kwa kutangaza malaika wengine kama Malaika. Danieli 10:21 inamweleza Mikaeli malaika kama "mkuu," na Danieli 12:1 inabainisha Mikaeli kama "mkuu ambaye analinda." Hata kama kuna Malaika wengi, inaonekana kwamba Mikaeli ni mkuu kati yao.
Neno la Kigiriki kwa "malaika" katika Agano Jipya, angelos, liko katika hali ya kiume. Kwa kweli, aina ya kike ya angelos haipo. Kuna jinsia tatu katika sarufi - uume (yeye, naye, yake), uuke (yeye, yake, kwake), na usawa (yake, wake). Malaika kamwe hawatajwi katika jinsia yoyote zaidi ya ile ya uume. Katika sehemu nyingi malaika wanazo onekana katika Biblia, kamwe malaika wanajulikana kama "yeye" au "yake." Aidha, wakati malaika wanafanya kuonekana, wao daima huonekana wakiwa wamevalia kama wanaume binadamu (Mwanzo 18:, 16; Ezekiel 9: 2).
Usikose "sehemu ya Pili" ambayo tutajifunza kuhusu Malaika Mkuu Jegudiel au Yehudiel na kazi zake.
Barikiwa sana.
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

Saturday, March 18, 2017

PARIS: “Allahu Akbar” screaming Muslim murders his own father and brother in broad daylight by cutting their throats


A Muslim man was arrested in Paris on Friday suspected of slitting the throats of his father and brother at the entrance to a building in the capital’s trendy 11th district, police sources report. The sources, who asked not to be named because they were not authorized to speak publicly, said the motive for the attack was being investigated. (What, they’re not rushing out with the “mental issues” excuse?)

The Local  The two men died at the scene despite efforts by paramedics to save them. “I came down and saw one body in the hall and another in the courtyard. There was blood everywhere,” one resident told Le Parisien newspaper.

Some witnesses said the suspect made remarks “linked to radical Islam” but the police urged caution, saying the killer’s motives were unknown. 

Newspaper Le Figaro cited a police source who said the knifeman shouted “Allahu Akbar” (‘God is greatest’, in Arabic). The attacked happened outside a building on Rue de Montreuil in the east of the French capital near Place de la Nation (see map below).

CANADIAN BACKLASH against Trudeau’s anti-Islamophobia motion M-103 which will soon make criticism of Islam a crime


Even Muslim and Muslim apostate women in Canada are speaking out against the government’s efforts to ban free speech about the evils of Islam.

Is there a new ‘Black Plague’ that is threatening Europe again?


Certainly looks as if this infectious disease, also know as the ‘Black Death,’ has re-emerged in London…only this time, there is a cure. Remove all the carriers.

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination

Contradictions in the Quran: A Theological and Textual Examination By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction Muslims ...

TRENDING NOW