Tuesday, August 1, 2017

DHAMBI ZILIZOSABABISHA KIFO CHA MOHAMMAD (SEHEMU YA 4)

Image may contain: people sitting and food

Huu ni mwendelezo wa sehemu ya 1, 2, na 3. Uchambuzi wa kina wa maradhi ya Mohammad.
Katika kueneza dini yake, Mohammad na genge lake walishambulia makabila kadha na miji yao, wakiuwa yeyote aliyepinga dini yake mpya, kuteka wanawake na kuwafanya watumwa, kuwaoza na kunyakua mali ya makabila walioteka. Yeyote aliyekashifu au kupinga madai ya kuwa Mohammad ni mtume wa Allah alichinjwa na Mohammad au magenge yake. Maovu haya yalitia shaka na kuzua utata kuhusu uhalali wa utume wa Mohammad. (Ibn Sa'd kurasa 251, 252)
Hivyo, Wayahudi, ambao pia walishambuliwa na kuuawa na genge la Mohammad, walitaka kudhibitisha kama kweli Mohammad alikuwa mtume wa Allah kama alivyokuwa anadai. Wao walijua kuwa mtume wa kweli angeonywa na Mungu mapema kabla ya kuila ile nyama iliyotiwa sumu HADITH (Bukhari's 3.786). Hakika shaka yao ilidhibitishwa-Mohammad hakujua chochote na hakuonywa.
Ni baada ya kula ile nyama ndio Mohammad aligundua kuwa imetiwa sumu (yaani baada ya mguu wa mbuzi ‘kuongea naye’ kama vitabu vingine vinavyosimulia na kudai hii ni miujiza). Mtu yeyote anaweza akahisi tofauti ya ladha ya chakula aliyoizoea ikiwa imetiwa sumu. Hivyo, Mohammad kudai kuwa nyama choma kuongea naye ni miujiza ni upuzi mtupu. Hata mtoto mdogo anaweza kutema chakula ambacho kina ladha mbaya. (Ibn Sa'd ukurasa 249)
Mara nyingi hapo awali, Mohammad alikuwa akidai kuwa amepata ‘ufunuo’ uliomwonya dhidi ya hatari. Alitumia huo ‘ufunuo’ wake kama kigezo cha kuwashambulia Wayahudi kwenye makazi yao ya Banu Nadhir. Cha kushangaza, huo ‘ufunuo’ wake ulichelewa kuja kule Khaibar alipotiliwa sumu. Ulichelewa kunusuru maisha ya Bishir na maisha yake.
Kadri ugonjwa wake ulivyozidi kuwa mbaya, Mohammad akaanza kuomba uponyaji kwa Allah. Alijisugua mwili mzima na mkono wake wa ‘uponyaji’. Jibril vilevile alianza kumwombea apone. Mohammad alianza hata kujidungadunga ili damu itoke na kutoa sumu mwilini ( Ibn Sa'd ukurasa 322)
Lakini hizi juhudi zote hazikufua dafu. Ugonjwa ulipoendelea kuwa mbaya zaidi, Mohammad aligundua kuwa anakaribia kufa. Akakoma kuomba (Ibn Sa'd ukurasa 322) na kudai kuwa Allah amemruhusu achague kati ya kuenda Jannah au kuishi hapa duniani. Mohammad akasema kuwa amechagua Jannah. Akijua vizuri kuwa maombi yake yamegonga mwamba, akaamua kujipa moyo.
TATHMINI:
Wayahudi walidhibitisha kuwa Mohammad hakuwa mtume wa kweli. Alikula sumu bila kujua au kuonywa na Allah. Alifanya juhudi zote ili apone, alitumia madawa, aliombewa na Aisha na hata Jibril alimwombea, lakini hayo yote yalikuwa ni bure. Kifo kilimzidi nguvu Allah. Allah aliyemtumikia na kumtetea kwa upanga maishani yake yote alimkana wakati ambao Mohammad alimhitaji zaidi.
***SEHEMU YA TANO INAHUSU MASWALI, INAKUJA HIVI KARIBUNI***

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW