Tuesday, August 1, 2017

SHETANI NDANI YA ALLAH

Image may contain: 1 person, text

Ni nani aliyewapa waislamu mamlaka ya kuhukumu wakati aliye na mamlaka hayo ni Mungu/Yahweh pekee yake?
Ikiwa Allah, Waislamu wanaodai ndiye Mungu/Yahweh, ndiye aliyeamuru Waislamu kuhukumu, iweje Mungu/Yahweh abadilishe amri yake?
Je, yawezekana Mungu/Yahweh wetu awe kigeugeu na mkatili jinsi hii hadi atese wanadamu aliowapenda akamtoa Yesu Kristo ili awaokoe?
HAIWEZEKANI KAMWE; ALLAH WA WAISLAMU SIO MUNGU/YAHWEH WA WAKRISTO.
ALLAH NI SHETANI/IBILISI/NYOKA

DHAMBI ZILIZOSABABISHA KIFO CHA MOHAMMAD (SEHEMU YA 3)

No automatic alt text available.
Huu ni mwendelezo wa sehemu ya 1 na 2. Aisha anamuuguza Mohammad na Jibril anamuombea kwa Allah amnusuru na sumu aliyoila.
KUMBUKA: Imenukuliwa kutoka kwa Ibn Sa’d (ukurasa 250) Mohammad alijaribu kujitibu kutokana na sumu aliyotiliwa kwenye chakula.
Kutoka kwa Ibn Sa'd, ukurasa 263
Hakika, wakati wa ugonjwa wake, mtume alisoma "al-Mu'awwadhatayn" [Sura 113, and 114], na kujipulizia hewa huku akisugua uso wake (hii ilifanyika kwa nia kuwa apone).
Kutoka kwa Sahih Muslim Juzuu 3, # 5440
Aisha alisimulia kuwa mtume wa Allah alipougua, aliswali Mu’awwidhatan kwenye mwili wake na ugonjwa ulipozidi nilimswalia na kumkanda nikitumai kuwa atapona.
Kutoka kwa Ibn Sa'd, ukurasa 265
Mtume wa Allah aliugua na Jibril akamswalia akisema, “Kwa jina la Allah naomba kila kitu kinachokudhuru akizuie mwenye wivu na kijicho, na Allah atakuponya.”
Kutoka kwa Ibn Sa'd, ukurasa 265
Aisha, mke wa mtume alikuwa akisema, “Mtume wa Allah alipougua, Jibril alimswalia akisema, ‘Kwa jina la Allah ambaye atakuponya katika maradhi yote na kukuepusha na macho mabaya ya ibilisi mwenye wivu.’
Bukhari's Hadith 5.713:
Amesimulia Aisha; mtume akiwa anaumwa, kabla ya kufa, alisema, “Ewe Aisha! Ninahisi maumivu yanayosababishwa na chakula nilichokila kule Khaibar, na wakati huu, ninahisi ni kama mshipa wa moyo wangu unakatwa na hiyo sumu.”
Kisha ugonjwa wa mtume ukawa mbaya zaidi na akateseka kwa maumivu makali. Akasema, “Nimwagilie mwilini ngozi saba za maji kutoka kwa visima tofauti ili niende kwa wafuasi wangu na niwape maagizo.” Tukamfanya akae kwenye karai la Hafsa d. Umar na tukamwagilia maji haki akasema, “imetosha, imetosha!”
Kutoka kwa Ibn Sa'd ukurasa 322:
Huku siku za mwisho za mtume zikikaribia, alikuwa akivuta shuka na kufunika uso wake; lakini alipohisi vibaya, alijifunua na kusema: “Hukumu ya Allah iwe juu ya Wayahudi na Wakristo ambao walifanya makaburi ya mitume yao sehemu za ibada.”
Kutoka kwa Ibn Sa’d ukurasa 239
Siku ya kifo cha mtume ilikuwa imekaribia na aliamriwa aswali akirudiarudia ‘tasbih’ (utukufu) na amwombe Allah msamaha.
TATHMINI:
Aisha alimuuguza Mume wake huku akimwombea kwa Allah apone kutokana na kula nyama ya mbuzi (vitabu vingine vinasema ni kondoo) iliyotiwa sumu. Malaika Jibril pia alimwombea kwa Allah. Alitumia madawa ili apone lakini yote hayo hayakufua dafu. Huku siku zake za mwisho zikikaribia, Mohammad alijawa na uchungu mwingi. Aliwalaani Wayahudi na Wakristo na kumwomba Allah awaadhibu.
***SEHEMU YA NNE ITAKUJA HIVI KARIBUNI***

KUMBE ALLAH NA YEYE ANASWALI NA KUTAWAZA KAMA VIUMBE!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Image may contain: 1 person

Jamani eeeh, huu ni MSIBA kwa ALLAH:::::
Ndugu zetu wa kambo wanasema kuwa eti Allah ni Muislam. Basi leo hii mimi nimekubali kuwa Allah ni Muislam, lakini kuna mambo machache ningependa tuyaangalie:
ALLAH ANASWALI:
Quran 33: 56. Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu
Hapo Allah na Malaika wake wanamswalia Mtume Muhammad. Kumbe Allah na yeye anaswali kama viumbe. Hebu endelea kupata darsa
KABLA YA SWALA WAISLAM WOTE LAZIMA WATAWAZE
Kumbe Allah na yeye kabla ya swala lazima afanye "Taharah" ILI ATOWE "Najas".
KUMBE BASI NDIO MAANA ALLAH ANAOMBA KUTAKASWA JIONI NA ASUBUHI KABLA YA KUMSWALIA MAREHEMU MUHAMMAD.
HUU NI MSIBA MKUBWA SANA
Bila ya kupoteza muda tuanze kwa kusoma SURAT AL-AH'ZAB
(Imeteremka Madina). Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani , alie fanya tarjuma hii ni Mzalendo wa Zanzibar, aliezaliwa 13 January 1919, akapata mafunzo ya dini kwa baba yake Sheikh Muhsin bin Ali na kwa wanazuoni wengineo wa Afrika ya Mashariki. Pia Sheikh Ali amesoma ilimu ya zaraa katika Chuo Kikuu cha Makerere (Makerere University) huko Uganda.
MAANA YA KUJITAKASA
a. Ni kujiweka wakfu kwa ajili ya Mungu
b. Ni kuamua kwa dhati kabisa kuchukua hatua ya kuacha kutenda dhambi, kuishi katika dhambi na pia kuchukua hatua ya kuondoa kila aina ya dhambi uliyo nayo.
ALLAH ANAOMBA MUMTAKASE ASUBUHI NA JIONI. JE, ALLAH ALICHAFUKA LINI MPAKA AOMBE KUTAKAWASA?
((Enyi mlioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru)) ((Na mtakaseni asubuhi na jioni)) ((Yeye na Malaika Wake ndio Wanakurehemuni ili kukutoeni gizani mwende kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini)) ((Maamkiano yao siku ya kukutana Naye yatakuwa: Salama! Na Amewaandalia malipo ya ukarimu)) [Al-Ahzaab: 42-44]
Al-Ahzaab 33: 41-42,
41. Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru.
42. Na mtakaseni asubuhi na jioni.
http://www.quranitukufu.net/033.html
Jamani eeeh, Allah wa dini ya Uislam anaomba kutakwaswa, sasa huyu Allah alichafuka lini?
Ndugu Waislam, mnaweza tuambia ni uchafu gani mnao taka kuutakasa? http://www.quranitukufu.net/033.html
Jamani eeeh, Allah wa dini ya Uislam anaomba kutakwaswa, sasa huyu Allah alichafuka lini?
Kufuatana na Surah Al Baqara, Allah anapenda watu ambao wanajisafisha. Lakini kama kukiwa hakuna maji basi Muislam anarughusiwa kufanya Tayammum ambayo ni "wudu" na au "ghusl". Si mnajua tena kule kwa Allah hakuna maji....
MASWALI:
1. Kwanini Allah aswali kama viumbe na alikuwa anasali kwa Mungu yupi?
2. Kwanini Allah afanye "tahara" ili kutoa Najis?
3. Ni uchafu gani huo allah huwa anatoa/usafisha?
Maswali haya yameenda shule. Nategemea wafuasi wa allah wataleta ayat kusaidia majibu zao bila ya Matusi.
Watakabahu
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE’ BWANA YESU ANAPATAJE KUWA MUNGU? (SEHEMU YA SITA)


Image may contain: 1 person, text
Maelezo hayo yanatoa kanuni ya jumla ya kuzingatia katika kuyajadili matamko ya Bwana Yesu ambapo Yesu mwenyewe anaweka wazi kuwa kauli zake zinaweza wakati Fulani zikawa na uzito kueleweka mpaka pale anapoamua kuziweka bayana yeye mwenyewe, na kikubwa zaidi hapa Yesu anataja wazi kuwa miongoni kwa kauli zake hizo zilizofumbika ni ile inayohusu habari ya Baba na ndipo anaahidi kuwa upo wakati ambapo atafumbua fumbo hilo lihusulo mahusiano yake na Baba.
Hebu sasa tuone namna Yesu alivyoweka wazi mahusiano yake na Baba’
Yohana 10:30-33
Mimi na Baba tu umoja.31 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.32 Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu
Hii ni sehemu ya kwanza ya maandiko ambapo Bwana Yesu anaweka bayana juu ya undani wake wa asili na mamlaka moja na Baba kwa kusema wazi kuwa yeye na Baba ni umoja, tamko ambalo Wayahudi walielewa moja kwa moja kuwa lilionyesha kuwa Yesu alikuwa akithibitisha Uungu wake.
Na katika tamko jingine Yesu aliweka wazi kuwa hakuna utofauti wowote baina yake na nafsi ya Baba hebu tusome:-
Yohana 14:7-9
Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Katika andiko hilo Bwana Yesu anaweka wazi zaidi na kufumbua fumbo hilo mbele ya wanafunzi wake ambapo wanafunzi hao wanamhoji na kumtaka awaweke wazi juu ya uhusiano wake na Baba huku wakidai kuwa awaonyeshe huyo Baba, na ndipo kwa namna ya kushangaza Bwana Yesu anawajibu kwa uwazi kuwa tendo la kumfahamu yeye ndiyo kumfahamu Baba mwenyewe na kuwa kwa kumwona yeye tayari wameshamwona huyo Baba hivyo hawakuwa na haja ya kudai kumwaona Baba.
Hapo tendo la kumfahamu yeye ndiyo kumfahamu Baba mwenyewe na kuwa kwa kumwona yeye tayari wameshamwona huyo Baba hivyo hawakuwa na haja ya kudai kumwaona Baba.
Hapo Yesu aliweka wazi kuwa yeye ni Mungu toka katika umoja wa nafsi tatu za Mungu mmoja na kamwe hakuna tofauti za kimamlaka baina ya nafsi hizo kwa kuwa ni Mungu yule yule anayetenda katika katika upana kupitia Nafsi tatu yaani ile ya Baba , Neno na Roho Mtakatifu kama tulivyoona katika uchambuzi mpana wa hoja hiyo hapo mwanzoni
Hivyo jambo la msingi ni kuweka utulivu tu katika usomaji wa maandiko matakatifu maana kimsingi maandiko hayo yanatoa majibu ya kila swali linalotutatiza katika ulimwengu huu wa imani wenye walimu na farsafa nyingi za kidini.
Kwanini alilia Mungu wangu mbona umeniacha?
Katika mijadala mbalimbali ya imani kumesikika swali hili likihojiwa na walimu mbalimbali na wachambuzi wa dini, kile kinachotatiza hapa ni tamko la Bwana Yesu akiwa msalabani Mathayo 27:46…Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Hivyo swali linajitokeza hapa kuwa sasa Yesu alikuwa akimwomba Mungu gani ili hali yeye ni Mungu?
Jibu la msingi la swali hili’
Tamko hilo la Yesu msalabani endapo utalichukulia kama lilivyo pasipo kutafuta undani wake linaweza kukuingiza katika jaribu la kufikiri kuwa Bwana Yesu alikuwa ni kiumbe tu kwa hali zote.
Lakini msingi wa maandiko ya Biblia ulihusianisha tukio hilo na upande wa pili wa utendaji wa Bwana Yesu yaani ule wa kutwaa husika ya ubinadamu na kujiweka katika viwango vya ubinadamu ili kuwa kielelezo na hatimaye kutukomboa. Na hivyo hali hiyo ilimpelekea wakati Fulani kutamka na kutenda kama mwanadamu pamoja na kuwa asili yake si ya kibinadamu, na ndipo mtume Paulo anaweka wazi kanuni hiyo:-
Filipi 2:7
Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Biblia inafafanua kuwa baada ya Yesu kutwaa mfano wa ubinadamu hali hiyo ilimfanya kujifanya kuwa hana utukufu yaani wakati Fulani alitumia hali ya kawaida tu ya ubinadamu na si Uungu wake (uwezo, mamlaka) hivyo ndiyo maana hata alitamka maneno hayo akibeba husika halisi ya ubinadamu na kwakweli hapo alitamka kwa hali hiyo ya ubinadamu kabisa, ingawa tamko hilo halihafifishi mamlaka yake ya kiasili ya Uungu kwakuwa lilikuwa katika mpango mzima wa hatua zake za kiukombozi na kuvaa kiatu chetu.
Pia Yesu alikuwa akitimiza unabii’
Kwa upande mwingine Biblia inaweka wazi kuwa tamko hilo lililenga pia kutimiza tabiri za kiunabii kama Yesu mwenyewe anavyojenga msingi wa ukweli huu kwa kutamka:-
Luka 24:44
Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.
Katika tamko hilo Bwana Yesu anaeleza kuwa kuna mambo yanayomhusu yaliyoandikwa katika vitabu hivyo vya manabii lazima ayatimize katika kipindi cha huduma yake mambo au unabii ambao uliandikwa tayari katika vitabu hivyo vya manabii lakini anataja kuwa mambo hayo pia yamo katika Zaburi ya nabii Daudi.
Katika Zaburi hiyo ya nabii Daudi unaposoma Zaburi ile ya 22:1’ utagundua kuwa hapo kuna tamko lile lile la Yesu alilotoa pale msalabani kwa kusema “Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha?
Hivyo kwa mtazamo huo utagundua kuwa tamko lile la Bwana Yesu msalabani lililenga pia kutimiza unabii huo wa Zaburi ya Daudi kwakuwa hata Yesu mwenyewe alionyesha wazi kuwa alipaswa kutimiza unabii ulio katika kitabu hicho cha Zaburi hivyo swala hilo halihafifishi asili yake ya mamlaka ya Uungu.
Yesu alitimiza kanuni ya Biblia ya kukabili matatizo kwa kuomba na kuimba.
Pamoja na ufafanuzi huo wa msingi hapo juu bado maandiko ya Biblia yan endelea kupanua wazo katika hoja hii kadri tunavyosoma katika andiko jingine la mtume Yakobo kama ifuatavyo:-
Yakobo 5:13
Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Mtume Yakobo katika mitabu chake hicho anataja kanuni za mbili za kimbingu za kukabili matatizo kuwa jambao la kwanza yule aliyepatwa na matatizo anapaswa kuomba na pia aimbe Zaburi.
USIKOSE SEHEMU YA SABA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE’ BWANA YESU ANAPATAJE KUWA MUNGU? (SEHEMU YA SABA)

Image may contain: 8 people, people standing and text

Sasa tumefikia sehemu yetu ya mwisho ya kuthibitisha kuwa Yesu ni Mungu.
Endelea
Hivyo kwa hali halisi tutakubaliana kuwa katika hali ya kibinadamu Yesu alikuwa akikabiliana na mabaya ya mateso ya msalaba na hivyo kwa tamko lile alikuwa akitimiza masharti hayo kwa njia hiyo ya kuomba lakini pia kuimba maana tamko alilolitoa ni Zaburi (tenzi) ya 22:1 katika kitabu hicho cha mfalme Daudi, na kwa hali hiyo tendo hilo haliathari kwa namna yeyote mamlaka ya asili ya Uungu wa Bwana Yesu.
Hebu nikualike tena tunapokwenda kwenye uchambuzi wa swali jingine muhimu juu ya Uungu wa Yesu.
Mbona alilala, je Mungu analala?
Swali hili la msingi ndilo litakalotufikisha mwisho wa uchambuzi wa mada hii juu ya Maarifa kuhusu Utatu na Uungu wa Bwana Yesu. Na hapa hoja ya msingi inatokana na tukio la Yesu kusafiri na wanafunzi wake naye akiwa amelala katika Shetri hivyo wanafunzi wake baada ya kupata taharuki ya kubwa ya dhoruba wakaanza kumwamsha ili awape msaada katika kadhia hiyo kama tunavyosoma:-
Marko 4:37-38
Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.
38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Tendo hilo la kulala kwa Bwana Yesu linalosimuliwa hapo ndilo linalozalisha hoja hiyo ambapo waulizaji wa swali hilo hukaza hoja yao kwa kusoma pia andiko la kitabu cha Zaburi hii ifuatayo:-
Zaburi 121:4-5 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
Andiko hilo la Zaburi linaeleza kuwa Mungu aliye mlinzi wa Israel hatosinzia wala kulala, hivyo wajengaji wa hoja hii hudai kuwa tendo la Yesu kulala kama yeye ni Mungu basi ni hatua ya kukana Uungu wake.
Jibu la msingi la swali hili’
kimsingi hili ni moja kati ya maswali rahisi sana katika hoja hii juu ya Utatu na Uungu wa Bwana Yesu, lakini kile kinachoonekana kuwa ni mapungufu kidogo kwa waulizaji wa swali hili ni kutochukua hatua ya usomaji linganishi wa maandiko na kupitia aya nyingi zaidi ili kutafuta mantiki ya kisa hiki cha Yesu kulala na maelezo ya Zaburi yanayotamka kuwa Mungu halali.
Lakini kwa kujibu swali hili niseme tu kuwa andiko la Zaburi ya Daudi liko sahihi tu kuwa Mungu yeye kimsingi halali usingizi, lakini bado Zaburi hiyo hiyo inaeleza kile anchoweza kufanya Mungu katika dhana hiyo hiyo ya kulala hebu tusome tena andiko jingine la Zaburi ili kuanza hatua hii muhimu ya kupata ufumbuzi juu ya swali hili lenye utata:-
Tusome pamoja katika andiko hilo la Zaburi:-
Zaburi 78:65
Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, Kama shujaa apigaye kelele sababu ya mvinyo;
Katika andiko hilo tena nabii Daudi aneleza kuwa kumbe Mungu anaweza kuwa ‘kama aliyelala’ kumbuka andiko la kwanza linasema Mungu halali usingizi ambapo kulala huku kunaonekana kuwa ni halisi, lakini hapa nabii Daudi anatumia neno ‘kama aliyelala usingizi’ neno linaloonyesha kuwa mlalaji hakuwa katika hali halisi ya ulalaji wa kutojitambua na kujiweza.
Hivyo baada ya kupata ufafanuzi huo tunaweza kufanya jumuisho la hoja hii kwa kusema kuwa’ aina ile ya ulalaji wa Yesu inaonekana kulingana na hii ya pili ya kama aliyelala’ maana kwa hali halisi utaona kuwa hapo Yesu alikuwa tu akipima imani ya wanafunzi wake kwa tukio hilo kama ambavyo maandiko ya Isaya yanavyosema juu ya mfumo wa utendaji wa Mungu ambapo wakati Fulani kwa makusudi tu Mungu huweza kuwaacha watu wake kwa muda ili kuwapima:-
Isaya 54:7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.
Kwahiyo Mungu anaweza kwa muda fulani kuwageuzia kisogo watu wake ili kuona imani yao itaelekea wapi, na kwa hali halisi utaona kuwa hilo ndilo ambalo Bwana Yesu alilifanya katika tukio hilo akiwa na wanafunzi wake kwakuwa mara baada ya kuona kuwa imani ya wanafunzi wake imejielekeza kwake ndipo maandiko yanasema:-
Marko 4:39-41
Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? 41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?
Hivyo ndivyo Yesu alivyohitimisha tukio hilo kwa kitendo hicho cha kukemea upepo na bahari mara baada ya kuridhika kuwa wanafunzi hao walikuwa na imani iliyoelekezwa kwake katika tukio hilo la dhoruba. Lakini jambo la msingi linalojitokeza hapo ni kuwa tendo hilo lenyewe la kutuliza hali ya Bahari bado pia ni kiashiria tosha cha mamlaka yake ya Uungu na pengine waulizaji wa swali hili wangekichunguza kisa hicho chote wangeona tu jinsi kisa chenyewe kinavyothibitisha zaidi Uungu wa Yesu na si badala yake kukanusha.
Rejea tamko la wanafunzi wake baada ya tukio hilo:-
Marko 4:41
Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?
Hivyo hata wanafunzi wa Yesu wenyewe walionyesha kushtushwa na tukio hilo na hata kujiuliza swali juu ya nguvu na uwezo huo wa Yesu wakihoji ni nani huyu hata pepo na bahari vinamtii!, hoja ambayo inajibiwa wazi na Zaburi ya Daudi;-
Zaburi 89:8-9
Bwana, Mungu wa majeshi, Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU? Na uaminifu wako unakuzunguka. 9 Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari. Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.
Nabii Daudi anaweka bayana kuwa ni Mungu pekee awezaye kutawala kiburi cha bahari na yakuwa mawimbi ya bahari yainukapo mwenye uwezo huo wa kuyatuliza ni Mungu pekee na kwahivyo tukio hilo la Yesu kutuliza bahari linaweka bayana kuwa Yesu ni Mungu.
Hitimisho
Matamko ya wazi juu ya Uungu wa Yesu
Nipende kwanza kukushukuru ndugu msomaji wangu kwa kufuatilia kwa makini uchambuzi wa mada hii , na pia nitoe wito kwako kuwa kadri ambavyo umepata bahati ya kujifunza ukweli huu umkubali na kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako kwakuwa uweza nguvu na mamlaka juu ya mbingu na dunia viko juu yake pekee.
Baada ya wito huo nipende sasa kumalizia mada hii kwa kukuwekea nukuu chache za Biiblia zinazohitimisha uchambuzi huu kwa kuonyesha wazi juu ya mamlaka hii tukufu ya Bwana Yesu:-
Tito 2:13
Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Mtume Paulo katika andiko hilo la Tito anaweka wazi kabisa juu ya Uungu wa Yesu kama Tomaso na Bwana Yesu mwenyewe katika fungu hili jingine;-
Yohana 20:28-29
Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Mungu akubariki unapotafakari ukweli huu na kuchukua hatua.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

DHAMBI ZILIZOSABABISHA KIFO CHA MOHAMMAD (SEHEMU YA 4)

Image may contain: people sitting and food

Huu ni mwendelezo wa sehemu ya 1, 2, na 3. Uchambuzi wa kina wa maradhi ya Mohammad.
Katika kueneza dini yake, Mohammad na genge lake walishambulia makabila kadha na miji yao, wakiuwa yeyote aliyepinga dini yake mpya, kuteka wanawake na kuwafanya watumwa, kuwaoza na kunyakua mali ya makabila walioteka. Yeyote aliyekashifu au kupinga madai ya kuwa Mohammad ni mtume wa Allah alichinjwa na Mohammad au magenge yake. Maovu haya yalitia shaka na kuzua utata kuhusu uhalali wa utume wa Mohammad. (Ibn Sa'd kurasa 251, 252)
Hivyo, Wayahudi, ambao pia walishambuliwa na kuuawa na genge la Mohammad, walitaka kudhibitisha kama kweli Mohammad alikuwa mtume wa Allah kama alivyokuwa anadai. Wao walijua kuwa mtume wa kweli angeonywa na Mungu mapema kabla ya kuila ile nyama iliyotiwa sumu HADITH (Bukhari's 3.786). Hakika shaka yao ilidhibitishwa-Mohammad hakujua chochote na hakuonywa.
Ni baada ya kula ile nyama ndio Mohammad aligundua kuwa imetiwa sumu (yaani baada ya mguu wa mbuzi ‘kuongea naye’ kama vitabu vingine vinavyosimulia na kudai hii ni miujiza). Mtu yeyote anaweza akahisi tofauti ya ladha ya chakula aliyoizoea ikiwa imetiwa sumu. Hivyo, Mohammad kudai kuwa nyama choma kuongea naye ni miujiza ni upuzi mtupu. Hata mtoto mdogo anaweza kutema chakula ambacho kina ladha mbaya. (Ibn Sa'd ukurasa 249)
Mara nyingi hapo awali, Mohammad alikuwa akidai kuwa amepata ‘ufunuo’ uliomwonya dhidi ya hatari. Alitumia huo ‘ufunuo’ wake kama kigezo cha kuwashambulia Wayahudi kwenye makazi yao ya Banu Nadhir. Cha kushangaza, huo ‘ufunuo’ wake ulichelewa kuja kule Khaibar alipotiliwa sumu. Ulichelewa kunusuru maisha ya Bishir na maisha yake.
Kadri ugonjwa wake ulivyozidi kuwa mbaya, Mohammad akaanza kuomba uponyaji kwa Allah. Alijisugua mwili mzima na mkono wake wa ‘uponyaji’. Jibril vilevile alianza kumwombea apone. Mohammad alianza hata kujidungadunga ili damu itoke na kutoa sumu mwilini ( Ibn Sa'd ukurasa 322)
Lakini hizi juhudi zote hazikufua dafu. Ugonjwa ulipoendelea kuwa mbaya zaidi, Mohammad aligundua kuwa anakaribia kufa. Akakoma kuomba (Ibn Sa'd ukurasa 322) na kudai kuwa Allah amemruhusu achague kati ya kuenda Jannah au kuishi hapa duniani. Mohammad akasema kuwa amechagua Jannah. Akijua vizuri kuwa maombi yake yamegonga mwamba, akaamua kujipa moyo.
TATHMINI:
Wayahudi walidhibitisha kuwa Mohammad hakuwa mtume wa kweli. Alikula sumu bila kujua au kuonywa na Allah. Alifanya juhudi zote ili apone, alitumia madawa, aliombewa na Aisha na hata Jibril alimwombea, lakini hayo yote yalikuwa ni bure. Kifo kilimzidi nguvu Allah. Allah aliyemtumikia na kumtetea kwa upanga maishani yake yote alimkana wakati ambao Mohammad alimhitaji zaidi.
***SEHEMU YA TANO INAHUSU MASWALI, INAKUJA HIVI KARIBUNI***

ABDUL SASA ANAITWA JOSHUA AKIBATIZWA BAADA YA MIAKA 38 KATIKA UISLAM AMBAKO HAKUWA NA AMANI

Image may contain: 1 person
"Miaka 38 katika dini ya uislamu sikupata Amani nafsini mwangu. lakini leo nimekuwa uzao wa MUNGU katika Kristo. Sina lawama tena kwa sababu Nami nitarithi Ufalme wa BWANA.Jina langu lilikuwa Abdul maana Yake "Mtumwa." Lakini BWANA Akaniambia katika Zaburi 2:6-7 ya kwamba leo nimekuzaa. Bwana kanizawadia jina la Joshua il niwe Na matumaini yakufika kwenye inchi ya Ahadi"
"For 38 years in the relogion of Islam i found NO peace in my soul. But today I am a seed of GOD in Christ. I am no longer guilty of sin for now i am assured to inherit the kingdom of the LORD. My name was Abdul meaning SLAVE. But the LORD told me in Psalms 2:6-7 that today i have begotten you. The LORD gifted me a new name "JOSHUA" that i may have the HOpe of reaching the promised Land"
Huu ndio ushuhuda wa ndugu yangu Abdul Ntawuburumwansi; i want to kindly ask all of you to rem Him and the team He leads in Burundi as they share the love of Jesus all over Burundi and Rwanda.
Kaka Joshua, yeye YESU aliyekuita ni mwaminifu kukutunza hata nchi ile ya ahadi aliyotuahidi. Zidi kumpenda na kumtumikia yeye.

UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO (SEHEMU YA SITA)

Image may contain: cloud, sky, ocean, text and outdoor
Usemi wenyewe hudai uwepo wake:
Usemi wowote uletao maana hupangika kisarufi bila kugongana kimantiki. "Duara ni pembe tatu" Sarufi? Sawa. Maana? Hakuna. “Mungu hayupo” huangukia hukumu hiyo hiyo. Vichwani mwetu, "Mungu" ni Yeye astahiliye kuabudiwa kwa kuwa ni Mkamilifu katika uweza na uadilifu. “Mungu” ataitwa Mungu kwa kuwa yupo. Mrembo aliyeko kwenye jeneza si mrembo, na “Mungu” asiyekuwepo si “Mungu.” Kusema, ‘"Mungu” hayupo’ ni kumhesabu Aliye hai miongoni mwa wasio hai. Mtu huthubutu vipi kusema “Mungu hayupo” kama hajateleza ulimi pasipo kujitambua? (Zaburi 51:1-2;14:1-2). “Duara ni nyuzi 360” na “Mungu yupo” ni tungo mbili sahii kwa muundo na maana zake.
HATIMA YA MISRI
Misri iliwahi pia kuwa dola yenye nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati. Ukubwa wake ulikuwa kama 1600 (K.K) wakati majeshi ya Mafarao wavamizi walipojisogeza kusini ndani ya Sudani, Magharibi kuambaa pwani ya Afrika ya kaskazini, kaskazini kupita ardhi ya Kaanani (baadaye Israeli), na ndani ya Syria. Uvumbuzi kaatika baadhi ya Mahekalu ya kale, minara na makaburi umedhihirisha utukufu wa Mafarao ulivyokuwa katika kilele cha kuu wao.
Lakini ilipofikia miaka ya 1400 K.K nguvu ya Misri ilianza kurudi nyuma kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukua kwa Ashuru, na baadaye Babeli. Hata hivyo katika kipindi Waisraeli walipokuwa wakiikalia Kanaani, 1400-600 K.K, Wamisri waliingilia kati kwa nyakati mbalimbali siasa za Mashariki ya Kati, kwa mafanikio fulani. Waisraeli, walipokuwa wakiogopa uvamizi kutoka Ashuru na Babeli mara kwa mara walishawishika kutafuta msaada Misri badala ya kumtumainia Mungu wao.
Sasa manabii wa Israeli walikuwa na kitu maalum sana kusema juu ya hatima ya Misri. Nabii Ezekiel, ambaye matamko yake yalitolewa katika siku za Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kuanzia kama 600 K.K, alitangaza kwamba kutokana na hukumu ya Mungu, Misri ingekuwa upweke kwa miaka 40. Baada ya hapo kungekuwa na uamsho, lakini usiofikia ukuu wa nguvu zake za awali.
"Maana Bwana MUNGU aseme hivi; Mwisho wa miaka arobaini
nitawakusanya Wamisri, na kuwatoa katika hizo kabila za watu, ambazo walitawanyika kati yao; nani nitawarudisha hata nchi ya Pathrosi, hata nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni (ufalme wa chini).
Utakuwa duni kuliko falme zote; wala hatajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza ili wasitawale tena juu ya mataifa... Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu (Memphis), wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri. Ezk. 29:13-15; 30:13
Hapa napo maana ya unabii huu inaeleweka: Misri ingekabiliwa na matatizo ya uvamizi na watu kuchukuliwa mateka. Ingawa hakuna kumbukumbu halisi zilizobakia za matukio hayo, lazima yatakuwa ni matokeo ya uvamizi wa Wababeli kwa Misri, kama Ezekiel mwenyewe alivyotabiri (tazama Ezek: 30:17-20). Lakini huo usingekuwa mwisho wa Misri. Maana baada ya miaka 40, mateka wangerudi tena katika nchi yao wenyewe. Misri, kama ufalme usingeangamizwa: ungedumu lakini nguvu yake ingeshushwa sana - "Ufalme mdogo," usioweza kutumainia nguvu zake kukabili mataifa yanayopakana nayo tena.
Ufalme mdogo
Na ndivyo ilivyotokea. Tangu kama mwaka 600 K.K, Misri aliangukia chini ya watawala wa kivamizi, kwanza wa Wababeli katika karne ya 6 K.K; kisha Waajemi kati ya karne ya 6 na 4; alafu Wayunani katika karne ya 4; wakifuatiwa na Warumi karne ya kwanza K.K mpaka karne ya 5 B.K. Walifuatiwa na Waarabu na Waturuki kutoka karne ya 7 B.K na kuendelea. Hata Waingereza wameitawala Misri kwa kipindi katika karne ya 19. Kwa miaka 2500, Misri imebakia kama alivyotabiri Ezekiel kuwa ingekuwa, "Ufalme wa chini," wakati wote ikikaliwa na wengine. Lakini Misri na Wamisri hawakutokomea. Bado wapo, na wameponea uhuru kiasi miaka ya karibuni, washukuru misaada mikubwa ya fedha wanayopata kutoka Marekani na Saudi Arabia.
Tuweke pembeni kidogo mawazoni swala la Misri wakati tukiangalia mfano wa tatu wa utabiri wa Biblia wa matukio ya mbele, kwa kutazama.
==== USIKOSE SEHEMU YA SABA==== UNABII KUHUSU ISRAELI
Huu ndio uliojaa kuliko wote, kimaelezo ya utabiri wake, na pia katika wingi wa thibitisho zihusuzo ukweli wake kimatukio kihistoria.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

KWANINI ALLAH WA WAISLAM SIO MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: one or more people and text

ALLAH JINA LAKE SIO NIKO AMBAYE NIKO:
Waislam wanadai kuwa Musa aka Moses ni Mtume wa Allah, lakini hawakubali na au Quran haisemi jina maalum la "MIMI NIKO AMBAYE NIKO" ambalo Musa alipewa na Mungu.
Katika Kitabu cha Kutoka "Moses' Pentateuch" kilicho kuwepo miaka 1312 KK - kabla ya kuzaliwa Yesu. Tunasoma.
Kutoka 3: 14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu. 15 Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.
Musa alipo kutana na mti ulio kuwa unawaka bila ya kuteketea. Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. --- > Soma Kutoka Mlango wa 3. Mungu alijitabulisha kwa jina la MIMI NIKO AMBAYE NIKO kama tulivyo soma hapo juu.
LAKINI ALLAH AMEGOMA NA AU KATAA KUTUMIA HILI JINA LA KIPEKEE LA "MIMI NIKO AMBAYE NIKO".
Katika Quran, hakuna aya hata moja ambayo Allah amejitambulisha kwa jina hili la NIKO AMBAYE NIKO, zaidi ya hapo, hakuna Sahih Hadith hata moja inayo kiri kuwa Allah jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO na au katika yale majina 99 ya Allah hili jina la NIKO AMBAYE NIKO HALIPO
Jina hili la Allah lina maana "miungu". Huu ni umoja wa miungu 360 ya kipagani iliyo kuwa inaabudiwa huko Kaaba wakati wa Muhammad na kabla ya Muhammad. Hivyo basi, Allah hawezi kuwa NIKO AMBAYE NIKO au YEHOVA bali ni mungu wa kipagani tu. Soma (Who Is This Allah?, G. J. O. Moshay, 1994, p 138) na au soma (The Moslem Doctrine of God, Samuel M. Zwemer 1905, p 24-25)
Kaa kweli Musa alikuwa Muislam, kwanini kwenye Quran hakuna JINA HILI LA NIKO AMBAYE NIKO?
HAKIKA ALLAH SIO MUNGU WA MUSA NA MUSA HAKUWA MUISLAM.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

YESU ALISEMA: KABLA YA IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NI MUNGU

Image may contain: crowd and text
Msipaniki Waislam. Kaa chonjo na fungua macho yako ya rohoni.
Kwa maneno rahisi, katika Yohana 8:58 Yesu alikuwa anasema “Kabla Ibrahimu asijakuwako mimi ni Mungu”
Yohana 8:58 Yesu aliposema;
“….Amin, Amin, nawambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko” Wayahudi kwanini waliokota mawe? Soma Walawi 24:16. “Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamuua kwa kumpiga kwa mawe;..”
Je Yesu alimaanisha nini aliposema mimi niko hata wakaona amekufuru? Hebu tuone niko ni jina la nani?
Kutoka 3:13-14; “….Tazama, nitakapofika kwa wana wa Waisraeli na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wataniuliza, Jina lake n’nani? Niwambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO…MIMI NIKO amenituma kwenu.”
Kumbe "MIMI NIKO" ni jina la Mungu.
YESU NI MUNGU
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

The Prophethood of Muhammad

  The Prophethood of Muhammad: A Critical Theological Evaluation By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute, New York, NY The cla...

TRENDING NOW